TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

Dah mwana kafa, dah aisee. Dah RIP huyu mwamba kanifundisha phyisics sana pale mzumbe motto mwenge, Dah mwamba alikuwa anajua sana madude sema, hakuna mtu alikuwa anahisi anaakili kama mwamba, alikuwa anajiita Eistein, dah huyu ni pigo kubwa kwa wanafunzi wa physics , jamaa kafa na physics yake, RIP MWAMBA.
Vipi ajamlisisha mtu yoyote ujuzi. Au wote mlikuwa mnashangaa tu anapofundisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mkuu kwa Msiba .

Yaani mtu amesomaaaa, kisha kafundishaaaa halafu kafa . Kweli maisha mafupi sana 😪

Vijana wengi sana wanaoshika hela mapema.. wanakufa mapema sana... stds zinawachukua sana vijana... vijana vichwa huwa hawaishi sana sabab ya wanawake
 
RIP Mwamba simjui lakini imenigusa poleni wanafamilia na marafiki na Mimi mwenyewe
 

Attachments

  • FB_IMG_1605857879723.jpg
    FB_IMG_1605857879723.jpg
    40 KB · Views: 74
  • FB_IMG_1605857918483.jpg
    FB_IMG_1605857918483.jpg
    88.9 KB · Views: 74
  • Screenshot_20201120-103046.png
    Screenshot_20201120-103046.png
    242 KB · Views: 76
  • FB_IMG_1605857722024.jpg
    FB_IMG_1605857722024.jpg
    37.1 KB · Views: 74
Ulitaka njibu vp
Ujinga wenu mnafikiri kwamba gifted person lazima agundue kitu
Kwa hyo Kama hakugundua ameendeleza walivyogundua wengine sio gifted
Ndio maana mnangangania eti alikuwa anakariri
Nadhani nyie ndio mnaokariri Sasa
Kweli elimu haijawasaidia

Mbona nyie hamjaweza kukariri basi mkapata hzo A tukawaandika hata hapa jf?
Mm simjui huyo kijana lakini nimesoma Phys na Chem mpaka chuo kikuu najua huwszi kukariri kea kiwango Cha huyo kijana
Naandika kitu ninachokifahamu
Hapo alikuwa na uwezo sio kukariri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Elias alkua anakupa alternative tatu ya swali moja utasemaje huyo mtu anakariri , Mimi tu physics nlkua sikariri and that made us different

Anyway sijataka kubishana na huyo da Vinci because hamjui

Mimi nmekaa nae nmeishi nae , nmesoma nae pia
Sure mwanangu,Physics ya A level ni ya moto balaa,nimesoma PCB,naelewa joto la physics.
 
Leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili.

Tunahitaji kuwa Karibu na Mungu wakati wote kwani safari yetu ipo mikononi mwake.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never Forget you My brother

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were. Rest in peace up in the heaven.

-----

ALAMA ALIZOACHA ELIAS KIHOMBO

Imepita miaka takribani miaka 14 sasa, tangia Tanzania ilipapata kumshuhudia mwanafunzi alishindikana katika masuala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama Kibaha, Ilboru, Mzumbe, Kilakala, Tabora Boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa Wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga Secondary kuendelea na masomo yake ya Advance Level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)

Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.

Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania, hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo, Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo (tetesi )

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011, 2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania kuwa na uwezo mkubwa darasani. Nlsikia jinsi ambayo eng elias alikuwa na kipaji cha kufundisha kuanzia asubuhi mpk jioni na kusitokee hata swali moja liliomtolea nje .siku ambayo alisolve maswali kuanzia saa moja hadi saa nne hakuna swali lililo msumbua saa tano hadi saa nane hakuna swali lililo msumbua saa tisa hadi saa kum na mbili hakukua na swali lililo msumbua tuliendelea na mwendo huo kwa muda wa wiki moja . Itabaki historia ktk maisha ya wanafunzi na elimu ya Tanzania kwa ujumla.

Lakin leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili. Tunahitaji kuwa Karbu na Mungu wakati wote kwan safari yetu ipo mikononi mwake. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never Forget you My brother

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were.

Rest in peace up in the heaven

View attachment 1630262
View attachment 1630283
Apumzike kwa amani huyu mhandisi, poleni wafiwa.

Hapo pia nimeona the tragedy of academic hyper-performance inayoambatana na arrogance. Mnisamehe sana kwa maoni yangu haya.

Kwa kutazama fates za hawa hyper-performers hasa wa O-level na A-level, naona bora mtoto apate passes za kawaida tu zinazotosha kwenda chuo na kuendelea na maisha, kwani hizi za kuzidi sana zinaleta pia mambo mengine magumu ambayo mtoto anashindwa kukabiliana nayo.

Usishangae kusikia kuwa hao wenzake walioorodheshwa pamoja hapo kwenye jedwali la matokeo sasa hivi wana maisha mazuri tu, wana makazi yao, familia zao, vipato vya uhakika na wanafurahia maisha, lakini mwenzao huyo waliyekuwa wakimsifu sana na hata kumuonea wivu ameishia maporomokoni.

Mnajua hawa "Tanzania-One" wanakoishia baada ya misifa hiyo? Tuwaombee sana hawa watoto na tuwasaidie sana.
 
Nenda kwenye kitabu cha waliohitimu 2013 if you can see his name, by the way alikuwa anapuuzia sana shule, tulikuwa nae field TPDC akiwa alihudhuria only one week, prof. Temu amekuja kutembelea he was explaining the thing that he don know, superviser alikuwa ndugu yake alimkataa pale pale kuwa alikuwa hahudhurii, sina uhakika kama ni hiki kilichomtoa chuo, baada ya hapo kuna shule alienda kufundisha kuna uzi humu unaelezea tafuta
"He was explaining the thing that he don know"
Nani alikuwa anaexplain? Prof Temu au Kihombo?
Ungetumia kiswahili ungeeleweka vizuri
 
Apumzike kwa amani huyu mhandisi, poleni wafiwa.
Hapo pia nimeona the tragedy of academic hyper-performance inayoambatana na arrogance. Mnisamehe sana kwa maoni yangu haya. Kwa kutazama fates za hawa hyper-performers hasa wa O-level na A-level, naona bora mtoto apate passes za kawaida tu zinazotosha kwenda chuo na kuendelea na maisha, kwani hizi za kuzidi sana zinaleta pia mambo mengine magumu ambayo mtoto anashindwa kukabiliana nayo.
Usishangae kusikia kuwa hao wenzake walioorodheshwa pamoja hapo kwenye jedwali la matokeo sasa hivi wana maisha mazuri tu, wana makazi yao, familia zao, vipato vya uhakika na wanafurahia maisha, lakini mwenzao huyo waliyekuwa wakimsifu sana na hata kumuonea wivu ameishia maporomokoni.
Mnajua hawa "Tanzania-One" wanakoishia baada ya misifa hiyo? Tuwaombee sana hawa watoto na tuwasaidie sana.
Umeongea ukweli

Ukweli kabisa
 
Imenibidi kupitia comments nyingi sana ili kujifunza kitu.

Apumzike kwa amani.
Ni hazina hiyo imeondoka, niaona ni jinsi gani ilivyo ngumu kwa waliomfahamu kuipokea habari hii.

Kikubwa ni kwamba sote tutaungana naye katika safari yake saa ikifika.
 
Back
Top Bottom