Sasa hapo kuna msaada gani kwenye point yako ya kitoto? CAG kawauliza wataalamu wa TANESCO, mmetumia upembuzi gani kuanza mradi? Wao wamemjibu, "tumetumia upembuzi yakinifu wa mwaka 1970 na 1980, kwa sababu ya uharaka wa kuanza mradi". Hiyo sababu ya uharaka wewe unaona inakuingia akilini kama siyo ufinyu wa mawazo? Umepiga hesabu ya kujenga nyumba kwenye Kiwanja mwaka 1980 unaanza ujenzi 2019 unatumia hesabu zilezile bila kujali kama humo kwenye Kiwanja kuna jirani alichimba shimo la taka, kuna miti mikubwa imeota, hali ya hewa imebadilika badala ya baridi kuna joto kwa hiyo paa linapaswa kuwa refu, wewe unapuyanga tu sababu ya uharaka? Mpingeni CAG kwa hoja siyo huu utopolo wa vioja.