Ripoti ya CAG 2021-2022: Rais Samia ataka baadhi ya mashirika yasiyo na tija kufutwa

Ikumbukwe NDC ni Moja ya mashirika ambayo hupata hasara Kila mwaka..

Naunga mkono hoja,yapo mengi ya dizaini hiyo ,pia Kuna utitiri wa wakala na mashirika ya serikali yasiyo na Tija yanafanya kazi zinazoendana.

 
Hahahaha nchi ngumu hii 😅 maza atafuta mashirika/Taasisi ngapi?
 
Naunga mkono hoja.
 
Serikali haifanyi biashara, mashirika kama TRC au TTCL waachiwe wawekezaji alafu serikali iwe mbia tu awe anakula tozo na gawio lake
Unajua principal za biashara? Wakitaka waende kibiashara hakuna nauli wewe mnyonge utalipa..

Ttcl ya kazi gani? Ifutwe.
 
Namuunga mkono kwa hili, hakuna haja ya kung'ang'ana na mavitu yanayotafuna pesa za walipa kodi tu bila umuhimu wowote.
Unaweza kuwa sahihi, lakini kuna baadhi ya mashirika yameuwawa na hawahawa tuliowaamini. TANESCO bila mikataba feki kama IPTL na kina DOWANS ingekuwa inajiendesha kwa faida.

Serikali makini ingeshughulika na hawa waliotuingiza kwenye mikataba tata ili kuwafundisha wengine wanaokusudia kutuhujumu kuwa kuna kuwajibika.

Tumewahi kuwapa wahindi TRC, hali ilikuwa mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa chini ya serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…