Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Njoo hapa tufanye kazi kijana usilalamike sana..

Mchongo upo hivi. Kampuni yetu unafanya kazi kwa siku ni 15000 hyo kwa ajili ya kula..

Akini pia mwisho mwezi unapewa chako kama kawaida yaani mshahara..

Sasa kazi ipoje.. kuwa mpole...
Kwanza hii kampuni yetu unajihusisha na uuzaji wa blue band. Na biadhaa nyingine kama mafuta pamoja na majiko ya gesi.

Kazi unafanya vipi. Utapata maelekezo ofisini.
Je ukiulizwa nyumbani unafanya nini jibu ni..... Bussness manager

Mkuu pesa ipo huku hatuzunguki sana mda mwingi upo kwa gari.

Ikitokea root ya mkoani utainjoi sana sana sana tena sana.

Kama ni mtu wa totoz mkuu hapa ndo.mahari pake mkuu..

Karibu sana mkuu.
Your warmly welcome
Mzee wa mshangazi umeamua kutoa tag inapendeza🤔😐

Nadhani hii comment yako ndo comment bora
 
pole sana mkuu lakini usikate tamaa kama kesho yako ipo ipo tu ,sasa hapo mkuu inabidi uwe makini na age ujiongeze usije ukazeeka hujafanya chochote tafuta ajira ujinyime upate mtaji uachane na maswala ya ajira,maana matajiri wote walipata elimu wakaitumia na kufanya kitu,kupata mtaji ndopagumu ukishapata kianzio cha mtaji mbona utaona kuajiriwa ni upuuzi.MUNGU AKUSAIDIE KWA KWELI.
 
Tafuta mchongo kasome nje na zamia huko bongo utasota sana. Utasema huna hela au connection hizo ni sababu uchwara, weka nia utafanikiwa.
 
Tafuta mchongo kasome nje na zamia huko bongo utasota sana. Utasema huna hela au connection hizo ni sababu uchwara, weka nia utafanikiwa.
Kuna jamaa Mbongo alifariki Mwaka Jana km sijakosea alipata zari Scholarship akaenda kusomea Bachelor ya Computer Science U.S akazamia huko huko Google wakamchukua akaja kupata ajali kwenye boti ndio ikawa hivyo akafia ndani ya maji
 
Pole sana mkuu, wako wengi. Kuna mmoja ana ufaulu mkubwa sana zaidi yako, Olevel div 1 ya 9, Advance div 1 ya 4, akaingia top 20 wanafunzi bora kitaifa, Chuo akasoma petroleum, mpaka sasa hana ajira rasmi.

Watu walianza kusoma PetEng 2010 wakati bongo imetanganza kupata reserve kubwa ya gesi kule kusini. Gesi kapewa mzungu wabongo wamebaki kuchoma mihogo tu kitaa, kazi nje zipo kibao za hiyo michepuo tatizo wabongo wote wanadhani maisha yapo kijijini kwao tu wakienda mbali sana wanaishia Dar. Moreover, serikali inadhani kumpa mtu passport ni uhaini. Nchi ya kipumbavu sana.
 
Kuna jamaa Mbongo alifariki Mwaka Jana km sijakosea alipata zari Scholarship akaenda kusomea Bachelor ya Computer Science U.S akazamia huko huko Google wakamchukua akaja kupata ajali kwenye boti ndio ikawa hivyo akafia ndani ya maji

Nampata. Wabongo wanaofanya kazi fortune500 wapo wengi sana, hao wachache ni wale ambao mmewasikia, huko google, apple, Microsoft, Tesla, amazon, Chase, BOA, Meta, Boeing, wall street hadi CIA wapo wengi tu. Na kazi sio lazima ufanye huko yapo makampuni mengi sana yakufanya kazi au kujiajiri mwenyewe huko nje. Maisha sio TZ tu, maisha popote bongo tutarudi kuzikwa tu kama miviongozi ya ccm si mnaona wote huwa wanafia nje.
 
Kazi zinahitaji connection ni kweli lakini connection unazitengeneza mwenyewe.

Kwa mfano,
1. kuna maonyesho ya uchimbaji wa madini kila mwaka je umewahi kuhudhuria angalau ukijua ni makampuni yapi yapo kwenye imdustry yako na yanafanya nini wapi.. Ukachukua na business card na ukafanya soft approach.

2. Kuna wanafunzi wenzio ambao walikuwa wamekutangua au mmemaliza pamoja na wamepata kazi. Je unawasiliana nao na kuwatembelea? Tembelea rafiki zako walioko kazini watakukutanisha na watu wengine kwenye industry.. Unatengeneza connection.

3. Kuna lecturers zako wa vyuo. Ulikuwa na uhusiano mzuri unawasiliana nao. Wale wana connection nyingi tu.

Connection zinatengenezwa hakuna aliye zaliwa akiwa ana ana connection, labda watoto wa viongozi ambao ni wachache sana.
 
Nampata. Wabongo wanaofanya kazi fortune500 wapo wengi sana, hao wachache ni wale ambao mmewasikia, huko google, apple, Microsoft, Tesla, amazon, Chase, BOA, Meta hadi CIA wapo wengi tu. Na kazi sio lazima ufanye huko yapo makampuni mengi sana yakufanya kazi au kujiajiri mwenyewe huko nje. Maisha sio TZ tu, maisha popote bongo tutarudi kuzikwa tu kama miviongozi ya ccm si mnaona wote huwa wanafia nje.
Ukweli kabisa mkuu ukitoka nje hamia huko huko huku ukitaka kuzikwa rudi tuje kukuzika au kufa huko huko utakuja kuzikwa huku
 
Miaka 27, bado mtoto mdogo hata usiogope sisi wengine tunakaribia umri wa kustaafu na hatujawahi kuwa na kazi inayoeleweka
Sasa mwanangu cannabis nkuchekeshe wakati naanza 🤣darasa la kwanza kipind hicho mule Kuna Watu walikuwa na miaka 18, 17, hapo ni darasa la kwanza na wakati namaliza darasa la saba mkubwa alikuwa na miaka 24🤣

Fomsix yetu mkubwa alikuwa na miaka 33🤣Huyu jamaa sahv ni mzee sana tukikutana huwa tunacheka sana maana walimu walikuwa wanashindwa kumpa adhabu sababu alikuwa na upaa afu ukumbuke kipindi hicho tunavaa suruali kubwa shati kubwa kishenzi🤣

Nilipokua Chuo wakawa wananiita uncle "sharpshooter"
Philomena ni KE sio ME -Khalid na Philomena walipendana na penzi lao lilidumu
Jamii forum hakuna mwny Jina halisi mkuu labda
 
Habari wana jukwaa. Kwa kweli hivi sasa bila connection ni ngumu kupata kazi, vinginevyo Mungu aingilie kati. Binafsi kwa neema ya M/Mungu nimefanikiwa kuwa nahistoria ya kufanya vizuri darasani, na kuwa mwanafunzi bora kuanzia nilipokuwa shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Historia yangu kwa ufupi ipo hivi.

Primary

Ufaulu mzuri nikapangiwa kwenda sekondari, japo ni ya kata, wakati huu ndo shule za kata zimeanzishwa kwa wingi, hivyo hata wenye ufaulu mzuri walipelekwa shule hizi ili kufidia gap la wanafunzi

Sekondari

Nilifanya vizuri sana. Nimekuwa mwanafunzi namba moja darasani tangu kidato cha kwanza mpaka cha nne na nikafanikiwa kuzawadia cheti cha mwanafunzi bora na uongozi baada ya kufanya vizuri kwa miaka yote minne ya sekondari.

Nikafaulu kwa ufaulu wa daraja la kwanza, nikiwa mwanafunzi pekee darasa nzima la wanafunzi 138 mwenye daraja la kwanza na nikapangiwa kwenda Advance kwa mchepuo wa PCM (Physics, Chemistry, Advance Math)

Advance

Hapa napo sikukaa kizembe, katika darasa la wanafunzi 38, kidato cha tano na cha sita vyote nilikuwa mwanafunzi namba moja ama namba mbili kwenye mitihani ya terms na kikanda. Katika wanafunzi 38 wa PCM, wanafunzi 2 pekee tukafanikiwa kupata Div I. Hivyo moja kwa moja tukapangiwa chuo kikuu, na wote tulikwenda chuo kimoja, UDSM (University of Dar Es Salaam)

Chuo Kikuu.

Nikasomea program ya engineering (Engieering Geology), ni program ya miaka minne. Kwa ufupi hapa shule ilikuwa ngumu sana, ukijumlisha na changamoto za kifedha, lakini historia ya nyuma ya shule ilinibeba nikapata mkopo wa serikali 100%. Chuoni tulianza wanafunzi 14, lakini tuliobahatika kumaliza mpaka mwaka wa mwisho ni wanafunzi 6, na katika hao sita, ni mimi pekee nilifanikiwa kufaulu kwa kiwango cha juu kidogo ukilinganisha na wenzangu cha Second class honors, Upper division ambacho na hakika si kiwango haba kutokana na ugumu wa program husika.

Hio ndo historia yangu ya shule kwa ufupi sana, nimeelezea matokeo tuu, sijaelezea matukio. Lakini nasikitika kuona kwamba rekodi hio haijawa na mchango chanya kuniwezesha kupata kazi. Mpaka sasa kijana natangatanga, hapa na pale. Nipo wazi kufanya kazi kwenye migodi ya uchimbaji, kampuni za ujenzi wa majengo na barabara. Na kwa sasa nina leseni ya ulipuaji (blasting licence for both Open pit & Underground mining)
Hahah! Ama hakika kupata kazi zama hizi connection... Wakuu nipeni CONNECTION!! Umri ni miaka 27.
Wakati mwingine muwe munajiongeza! Sasa "Engieering Geology" kwa hapa bongo unategemea nini? Labda utafute vyuo vikuu vipya uajiliwe kama "tutorial assistant "
 
Jamii forum hakuna mwny Jina halisi mkuu labda
Labda ni la demu wako
Screenshot_20241113-201021.png
 
Watiaji moyo hamkosekani mwamba anataka channel yenye connection sio kumtia moyo mpigieni pande hilo
Binadamu tunaishi kwa matumaini. Kinachotufanya tulale tuamke kesho tukahangaike ni matumaini. Ukikosa matumaini unachanganyikiwa. Hivyo ni muhimu kuwapa watu matumaini kwa kuonyesha experience ya wengine.
 
Binadamu tunaishi kwa matumaini. Kinachotufanya tulale tuamke kesho tukahangaike ni matumaini. Ukikosa matumaini unachanganyikiwa. Hivyo ni muhimu kuwapa watu matumaini kwa kuonyesha experience ya wengine.
Toa Connection mkuu wewe upo kwenye Channel toa Connection
 
Back
Top Bottom