Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 8,939
- 10,403
Kijana kwa nini ukubali kukaa nyuma ya mtu??Kutokana na uzalendo, uadilifu, unyenyekevu, ucha Mungu na mapenzi yake kwa Watanzania basi mtoto huyu wa Rais anafaa kuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano.
Rais Samia naomba mkumbuke hata kwa kumpa uwaziri wa michezo kwani kijana huyu anauwezo mkubwa wa kuongoza.
Imewezekana vipi kwa Huseni Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar na Ridhwani asiwe Rais wa JMT?
Nakushauri Kaka yangu Ridhwani usibaki nyuma, ukifika muda wa kuchukua fomu nenda kachukue.Usiogope, huna mambo mengi. Wewe sio kama vihelehele akina Polepole ingawa baba yako alikuwa Rais wa nchi hii.
Vijana wote tuko nyuma yako,
wewe ni muadilifu kama baba
yako Jakaya Kikwete.
Kachukue akili zako, tafadhali!!