Ripoti Maalum: Kutajwa kwa Vyombo vya Usalama na Wengine kwenye Madawa ya Kulevya ni Mtego kwa JK

Status
Not open for further replies.
Nampongeza kidogo kwa ujasiri wake, lakini bado namdai zaidi. Mkuu mfano ulinikopesha Shs1000,000 nimekurudishia 400,000, je hizo 600,000 utasema basi?
kumbe jamaa ni muungwana kakulipa japo hiyo laki nne kuliko wale waliokudhurumu,sasa watafute na hao ambao hajakulipa hata mia ili ukiunganisha na hiyo 400,000 uwe umepata kitu kamili.
 
Serikari dhaifu sana hii,ni aibu kwa tz kusema tuna rais, ni kama tunajiongoza wenyewe vile,bila mkuu wa kaya.
 
Hujawahi kusikia ule usemi unaotumiwa na wafanyabiashara "Ukitaka biashara yako iende vizuri nchi hii jiunge na CCM"
Wakikuona we mfanyabiashara mkubwa watakufatilia uchangie chama ukikataa inakula kwako.





Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ninachojiuliza ni hii hali inatokana na chutzpah, brazenness au utter stupidity? Unabebaje kilo 150 za madawa au ingedients zake na kuzipakia kwenye scheduled flights! Unamchukuaje mtu asiye na uzoefu ambae hali yake ishakuwa taabani na kumpeleka mahali ambapo lazima atashtukiwa tu! Ni kama vile walitaka wakamatwe au waliamini kote huko wameshika nchi! Hii nayo ni ngumu kuamini maana mtu yeyote makini kidogo anajua kuwa watanzania tunachunguzwa tangu tunapoingia kwenye ndege hadi tunaposhuka! Unakula? Unakunywa? Unaenda chooni? Na kadhalika. Na hakuna mfanyabiashara makini atakaetosa kilo 150 za crystal meth ili amshikishe adabu binti wakati kilo 1 ingetosha!

Inaelekea biashara hii imekuwa so pervasive kiasi kuwa hata majuha wamejiingiza. Au wahusika wameanza kutumia bidhaa zao kiasi kuwa zinawaathiri. Au wenyewe kwa wenyewe wanachomeana. Kwa vyovyote vile, hii hali inatisha maana hatua iliyobaki ni kugeuza nchi yetu kuwa uwanja wa kina Zeta, Crips n.k.

Mwenyezi Mungu atunusuru.

Amandla.....
 
Huu ni upande mmoja wa shilingi, upande wapili ni pale kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya kilipowatuma askari wake kwenda Afrika kusini kuwahoji hao mabinti.

Kwa akili za kawaida kabisa zisizohitaji certificate ya VETA mahali pa kuanzia ilikuwa uwanja wa ndege Dar.

Mzigo mzito kama huo uwe katika mafungu au gunia uliwezaje kupita hapo uwanjani?
Kuna sababu ya kuwa na mashine za kucheki mizigo au wale polisi wa kupapasa hadi nyeti za watu? Hivi kama ni bomu si ndege ingeteketea bila kuonekanahata kipande. Sasa security gani tuliyo nayo?

Ilibidi kwanza hao wa uwanja wa ndege wote na viongozi wao wahojiwe kikamilifu.
Sidhani kuwa vile vibinti vilikuwa na nguvu ya ushawishi kiasi hicho hata kama vingetumia maungo yao ya kibailojia bado kungekuwa na mtu wa kusema mh mh! hapana!

Nilitegemea viongozi wa uwanja wa ndege wawe nje ya kazi ili kutoingilia uchunguzi, eti wanakwenda kuhoji vi miss na kuacha magurumembe yakiendelea na kazi JNIA

Hivyo vibinti pengine havimjui Lord vina deal na go betweens ambaye keshatimka sasa watampata wapi mhusika.

Hii ni moja ya security breach ya hali ya juu sana nilitegemea uongozi wa nchi ungekuwa on top, lakini kimyaa wamemwachia Nzowa. Hili si suala la madawa ni suala la usalama, kwamba uwanja wa ndege unaweza kuingiza na kutoa kitu chochote hatari bila serikali kushtuka.

Pinda aliwahi kusema mafisadi ni watu hatari sana kwa usalama wa nchi, sijui na hawa madawa wanaingia kundi gani 'hatari sana saaana' au ni wajasirimali waachwe tu maana ni upepeo utapita.
 
Hakuna cha kufunika kombe, mambo yanaratibiwa kutoka Vatican na nimekubandikia hapo juu ukajisomee mwenyewe zaidi. Haya mambo si madogo na mnayajuwa hayo. Kama ni wenye kufikiri.

Jadili mada ya Mwanakijiji usitutoe kwenye mada with your religiousy bigotry, unless of course kama watuhumiwa wa hii biashara wanatmumwa na Vatican!
 
Jadili mada ya Mwanakijiji usitutoe kwenye mada with your religiousy bigotry, unless of course kama watuhumiwa wa hii biashara wanatmumwa na Vatican!

Sasa kanisa linatumwa na nani na ikiwa Vatikan ndio mwanzo wa hayo madudu, umepitia link lakini? au unataka kubisha kwa ushabiki tu? au umeshindwa kupitia link lugha ya watu inakupiga chenga?
 
Sasa kanisa linatumwa na nani na ikiwa Vatikan ndio mwanzo wa hayo madudu, umepitia link lakini? au unataka kubisha kwa ushabiki tu? au umeshindwa kupitia link lugha ya watu inakupiga chenga?
Lugha ya kikristo ni ngumu siyo ya kukaririshwa kama ile nyingine Mkuu
 
Madawa ya kulevya hayana chama wala itikadi za kisiasa, wavuta na wauza unga wapo kotekote.

Na wanao na Ndugu zako waanze kutumia ili upate akili ya kujua nani upambane nae... Viongozi wa serikali ya CCM wanaojihusisha na Madawa ya kulevya tayari wameniharibia ndugu zangu... wewe watetee ila ulipwe kwa jinsi unavyofikiria....
 
Sasa kanisa linatumwa na nani na ikiwa Vatikan ndio mwanzo wa hayo madudu, umepitia link lakini? au unataka kubisha kwa ushabiki tu? au umeshindwa kupitia link lugha ya watu inakupiga chenga?


Kwa huu udini wako .... watoto wako wote wataoa au kuolewa na wakristo.....
 
Hakuna cha kufunika kombe, mambo yanaratibiwa kutoka Vatican na nimekubandikia hapo juu ukajisomee mwenyewe zaidi. Haya mambo si madogo na mnayajuwa hayo. Kama ni wenye kufikiri.

Naona Vatican ni shida kwako!kwenye link zako hao maaskofu ulioweka sijaona katoliki babda ni nimeona vibaya nitafurahi ukiendelea leta ushaidi zaidi kwenye hilo ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe!
 
Nimegonga tu lakini lakini sijafahamu chochote, maana kwangu kidhungu ni kidhungudhungu tu
 

Hapo uwanja wa Nyerere hakuna kaupenyo ka wakubwa kupita bila kukaguliwa!!! Nahisi hako ndo kazuri kwa wajamaa kupitishia.
 
Mnachagua rais anaeshinda kwenye vijiwe vya gahawa na mkimbiza sketi kisha mnatarajia awe mwarobaini wa matatizo yenu,mna muda mwing sana wa kusubiri na mtasubiri sana.
 
Hayo ni mawazo yako na Tanzania kuna uhuru wa maoni wakati huu wa Kikwete.

Kwa vile umejua kuchangia 2011 ndiyo unafikiri forum hii ndiyo ya kwanza??

Kwa taarifa tu members wengi wa zamani walikuwa ni members wa BCS toka 2003. Wakati huo Mzee Mwanakijiji akijulikana kama Mwanakijiji na Ze Mutuz / Sauti ya umeme akijulikana kama ES. Marehemu Nyaulawa kwa ambitions zake za kisiasa akaamua kuiua. Sasa hii ya kitu ya uhuru wa maoni wakati wa JK ni uongo uliozidi mipaka. Tatizo lako furum yako ya kwanza ni JF .............. inaelekea hata hujui kuwa ilikuwa inaitwa Jambo Forums before. Na kama ni kweli kuna uhuru wa kuchangia wakati huu wa JK waulize wadau kwa nini jina la Jambo forums lilibadilika baada ya mtandao kuzimika kwa kama wiki na na misukosuko ambayo akina Invisible na Mello waliipata!!

By the way, kama kuna uhuru wa kuchangia kwa nini zaidi ya 99 % ya members hawatumii majina yao ............ including wewe mwenyewe na vijana wa Lumumba!!??
 
huyo CHONJI wamekosea jina lake maarufu pale mwembechai ni CHONCHI,huyu mshikaji namjua tokea nakaa mwembechei(ofcourrse mi mzaliwa wa pale)miaka ya katikati ya tisini,kitambo kile sisi wadogo(teenagers0huyu jamaa alianza kama small time dealer,big time cocaine hustlers walikuwa ni SALUM KAJONA NA ASLI NETI a.k.a BABU NETI,maskani ya chonchi ilikuwa ni GEBI(mitaa ya mwembechai pia),alikuwa amechoka anavaa kipensi daily,hawa wakina kajona walikuwa wanampa "mabusta" yenye kete kama mia mia hivi anauza locally,badae wakina kajona wakaanza kumtuma,nchi zao maarufu za kuchukulia bwimbwi enzi zile ni upakani(pakistan),ubatani(turkey)na kwa pilato(italy)
by the time nahama home mwembechai mshikaji hakuwa DON kama nilivyostuka kuona jina lake ni among big tyme cocaine hustlers.
 
Sasa kanisa linatumwa na nani na ikiwa Vatikan ndio mwanzo wa hayo madudu, umepitia link lakini? au unataka kubisha kwa ushabiki tu? au umeshindwa kupitia link lugha ya watu inakupiga chenga?
suala kubwa hapa ni kuwa Watanzania wanaangamizwa na haya madawa lakini juhudi zikianza kama hivi mara wengine mnaibuka na mambo ya dini, makabila, vyama nk.
Vatican wanaweza wakawa wameliona hilo na wanaliongelea kutoka ndani mwao lakini usisahau kuwa hata Saudia kuna adhabu ya kifo kwa dealers ikiwa ni ushahidi kuwa hii kitu haitakiwi huko. Pia usisahau kuwa kuna mtu mmoja prominent aliwahi kufia hoteli moja kubwa hapo Dar es Salaam nafikiri wakati wa awamu ya pili ambapo ilisemekana kisa cha mauti ilikuwa madawa na hakutokea Vatican bali kwenye nchi unazotaka 'kuzitetea'.
Acha kuondoa wachangiaji kwenye hoja ya msingi ambapo ukweli ni kuwa serikali imeshindwa kupambana na wauza madawa kwa maana huenda wameiweka mfukoni au watu wa serikali wenyewe ndio dealers pia kama mleta hoja anavyoainisha.

 
Na pia namsubiria sana Philip Marmo naye aongee kuhusu wafungwa kule Hong Kong pamoja na Watanzania walionyongwa kule China...........

Aongee nini kupoteza wakati? hao wamebeba unga wamejitakia wenyewe wamenyongwa, wamefungwa kazi kwao.

Waambieni wale wanaharakati wenu wanaojidai kutetea upuuzi kama wa Ulimboka waende wakawatee, mnangoja nini?

Hivi Ulimboka yuko wapi? Kiranga Komo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…