Ridhiwani Kikwete: Asilimia kubwa ya waandishi wa Habari ni makanjanja

Kweli Vyuo Vikuu sasa vimekosa thamani ......................... yaani magraduate wazima wanamwalika Riz kuja kuwahutubia!! Hata kama ni njaa lazima ujali your dignity. Ingawa ni mambo ya kichama but I still insist that was too low for the graduates!!
 
Waandishi ni kama Waalim katika nchi hii wanatukanwa, wanadhalilishwa lakini hatimaye wakiitwa kula ubwabwa na kupewa shilingi kidogo unaona wanapayuka kupamba watu hata wasio na sifa. Acha Riz awatukane maana jioni atawapoza na ubeche halafu kesho wanaanza kumpamba
 

Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia zote kuwa walimu na wanahabari wamekua kama tambara la deki, hutumika kusafisha wanasiasa wachafu lakini baadaye wanakuja kukanyagwa. Walimu na wanahabari wabadilike sasa wakati ni huu.
 
Haya maneno ya huyu mtoto yanamuumbua Pasco na kupenda bahasha za khaki na kuzigawa .Pasco yuko humu humu muumini mzuri wa bahasha ili kuandika ukanjanja .Haya kazi kwenu akina Pasco .

Em jifunze sasa unapo reply with quote post ndefu kama hiyo unaiounguxa, tunachoka kupita kwenye wall story ileile inajirudia wee afu ndefu ati kisa mtu umequote yote, sio maana ya hiyo button kuwepo hapo
 
Huenda anapoona hawanunuliki tena anawageuka, alipowahitaji aliwanyenyekea, na sasa baada ya kupata kile alichokichuchumia hana haja nao na hata zile bahasha za kaki hawapi tena.


2015 siyo mbali, atarudi kwa maknjanja hao hao. Na mbaya zaidi makanjanja kwa njaa zao watampigia magoti. Acha watukanwe tu na IQ zao za kuunga.
 
Riz yupo sahihi kabisa waandishi ni makanjanja asilimia kubwa
Kweli yupo sahihi kuita makanjanja maana yeye mwenyewe ni miongoni mwa watu wanaowatumia wanasiasa kwa masilahi yao yaani kama upo kwenye msafara wake lazima uandike ya kumpamba kwa kuwa amekulipa na ndio maana vyombo vya habari hasa magazeti yanatakiwa wajitegemee kila kitu pindi wanapokwenda kuandika habari ili ku-balance, mfano mzuri waandishi wa magazeti ya mwananchi walikuwa wanafukuzwa kwenye kampeni za JK those days na kulikuwa na mratibu ambae anafanya uhakiki
 

kibaya zaidi ni kwamba waandishi wa habari wanafanywa kama ni toilet paper,yaani ukisha itumia na kumaliza matatizo yako basi huitaki tena na inakuwa haina dhamani tena kwako.
Huu ni ukweli ulivyo na hata wenyewe waandishi wa habari wanalielewa hili na kila siku tumekuwa tukisia wakisemwa vibaya na bado kesho utawakuta wapo na mtu yule yule na wanampamba kweli kweli.mambo kama haya yanawafanya watu kuichezea fani ya uandishi wa habari.
Waandishi wa habari ni watu muhimu sana ktk taifa lolote lile,ni vyema heshima hii kwao ikaendelea kulindwa na kuheshimiwa na hii iendane sambamba na wao wenyewe kujiheshimu,kujidhamini na kuipenda kazi yao na kutoruhusu wachache kuwatumia kwa matakwa ya kisiasa na baada ya mafanikio muhusika huwakana waandishi wa habari na kuwaona si lolote lile.
waandishi wa habari ni wakati wenu sasa wa kubadilika na kuacha kuwa wepesi,mjitahidi sana kuwa mwiba na ikiwezekana mridhike na kile mkipatacho,hii itasaidia sana kupunguza sana kuitwa makanjanja.
Mungu aendelee kuwapa nguvu na moyo wa upendo,lakini chonde chonde msiwe kama mshumaa kuungua huku mkiwamulikia wasio ona nini maana ya mwanga muutoao
 
Ohooo!
Ukweli unauma ,
Lakini Bwana mdogo anata ligi na waandishi makanjanja!
 
Haya maneno ya huyu mtoto yanamuumbua Pasco na kupenda bahasha za khaki na kuzigawa .Pasco yuko humu humu muumini mzuri wa bahasha ili kuandika ukanjanja .Haya kazi kwenu akina Pasco .

Pasco njoo huku njaa yako imeanikwa.
 

kama maslahi ya boss wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…