Rev. Moses Maghembe ajitoa T.A.G

Rev. Moses Maghembe ajitoa T.A.G

Kifupi
Hakuna dini itakayompeleka mtu mbinguni

Naamini haya makanisa nayo hayamfikishi mtu Mbinguni

Sambazeni injili ya Yesu aliehai

Sio maghembe tu

HATA yulepast alikuwa mbagala sasaivi.yuko.mbele.kidogo anamsimamo sanaa

Nae kajitoaa TAG
KAANZISHA LALE CHRIST.....USIMFWATE MTU FWATA MUNGU ALIE HAI
 
Nipo upande wa Mosses Maghembe na huyu ndio miongoni mwa watumishi wa Mungu
Nipo upande wa Mossess Maghembe huyu ni miongoni mwa watumishi wa Mungu wa kweli wanaohubiri injili ADIMU sana ile injili ya kweli 100% pure concentrated isiyo kuwa diluted na mambo ya uraia wa dunia zaidi Mkristo wa kweli anatakiwa awe raia wa mbinguni anayeko safarini hapa duniani lakini aishi maisha ya mbinguni akiwq hapa duniani.
Kwa hiyo injili adimu ni kuhubiri msicheze nyimbo zenye hadhi ya hip hop au regae,kablabya kuoana msifanye friendship and dating,n.k.
 
Kwa hiyo injili adimu ni kuhubiri msicheze nyimbo zenye hadhi ya hip hop au regae,kablabya kuoana msifanye friendship and dating,n.k.
hip hop/reggea ni utamaduni(ni imani,ni roho) UTAMADUNI wa kidunia ,haitakiwi kuingiza utamaduni wa midundo ya hip hop kanisani katika nyimbo za injili.Sio hip hop pekee miziki yote ya kidunia ni ibada kamili /roho kamili za miungu ya dunia(kuzimu).Na lengo lake ni kulaani maisha ya wasikilizaji na kuwajaza roho chafu za dhambi.

UZINZI ni dhambi vijana ,waepuke UZINZI
wanatakiwa waombe kwa Mungu awapatie NDOA sio ku date sex partners washikaji,wapenzi/UZINZI.

DHAMBI zinajulikana kwa mujibu wa neno la Mungu BIBLIA na muongozo wa Roho mtakatifu.

Hitimisho..KILA MTU afanye kama alivyokusudia moyoni mwake si kwa lazima ,na amani ya Mungu iamue moyoni mwake anacho ona ni sahihi kwake kufanya.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Tumesikia na tunaheshimu maoni yako. Swali dogo ni hayo uliyoyatqja hapo juu ni maoni yako namna vile wewe unavyoona?
Yote yamekatazwa na neno la Mungu na Roho mtakatifu pia anatuarifu kuyaacha.
 
Mchungaji mwenye msimamo mkali inapokuja suala la kumtumikia Mungu aliye hai Rev. Moses Maghembe ameamua kujiondoa kuwa chini ya usimamizi wa kanisa la mahali pamoja laTanzania Assemblies of God T.A.G

Kama ilivyokuwa kwa wajina wa Maghembe, alikuwepo Moses Kulola ambaye alijitenga na T.A.G na kuanzisha E.A.G.T kwa kutokukubaliana na baadhi ya misingi ya kanisa haswa inapokuja suala la kumtumikia Mungu ipasavyo. Wengi tunafahamu uhodari wa Moses Kulola na huduma yake katika kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Rev. Maghembe ndiye mchungaji pekee alikuwa na uthubutu wa kukosoa uongozi wa askofu Mkuu wa kanisa la T.A.G Dr. Barnabas Mtokambali. Alikosoa kitendo cha kanisa la kiroho kutoa tuzo ya amani kwa mwendazake wakati matukio ya mauaji yalikuwa juu.

Pia alikosoa waziwazi maadhimisho ya chama cha vijana ndani ya kanisa C.A.S yaliyofanyika Iringa kwa kufanya bonanza la mpira wa miguu. Maghembe alidai ile siyo njia ya kuhubiri injili ila ni kuishiwa kwa maono na kanisa kuanza kuiga mambo ya kidunia, kanisa linatakiwa kuleta athari duniani na siyo dunia ilete athari kanisani

Kuwa na ministry binafsi au kuwa chini ya uongozi. Wewe uko upande gani?

View attachment 3180718
Huyu si ndiye aliwakosoa mabinti wanaochekacheka siku ya Harusi kwamba bangili zao tayari zina crack
 
Embu twende mstari kwa mstari. Taja mstari na jambo lililokatazwa
Kuna mstari gani unaokataza SIGARA,SHISHA,MADAWA YA KULEVYA...je kwa vile hakuna mstari unaokataza kuvuta sigara ,je tuseme sigara si dhambi??
Tunatakiwa tuenende tukiongozwa na ROHO mtakatifu amani ya Kristo iamue mioyoni mwetu.
.Kila mtu na afanye kama alivyokusudia moyoni mwake si kwa lazima wala si kwa huzuni
akiongozwa na amani ya moyo wake na neno na Roho mtakatifu.
 
Kuna mstari gani unaokataza SIGARA,SHISHA,MADAWA YA KULEVYA...je kwa vile hakuna mstari unaokataza kuvuta sigara ,je tuseme sigara si dhambi??
Tinatakiwa tuenende tukiongozwa na ROHO mtakatifu amani ya Kristo iamue moyoni mwetu..Kila mtu na afanye kama alivyokusudia moyoni mwake kama akiongozwa na amani ya moyo wake na neno na Roho mtakatifu.

Hiyo mifano uliyoweka kuna mistari inayoelekeza kuwa ni mbaya

Tupatie mifano mingine kuntu
 
Back
Top Bottom