Ama kweli mla kunde husahau, ila mtupa maganda..... Hivi Ridhiwani hajui kuwa baba yake alibebwa mno na waandishi hadi akafika hapo alipo? Yeye mwenyewe anasafiria umaarufu wa baba yake. Isitoshe mwenyewe Riz anawatumia waandishi kama bazoka, halafu leo anawatukana! Sawa inawezekana waandishi tuna kasoro, lakini Babaako kama Rais amefanya jitihada gani kuwasaidia waandishi? Mbona utawala huu ndio umekuwa wa mateso kwa waandishi na wanaharakati? Wanang'olewa kucha, wanauawa, wananyofolewa macho! Lo! TZ tuna safari ndefu. Basi kama wengi ni makanjanja, wakamateni mkawashitaki. Mbona mnawaacha wakati mna kila madaraka?