Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Bila shaka we ni mchimbaji mdogo. Ama la umekaa sana na wachimbaji wadogo. Yoote uliyoyaongea, kwakuwaza tuu yanawezekana yote. Ukiyaingiza katika uhalisia huambulii hata moja.
 
Wew msomi ama mpumbavu yaani kusoma kote huko hukutambua lengo la elimu ya kiafrika ni kuwafunza raia kusoma&kuandika then wajiendeleze wenyewe ktk kazi za mikono? Na baadhi yao kwa uchache wanachukuliwa kama cheap labour/wafanyakazi wa serikali ktk secta mbalimbali.

Nyie wasomi wa kukalili mambo mtaendelea kusota na maisha mpka mtakapogundua lengo la elimu si kukupa maisha mazuri wala kukupa ajira, bali kukupa mwanga wa wewe kupambana na changamoto ktk mazingira.

Hakuna ajira muelewe na mtambue kuwa serikali haiwezi kumfuraisha kila mtu, matokeo yako darasani hayakupi uhalali wa maisha mazuri wala kupredict future yako, bali maono yako na kujituma kwako ktk shughuli za uzalishaji&biashara&sanaa.

Narudia tena, enyi wasomi vilaza muelewe kuwa, lengo la elimu hasa ya kibongo, si kukupa maisha bora wala si jukumu la serikali kukupa maisha bora, hilo ni jukumu la mzazi wako na wewe mwenyewe.

Shule tulienda kujifunza vitu vichache vitusaidie kuyaelewa mazingira&namna ya kuwasiliana na jamii , na kwa wachache sana kuwafanya wajakazi wa kuwatumikia raia wengine ktk nyanja mbalimbali.

Mtaisoma namba, mlidhani kufaulu darasani ni tiketi ya kufaulu maisha? Wake up and change your mind, dunia haina huruma, acha kujilizaliza na kutaka huruma hapa, ukweli mchungu, rudi mtaani tafuta uhalisia wako wa maisha yako utaukuta huko, uzuri wa mtaa njoo na akili zako tu, ujuzi utaukuta huku huku.

Shame on you.
 
Safi
 
Watu bado hawajatambua kuwa zama zimebadirika, inashangaza msomi wa marks nzuri nayeye analialia ajira ngumu, mtu huyu kama aliweza kuelewa michezo ya darasani alishindwa vipi kuusoma mchezo wa maisha ya uhalisia kuwa mahitaji ya waajiriwa yanahitajika kwa watu wa Elimu ipi, nafasi ipi, na secta zipi zilizo na magape ya kutoa ajira&mahitaji ya taifa ni yapi?

Vijana wengi wakishafanikiwa kufaulu vizuri basi hata hawafikilii tena mambo ya baadae wao wanabeti maisha kuwa chochote atakachokisomea ilimladi kafaulu basi atatoboa na yalivyo majinga yanachagua zile course ngumu zenye majina ya kutisha, kumbe deep down yanajikomoa yenyewe.

Wasomi wetu bado hawajui kuusoma mchezo wa maisha unaenda vipi, wao wanaishi kwa kubeti na kutegemea bahati
 
Nenda Ajiraportal omba hizi nafasi then uendelee na kutafuta vijiwe vya kupata hela ya kula.
 
Mimi namjua mmoja aliajiriwa akiwa na 34, maisha si mchezo kwa mwanaume.
 
Hahahaa.

Jamaa umeburudisha ila ni ukweli mchungu sana uliousema.

Niongezee tu hapa, Mzazi kama unajiweza hakikisha unamtengenezea mwanao mazingira ya kuchomoka mapema, kusoma kwa mfumo wetu huu ili baadae uje ujikwamue ni jau sana, Dunia imebadilika
 
Njoo hapa tufanye kazi kijana usilalamike sana..

Mchongo upo hivi. Kampuni yetu unafanya kazi kwa siku ni 15000 hyo kwa ajili ya kula..

Akini pia mwisho mwezi unapewa chako kama kawaida yaani mshahara..

Sasa kazi ipoje.. kuwa mpole...
Kwanza hii kampuni yetu unajihusisha na uuzaji wa blue band. Na biadhaa nyingine kama mafuta pamoja na majiko ya gesi.

Kazi unafanya vipi. Utapata maelekezo ofisini.
Je ukiulizwa nyumbani unafanya nini jibu ni..... Bussness manager

Mkuu pesa ipo huku hatuzunguki sana mda mwingi upo kwa gari.

Ikitokea root ya mkoani utainjoi sana sana sana tena sana.

Kama ni mtu wa totoz mkuu hapa ndo.mahari pake mkuu..

Karibu sana mkuu.
Your warmly welcome
 
Aombe hizi nafasi
 
Point mkuu
Ukiona kama hujiwezi jaribu kijinyenyekeza kwa mwenyezi mungu anaweza kufungulia njia sehemu yoyote ile sio lazima uajiriwe.
Ika kama unahisi bado una nguvu na vyeti unaweza kujipambania mwenyewe endelea
 
Inachukua mtu yeyote au vigezo ni vipi mkuu nije na Mimi hapo
 
Umerogwa?
 
Watiaji moyo hamkosekani mwamba anataka channel yenye connection sio kumtia moyo mpigieni pande hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…