Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Ebu tuanzie hapa mkuu job creators wa uchuuzi ama?? Maana tunachofanya ni kuuza biashara za wenzetu(maproducer China, Japan and so on)
Vyovyote vile wewe kua mbunifu pika chapati,Maandazi fanya bunifu mbali mbali pia kubali kuanzia Chini unatoboa mkuu.

Mbona hata wahindi wanachuuza dawa

Apply MERCANTILISM yaan una buy cheap na una sell dealy
 
Baada yakumaliza shule sasa uko field unajifunza mambo ya field kuhusiana na maisha...

Mimi baada yakumaliza shule nilikaa kitaa na nikapitia hali kama yakwako, ila sasa maisha hayatokaaa tena kuwa kama ya mwanzo. Wakati sina kazi nilijifunza jinsi yaku manage pesa.
 
Pole sana ndugu yetu. Bahati mbaya dunia haina fair play na hata elimu yetu ya sasa haioanishi mafanikio na kiwango cha elimu ulicho nacho. Cha msingi pambana hata kwa kufanya mambo mengine ili maisha yasonge. Sasa hivi wazazi tumebaki kuwahimiza wanafunzi wasome ili kufuta ujinga. Yaani mtu anasoma hadi degree kufuta ujinga 🤣🤣🤣🤣
 
Ushauri pekee na mwisho tumia Kinga kwa Kila Kitendo kama huna mtoto. Usijiroge ukajipa mtoto wa mtu mimba sahivi. Utajua hujui??
 
Majibu ya ki gentleman haya murua kabisaa 😊☺️
 
Mining Engineer 😂😂😂 nacheka kama mazuri ,vile .
Hii nchi ni mazafaka , sishauri mtu asome Engineering ,ni usenge kusoma course ngumu na expensive halafu inamaliza masomo unapiga hata appreticeship na bado mtaani ajira hamna na chache zilizopo ni kwa rushwa na connection .
Naongea kutokana na experience ya hii issue niliyonayo .
Don't you dare !
Danganyika nation inahitaji socialogists , waalimu na nurses
Engineers tujitafute Kwa shughuli nyingine la sivyo utashtukia mvi zimejaa kichwani bado inatafuta ajira tu
 
Ebu elezea kwa kina hapa socialigists (watendaji wa Kata ama vitengo vipi kwenye ajira)
 
Pole sana mkuu ila usikate tamaa bado mapema mno, endelea kupambana kwa shughuli zingine nje ya ulichosomea..... wakati wako utakuja tu, amini hilo.
 
Wewe ni muongo umri miaka 27 wakati umeanza seko kpnd kata seko ndo znaanza
 
Shida ipo kwenye kozi uliosoma.
Ukisema kwenye mining kuna vijana hata hwana elimu wanatega baruti na kulipua miamba migaodi midogo na ya kati
MIgodu mikubwa GGM hapa geita mchina amekuja na kifaa cha kupasua miamba ww utafit wap?


Ujenzi nako na hicho cheti chako unaenda kufanya kaz kama nani? Maana wanaitaji man power wTu wakujenga na kuchangany zege ww uta fit wap?

Labda ujaribu TARURA Angalau uwe unapata tenda za kukwangua murramu Road.
Shusha expectation za kuajiriwa kwa hii Taaluma uliosoma angalia field nyngne cha muhimu ni kupata pesa
 
Hatari. Halafu wakati tupo chuo tunajiona, mainjinia si ndo sisi😅😅
 
Ilikuwa ni 2005/2006 sio??
Kitu kama hicho rafiki, wekapo miaka 7 kabla ya s/msing na miaka 7 baada ya s/m hapo aseme anaelekea 40yrs.

Halafu wakat anamalza chuo nna uhakika kwa kiwango chake cha ufaulu na rekod yake tangu s/m, migod mikubwa kama GGM na Buzwag wangekua washa mgongea/ kumwekea oda kabla hata hajamaliza chuo labda kama fields zake alikua anazifanyia kwenye tumigod tudogo tudogo coz najua walokua wanapga fd migod mikubwa na wakaonyesha uwezo mkubwa walikua wanakua booked mapema sana.

Kitu kimoja tuwekane sawa hapa, practical sio theory na theory sio practcal so unaweza kua mzuri kwenye makaratas halafu ukawa wa hovyo unapopewa mashine ufanye kaz.

Ushauri, kuna watu hawana hata chet cha la7 ila n wakemia migod midogo ya uchenjuaji madn (dhahabu) maarufu kana migod ya kuozesha (vat reaching plants) nenda kajifunze hyo fan for free kikubwa uwe na hela yako ya kula wskat wa mafunzo. Migod mingine mtu kama wewe unaweza kwenda kujfunza ni elution plants na sp plants.

Geology mnasoma miamba halafu unakua na njaa kweli?? Kwahyo hujui jinsi ya kuipata miamba ya dhahabu eti? Au umesomea miamba ya chumvi? Tafta mashine za kufanyia survey ya miamba (we unajua mnafanyaje) ukipata hyo mashine nenda machakani huko katafte miamba ukiipata nenda ofis za madini omba resen ya kuchimba umiliki claim (kilempu, kwa kibongo bongo). Then tafta mtu mwenye mtaji mkachimbe hizo dhahabu. Kumbuka uki claim eneo hata la kituo cha afya au police unaweza kuwalipa wenye eneo wakahama we ukapiga kaz kama huwez kuwalipa bas mtagawana dhahabu. NB NB NB Vipimio vya miamba vipo had vya laki na nusu
 
Kuna mimi form 4 three ya mwisho ,form 6 two ya mwisho chuo GPA ya 3.2 . Law School first sitting

mambo sio mabaya .. Point yangu ni ufaulu sio kigezo cha kufanikiwa jua pa kupiga na kwa wakati gani upige .akili ya darasani na kwenye Field ni vitu viwili tofauti
 
Huwezi kua umeingia seko kipindi shule za kata zinaanza ukawa na miaka 27.

That aside, kwanini usirudi chuoni kwenu ukaomba kufundisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…