Ripoti ya CAG juu ya kutohuisha upembuzi yakinifu mradi wa JNHPP ni upotoshaji mkubwa, kuna uwezekano CAG anatumika kisiasa

Ripoti ya CAG juu ya kutohuisha upembuzi yakinifu mradi wa JNHPP ni upotoshaji mkubwa, kuna uwezekano CAG anatumika kisiasa

Miradi ya Mazingira iliyotajwa ilikuwa Ofisi ya Zimamoto.
Mbona hawaulizi ilipo ripoti ya ofisi ya Magufuli kama kweli CAG alikuwa na nia ya kumchafua Malaika wao?
jamaa wameonesha udhaifu mkubwa sana wa kupima na kuchanganua mambo, ni tanzania pekee CAG haaminiki...
 
Ukiisoma kwa umakini ripoti ya CAG miradi ya maendeleo ukurasa wa 98 utagundua kuwa kuna upotoshaji mkubwa kuwa upembuzi yakinifu haukuhuishwakabisa na hivyo data zinazotumika kutekeleza huu mradi ni za mwaka 1970 na mwaka 1980. Jambo ambalo sio kweli.

Huu mradi unaosimamiwa na TANESCO kupitia kitengo chake cha ushauri wa kihandisi una umuhimu kwa taifa letu.

Ni kweli upembuzi yakinifu ulifanyika mwaka 1970 na ule wa utalaamu wa kiufundi ulifanyika mwaka 1980. Kampuni ya Ms Norconsult na M s Norplan zote za Norway.

Lakini taarifa aliyotoa CAG kuwa upembuzi yakinifu haukuhuishwa na sasa watu wanajua ule wa mwaka 1970 na 1980 unatumika sio kweli.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG huu mradi unatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ya umeme ya mwaka 2008, sheria usimamizi vyanzo vya maji ya mwaka 2009 na sheria ya mazingira ya mwaka 2004. Hivyo kuutekeleza bila kuhuisha upembuzi yakinifu ilikuwa ni vigumu.

Kwa uharaka wa mradi wenyewe vipengere muhimu vya upembuzi yakinifu kama, tathimini ya mazingira,usanifu wa kiufundi,utafiti wa kitaamamu na ufanisi wa miamba ulihuishwa. Hivyo vipengere vingine kama umuhimu wa kiuchumi na uwezo wa kutekelezeka vilibaki kama awali sababu ni mambo ambayo yanaonekana kuwa yapo vilevile. Hii ipo ukurasa wa 98 wa ripoti ya CAG miradi ya mendeleo.

Kwa mantiki hii hivi inaingia akilini kuwa watalaamu wa CAG mlienda kufanya ukaguzi na kudai kuwa kwa sababu upembuzi yakinifu wote haukuhuishwa kwa vipengele vyote hivyo huu mradi hauwezi kutekelezeka?

Yaani kwa akili ya kawaida mnataka kampuni ipewe kazi ya kufanya feasibility study kujua kama maji yatatosha kuzalisha umeme mto rufiji? Kwamba huu mradi una umuhimu gani kwa uchumi wa taifa letu?

Hata kama ni fitina za kisiasa muwe na aibu.
Wanajaribu kuvunja legacy yote ya Hayati lakini inawabidi wajipange sana.

Wanautaka umeme wa gas ambao unit moja ni karibu shilingi 150 ili biashara zao ziweze kufanikiwa.

Rais Samia ajipange vizuri ili aweze kusimamia ile ahadi ya kuhakikisha urithi wa waliomtangulia unakwenda kuifaidisha Tanzania ya kesho.
 
Back
Top Bottom