Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Kama ulianza form1 wakati shule za kata zinaanzishwa na ukasoma Enginnering geology chuo, basi itakuwa uligraduate 2014.
You are my classmate. 2014 hadi leo ni miaka 10. Bado unahaha kutafuta kazi. Utafutaji wa kazi ukiuendekeza sana utashtukia uzee huu. Hamna cha maana ulichofanya.

Ushauri wangu. Ni wakati sasa wa kupunguza au kuacha kabisa kutia effort kwenye kutafuta kazi. Anza kujitafuta wewe. Japo hata kwenye kujitafuta bado ni kwamoto lakini niamini ukitia nia, ipo siku utajipata. Nilikuwa kama wewe zamani. Mimi nimesoma mining Engineering. Zoezi la kutafuta kazi nimeabolish rasmi mwaka 2020. Saivi nashukuru am good the other way.
KILA LA KHERI MPAMBANAJI.
Huyu kasema Ana miaka 27 ko hio 2014 alikua anamaliza form four au alikua form three.
 
Hatari. Halafu wakati tupo chuo tunajiona, mainjinia si ndo sisi😅😅
Nakwambia ,nà shule ya Engineering ni ngumu haswa sasa unamaliza unakuja kukutana na nyundo za kichwa za ukosefu wa ajira huku kitaa na hauna mtaji wa kusajiri kikampuni uchwara cha kujiajiri ili kuanza kupata tender ndogondogo ,lazima kichwa kiwake moto
 
Pole sana mkuu, wako wengi. Kuna mmoja ana ufaulu mkubwa sana zaidi yako, Olevel div 1 ya 9, Advance div 1 ya 4, akaingia top 20 wanafunzi bora kitaifa, Chuo akasoma petroleum, mpaka sasa hana ajira rasmi.
Unaemsemea c alhamia chemical engineering
Graduate wa tabora boys
 
japo tayari umeshasoma ila ulibug sana kusoma engineering geology,

vp akina lupogo hawakukukamata, kessy, mshiu et al, ulitoboa miaka yote bila sup.
Hahah! Lupogo nilipiga A course yake, akaniahidi kazi, baadad akapotelea kusikojulikana.
 
Sina hapana ni mtakatifu kwenye

Ukiangalia record yako ya ufaulu kwa maoni yangu inaonesha trend mbovu ya mahusiano tangu shuleni.

O-level umepata div one peke yako kati ya watu 138
A-level mmepata div one wawili tu
Na chuo trend ni the same.

Connections huwa zinaanza kujengwa level za primary, mtu anaweza asiwe na uwezo mzuri sana class ila ana connections ambazo ukiwa na mahusiano mazuri anaweza kukuconnect na watu ukapata unacho hitaji.

Matokeo na ufaulu wako yanaakisi kiwango flani cha ubinafsi wa kujitenga na kutotaka kushare knowledge na wenzio nao wakafanya vizuri nadhani ni sababu kubwa unastruggle kupata japo ajira pamoja na ufaulu mzuri.

Watu wa aina yako mara nyingi ikitokea hawajabebwa na matokeo yao kwenye kazi/maisha huwa wanapitia unachopitia.

Hujachelewa, change mindset yako, ongeza kiwango chako cha interaction na watu mtaani bila kujali status zao sana ilimradi unaona wanaweza kukuvusha kwa jambo lako.

Ile mindset ya shule kutaka kufaulu prke yako mtaani haiko relevant. Mtaani we ukifanikiwa haizuii mtu mwingine kufanikiwa bali ili ufanikiwe zaidi unahitaji kuzungukwa na walio fanikiwa zaidi pia.

Ukiwa matured utagundua kuwa Maisha ya mtaani ni about improving and helping each other na si kushindana. Mtaani, matokeo ya jitihada za mtu yanategemea zaidi volume ya watu ulionao (network) wakati shule unaweza komaa kivyako na ukatoka na flying colors.
Mkuu umenigusa sana mimi mtaa ninao ish wengi ninawazidi uwezo. Wachonizidi ni uzee tu, Na umr Kila mara napigwa vizinga🤣natamani Ata nihame mtaa maana nahitaji watu waliofanikiwa ili nijifunze zaidi najiona bado sana level ninayoitaka

Nakunukuu"ili ufanikiwe unahitaji kukaa na waliofanikiwa zaidi"
Matokeo ya jitihada za mtu ya nategemea zaidi volume ya watu ulionao(network) KMkhalid ish humo.
 
Umri wako bado tender sana usihofu we pambana utakaa pazuri sana hautaamini kijana bado maxi zako zitakubeba wakati na sehemu sahihi
 
Habari wana jukwaa. Kwa kweli hivi sasa bila connection ni ngumu kupata kazi, vinginevyo Mungu aingilie kati. Binafsi kwa neema ya M/Mungu nimefanikiwa kuwa nahistoria ya kufanya vizuri darasani, na kuwa mwanafunzi bora kuanzia nilipokuwa shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Historia yangu kwa ufupi ipo hivi.

Primary

Ufaulu mzuri nikapangiwa kwenda sekondari, japo ni ya kata, wakati huu ndo shule za kata zimeanzishwa kwa wingi, hivyo hata wenye ufaulu mzuri walipelekwa shule hizi ili kufidia gap la wanafunzi

Sekondari

Nilifanya vizuri sana. Nimekuwa mwanafunzi namba moja darasani tangu kidato cha kwanza mpaka cha nne na nikafanikiwa kuzawadia cheti cha mwanafunzi bora na uongozi baada ya kufanya vizuri kwa miaka yote minne ya sekondari.

Nikafaulu kwa ufaulu wa daraja la kwanza, nikiwa mwanafunzi pekee darasa nzima la wanafunzi 138 mwenye daraja la kwanza na nikapangiwa kwenda Advance kwa mchepuo wa PCM (Physics, Chemistry, Advance Math)

Advance

Hapa napo sikukaa kizembe, katika darasa la wanafunzi 38, kidato cha tano na cha sita vyote nilikuwa mwanafunzi namba moja ama namba mbili kwenye mitihani ya terms na kikanda. Katika wanafunzi 38 wa PCM, wanafunzi 2 pekee tukafanikiwa kupata Div I. Hivyo moja kwa moja tukapangiwa chuo kikuu, na wote tulikwenda chuo kimoja, UDSM (University of Dar Es Salaam)

Chuo Kikuu.

Nikasomea program ya engineering (Engieering Geology), ni program ya miaka minne. Kwa ufupi hapa shule ilikuwa ngumu sana, ukijumlisha na changamoto za kifedha, lakini historia ya nyuma ya shule ilinibeba nikapata mkopo wa serikali 100%. Chuoni tulianza wanafunzi 14, lakini tuliobahatika kumaliza mpaka mwaka wa mwisho ni wanafunzi 6, na katika hao sita, ni mimi pekee nilifanikiwa kufaulu kwa kiwango cha juu kidogo ukilinganisha na wenzangu cha Second class honors, Upper division ambacho na hakika si kiwango haba kutokana na ugumu wa program husika.

Hio ndo historia yangu ya shule kwa ufupi sana, nimeelezea matokeo tuu, sijaelezea matukio. Lakini nasikitika kuona kwamba rekodi hio haijawa na mchango chanya kuniwezesha kupata kazi. Mpaka sasa kijana natangatanga, hapa na pale. Nipo wazi kufanya kazi kwenye migodi ya uchimbaji, kampuni za ujenzi wa majengo na barabara. Na kwa sasa nina leseni ya ulipuaji (blasting licence for both Open pit & Underground mining)
Hahah! Ama hakika kupata kazi zama hizi connection... Wakuu nipeni CONNECTION!! Umri ni miaka 27.
I feel maumivu yako hayaelezeki nakumbuka nilikuwa kama wewe na fikra zako cha moto nilikiona dunia haina huruma hata kidogo usikate tamaa Allah yupo
 
Nenda maeneo iliyopo migodi ya Barrick, Bulyanhulu au North mara fanya Assessment kupitia wale wananchi wanaoishi maeneo yale huwa wengi sana wanapata kazi kwenye hiyo migodi wengine ni mechanics tu wanaajiriwa kuoperate mitambo na hiyo mitambo yenyewe wanajifunzia kazini humo humo.

Ukipata ajira hata isiyoendana na fani yako siku ikitokea ajira za fani yako na upo ndani unakua na advantage kubwa ya kupata, ila hii kuomba ajira baada ya kuona online ni ngumu sana kupata huko migodini
Ahsante sana mkuu!
 
Nina jambo moja lenye njia mbili za kufuata ama kufanya chagua yote ama moja,,tafuta kibarua chochote ufanye hususani Cha kufundisha mashuleni au vyuoni. Siku hizi kuna shule na vyuo vingi sana.Jambo lingine wakati unafanya hicho kibarua utakuwa unapata pesa za hapa na pale hizo sio za kukutoa kwenye dimbwi Isipokuwa badala yake tumia hizo pesa kuongeza ujuzi.Zingatia kuongea ujuzi juu ya Degree Yako,ujuzi upi sasa?.Ukiwa kama kijana naamini una smartphone,una laptop na una internet connection,kama huna tafuta uwe navyo.Ingia online tafuta online courses kutoka vyuo kama coursera na udemy hivyo ni mfano tu,huko nenda kaongeze ujuzi mbali mbali ada zao ni kuanzia Dola 10 Hadi 100 kwa kozi.Na kwa background Yako nakushauri chukua sana sana ujuzi wa Data science, Data analytics, Cognitive Science na Kila unapopiga hatua ya kumalizia course utapata vyeti.Kusanya ujuzi kadri uwezavyo.Na katika hizo kozi usiache kozi moja muhimu sana inatumika Kila sekta kwa sasa,iyo ni excel.Chukua kozi ya ujuzi wa excel Tena katika level ya advanced level,usiache.Hayo yote huku ukiongeza ujuzi wa kuwasiliana kisasa,kikazi na kibiashara.Hayo yote unaweza kuyafanya ndani ya mwaka mmoja tu.Baada ya hapo nakuhakikishia utakuwa fit kuingia sekta yoyote hata banking nakuambia na nakuhakikishia utakuja kunishukuru.
Umetisha sana kiongozi. Thank you sana. Nitalifanyia kazi.
 
Miaka 27 bado mkuu! Wengine tumepata kazi serikalini tukiwa above 30 yrs! Wengi wanajichanganya kwenye kuchagua course mavyuoni, kwa ufaulu wako ungekuwa umesomea course zingine mfano civil, mechanical, Electrical, IT hizo course hata usipoajiriwa na serikali huwezi kulala na njaa!!

Note: mimi sio muumini wa connection toka nafanya usaili pale utumishi nimepiga saili nyingi sana mpaka nakuja kupata kazi ilikuwa nafasi moja na nikaenda nikapiga nikachukuliwa kwa hiyo usiamini kwenye connection pambana sema wewe ulichagua course zenye nafasi za ajira chache ndo maana unaangaika mkuu! Ila kuwa na subira siku yako ikifika utafidia miaka yote uliokaa mtaani
Shukrani sana.
 
Ndiyo maana mi mtoto wangu nimempangia asome mwisho form 4 then peleka SUA akasomee KILIMO NA UFUGAJI then akiwa anaingia Degree namuanzishia duka la pembejeo akimaliza nauza viwanja viwili namfundisha kufuata madawa ya mifugo na shambani KENYA NA CHINA likiwa pumbafu shauri lake nahamia kwa mdogo ake.
KAMA UMEPENDA HUU MPANGO WANGU GONGA LIKE TWENDE WOTE
Mambo sio rahisi hivyo
 
wakati namaliza chuo nilikuwa na rafiki yangu mmoja alisoma Minning engineering huku mimi nasoma computer engineering miaka ya 2000 mwishoni
kuna mzee mmoja aliniambia kwenye kutafuta kama huna connection basi hakikisha uwe kwenye eneo sahihi
natamani kujua uko wap

ila kama plan yako ni migodini anza na ma contractor wadogo migodini(dar) pasahau kwa muda nenda kahama,shy,geita,mara
 
Shukrani sana.
Sawa ina maana umemaliza na miaka 24 usiwaze mkuu kimsingi una viungo vyote kamili Usijali nimeeleza juu asilimia kubwa wanaomaliza hivi karibuni kupata kazi inachukua 1-5 kwahyo "changamoto itumie kama fursa" ipo siku utafanikiwa

Mimi nipo geita kuna fursa nyingi mgodini Geita gold mine zinatoka Ila mchawi sasa atleast uwe Ata leseni ya udereva(buses, manual cars like land cruiser, HAice, Hilux hizi ndo aina na magari zinazotumika huko unaweza ukaanza kama dereva wa boss then Mungu s athumani ukapata pande) ku-operate machine huwezi kosa fani yoyote mule


Mwisho watu wengi wameshauri mengi mazuri, sasa muhimu ni wewe kufanya maamuzi yako sahihi. Maana wahenga walisema "kelele nyingi humtoa mtu kwenye focus"

Mungu akubariki, Sali sana, Amka mapema, ujifunze zaidi elimu kitaa haina mwisho. Cheti cha mtaani tunapewa siku tukifa.
 
Back
Top Bottom