Ridhiwani Kikwete: Asilimia kubwa ya waandishi wa Habari ni makanjanja

Ridhiwani Kikwete: Asilimia kubwa ya waandishi wa Habari ni makanjanja

Kajanja mmoja awashambulia wengine kwa ukajanja.
 
Hivi huyu anajua babake anajiita degree holder wa uchumi alipata gpa ya ngapi kule UDSM? Mbona riz huzungumzi kwa nini ulifeli masters degree yako kule YALE ? Kaa kimya mdogo wangu utavuliwa suruali
 
Ama kweli mla kunde husahau, ila mtupa maganda..... Hivi Ridhiwani hajui kuwa baba yake alibebwa mno na waandishi hadi akafika hapo alipo? Yeye mwenyewe anasafiria umaarufu wa baba yake. Isitoshe mwenyewe Riz anawatumia waandishi kama bazoka, halafu leo anawatukana! Sawa inawezekana waandishi tuna kasoro, lakini Babaako kama Rais amefanya jitihada gani kuwasaidia waandishi? Mbona utawala huu ndio umekuwa wa mateso kwa waandishi na wanaharakati? Wanang'olewa kucha, wanauawa, wananyofolewa macho! Lo! TZ tuna safari ndefu. Basi kama wengi ni makanjanja, wakamateni mkawashitaki. Mbona mnawaacha wakati mna kila madaraka?

Ndio tabia ya watu wa pwani ilivo
 
Ridhiwan-Kikwete-June18-2014.jpg

Mbunge wa Chalinze (CCM),Ridhiwani Kikwete

Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amewashambulia wanahabari nchini kuwa asilimia kubwa ni makanjanja na kwamba wanapoandika habari wanasukumwa na weledi wa jinsi wanavyofikiria vichwani na itikadi zao za kisiasa.

Ridhiwani alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa mahafali ya wanafunzi ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vyuo vikuu vya mjini Morogoro yaliyofanyika katika ukumbi wa bwalo la Umwema mjini humo.

“Asilimia kubwa ya waandishi tuliokuwa nao ni makanjanja, ni ukweli kabisa wanapokaa kwenye meza zao wanaandika vitu tu, wanapokaa kwenye ofisi zao wanaandika vitu tu, yaani mtu anapikapika tu vitu,” alisema.

Alisema siyo dhamira yake kuwasema vibaya wanahabari, lakini waandishi wengi hapa nchini wanasukumwa sana na weledi wa siasa zao jinsi wanavyofikiria vichwani mwao na itikadi ya siasa.

Aliongeza kuwa wakati mwingine hata jambo zuri likifanyika hawezi kulisifia badala yake kazi yake kubwa ni kuandika mambo ya ovyo ovyo tu.

“Mimi ningependa sana kuwasihi waandishi wetu hebu kidogo tuandike vitu vinavyofanana na hali halisi, hatusemi kuwa watu wanapofanya mabovu wanyamaziwe, hapana, wabovu waandikwe na mabovu yao, wanapofanya mazuri wasifiwe ili kuendelea kutiana moyo katika kulijenga taifa,” alisema.

Ridhiwani alisema Watanzania jambo kubwa wanalolihitaji ni amani na kwamba wasomi watambue kuwa nchi ipo mahali pazuri sana na amani inazidi kutawala tofauti na inavyoripotiwa na magazeti.

Alisema wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2014/15, mambo yaliyofanywa na wizara hiyo katika kipindi cha 2013/2014 ni mazuri sana, lakini cha ajabu siku moja kabla ya kuanza kwa mjadala wa wizara hiyo, magazeti yaliandika Waziri Muhongo kikaangoni.

“Kikaango hicho kipi, haya ndiyo magazeti tuliyonayo, yanaandika andika tu yaani mpaka wakati mwingine nashindwa kuelewa,” alisema Ridhiwani.

Aliongeza kuwa wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulizuka kelele kwa baadhi ya watu kwamba wanataka waandishi wawe huru, lakini yeye (Ridiwani) akawa anajiuliza moyoni hivi huo muswada wa habari ukipelekwa Bungeni hawatalia?

Wakati Ridhiwani akiwashambulia waandishi wa habari, amekuwa mwanasiasa kijana ambaye kila anakokwenda kwenye shughuli za kisiasa anafuatana na msururu wa waandishi ambao humpamba kwa habari nzuri.

Miongoni mwao, ni kikosi kikubwa cha waandishi alichokuwa nacho wakati wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu.

Katika harakati zake za kisiasa amekuwa akitumia waandishi wa habari kumpamba kwa nia ya kujijenga kisiasa kama ambavyo wamekuwa wakifanya wanasiasa wengi, wakiwamo ambao anawachukulia kama mfano wa kuigwa.

Source: Nipashe

Sasa anawalenga waandishi wa Habari Leo,Jambo leo, na uhuru au wengine?, maana magazeti hayo siku hizi ni mipasho tu na kuandika mambo na naelekezo kutoka lumumba
 
Amewapa za kichwa HABARI LEO, JAMBO LEO, TBC, UHURU,TAZAMA na RADIO UHURU.Hawatakaa wasahau.
 
Ni kweli kawaambia na yeye hawakumbeba bali he spent his own money kuwanunua .So aliwanunua kufanyia ukanjanja akapata ubunge now anawapa kweli when the time comes again he will buy them and life goes on .
 
Ridhiwan-Kikwete-June18-2014.jpg

Mbunge wa Chalinze (CCM),Ridhiwani Kikwete

Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amewashambulia wanahabari nchini kuwa asilimia kubwa ni makanjanja na kwamba wanapoandika habari wanasukumwa na weledi wa jinsi wanavyofikiria vichwani na itikadi zao za kisiasa.

Ridhiwani alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa mahafali ya wanafunzi ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vyuo vikuu vya mjini Morogoro yaliyofanyika katika ukumbi wa bwalo la Umwema mjini humo.

"Asilimia kubwa ya waandishi tuliokuwa nao ni makanjanja, ni ukweli kabisa wanapokaa kwenye meza zao wanaandika vitu tu, wanapokaa kwenye ofisi zao wanaandika vitu tu, yaani mtu anapikapika tu vitu," alisema.

Alisema siyo dhamira yake kuwasema vibaya wanahabari, lakini waandishi wengi hapa nchini wanasukumwa sana na weledi wa siasa zao jinsi wanavyofikiria vichwani mwao na itikadi ya siasa.

Aliongeza kuwa wakati mwingine hata jambo zuri likifanyika hawezi kulisifia badala yake kazi yake kubwa ni kuandika mambo ya ovyo ovyo tu.

"Mimi ningependa sana kuwasihi waandishi wetu hebu kidogo tuandike vitu vinavyofanana na hali halisi, hatusemi kuwa watu wanapofanya mabovu wanyamaziwe, hapana, wabovu waandikwe na mabovu yao, wanapofanya mazuri wasifiwe ili kuendelea kutiana moyo katika kulijenga taifa," alisema.

Ridhiwani alisema Watanzania jambo kubwa wanalolihitaji ni amani na kwamba wasomi watambue kuwa nchi ipo mahali pazuri sana na amani inazidi kutawala tofauti na inavyoripotiwa na magazeti.

Alisema wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2014/15, mambo yaliyofanywa na wizara hiyo katika kipindi cha 2013/2014 ni mazuri sana, lakini cha ajabu siku moja kabla ya kuanza kwa mjadala wa wizara hiyo, magazeti yaliandika Waziri Muhongo kikaangoni.

"Kikaango hicho kipi, haya ndiyo magazeti tuliyonayo, yanaandika andika tu yaani mpaka wakati mwingine nashindwa kuelewa," alisema Ridhiwani.

Aliongeza kuwa wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulizuka kelele kwa baadhi ya watu kwamba wanataka waandishi wawe huru, lakini yeye (Ridiwani) akawa anajiuliza moyoni hivi huo muswada wa habari ukipelekwa Bungeni hawatalia?

Wakati Ridhiwani akiwashambulia waandishi wa habari, amekuwa mwanasiasa kijana ambaye kila anakokwenda kwenye shughuli za kisiasa anafuatana na msururu wa waandishi ambao humpamba kwa habari nzuri.

Miongoni mwao, ni kikosi kikubwa cha waandishi alichokuwa nacho wakati wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu.

Katika harakati zake za kisiasa amekuwa akitumia waandishi wa habari kumpamba kwa nia ya kujijenga kisiasa kama ambavyo wamekuwa wakifanya wanasiasa wengi, wakiwamo ambao anawachukulia kama mfano wa kuigwa.

Source: Nipashe

- Saafi sana balck and white kuna waandishi mimi nawaona hapa mjini kila siku ni aibu tupu, ukikutana nao kazi kuomba hela tu wabadilike huu ni ukweli mtupu tena mimi naweza kuwataja hata kwa majina kazi kuharibu fani ya uandishi hapa mjini, wewe tizama gazeti la Mwananchi yaani CCM haijawahi kufanya zuri hata moja ila Chadema na UKAWA tu kwao ndio wazuri, as if wote ni wajinga waliposhindwa kulinunua gazeti la Jambo Leo kama hayo mengine wakadai Mmiliki wake ni Rdihiwani na wauza unga, tunawajua sana ujumbe kama huu mbadilike sasa!!

Le Mutuz
 
Kipimo cha ukanjanja ni kipi? Riz1 umewatumia kama Shonza na Ccm na kuwabwaga puu kama gunia la mashudu. Kanjanja na porojo ziko Uhuru, tazama, kiu na Gazeti la vita (Jambo Leo)
 
Tulia kijana hii dunia haijasimama inazunguka acha machepele!!!! Unakumbuka yaliyotokea kwa kile kizazi cha SADDAM HUSEIN, GHADAF na wengineo???!!! hata wao walianza hivi hivi na leo jiulize wako wapi??!! sio lazima baba akiwa mwanasiasa na wewe upitie njia hiyo hiyo tena mbaya zaidi kwa ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma hadi jamii yote inastuka!!!!! ingekuwa Tanzania ni nchi ya kifalme at least ungeweza hata kufanya unayofanya ila sio hivyo mkuu!!!! watch out!!!!!
 
- Saafi sana balck and white kuna waandishi mimi nawaona hapa mjini kila siku ni aibu tupu, ukikutana nao kazi kuomba hela tu wabadilike huu ni ukweli mtupu tena mimi naweza kuwataja hata kwa majina kazi kuharibu fani ya uandishi hapa mjini, wewe tizama gazeti la Mwananchi yaani CCM haijawahi kufanya zuri hata moja ila Chadema na UKAWA tu kwao ndio wazuri, as if wote ni wajinga waliposhindwa kulinunua gazeti la Jambo Leo kama hayo mengine wakadai Mmiliki wake ni Rdihiwani na wauza unga, tunawajua sana ujumbe kama huu mbadilike sasa!!

Le Mutuz

Lakini kichwa cha habari kwenye source ya habari hii kutoka gazeti la nipashe ni kwamba huyu Ridhiwan hana shukrani, kwamba anapohitaji waandishi wa habari anawajali na akishatumia anawageuka. Wanasiasa wenyewe wako hivi wanapowahitaji waandishi wa habari huwakimbilia kwa kuwahonga wakiwa mikononi wameshika bahasha za kaki, na wakishafanikiwa malengo yao kupitia migongo ya wanahabari huwageuka na kuwadhihaki. Je kuna ukweli W. J. Malecela?
 
Anayewaponda waandishi mwenyewe ni kanjanja.Nashangaa sana.

Huu ndo ukanjanja wenyewe, elimu ya Riz1 inatosha sana shehe wangu, yeye siyo wa kwanza kuuponda uandishi wa habari wa kitanzania. Nakumbuka Mkapa baada ya kuhojiwa na Khan wa CNN alipokuwa Rais aliwahi kusema hayahaya na leo say baada ya miaka 14 or so, bado ukanjanja upo. Waandishi na taasisi zenu MJISAHIHISHE.
 
Amesema ukweli lkn hatutaki kukubali. Asilimia kubwa ya habari za kuvutia huwa za kupikwa.
 
Ni kweli ni makanjanja ila asisahau pia nchi pia inaongozwa na rais kanjanja kuwahi kutokea na mtoto wa kanjanja ni kanjanja pia.
 
Atuambie kwanza kama ameacha kusafirisha madawa ya kulevya. Vinginevyo naye ni kanjanja nguli.
ndo jambo la msingi wakiambiwa ukweli wanaona waandishi wa habari hawafai ni ujinga wa kifikra huo
 
Waandishi walioenda kwenye huu mkutano nao ni makanjanja pia.. si ndio? Kuna mambo ya maana kureport kuliko haya ya RIZ1
 
Ridhiwani alisema Watanzania jambo kubwa wanalolihitaji ni amani na kwamba wasomi watambue kuwa nchi ipo mahali pazuri sana na amani inazidi kutawala tofauti na inavyoripotiwa na magazeti.

Hiyo amani wakati umaskini unaongozeka.......iko siku itatoweka tu...
 
Back
Top Bottom