Tetesi: Ridhiwan Kikwete, Freeman Mbowe, Halima Mdee, miongoni mwa wadaiwa Twiga Bancorp

Tetesi: Ridhiwan Kikwete, Freeman Mbowe, Halima Mdee, miongoni mwa wadaiwa Twiga Bancorp

Awali Rais wangu John Pombe Magufuli aliposema kuwa kuna wanasiasa wanaongea sana ilhali ni wadaiwa sugu kwenye mabenki hakika sikuelewa. Ila kadri siku zinavyoenda, inazidi kudhihiri kuwa hakika maneno ya Rais wetu ni kweli kabisa.

Taarifa rasmi nilizonazo ni kwamba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ni miongoni mwa watu waliochangia kufilisika kwa Benki hiyo. Taarifa hizo zinasema kuwa Freeman Mbowe peke yake anadaiwa mkopo wenye thamani ya shilingi bilioni saba hii ikijumuisha mkopo wenyewe na riba. Taarifa hizo zinasema kuwa kwa sasa Freeman Mbowe anahaha kuhakikisha anapata fedha za kulipa deni hilo ili kunusuru mali anazomiliki.

Taarifa hizo pia zinasema kuwa Halima Mdee alikopa Twiga Bancorp Juni 2011 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Ghorofa mbili ambalo hata hivyo halijafahamika liko wapi. Kwamba, Halima Mdee alikopa shilingi Bilioni 2.3 kwa ajili ya mradi huo deni ambalo mpaka sasa halijalipwa.

Niwasihi tu wale ndugu zangu wakopaji, dawa ya deni ni kulipa. Basi. Kuruka ruka haijawahi kuwa dawa ya kukwepa ulimbo.
Umekuwa jasiri wa kutaja wadiwa sugu wa benki ya Bancorp lakini umekomea kwa watoto wa kambo hao wawili, na vipi wale nyumba kubwa ni wa ngapi na wanadaiwa kiasi gani ili uwe mkweli ??!!.
 
Hii haiwezi kuwa kweli. Sasa hivi Mbowe na Mdee wangekuwa mahakamani kuzuia mali zao zisitaifishwe.
 
[emoji23] [emoji23] walituambia vitaru vya gesi walipewa wachina kwa ajili ya Ridhiwan.
Sasa mtu ana vitalu na bomba LA gesi aligawana pasu kwa pasu na contractor yaani alipata 1 Billion US $ leo hii benki uchwara inamfilisi
 
Hahahaha Mbona Mimi nilishalipa lakini naona jina langu lipo kwa wadaiwa. Shame for those prepared
 
Hahahahahaaaaaaa! Aiseeeeee! Mbowe atajinyonga mwaka huu. Maana deni la NHC hajalipa linaibuka la Twiga! Kweli mwaka wa hasara huu
Dah.. billion 7 kitu gani kwa mwenyekiti bana...[emoji13] [emoji13]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Hawa watu wa ajabu sana. Mkuu una taarifa zozote juu ya lile deni la mwenyekiti?
Mbowe NSSF wakimgusa utasikia wananionea kwasababu ya msimamo wangu kisiasa na nao wanaunga mkono
 
Awali Rais wangu John Pombe Magufuli aliposema kuwa kuna wanasiasa wanaongea sana ilhali ni wadaiwa sugu kwenye mabenki hakika sikuelewa. Ila kadri siku zinavyoenda, inazidi kudhihiri kuwa hakika maneno ya Rais wetu ni kweli kabisa.

Taarifa rasmi nilizonazo ni kwamba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ni miongoni mwa watu waliochangia kufilisika kwa Benki hiyo. Taarifa hizo zinasema kuwa Freeman Mbowe peke yake anadaiwa mkopo wenye thamani ya shilingi bilioni saba hii ikijumuisha mkopo wenyewe na riba. Taarifa hizo zinasema kuwa kwa sasa Freeman Mbowe anahaha kuhakikisha anapata fedha za kulipa deni hilo ili kunusuru mali anazomiliki.

Taarifa hizo pia zinasema kuwa Halima Mdee alikopa Twiga Bancorp Juni 2011 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Ghorofa mbili ambalo hata hivyo halijafahamika liko wapi. Kwamba, Halima Mdee alikopa shilingi Bilioni 2.3 kwa ajili ya mradi huo deni ambalo mpaka sasa halijalipwa.

Niwasihi tu wale ndugu zangu wakopaji, dawa ya deni ni kulipa. Basi. Kuruka ruka haijawahi kuwa dawa ya kukwepa ulimbo.
Hiyo bank ni halali yao kufirisika kama wanamkopesha mtu mmoja 7 billion hawa jielewi!!!!
 
Kila mtu akiandika na kusema 'TAARIFA KAMILI NILIZO NAZO' nadhani michango itakuwa na hukumu zisizo za haki.
Weka ambatanisho la ushahidi wa orodha ya wadaiwa, baraua ya wito wa kulipa deni, or any related evidence.

KADA
 
Wadaiwa sugu benk ya Twiga Bancorp iliyochukuliwa na BoT wanaendelea kuhenya na kuhenyeshwa mitaani, imefahamika. Watu hawalali, watu hawanywi na watu hawali!

Zipo taarifa nyeti kutoka vyanzo vya uhakika kabisa kuwa mjengo wa Ridhiwan ulioko maeneo ya Sinza Mori huenda ukakumbwa na kimbunga kama dhamana juu ya deni analodaiwa kijana huyo na benki hiyo iliyofilisika hivi karibuni.

Hata hivyo thamani halisi ya jengo hilo bado haijajulikana.
Kweli acha na waisome namba ee

CCM ni ile ileeee Chalinze mnasemajee... tumejipangaa mwaka huu tumejipangaa.. tumejipangaa acha waisome nambaaa....!
Huyo fisadi mdogo afilisiwe tu maana hakuna namna nyingine...tumechoka.
 
naona kundi la nyuki waliojaa kwenye kiroba chenye pilipili kichaa limetupwa hapo lumumba

Ahh hacha mzaa wako wewe, nyuki katika ilo gunia lenye pilipili kibiolojia tu lazima watakufa, usithubutu mkuu...
 
Back
Top Bottom