Ripoti ya CAG juu ya kutohuisha upembuzi yakinifu mradi wa JNHPP ni upotoshaji mkubwa, kuna uwezekano CAG anatumika kisiasa

Kama nakuelewa hivi
 
hayo manunuzi ya ndege na utekelezaji wa fedha za miradi ya maendeleo na ya kimkakati yanahusisha wizara ya kilimo na umwagiliaji sio?!...
Miradi ya Mazingira iliyotajwa ilikuwa Ofisi ya Zimamoto.
Mbona hawaulizi ilipo ripoti ya ofisi ya Magufuli kama kweli CAG alikuwa na nia ya kumchafua Malaika wao?
 
Mbona unashindwa kusema huo upembuzi yakinifu uliohuishwa ulifanywa na kampuni gani na Ni ya nchi gani? Au wewe ndio umelipwa kuja kutetea ujinga hapa?
 
Nimesoma, lakin mbona yuko sahihi bado.
Hoja iko pale pale hii feasibility study ni ya 1970s as a whole, kilichohuishwa ni vipengele vichache lakin study yenyewe ni ya miaka hiyo.
Unaelewa feasibility study ni kitu gani? Inakuwa na vipengele gani? Katika ile study ya mwaka 1970 vipengele viwilii tu ambavyo ni umuhimu wa kiuchumi wa mradi na uwezekano wa mradi kuendeshawa ndio havikuhuishwa. Kwa sababu hivi vipo Constant maana huwezi kusema vimebadilika. Vipengele vingine kama walivyomjibu vilihuishwa tatizo wapi?
 
Mbona unashindwa kusema huo upembuzi yakinifu uliohuishwa ulifanywa na kampuni gani na Ni ya nchi gani? Au wewe ndio umelipwa kuja kutetea ujinga hapa?
Ungekuwa unajua upembuzi yakinifu ni kitu gani usingehangaika. Kwa ufupi ulifanyika tena mara mbili na baadhi ya wapinzani walidai huu mradi utaharibu mazingira kumbe kiuhalisia unatumia eneo dogo sana la Selous
 
Hivi arobaini lini mkuu!?
Niulize tu, hivi mbona hatusomi chochote kuhusu report ya CAG kutoka ofisi mbili, ofisi ya makamu wa raisi na ofisi ya waziri wa fedha?

Kwamba ofiri aliyokuwepo SSH ilikuwa safi au ofisi aliyokuwepo mpango ilikuwa safi? Nchi ngumu sana hii.
 
View attachment 1748957
Soma vizuri ukurasa wa 98 ripoti ya CAG majibu mazuri aliyopewa CAG.
Sasa hapo kuna msaada gani kwenye point yako ya kitoto? CAG kawauliza wataalamu wa TANESCO, mmetumia upembuzi gani kuanza mradi? Wao wamemjibu, "tumetumia upembuzi yakinifu wa mwaka 1970 na 1980, kwa sababu ya uharaka wa kuanza mradi". Hiyo sababu ya uharaka wewe unaona inakuingia akilini kama siyo ufinyu wa mawazo? Umepiga hesabu ya kujenga nyumba kwenye Kiwanja mwaka 1980 unaanza ujenzi 2019 unatumia hesabu zilezile bila kujali kama humo kwenye Kiwanja kuna jirani alichimba shimo la taka, kuna miti mikubwa imeota, hali ya hewa imebadilika badala ya baridi kuna joto kwa hiyo paa linapaswa kuwa refu, wewe unapuyanga tu sababu ya uharaka? Mpingeni CAG kwa hoja siyo huu utopolo wa vioja.
 
Kazi ya kuhuisha baadhi ya vipengele ilifanywa na kampuni gani na mwaka gani? Tupe hizo taarifa kama ulizisoma mkuu, kama ni kweli tujue CAG anatumika kisiasa kama hauna basi unatumika kueneza propaganda za kisiasa ili kumchafua CAG
Mlishazoea kushibisha kampuni zenu za kifisadi
 
Pole sana, kosa lako ni kukosa elimu bora.
 
View attachment 1748957
Soma vizuri ukurasa wa 98 ripoti ya CAG majibu mazuri aliyopewa CAG.
Sasa huoni vipengele ambavyo Ni muhimu zaidi havikufanyiwa upembuzi yakinifu..
1. Kipengele cha uchumi wa mradi ( gharama za mradi)
2. Uwepo wa maji ya kutosha kuendesha mradi.
Kila mtu anajua mvua zilizokuwa zinanyesha miaka ya 70(miaka 50 iliyopita) Ni tofauti na mvua za Sasaiv.. na matumizi ya watu ya maji ya wakati ule Ni tofauti na sasa.
Sasa unatetea nini hapa. Na kwanini unakuwa mjinga kiasi hiki hata usiweze kuona vitu hivi waziwazi?
 

Wote hao ni CCM,

Ujinga na upumbavu mwingi kutetea walewale
 
Ungekuwa unajua upembuzi yakinifu ni kitu gani usingehangaika. Kwa ufupi ulifanyika tena mara mbili na baadhi ya wapinzani walidai huu mradi utaharibu mazingira kumbe kiuhalisia unatumia eneo dogo sana la Selous
Najua upembuzi yakinifu Ni feasibility study..mi nimesoma mambo ya miradi hivyo usitake kunifundisha vitu usivyovijua. Tunajua kabisa upembuzi yakinifu uliofanywa na Mashirika makubwa ulionyesha uharibifu utakaofanywa na huo mradi Ni sawa na kukata miti eneo lote la mkoa wa Dar es Salaam na ripot hiyo ilikataliwa na Jiwe akisema Ni wa mabeberu..na akaenda kumchukua professor uchwara hapo UD ili aandike kitu kinachomfurahisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…