Ripoti ya CAG 2021/2022. ATCL, NHIF, Deni la Taifa, Vyura wa Kihansi, risiti za kielektroniki, Biswalo. Vyazua Mjadala

Hivi yule Zito Zuberi Kabwe, MWAMI inamaana Hadi sasa hajaipata Ripoti ya CAG?
 
Hatimae kichaka cha hayati Magufuli kimeisha sasa wizi wao, ufisadi wao, uongo wao, unafiki wao upo hadharani sasa.
Bora hata Hawa wanaweka hadharani kuliko wale waliokuwa wanaiba harafu wakiwekwa hadharani wanafukuza CAG 😁😁
 
Katika nchi ambazo watu wake wajitambua na wawajibikaji hiyo ripoti baada ya kusomwa na mkaguzi vyombo vya habari vyote (vile vinavyoheshimika) hupewa nakala ili wajiandae kwa uchambuzi na masuali.

Kisha baada ya hapo huandaliwa mkutano wa mkaguzi na waandishi wa habari ili kuwepo uwazi na ufafanuzi wa masuala mengi tu.
 
Waandishi aina Moloto, mbona aongelei na kuchambua report ya awamu ya sita
 
Hatimae kichaka cha hayati Magufuli kimeisha sasa wizi wao, ufisadi wao, uongo wao, unafiki wao upo hadharani sasa.
Kwa hiyo ripoti ya CAG mwakani itakuwa swaaaafi au siyo? Hiyo ni ndoto. Acha kujidanganya
 
Waandishi na wapashaji habari walipaswa kuja na masuali ambayo yametokana na kuchambua ripoti hiyo.
Wana muda wa kuichambua hiyo ripoti mpaka wawe na maswali ya kuuliza ?
 
Pascal Mayalla unakubaliana na hili ?..
 
Mkaguzi mkuu ndio aje aongelee uchakavu wa miundombinu ya Choo uwanja wa ndege?

Hakuna Menejimenti huko Airport. Sio swali hili, nasema Hakuna Menejmenti huko Airport kwa sababu ndio picha anayotoa CAG.

.... naamini kuna miongozo ya CAG katika kuwakilisha picha nzima ya ukaguzi anaofanya -kwamba mambo muhimu ya uhakiki huo ni ya kweli na ya haki-hapa naona mambo muhimu ya uhakiki kuwa ni ya kweli lakini sio ya haki-ni kama amepuuza sehemu ya haki na huo ndio mtazamo wangu yaani, si haki kuweka picha nzima ya usimamizi kama ile ya miundombinu ya choo ni chakavu- na sio kwamba nasema miundombinu ya choo ni mbaya per se lakini, again kwa maoni yangu ni -kama kuna harufu ya upigaji na ni mbaya kana harufu ya choo.
 
Wizara ya fedha kwenye mambo ya fedha waziri anayehusika hatoshi ktk hyo nafasi,awajibishwe
 
Muungwana huchutama wambile wale wa kale, na walau pamoja na madudu mengi yaliyomo kwenye report ya CAG, Muungwana kachutama.

Nasema nini!!? Kwa Siasa za nchi nyingi za Kiafrika na hata Tanzania, Rais anayo mamlaka kubwa na ikiwa ataamua kuitumia vibaya, taasisi hazitafanya kazi zake kwa Uhuru, na hivyo ikiwa Rais Samiah angetaka kuficha madudu yaliyomo kwenye report ya CAG na hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba idadi ya Wabunge wa chama chake ndiyo kubwa Bungeni, madudu hayo yangebakia kuwa minong'ono tu. Kaamua kuchutama na huu ni Uungwana.

Hata hivyo, ni makosa ya kimantiki kuacha report hii itaje madudu yote haya na bado ipite tu bila kuchukua hatua dhidi ya uzembe, usaliti na ufisadi mbaya kabisa unaotajwa humo. Hii itakuwa alama ya dharau kwa Watanzania, ama ishara ya kwamba kuna "the untouchables" ndani ya nchi hata kwa Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu, hili litakuwa jambo la kutisha sana.

Yaani kama kumekuwa na hasara, uzembe na ufisadi mkubwa namna hii na hadi sasa hakuna hata anayehofia nafasi yake, hii inamaanisha it's just business as usual, na hii ni mbaya.

Binafsi ni muumini wa kwamba siyo lazima wote tumpende mtu anqyekalia kiti cha Rais, lakini tunawajibika wote kumheshimu; na wakati watendaji wanapofanya mambo ya hovyo without any fear or remorse, ni dalili mbaya sana ya dharau. Najiuliza tunamdharau kwanini!!?

Sina ninalojua Nanga miye, nawaza tu kibanangabananga!!!
 
Hizo zilizoshindikana kutolea maoni ziwekwe hapa wanajukwaa watatoa maoni
 
Chawa Lucas Mwashambwa tangu itoke ripoti ya CAG hajaonekana, sijui ni hasira ya kukosa mgao wa ile 80 b iliyotengwa katika kampeni ya kumsifia Mama. Chawa wameadimika sana wiki hii

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Anayejua sehemu sahihi ya kuipata Hii report aseme hapa.

Au kama MTU anayo, share it here maana inaonekana kuna madudu Mengi Ambayo hatuyajui.
 
Magufuli alikuwa anamchukia Assad. Sasa Magufuli ameondoka tuone jambo gani litawafika hawa watu wanaotiliwa mashaka na CAG.
Je,watu wanayo appetite ya hawa vigogo kusakwa mmoja baada ya mmoja na kutiwa pingu?
Mambo ya Magufuli haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…