Ridhiwani Kikwete yuko live, anaongea kama Jakaya Kikwete. Like father like son, atatufaa sana in future baada ya zamu yetu!

Ridhiwani Kikwete yuko live, anaongea kama Jakaya Kikwete. Like father like son, atatufaa sana in future baada ya zamu yetu!

Naunga mkono hoja, kila mwenye merits, asimame na merits zake na sio kwa jina la mzazi wake, Kabila lake, dini yake, au

P
Yes mkuu. Alafu kama suala ni pedigree ya mtu au ukubwa kwa jina la mzazi wake, mbona January Makamba alikatwa jina akapitishwa baba Levo mtoto wa masikini??

Ridhiwani, January, Baba Levo, Mwana FA au mtanzania yeyote mwenye sifa ya kuwa kiongozi na apewe nafasi.
 
Ukweli ni huo mkuu, ukiachana na hilo ukiwa na maisha ya chuki na kuangalia mabaya au kutafuta mabaya ya watu kila jambo utaishia kuona tatizo
That's for sure mkuu. Mimi ninatoka katika familia ya kimasikini sana lakini ninamtambua fika umasikini wangu hautokani na watu wa oyster bay, Masaki, Ununio au Mbezi beach.

Suala la matabaka ya kiuchumi lipo mpaka Marekani, China na Russia ndio maana October 2025 sikwenda kufanya vurugu kama Mange Kimambi alivyotaka.

Tuwachukie watu wa tabia zao binafsi na sio kwa hali zao za kiuchumi.
 
Yes mkuu. Alafu kama suala ni pedigree ya mtu au kubwa kwa jina la mzazi wake, mbona January Makamba alikatwa jina akapitishwa baba Levo mtoto wa masikini??

Ridhiwani, January, Baba Levo, Mwana FA au mtanzania yeyote mwenye sifa na kuwa kiongozi na apewe.
Naunga mkono hoja, japo siungi mkono yale mambo ya kule kukatana majina kwa figisu, kama CCM ilivyowakata hawa, kina January na yule mapingili. GE2025 - Masikini Nchi Yangu, Tanzania, Tunakosa Viongozi Wazuri kwa Dhulma!. Waliokatwa kwa Zengwe, Wangegombea as Independent, Wangeshinda!. angalau mapingili kakumbukwa, January bado!.

Pia siungi mkono mtu hana sifa ila ni mambo ya kubebaba, kile kilichotokea Kigoma kuteuliwa kwa Baba Levo, mwanzo nilikupinga kuwaacha very good fine men na kulipitisha lichawa pro max, ila nilipo msikia Baba Levo akichangia Bungeni, nikamkubali mwenyewe Japo Nilikuwa Simkubali Baba Levo Kwa Uchawa Compared to ZZK, Leo Nimemsikia Bungeni, Kumbe ni Bonge la Kichwa, ni Akili Kubwa!, Nimememkubali Sana!.

P
 
Mkuu Manjaga, kama baba alikuwa kiongozi mzuri aliyependwa na watu, kisha mtoto wake akafanana copy right na baba yake, then it's likely akiwa rais na yeye atakuwa rais mzuri.

Kama mtoto wa rais ana sifa za urais, na ana kidhi vingezo, kwanini asiwe?.

Hakuna Mtanzania yeyote mwenye sifa na vigezo vya kugombea urais, hata wewe kama unavyo gombea tuu tutakuchagua wewe Manjaga ndio uwe rais wetu, jitokeze tuu, lakini hatuwezi kuacha kumchagua mtu mzuri mwenye uwezo mzuri, na sifa nzuri, eti tu kwasababu baba yake tayari aliisha kuwa rais!, kuna vitu ili uwe, sio sifa tuu vigezo na uwezo!, vitu vingine ni nyota!
P
Wewe Ng'wanangwa hebu niambie ni lini Kikwete alikuwa Rais mzuri? Rais legelege ndiyo uzuri huo? Kuna tofauti gani na hizi takataka sasa hivi?
 
Unapata wapi muda wa kujipinda na kuandika haya matakataka?
Unalipwa?
Bado unautaka uteuzi?
Usomi alama za nyakati?
Ccm haina miaka 10 mbele, kataa kubali ni jambo la mda tu, watatumia kila njia
 
Wanabodi,

Kwanza watch TBC Live Mubashara
View: https://www.youtube.com/watch?v=wMOElr9lFGI

Japo enzi za Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sisi humu JF, tulimpiga spana za kutosha zikiwemo spana zangu, za kumkosoa JK, Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

Pia JK, alikuwa na mazuri yake pia tulimpongeza Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour" haya mazuri ya Kikwete pia Ridhiwani Kikwete anayo!, ni mtu rahimu sana, cool, humble na down to earth!, japo ni mtoto wa rais, sio mtu wa kujimwambafy kama nanii!. Mungu ambariki sana!.

Siku Jakaya anaaga alisema tutamkumbuka, kiukweli aliyefuatia, tulimkumbuka JK! Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma na kuna watu wa JK walishughulikiwa Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete Anajisikiaje?!. Anajisikia Sifa Au Anajuta?!. pia niliwahi kuuliza, Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete?!

Hakuna Tanzania nzuri kwa uhuru wa vyombo vya habari uhuru wa kujieleza kama Tanzania ya JK!, ni kipindi hiki PPR ndio ilizaliwa, na kuneemeka!. Media tulikuwa huru hadi kumpiga biti rais wa JMT, enzi za JK Ushauri wa bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya October 25!, just imagine media tulivyokuwa huru!, leo lile tukio la October 29, watu 518 wamethibitishwa kufa, kuna media yoyote inaweza kujitokeza hata kuuliza tuu, aliyetoa amri ile ni nani?, ukiondoa JF kuulizia hoja kaa hii PostGE2025 - Voices from Within: Mauaji ya wananchi Dar, tusiwalaumu Polisi. Je Amri ya kuua Ilitoka kwa muuaji huyu? kuna media yoyote imeweza kukohoa na kufanya IJ yoyote ya kilichotokea au hata kumwambia Rais Samia ili angalau kuonyesha ameguswa, awaombe radhi Watanzania kwa kilichotokea, awafariji waliofiwa kwa mauaji ya makosa kama wale watoto wadogo au wale wa kibanda umiza kule Mwanza?, enzi za Kikwete, hili lingewezekana, tungemshuhudia JK akitembelea majeruhi Muhimbili, JK angewaomba wasaidizi wake watatu, CDF, IGP na DGIS, wakae pembeni kupisha uchunguzi, hivyo ikitokea akaja Ridhiwani, enzi za uhuru huu wa habari na uhuru wa kujieleza, zitarudi kama enzi za Jakaya, na tukio kama la October, lisingeweza kutokea!, na labda hata PPR chini Pasco Jnr pia itafufuka!.

Sasa leo nIkImuangalia Ridhiwani Kikwete live mubashara, kupitia TBC Ridhiwani Kikwete , nimegundua Jakaya Kikwete hapa alijizaa!, Jamaa ni copy right like father like son!, wanafanana mpaka sauti na jinsi anavyoongea, ni kama Jakaya, na vile vineno vya JK hadi raha kumsikiliza!, kitu kikubwa kumhusu Ridhiwani, ana karama ya uongozi, ana kipawa cha uongozi na ana uwezo wa uongozi kama baba yake!, ama kweli mwana wa nyoka ni nyoka!.

Kufuatia Abedi Karume Amani Karume, Ali Hassan Mwinyi, Dr Hussein Mwinyi, then in future huyu Ridhiwani Kikwete atatufaa sana latika lile jambo letu baada ya kukamilika, kwa zamu yetu kwenye lile jambo letu, ili pia tuje kumpata Jakaya Kikwete Ridhiwani Kikwete!
View attachment 3599484
Hii sio marayangu ya kwanza, kuwanenea watu huwa, wawe na wakawa,
Japo mimi Pasco Mayalla nimeisha mfanyia endorsement yangu huyu kijana kwa kushauri awamu ijayo apelekwe MFA kumpatia an international exposure, mimi ni nobody, na ninachofanya hapa ni ku proposes tuu, anayeamua nani awe, sio mimi, sio wewe wala sio yeye, ni YEYE!, kama huyu yeye ameandikiwa na YEYE, kuwa siku moja atakuwa, then no one can do anything kuzuia asiwe!.

Mungu Mbariki Ridhiwani Kikwete

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali

In reference ya WALAKA WA MWITONGO ni kweli
 
Back
Top Bottom