TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

Vijana wengi sana wanaoshika hela mapema.. wanakufa mapema sana... stds zinawachukua sana vijana... vijana vichwa huwa hawaishi sana sabab ya wanawake
Ina. Mana pamoja na kujua sana kemia na phisikia alishindwa kabisa kuitumia japo kujikinga na ngoma?
 
Sasa kama hizo akili umekaa nazo nyumbani kwenu jamii itakujua vipi kama una akili zaidi? Kihombo katunga vitabu, kafundisha vijana na ndio wanashuhudia kuwa alikuwa na akili zaidi.
Kama umekaa nazo nyumbani[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Elimu ya bongo na wasomi wetu inatia huruma sana. Kama huyu ndo alifananishwa na Einstein basi mie ndio Tesla😀😀 Huyu jamaa kwa nilivyokuwa naona approach zake za kusolve maswali sidhan kama mitihani ya olympiad angepewa angetusua hata 40%

Anyway, aliwahi kuja pale mzumbe nikiwa A-level akasema kwamba Yeye na shetani wakikaa wakatunga swali la physics basi mungu hawezi solve(hii ni sacrilege kubwa sana).

R.I.P Kihombo, you'll be remembered
MLEVi Mmoja kumbe umesoma mzumbe!?!
 
Ndio unakalili sasa kaitendea nn physics kama alikua anaijua vizuri yani kaleta nn kipya kama sio kukalili
.................Haya mfano wewe tuiweke physics pembeni.

Kiswahili tu kinakushinda,umekisaidia nini au umeongeza nini kwenye Kiswahili pamoja na kuwa ni lugha yako ya taifa?kukalili ndo lugha gani!

Kujua kwako sana physics ndo kulikokufundisha “kukariri” uitamke “kukalili”?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina. Mana pamoja na kujua sana kemia na phisikia alishindwa kabisa kuitumia japo kujikinga na ngoma?
Sikh hizi karibia kila kifo cha MTU maarufu,hiyo kitu lazima itajwe. Ikiwa ni kweli,inawezekana kitaa hali sio nzuri.
 
Afadhali kama alipata angalao wasaa wa kuowa na kupata mtoto,simjui ila nimesikitika sana watu smart na msaada kama hawa kufa hata hawajazifurahia elimu zao,duniani huko watu level yake wanagombania yupi awe tajiri wa dunia wa kwanza na nani awe wa pili ila kibongo bongo sometimes huyu kafariki hajaijengea hata familia yake msingi wa maisha.

Mungu amrehemu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani jamii yetu huwa siilewi hapa mtu kaacha mtegemezi mnasema afadhali?
 
Namuomba MUNGU amlaze roho yake mahali pema peponi Elias Kihombo na Mohamed Ngaola. Hakika wameacha pengo kubwa kwa wanafunzi wa sasa lakini naamini materials yao yatakumbukwa vizazi na vizazi. Mimi nna notes zote nilizoandika za Mudy Physics na Hidden kuanzia form 3 ad 4 toka mwaka 2007 na ad leo ninazo na ntamuhifadhia mwanangu akikua insha'Allah aje aone.

Elias Kihombo na Mohammed Ngaola wamepigana Vita vilivyo vyema na wamevishinda na Imani wameilinda.
 
Kuna yule mwl, wa tuition wa physics muddy juzI kati kafariki... Huyo ndio tunafahamu.... Sasa Elias kamaliza juzi petroleum engerering chuoni kwetu..
Kafa lini?

Binafsi kama wewe tu ulivyoshitushwa na hizo Habari, Juzi kati nimesikia Muddy physics kavuta ..! Leo hii tena huyu [emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]. Kama ni kweli basi watupatie taarifa za kutoka chanzo cha kuaminika.

Lakini serikali yetu pendwa ingekuwa na program maalum kwaajili ya watu extraordinary kama Elias na kuwadhamini kwenda kusoma huko nje kwa mfano course aliyokuwa anachukua angesomeshwa Telecom huko Nje ya nchi kama RUSSIA AU US, Huenda angekuja na kitu cha kuinufaisha nchi yake Tanzania.
Daaah Rest in peache bro.!
 
Yaani jamii yetu huwa siilewi hapa mtu kaacha mtegemezi mnasema afadhali?
Jamii yetu na kina nani!!!wewe na familia yako au na kina nani?usilazimishe kila mtu aamini unachoamini wewe.

Unajua huyo mtoto atakuja kuwa msaada kwa kina nani?mf;mimi baba yangu alikufa akaniacha na miezi minane (8) tu ila unajua sasa hivi ni kwa kiasi gani nimekuwa msaada kwa mama yangu,ndugu zangu na jamii inayonizunguka?unadhani kila mmoja angekuwa anakufa bila kuacha mtoto even wewe ungekuwepo leo?

Imani yangu wewe bado mtoto hujajitambua.
 
"Aliugua mda mrefu" [emoji848]

Kuna gonjwa naliwaza hapa
Cancer watu wanaugua muda mrefu,sukari watu wanaugua muda mrefu,figo wanaugua muda mrefu even frustration ni maradhi endelevu na mengineyo sasa wewe unataka kusema nini alikuwa akiugua je aliwahi kuja kwako kutaka ushauri ukampima?

Ujinga tu,au unadhani kuwa TO kunamtenga kuwa kama binadamu wengine?
 
Back
Top Bottom