Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Hadi ripoti ya CAG inafika bungeni ni kwamba kila mhusika ameshapewa nafasi ya kutoa maelezo na utetezi wake sehemu alipohitajika kufanya hivyo. CAG kashamaliza kazi, sasa ni kazi ya bunge la kina Musukuma, Gwajima, Babu Tale, Kibajaji n.k kuziwajibisha hizo taasisi.

Babu Tale aka Building Financier ndio anaenda kuchambua ripoti ya CAG ,Aisee JIWE alikuwa halitakii mema hili TAIFA.
 
Sikubaliani na kinacholengwa na mada hii; kwamba "JPM alikuwa fisadi mkubwa na anaumbuliwa na ripoti ya CAG". Ukweli ni kwamba ni kweli kulikuwa na maovu yaliyokuwa yanaendelea tangu awamu zilizotangulia na JPM alikuwa akipigana na hayo na kuwaasa Watanzania wamsaidie kuyafichua na kumuombea. Hivi ni sahihi kweli kumlaumu JPM kwamba alijenga ukuta Mererani lakini wizi unaendelea na kwa hiyo hatua alizochukua zilikuwa ni za kidhalimu? Kitu sahihi ni kusema hatua zilichukuliwa kwa nia njema kutatua tatizo lililokuwepo lakini hazikuzaa matunda yaliyotarajiwa. Siyo kwa sababu mtekelezaji alikuwa na nia mbaya ya ufisadi. Mada inaashiria kwamba JPM alikuwa fisadi mkubwa akijificha kwenye kivuli cha kutetea wanyoge. Huo ndio ukweli wenyewe japo hakufanikiwa katika matakwa yakwe sawasawa na Nyerere alivyoshindwa katika siasa yake ya ujamaa na kujitegemea. JPM alifichua ufisadi uliokuwa ukifanyika Muhimbili na mahospitali mengine. Akaweka kingingi. Mashine za kupimia zikafufuliwa ndani ya wiki mbili; wagonjwa wakawa wakipata dawa kwenye famasia za hospitali ambapo awali ya hapo walikuwa wanaambiwa wakanunue kwenye famasia za binafsi; vitanda vikapatikana kwa wagonjwa ambapo zamani walikuwa wakilala wagonjwa kadhaa kwenye kitanda kimoja na wengine sakafuni. Siyo sahihi kusema kwamba Awamu ya Tano ilikuwa imejaa uozo na kiongozi wake alikuwa fisadi. Hii nakataa kabisa. Sahihi ni kusema kwamba Awamu hiyo ilijitahidi kurekebisha uozo lakini haikufanikisha iliyotarajia kwa asilimia 100; na tuongeze kwamba kutofanikiwa huko kulitokana na ushirikiano mdogo kutoka kwenye jamii kuwafichua wapinga maazimio ya juhudi za serikali.
Hakuna KITU kibaya Kama KUDHULUMU KULA HALALI ZA WAJANE,WAZEE NA WAMAMA,UKAZIGEUZA JUU CHINI...ZIKAWA ZAKO USIZOZISTAHILI...hi laana ITAKUTAFUNA MPAKA KIZAZI CHAKO CHA 7..TUTAENDELEA KUONA MENGI KABLA YA 40
 
Yaan hapa ndipo ninapowanyooshea CCM wanaharibu then wanatwambia walichoharibu kwa kujiegemeza kwa Rais(mtu) ili kutengeneza Imani kwa chama na aliyepo madarakani. Nae ataharibu watakuja kusema ili tumwamini aliyesema n.k na wananchi tunakubali tu. Nyerere alifanya, wakaja kumbeza kupitia mwinyi, nae akaharibu, mkapa akaharibu, kikwete usiseme, magu nae Kama mnavyosikia. Na ujanja wa CCM ni kuhakikisha wao ndio wanaibua madudu mengi ili kumpa credibility aliyepo madarakani. Kwa kifupi CCM anajigeuza kwa wananchi kwa kuwa mpinzani wa aliyoyafanya anavyoona kuna faida ya kufanya hivyo kwa wananchi na wananchi nao wanajaa. Wakijaa anarudi kuwa mtawala na anaharibu tena yaan ni mwendelezo. So everything is f*ucked.
Nimekuelewa
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri
Ndugai kaanza kutumia ubongo?
 
Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha, je Fedha hizi ziliibiwa zilipelekwa nchi gani,au bank gani ? Kwà sababu kwenye mabank hakuna fedha na mitaani hakuna fedha. Je aliyekuwa katibu mkuu wizara ya fedha ,Doto James kwanini asilale kwanza segerea uçhunguzi ukiwa unaendeleaje?
Swali zuri sanaaa, una akili mno unless unajua ninachokijua ila itoshe kusema kuna mambo hayatoweza kutangazwa itakuwa fedheha kubwa mnoo.
 
Atahukumiwa siku ya mwisho kulingana na matendo yake.
 
Tatizo lipo kwa wakuu wa Idara husika, na viongozi wenye wajibu wa kusimamia Matumizi ya fedha za serikali.
wahusika ktk ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha za serikali wachukuliwe hatua bila kuoneana aibu.

kuleana na kuoneana aibu ndio kutaiangamiza taifa letu, hatua kali zichukuliwe.

Hata Hayati JPM ange kuwa haki ange chukua hatua kali vivo hivyo tunategemea kwa Rais wetu Mama Samia atachukua hatua kali kwa kila idara na viongozi wake.
Tatizo hizi taarifa asingezipata... maana kwake, yeyote aliyekuwa anamkosoa au anamueleza mabaya yake au ya watendaji wake alikuwa adui yake... Kuna wakati ofisi zingine zinazotajwa kuwa na makorokocho leo, ZILIHAMISHIWA IKULU... na huko tunajua CAG haingii
 
Swali zuri sanaaa, una akili mno unless unajua ninachokijua ila itoshe kusema kuna mambo hayatoweza kutangazwa itakuwa fedheha kubwa mnoo.
Statement kama hii, wakati wa yale makashfa (Nadhani wakati anaongelea MEREMETA) Pinda akiwa PM, alishawahi itoa ... kwamba kuna watu hawagusiki
 
Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha, je Fedha hizi ziliibiwa zilipelekwa nchi gani,au bank gani ? Kwà sababu kwenye mabank hakuna fedha na mitaani hakuna fedha. Je aliyekuwa katibu mkuu wizara ya fedha ,Doto James kwanini asilale kwanza segerea uçhunguzi ukiwa unaendeleaje?
Labda zipo kwa wachache kwenye masandarusi na mandoo huko majumbani... Au zipo benki za nje
 
Ulishawahi sikia report zingine za CAG au hii ndio ya kwanza?
Report hii ni peculiar kwakuwa ni ya shujaa wa Africa anayemtanguliza mungu Mbere! Halafu alishasema haibiwi! Imetushangaza sana
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri
Wakati madudu haya yanatendeka alikuwa wapi? Mbona hakusikiliza hoja za wapinzani? Aache kujipendekeza kwa SSH. Kilangila.
 
Back
Top Bottom