Ripoti ya CAG juu ya kutohuisha upembuzi yakinifu mradi wa JNHPP ni upotoshaji mkubwa, kuna uwezekano CAG anatumika kisiasa

Kama kila kitu kikisemwa ni uharaka ili kuvunja taratibu, huoni ni UHOLELA katika utendaji wetu?
Kulikua na ugumu gani kufanya Review ya Feasibility Study na kuboresha mapungufu?
 
Kwahiyo CAG aliyeteuliwa na mkuu wa malaika waasi leo mnamuona hafai tena kisa amesema kuna mambo hayako sawa!? Kazi mnayo mwaka huu kumtetea marehemu ambae hatakaa afufuke
 
Kumbukeni Rais Magufuli wakati huo alisema alipokea taarifa mbili za upembuzi akaziikataa kwa sababu zilitetea mazingira. Je anayesema haikuwepo tathmini au feasibility ni muongo.
 
Ofisi yake haina chochote zaid ya kero za muungano na Mazingira.vitu vyote vya Hela mwendazake aliviweka chin yake.Ni Mara ngapi mama ameomba kujiudhuru Ili amuachie serikali yake lakn wenye busara wakamuambia subir
Toa uongo wako wa kwenye kahawa hapa.
 
Kama kila kitu kikisemwa ni uharaka ili kuvunja taratibu, huoni ni UHOLELA katika utendaji wetu?
Kulikua na ugumu gani kufanya Review ya Feasibility Study na kuboresha mapungufu?
Kwa uharaka, hivyo vipengele muhimu vilifanyiwa updating. Kwa umuhimu wa huu mradi kiuchumi umebadilika? Maji yamepungua kiasi kwamba hautekelezeki?
 
CCM inapasuka vipande vipande.

Ukifuatilia malumbano huku mitandaoni utadhani ni kati ya chama tawala na upinzani, asilimia kubwa ni ccm wenyewe kwa wenyewe.

Upinzani wangekuwa smart wakatumia huu mwanya, 2025 wangechukua nchi.
CCM tunajielewa tutapingana wee mwisho wa siku tunavunja makundi tunaunda team moja kukabili adui wa upinzanitukiona ni hatari kwetu kunyang'anywa dola
Tutaendelea kupingaa tukishaishika
 
Kama kila kitu kikisemwa ni uharaka ili kuvunja taratibu, huoni ni UHOLELA katika utendaji wetu?
Kulikua na ugumu gani kufanya Review ya Feasibility Study na kuboresha mapungufu?
Kwa uharaka, hivyo vipengele muhimu vilifanyiwa updating. Kwa umuhimu wa huu mradi kiuchumi umebadilika? Maji yamepungua kiasi kwamba hautekelezeki?
Rudi shule ukaanze la kwanza.
 
Kwa uharaka, hivyo vipengele muhimu vilifanyiwa updating. Kwa umuhimu wa huu mradi kiuchumi umebadilika? Maji yamepungua kiasi kwamba hautekelezeki?

Rudi shule ukaanze la kwanza.
Hivi ndo upeo wako umeishia hapa katika kujibu hoja? Pole sana. Nenda tu ukawe mlinzi wa kaburi la Mkuu wa malaika waasi
 
Niulize tu, hivi mbona hatusomi chochote kuhusu report ya CAG kutoka ofisi mbili, ofisi ya makamu wa raisi na ofisi ya waziri wa fedha?

Kwamba ofiri aliyokuwepo SSH ilikuwa safi au ofisi aliyokuwepo mpango ilikuwa safi? Nchi ngumu sana hii.
Hii ya MAKAMU hata ikiwepo, na ipo, mama haimhusu. Kule kuna waziri/mawaziri na katibu mkuu. Asante kwa uchambuzi
 
Umepanick. CAG amepitia feasibility & design report inayotumika na akakuta ni ya 1970/80, na kwa muda wote huo ilitakiwa ifanyike design review kuona kama mradi bado uko feasible. Au mwenzetu una current data zinazoonesha design review ambazo CAG hakuzipata?
 
Kati ya CAG na wewe nani alituma watu kwenda kufanya ukaguzi wa huo mradi? Lete data zako za kweli ulizoenda kufanya ukaguzi ambazo hazina upotoshaji

Wamebaki kuongea kwa hisia tuu kulingana na matakwa ya nafsi zao. Ukweli utabaki kua zile ni taarifa za kiuchunguzi.

Hao waache waendelee kupiga mayowe wataona wenyewe.
 
Kama ule wa miaka nenda ulifanywa na Hiyo Kampuni ya Norway huu uliotumiwa na Serikali ya Magufuli ulifanywa na nani!
Unatumiaa nguvu kubwa badala ya kuleta facts hapa umsafishe!
Ulifanywa na kamati ya ufundi ya Tanesco kwa kusaidiana na wataalamu wa Wizara ya maji na Nishati. Ilikuwa ni serikali inayohimiza kujitegemea. Msiturudishe kwenye ulaji wa bomba la gesi na majenereta . Prof yule wa huko kwa baba wa Taifa anataka arudi tena hahahaaaa. Haikutosha ile ya Mtwara na vitalu alivyonyimwa marehemu wa ITV
 
Pole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…