Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?

Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?

Petro Mselewa wakati Bunge linahitimishwa, nini azimio la Bunge juu ya ubadhitifu ulioonekana katika ripoti ya CAG? Kama Bunge halikuazimia chochote basi tusitarajia chochote.
 
Ombea adui zako waishi siku nyingi ili wewe mnyonge fundi wa manung'uniko unapobarikiwa huyo adui yako fisadi ajionee mwenyewe,

Nami nakuombea wakati huu unapojongea kwenye mahangaiko yako ya kujitaftia chochote kitu kinywani kwaajili yako na na familia yako, Baraka na Neema za Mungu ziambatane nawe leo, kesho daima na milele Aimen.
Aimen ..
Niwaombee mafisadi na wanafki kama ninyi ili mpate nn labda?
 
Ombea adui zako waishi siku nyingi ili wewe mnyonge fundi wa manung'uniko unapobarikiwa huyo adui yako fisadi ajionee mwenyewe,

Nami nakuombea wakati huu unapojongea kwenye mahangaiko yako ya kujitaftia chochote kitu kinywani kwaajili yako na na familia yako, Baraka na Neema za Mungu ziambatane nawe leo, kesho daima na milele Aimen.
Aimen ..
Dua yako kwako nasema AMIN..... ila uo utumbo wa juu baki nao mwenyewe chawa wa mafisadi
 
Kwanza sijaona mahala popote ambapo jina la Waziri specific limetajwa achilia mbali kuhusika.

Labda Maafisa masuuli lkini pia Serikali imeshachukua hatua nyingi tuu.
Akina Lucas mpo wengi, siyo? Samia atapata matatizo sana akirudi kwenye kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa kutegemea kupigiwa debe na watu kama nyie. You are not objective. Unamwita Rais ni mnyenyekevu na msikivu atafanyia kazi ripoti ya CAG baada ya mjadala wa bunge, swali langu lilikuwa raisi tu kwamba, "hii ripoti ni mpya"? Rais amekuwa nayo miezi kadhaa kabla ya kujadiliwa na bunge, je nani kesha wajibishwa?

Tumeona marumbano yasiyokuwa na tija kwa taifa kati ya Wabunge na Mawaziri, hasa Mawaziri ambao ni washahuri wa karibu wa Rais wakiwatetea wezi, unategeme kuna kitu pale. Endeleeni kumpotosha kwa kumpamba lakini mnamuaribia. Kumsaidia mwambieni ukweli hali ilivyo huku mtaani.
napenda nikusaidie kajambo kidogo tu, labda umeghafilika ama hujui.
Kupanga ni kuchagua,
Shughuli za bunge zinaendeshwa kwa kanuni taratibu na Sheria, hawakurupuki tu kufanya mambo....

Lipo bunge kwaajili ya bujeti ya serikali, lipo Bunge kwaajili ya Miswada na sheriaa mbalimba, lipo Bunge kwaajili ya Report ya CAG na kadhalika na kadhalika.....

Haiwezekani kikoa cha bunge la bajeti kujadili report ya CAG, wakati huo ukijadili hivyo inakua kama reference tu Lakini kinachojaduliwa ni bajeti.....

Huu ndio Muda muafaka kujadili report ya CAG, sawala la upya au uzamani linabaki binafsi kwako peke yako.

Jambo la mwisho,
Nikuhakikishie kwamba uchaguzi wa 2025 kwa CCM ni miongoni mwa chaguzi raihisi sana Tz hapajawahi kutokea kwasabb moja kubwa...

Hakuna kabisaa Upinzani.
Chama tawala hata kisimamishe gunzi kuwa mgombea urasi, Ushindi wa uhakika wa kishindo ni dhahiri....
Upinzani umeathirika sana na ukaribisho wa vibaraka ndani yake ndio maana umegawanyika na kukosa uelekeo kabsaa....
 
Dua yako kwako nasema AMIN..... ila uo utumbo wa juu baki nao mwenyewe chawa wa mafisadi
mimi kwangu,
anae kubali au kubeza maoni au mtazamo wangu ktkt mambo ya dunia hii, sina neno nae, awe huru kufanya vyovyote impendezavyo,

Lakini kwa kazi ya kwenda kwa Mungu wa mbinguni nitahakikisha naataambatana nawe na wengine wenge kwa maombi katika ulimwengu wa Roho na hata ukigoma ntakuburuza hadi nifike nawe pamoja kwa Baba yetu wa Mbinguni tukafurahi pamoja nae katika ufalme wake,
Kwa Jina La Baba, Mwana na Roho Mtakatifu....
Ubarikiwe sana with happier and very long smile.....
 
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG).

Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge wamesikika hata wakishauri adhabu kali wapewe wahusika.

Bunge limehitimisha mjadala wa Ripoti husika. Nini kitafuata? Wahusika wa ufisadi na ubadhirifu huo mkubwa watafanywa nini na ni nani hasa mchukua hatua hizo?

Kiukweli, sisi walipa kodi wa nchi hii tungependa kuona hatua kali zinachukuliwa dhidi ya mafisadi na wabadhirifu waliotajwa au kuhusishwa na mambo hayo ndani ya Ripoti ya CAG.

Tunalipa kodi kwa maendeleo yetu. Kutumiwa isivyo kwa kodi na wale tuliowapa dhamana ya matumizi ya kimaendeleo ya kodi zetu kunaumiza sana. Tunatamani na kutaka hatua zichukuliwe. Wabunge wameona na kusema; wachukua hatua wafanye hivyo.
Hakuna kitu hapo.., maana serikali na Bunge ni mtu mmoja ni sawa na wew kutoa buku ten mfuko wa kushoto ukaihamishia mfuko wa kulia.

Hakimu ni Mjomba na aliyeiba ni Binamu, huku Hakimu ni baba mdogo aliyepewa kazi na Shangazi, Kule Hakimu ni mtoto wa baba mdogo aliyepewa kazi na baba, ha ha ha haaaa hakuna kitu hapo. Watafungwa tu kina Maria wanaokutwa na nyama za pori.
 
Usikivu wa Dr.SSH unadhirika zaidi na uko wazi na bayana.
Taifa ni tulivu haijawahi kutokea, ulinzi na usalama ni madhubuti kupindukia, uhuru wa maoni, habari na uwazi serikalini ni vya kupigiwa mfano, umoja na utangamano miongoni mwa waTanzania imeimarika mara dufu.

Kwenye Maendeleo sasa heheeheee,
Dr.SSH anaonekana kwa uwzi zaidi kwenye maji, afya, elimu, kilimo, biashara,miundombinu, michezo, usafirishaji nakadhalika nakadhalika dah.....
unamkosa wapi na kenye nini Dr. SSH nchin Tanzania.....
Bado kupewa bahasha mmoja tu na Dr. Samia ili akupelekee moto
 
Hakuna kitu hapo.., maana serikali na Bunge ni mtu mmoja ni sawa na wew kutoa buku ten mfuko wa kushoto ukaihamishia mfuko wa kulia.

Hakimu ni Mjomba na aliyeiba ni Binamu, huku Hakimu ni baba mdogo aliyepewa kazi na Shangazi, Kule Hakimu ni mtoto wa baba mdogo aliyepewa kazi na baba, ha ha ha haaaa hakuna kitu hapo. Watafungwa tu kina Maria wanaokutwa na nyama za pori.
Nimeupenda sana huu ukweli mkuu😀💪💪
 
Bado kupewa bahasha mmoja tu na Dr. Samia ili akupelekee moto
mie kwanza ncheke....
🤣tssastssaaaatsszzaaaaaaaahhhhh

🐒sijui niwe upandree wa bwashee Mbowe, sijui upandre wa homeboy now puppet mtoa taarrifa msaidizi Taifa, sijui nijiunge Nov 9 na wasaka tonge watetezi wa wanyonge au na huyu muenezi ambae anazungumzwa sana ufipani🐒
 
Chini ya serikali sikivu na imara ya Dr.SSH.ni imani ya waTanzania walio wengi kwamba,
hakuna muhuusika hata moja alie tajwa kwenye report ya CAG na kulalamikiwa na waheshimiwa wabunge atasalimika na mkono wa Sheria, wote watawajibika na kuwajibishwa kulingana na makosa yao...
Ila aliyelalamikiwa Sana ni mwigulu na ndo kipenzi cha mama je atamtengua
 
mie kwanza ncheke....
🤣tssastssaaaatsszzaaaaaaaahhhhh

🐒sijui niwe upandree wa bwashee Mbowe, sijui upandre wa homeboy now puppet mtoa taarrifa msaidizi Taifa, sijui nijiunge Nov 9 na wasaka tonge watetezi wa wanyonge au na huyu muenezi ambae anazungumzwa sana ufipani🐒
Hahahah
Tssastsaaaatsszaaaaah nimecheka sana kusikia hiyo kitu 🤣🤣
 
Ila aliyelalamikiwa Sana ni mwigulu na ndo kipenzi cha mama je atamtengua
Tatizo ni moja tu,
analalamikiwa pakubwa kwa tuhuma za kusadikika nje ya report ya CAG.
Na hivyo kisiasa tunasema thuhuma dhidi yake ni political motivated allegations na opponents wake binafsi wa kisiasa na hivyo hazina madhara kisheria wala kiutendaji.
hivyo basi waziri husika atasavive vizuri tu hadi 2025,
ikitokea kaguswa ni basi ni kuhamishwa wizara tu na sio kutupwa nje ya Baraza.
 
mkuu sio Tuhuma za kusadikika ila tuhuma zote zinarudi nyuma kuanzia miaka ya 2020 na 2019 ambayo miaka hiyo aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa sasa ni Makamu wa Rais na hiyo ndyo ngumu kumeza hata mwigulu aliposema kweli hela zimechukuliwa kimahesabu alipoambiwa ataje ni nani akasema yeye hafahamu..
Ni kwamba kipindi hicho alikuwepo mheshimiwa Mpango na hiyo ndo ngoma ngumu kumsakizia Makamu wa Rais maana unaweza shangaa umemtaja ukala Tenguzi 🤣🤣

Na ndo maana wanaishia kusema tu hela zimepigwa ila wakiulizwa na nani hawasemi
 
Cha kwanza ilitakiwa Baraza la Mawaziri livunjwe na baadhi wakamatwe na kufikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi haswa hawa(Majaliwa, Makamba, Ummy, Bashe, Mwigulu, Nape, Angela, Aweso, Kijachu, Jafo, Mbarawa na Masa

Cha kwanza ilitakiwa Baraza la Mawaziri livunjwe na baadhi wakamatwe na kufikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi haswa hawa(Majaliwa, Makamba, Ummy, Bashe, Mwigulu, Nape, Angela, Aweso, Kijachu, Jafo, Mbarawa na Masauni).
Unataka kutuambia hawa wote uliowataja ndo Mafisadi wenyewe???
 
mkuu sio Tuhuma za kusadikika ila tuhuma zote zinarudi nyuma kuanzia miaka ya 2020 na 2019 ambayo miaka hiyo aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa sasa ni Makamu wa Rais na hiyo ndyo ngumu kumeza hata mwigulu aliposema kweli hela zimechukuliwa kimahesabu alipoambiwa ataje ni nani akasema yeye hafahamu..
Ni kwamba kipindi hicho alikuwepo mheshimiwa Mpango na hiyo ndo ngoma ngumu kumsakizia Makamu wa Rais maana unaweza shangaa umemtaja ukala Tenguzi 🤣🤣

Na ndo maana wanaishia kusema tu hela zimepigwa ila wakiulizwa na nani hawasemi
skiza,
Uwajibikaji wa viongozi wa kitaifa siku zote hokea kwa mipango Mahiri na mahususi ya kisiasa, kinyume cha hapo ni mbinyo au mgandamizo kutoka chini kwenda juu na kusalitiani kisiasa....

Lakini ninachokiona hivi sasa bungeni na kwenye mitanda ya kijamii ni ni mipasho na sarakasi za siasa kwamba nani anajua nini kuhusu fulani, whether ni kweli au si kweli, as results hili nalo litapita kama ilivyopita issue ya katiba mpya, tume huru na Bandari .......

Political statements never work, it remain political statements
 
Back
Top Bottom