Mzee Mwanakijiji amesahau kuna mtoto wa kigogo mmoja alinusurika kunyongwa kule China na hadi leo hajakanusha kuhusiana na yeye kunusurika kunyongwa kwa kukamatwa na sembe kule China.Umeichambua vizuri hiyo barua lakini ulipoingiza mambo ya CHADEMA na CCM uchambuzi wako umekosa nguvu, kama suala la polisi kuwasumbua vyama vya siasa hawajaanza leo mbona haujawasema CUF wewe na CHADEMA tu.
Mkuu mimi muuza kahawa tu wala sina kazi zaidi ya hiyo.
Kwanini kanisa lifungwe?msikiti wa Ponda umefungwa?Na yule mchungaji aliyeshikwa umesahau? List iliyo kuwepo kanisa ndani. Si kasheshe hiyo? Ulitakiwa afunge makanisa?
Mkuu hii ni issue humu mitandaoni,lakini mtaani ni kawaida kabisa.Nenda hapo Dar,ukiwaulizia hao mazungu unatajiwa wote.Kila mtu anawafahamu.Wasiowafahamu watakuwa wanasikia tu majina yao,lakini wakiulizia wataambia ni mazungu......whaaat!!! eti!
kuna jamaa mmoja........kwenye pita pita zangu za hapa na pale aliniambia kuwa Tanzania ni sehemu moja nzuri sana ya "kusafisha pesa".......Sasa nikiunganisha na haya matukio.........naelewa......
Whats your point? Serikali iliyopo madarakani ni jukumu lake kuchukua hatua kama imeshindwa ijiuzulu.
Umepotea, wanaobugia ni victim wa wauzaji. na katika wauzaji wako wale wakubwa wanaofadhili usafirishaji na kuwapa wale wanaofanya biashara ya rejareja. Kama ukitaka kushinda vita hii upigani na victim bali na wauzaji...
Ni kama yana DINI vile ukiangalia wanaotajwa sana na NCHI wanakokamatiwa kwa wingi.
Any way, kama ni kutajwa kwa uhalifu wowote ule nchi hii, huwa tunaishia hapo tu, kutajana, basi. Ntatoa mifano michache:
-Dr Slaa na ile "list of shame" pale MwembeYanga. Waliotajwa ni wazito kabisa nchi hii. Hawashtakiki;
-Lowasa na wengine waliotajwa Richmond. Ndio kwanza wanajiandaa kukamata DOLA come 2015, God willing or not;
-Wameuwawa watu hapa Tanzania hadharani, tena kwenye mikutano. Wametajwa watu hapa na pale. Wengine wamepandishwa vyeo, wengine wamevishwa nishani za UTUMISHI ULIOTUKUKA!
Hii ndio TANZANIA baada ya Mwalimu.
Miss Foxy please don't insult our intelligence!Ulitaka wafunge makanisa? Hususan la Katoliki? soma hapa:
"The Vatican Connection With the Mafia" by Richard Hammer, where the existence of a Sacred Mafia is proven without a doubt, and where the names of papal cardinals and delegates, which have been caught in the traffic of Money laundering, drug trafficking, and the unlawful sales of armaments, and who surround the pope and mock the law with their Vatican passports, are mentioned. Diplomats, Nuncios, Papal Delegates, Cardinals, Primates, Archbishops etc. ... Gordan Thomas' and Max Morgan Witt's book "PONTIF," of 543 pages, where those who form part of the Vatican's Sacred Mafia are described with extravagant details, along with their different Vatican's Organism.
Source: http://www.bibliotecapleyades.net/vatican/vatican_mafia01.htm
Ndio umechangia nini hapa?
mwanakijiji umesahau na majina ya viongozi wa kiroho
Mimi sidhani tatizo letu hapa ni JK, CCM au serikali. Huu si uchafu mdogo ni uchafu unaohitaji tuunganishe vichwa bila kujali itikadi tutengeneze vita na mikakati ya kuendesha mapambano dhidi ya majanga haya. JK alilivalia njuga lakini kaona hana ubavu nalo na hata akija nani hawezi kuwa na ubavu kama hatuamui kuwa wawazi na kupambana nalo kama vita ya ukweli. Anayebugia anyongwe au akimtaja aliyemuuzia apewe kifungo cha maisha; mbebaji akimaliza kifungo nje akirudi ni kunyongwa na akiweza kuwataja wahusika ni kifungo cha maisha. Wahusika wakuu ni kunyongwa tu moja kwa moja na nchi nzima tuendeshe kura ya siri kuwataja na kuwamaliza.
Mimi naona watajwe tuuu kwani uwepo wao umesaidia hii nchi kitu gani wakati mauchafu ndio yanazidi kukomaa hizo intelijensia zao si zingetusaidia basi kujua madawa yanavyosafiri au zipo kwa ajili ya kukamata makonteina ya kura tu; wote ndio hao hao hakuna cha cdm wala ccmKutajwa kwa chadema kumekuuma kweli!
Huo uchambuzi umemnufaisha nani?
Tuweke wazi kwenye katiba suala la unyongaji na ruhsa ya saini za watu kumuondoa rais madarakani kama hafai au kumshinikiza atekeleze matakwa ya umma sio kungoja fadhila za mtawalaHakuna vita isiyokuwa na Jemedari, viongozi wetu wanawajua na hata Mkuu wa nchi ameshakiri kuwa anawafahamu Mabwana wa biashara ya dawa za kulevya lkn amenywea, unategemea Watanzania gani watapigana hivyo vita bila kuwa na Jemedari wa kuongoza vita hivyo?
Tumeshawazoea, nyinyi kila kitu ni kupinga tu, hata kama ni cha masilahi ya taifa.
Ghahawa mchagga ndiyo analima, mimi kijiwe changu kipo Kimara Temboni, ukishuka tu kituoni.Acha uongo,dili mnachungulishana magamba kwa magamba.Kahawa unauza wapi nije piga kikombe?ama utasema mchagga na ghahawa wapi na wapi?utakachosema ni mbege ya kibosho?