Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?

Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?

Chini ya serikali sikivu na imara ya Dr.SSH.ni imani ya waTanzania walio wengi kwamba,
hakuna muhuusika hata moja alie tajwa kwenye report ya CAG na kulalamikiwa na waheshimiwa wabunge atasalimika na mkono wa Sheria, wote watawajibika na kuwajibishwa kulingana na makosa yao...
Haki itendeke na ionekane inatendeka !
Wanasemaga !!
 
Ukiwaangalia bungeni wanajadili kama wako serious kumbe sasa hayo yameisha nadhan kilakitu kimeisha tusubiri uchaguzi nasikia wanaweka technology hata bibi aliyeko ndan hawez kutoka apge kura ila maji masaf hayawezi kumfikia
 
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG).

Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye
Hakuna kitachoendelea bc's hii ni FAILED STATE.
 
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG).

Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge wamesikika hata wakishauri adhabu kali wapewe wahusika.

Bunge limehitimisha mjadala wa Ripoti husika. Nini kitafuata? Wahusika wa ufisadi na ubadhirifu huo mkubwa watafanywa nini na ni nani hasa mchukua hatua hizo?

Kiukweli, sisi walipa kodi wa nchi hii tungependa kuona hatua kali zinachukuliwa dhidi ya mafisadi na wabadhirifu waliotajwa au kuhusishwa na mambo hayo ndani ya Ripoti ya CAG.

Tunalipa kodi kwa maendeleo yetu. Kutumiwa isivyo kwa kodi na wale tuliowapa dhamana ya matumizi ya kimaendeleo ya kodi zetu kunaumiza sana. Tunatamani na kutaka hatua zichukuliwe. Wabunge wameona na kusema; wachukua hatua wafanye hivyo.
Majina?
 
Usikivu wa Dr.SSH unadhirika zaidi na uko wazi na bayana.
Taifa ni tulivu haijawahi kutokea, ulinzi na usalama ni madhubuti kupindukia, uhuru wa maoni, habari na uwazi serikalini ni vya kupigiwa mfano, umoja na utangamano miongoni mwa waTanzania imeimarika mara dufu.

Kwenye Maendeleo sasa heheeheee,
Dr.SSH anaonekana kwa uwzi zaidi kwenye maji, afya, elimu, kilimo, biashara,miundombinu, michezo, usafirishaji nakadhalika nakadhalika dah.....
unamkosa wapi na kenye nini Dr. SSH nchin Tanzania.....
Akina Lucas mpo wengi, siyo? Samia atapata matatizo sana akirudi kwenye kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa kutegemea kupigiwa debe na watu kama nyie. You are not objective. Unamwita Rais ni mnyenyekevu na msikivu atafanyia kazi ripoti ya CAG baada ya mjadala wa bunge, swali langu lilikuwa raisi tu kwamba, "hii ripoti ni mpya"? Rais amekuwa nayo miezi kadhaa kabla ya kujadiliwa na bunge, je nani kesha wajibishwa?

Tumeona marumbano yasiyokuwa na tija kwa taifa kati ya Wabunge na Mawaziri, hasa Mawaziri ambao ni washahuri wa karibu wa Rais wakiwatetea wezi, unategeme kuna kitu pale. Endeleeni kumpotosha kwa kumpamba lakini mnamuaribia. Kumsaidia mwambieni ukweli hali ilivyo huku mtaani.
 
Chini ya serikali sikivu na imara ya Dr.SSH.ni imani ya waTanzania walio wengi kwamba,
hakuna muhuusika hata moja alie tajwa kwenye report ya CAG na kulalamikiwa na waheshimiwa wabunge atasalimika na mkono wa Sheria, wote watawajibika na kuwajibishwa kulingana na makosa yao...
Hapo watakao wajibika ni dagaa tu ( wakurugenzi, watendaji wa vijiji, walimu wakuu, wahasibu wa halmashauri na madaktari) makambale hakuna wakuwagusa
 
Chini ya serikali sikivu na imara ya Dr.SSH.ni imani ya waTanzania walio wengi kwamba,
hakuna muhuusika hata moja alie tajwa kwenye report ya CAG na kulalamikiwa na waheshimiwa wabunge atasalimika na mkono wa Sheria, wote watawajibika na kuwajibishwa kulingana na makosa yao...
Kwanza sijaona mahala popote ambapo jina la Waziri specific limetajwa achilia mbali kuhusika.

Labda Maafisa masuuli lkini pia Serikali imeshachukua hatua nyingi tuu.
 
Tunasubiri kuona hatua zikichukuliwa, ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha iliyoibiwa na kutaifisha mali zao hao majizi.
 
Kama Waswahili wanavyosema,IMEENDA HIYO! Mafisadi yataendelea kupeta mitaani kama kawaida.
 
sasa endelea kuamini wanadamu upate makwazo na maradhi ya Moyo.

Amini Mungu, na umtumainie yeye pekee.
Jiombee wewe mwenyewe na uwaombee maadui zako na watenda maovu wote ikiwa ni pamoja na mafisadi na Utabarikiwa
Niwaombee mafisadi na wanafki kama ninyi ili mpate nn labda?
 
Back
Top Bottom