RIHANNA: Sipo tayari kuwa single mother hata kama najitosheleza kulea mwenyewe

RIHANNA: Sipo tayari kuwa single mother hata kama najitosheleza kulea mwenyewe

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Haya ni maneno aliyoongea billionea Rihanna kwenye moja ya interview zake ambayo ilizua hisia tofauti tofauti miongoni mwa mashabiki zake.

" Sitaweza kuachana na mme wangu hata kama akinichiti kwa sababu wanangu wanamuhitaji baba yao na pia hata mimi nahitaji niwe na familia iliyotimia."

"Nilipofunga ndoa na kupata watoto, sitaki kabisa kuwa na talaka kwa sababu sifikiri kama niko tayari kuwa single mother. Napendelea familia kamili hata kama najua naweza kujitosheleza na kulea wanangu kama nikitaka lakini, hicho sicho ninacho kitamani wala kukitaka.

Wanangu daima watamuhitaji baba yao, watahitaji uwepo wake. Na kuwa single parent hii sio utamaduni wa watu weusi na mimi ni mwanamke mweusi niliyekuzwa kwa misingi ya kuthamini thamani ya watu weusi."- Rihanna🗣️

20240909_093906.jpg
 
Hakuna mwanamke anayependa kulea mtoto/watoto peke yake. Kuna vitu vinatokea, viko nje ya uwezo wa mtu. Kuna mwanaume anaondoka anaenda kuoa mwingine, utamfata? Kuna kufa, kuna kutokuelewana kabisa kimtazamo, baada ya kupata watoto. Tuombe uzima, muda ni msema kweli.
 
Kila single mother niliyekutana nae lazima awe na sababu niliyoiona kwamba hata ningekua mimi ningeachana nae tu.

Single mother wana shida fulani ya kisaikolojia, wana tabia ngumu sana zisizovumilika, jaribu kujenga ukaribu hata na single mother mmoja utajua hujui.
Hii vita za kuwashambulia hawa ndugu zetu ni muhimu sana kuwarekebisha baadhi ya madhaifu makubwa waliyonayo ili wakae sawa kidogo
 
Hakuna mwanamke anayependa kulea mtoto/watoto peke yake. Kuna vitu vinatokea, viko nje ya uwezo wa mtu. Kuna mwanaume anaondoka anaenda kuoa mwingine, utamfata? Kuna kufa, kuna kutokuelewana kabisa kimtazamo, baada ya kupata watoto. Tuombe uzima, muda ni msema kweli.
Single mother ujuaji mwingi, full kiburi na kupenda mashindano katka mahusiano. Hakuna mwanaume anayeweza kuacha mke anayempenda na kumheshimu.
 
Kwani waliokuwa single mothers walikuwa tayari?

Yeye aombee bwana ake asimuache tu kwasababu akiamua kumuacha hakuna kitu atafanya
Nimekutana na sampuli zile za “nipe mtoto tu nitalea mwenyewe”
And hiyo rate inazidi kuongezeka.

But then si wote wanaotaka, kuna case inatokea so yah but mambo si mazuri kwa ground
 
Back
Top Bottom