Ripoti Kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Ripoti Kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Najitahidi kuanzisha threads zenye kuleta sehemu muhimu za kuangalia ambapo CAG amebaini upigaji mkubwa.
Mkuu kwanza nashukuru kwa jitihada kubwa ya kutuletea habari na taarifa muhimu kwa ajili ya mustakabali mzima wa uhimilivu na uendelevu wa nchi yetu. Kula gwala
 
200
kwa kuainisha kiwango cha malipo ya posho la hitimisho la kazi."
Tusisahau kuwa Katiba inayoainisha mipaka ya spika, cag na wengine ndiyo hiyo hiyo iliyompa rais mamlaka makubwa ya kifalme. Kwa nini asitumikishe mali ya taifa kifalme?
199 na 2015 tayari kulikuwa na upinzani!..... kwenye maslahi yao binafsi jamaa wote kwa pamoja huwa jambo moja kutunga sheria legelege.
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji851] Nchi ina vituko, si tulisema akisaini Prof. Assad hatupokei au? Jamani kwani kiswahili kigumu sana au? [emoji86][emoji86][emoji86][emoji86] LMFAO...!! haaa
Mkuu lakini si ni wana-ccm wenzako waliotoa hilo azimio?
 
Miongoni mwa mapendekezo ya kaguzi zilizopita ambayo hayakutekelezwa ni: Benki ya Azania kutokuwa chini ya usimamizi wa Msajili wa Hazina, Wizara ya Nishati kutokulipa deni la pango la Sh. bilioni 1.12 kwa Kampuni ya Umeme Tanzania (TANESCO), kukosekana kwa mkataba na dhamana kwa mkopo wa Sh. bilioni 44.29 uliotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF); Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania kuchelewa kuanzisha mradi wa utafutaji wa gesi katika vitalu 4/1B na 4/1C, Sheria kutompa mamlaka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kukagua Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Mwanza (MWAUWASA) kuchelewa kukamilisha Mradi wa maji wa Sh. bilioni 6.66.


Hii sekta ina nini hadi isikaguliwe?
 
Kwa hili la CAG siwaungi mkono ng'ooooo... Mm sio CCM wa NDIOOOOOO, jua hilo vizuri kabisa, am an intellectual..!! Uliwahi sikia wapi Bunge likatae kufanya kazi na CAG? Na iko kikatiba..!! Hapa natofautiana na bunge na CCM yeyote yule..!!
Hongera kwa hilo kama kweli limetoka rohoni
 
Du!! Imejaa madudu usipime. Ngoja nikapige kazi, ccm ni ile ile, hata hivyo unategemea kibajaji na msukuma wabadili hali ya matumizi ya nchi?
 
View attachment 1067472
View attachment 1067459

Wakuu,

Mnaweza kuipakua ripoti kamili hapa:


Lakini, endapo tovuti itakuwa na shida basi naambatanisha hapa mafaili yote

NB: Ripoti imesainiwa na Prof. Assad

Kwa ufupi...

BUNGENI Ofisi ya CAG imetisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma. Inatarajiwa kuwa CAG, Prof. Mussa Assad, atawaeleza waandishi wa habari kuhusu mukhtasari wa kile kilichomo kwenye ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2017/18.

Miaka iliyopita, CAG alikuwa anatoa mukhtasari huo kwa waandishi wa habari bungeni mara tu baada ya ripoti yake kuwasilishwa kwenye chombo hicho.
Bunge limeshaazimia kutofanya kazi na Prof. Assad, hivyo ni wazi kwamba hawezi kuzungumza na waandishi wa habari bungeni.

=> CAG assad: Tumezoa kufanya mkutano huu mara tu baada ya ripoti hii kuwasilishwa.

=> CAG assad: Mimi nimetazama kwa TV ripoti imewasilishwa bungeni na 'order paper' (karatasi yenye orodha ya shughuli za kikao cha Bunge) ninayo hapa inaonyesha ripoti imekabidhiwa bungeni leo asubuhi na nimetazama ikiwasilishwa.

=> Prof Assad: Mwaka huu tumetoa ripoti yetu kwa CD ili kuepuka gharama nyingi za uchapishaji.

=> Prof Assad: Mapendekezo yetu tuliyotoa katika ripoti iliyopita yalikuwa 350 lakini ni 80 tu yaliyotekelezwa kikamilifu.

=> Prof Assad: Serikali kuu kulikuwa na mapendekezo 91, mawili tu ndiyo yametekelezwa kikamilifu.

=> Prof Assad: Halmashauri za Kigoma Ujiji na Nyng'wale zimepata hati zisizoridhisha na hati mbaya katika mwaka wa fedha 2017/18.

=> CAG Assad: Tumebaini kuwapo kwa malipo hewa ya mabilioni ya shilingi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

=> Prof Assad: Pia tumebaini Wilaya ya Hanang' haikuwasilisha vitabu vya fedha na kuna upotevu wa mapato ya Sh. bilioni 1.4 na walilipa fedha kwa wakandarasi kwa kazi ya dharura pasipo kuwapo kwa kazi ya dharura.

=> Prof Assad: NEC ilinunua BVR 8,000 lakini mashine 5,000 kati ya hizo zilikuwa haziendani na mfumo uliotakiwa hivyo kuisababisha serikali hasara ya mamilioni ya shilingi.

=> Prof Assad: Kuna mafunzo kwa maofisa wa NEC hayakufanyika licha ya mzabuni kulipwa.

=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lililipa Sh. bilioni 16 kwa ajili ya ununuzi wa sare za polisi bila kuwapo kwa ushahidi wa ununuzi.


=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lilipa Sh. milioni 600 kwa ajili ya mafunzo ambayo hayakufanyika.

=> CAG Assad: Tumebaini Chadema ilinunua gari jipya aina ya Nisan Patrol kwa Sh milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini.

=> CAG Assad: Tumebaini CCM haijawasilisha NSSF makato ya Sh. bilioni 3.74 ya wanachama wake.

=> CAG Assad: Majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya Bodi ya Wadhamini.

=> CAG Assad: Kuna miradi 27 serikali za mitaa imekamilika lakini haitumiki licha ya kugharimu mabilioni ya shilingi.

=> Prof Assad: Tumebaini mashirika 14 yana matatizo makubwa ya kifedha na yanaendelea kutengeneza madeni makubwa.

=> CAG Assad: Tumebaini mradi wa umeme wa REA umetekelezwa kwa asilimia 36 tu ndani ya miaka mitano.

=> CAG Assad: Tunaishukuru Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge kwa kutusaidia kukamilisha ripoti hii.

=> Prof Assad: Deni la Taifa limeongezeka lakini bado ni himilivu.

=> Prof Assad: Tumewaalika wenyeviti wa kamati za Bunge (PAC na LAAC) lakini hawajaja hapa. Tutawapatia nakala hizi.

=> Prof Assad: Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma.

=> CAG: Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia.

=> Prof Assad: Kampuni ya Uhuru Publications haina mfumo mzuri wa udhibiti wa fedha.
Wale wenye kusubiri MATUKIO ili waseme basi tukio ni hilo hapo. Someni hiyo ripoti, tafute na zusheni ubovu na kisha muusemee kwa nia na lengo la kuichafua serikali hii. Nasema hivyo kwani siku hizi HAWANA HOJA tena bali wanagoja MATUKIO ili wapate cha kusema kwani vile vihoja vyao walivyoviona in the 3rd and 4th phase governments vimevyekeelwa mbali na kutekelezwa na hili LI AWAMU LA TANO! Hongera sana Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kuongoza na kuisimamia serikali hii ya Awamu ya Tano. Keep it up.
 
Back
Top Bottom