Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Only Tanzanians can determine the fate of Tanzania!
 
MOST WANTED

View attachment 1079


WATAJWA HAPO JUU NI WATUHUMIWA WA UFUJAJI WA MABILIONI YA PESA ZA WATANZANIA KWA KUTUMIA KAMPUNI HEWA.YEYOTE MWENYE TAARIFA ZITAKAZO SAIDIA KUKAMATWA KWAO ANAOMBWA KUTOA TAAFIRA MARA MOJA KWA WATANZANIA

Kuna Dau lolote limeisha tolewa tuanze kazi ya kuwatafuta? Je unafikiria wamekimbilia wapi? na wanapenda kukaa viwanja vipi?
 
Watuhumiwa wa ufisadi Richmond washindwa kumpokea Rais Kikwete

Na Waandishi Wetu, Dodoma

WATUHUMIWA wote wa ufisadi ambao walihusika katika kuipa zabuni ya uzalishaji wa

umeme wa dharura hatimaye kuipa ushindi Kampuni ya Richmond Development ya nchini Marekani mwaka 2006 jana walishindwa kumpokea Rais Jakaya Kikwete alipowasili mjini hapa kutokana na watuhumiwa hao kuwa na kikao maalumu na Kamati ya Uongozi ya wabunge.


Rais Kikwete aliwasili jana saa 9 alasiri akitokea jijini Dar es Salaam ingawa haikuwekwa bayana sababu ya ziara hiyo ya ghafla, lakini wachunguzi wa mambo wanasema kuwa amekuja ili kuweka sawa mgawanyiko unaonekana kutokea ndani ya CCM.


Mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge ambapo pamoja na mambo mengine

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Harrison Mwakyembe aliwasilisha muhtasari wa ripoti hiyo, viongozi wote waliotajwa kuhusika na ubadhirifu huo wakiongozwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa walijifungia ndani ya ofisi za Spika kwa ajili ya kikao

maalum.


Watuhumiwa hao ni pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahimu Msabaha, Waziri

wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mwanansheria Mkuu wa Serikali Johnson

Mwanyika waliingia katika ofisi hiyo ili kukutana na Kamati ya Uongozi ya Bunge

tangu kuahirishwa kwa shughuli za Bunge, lakini mpaka tunaenda mitamboni walikuwa

bado hawajatoka.


Kamati ya Uongozi wa Bunge inaongozwa na Spika wa Bunge ambaye ni Mwenyekiti,

Naibu wake ni Makamu Mwenyekiti na Wakuu wote wa Kamati za Kudumu za Bunge ni

Wajumbe wa Kamati hiyo ambapo kwa upande wa serikali inawakilishwa na Waziri Mkuu.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Injinia Stella Manyanya aliwasilisha Bungeni hapo hoja ya ya kuwasilisha Taarifa ya Kamati hiyo huku shughuli za maswali ziliendelea kama kawaida.


Mara baada ya shughuli za maswali kwisha Spika alimuita Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Mwakyembe kuja kutoa ripoti hiyo kwa wabunge kwa muhtasari kwa kuwa ripoti hiyo ilikuwa kubwa sana na ilikuwa na viambatanisho zaidi ya viwili.


Baada ya Kauli hiyo, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge alisimama na kuomba muongozo wa Spika kuwa kutokana na utaratibu wa Bunge shughuli za maswali zilipaswa kuisha kwanza ndipo shughuli nyingine zifuate kama kuwasilisha ripoti

hiyo hivyo kutaka hoja hiyo isijadiliwe kwa wakati huo.


Hata hivyo, Spika alipinga hoja hiyo na kusema kuwa ?kwa utaratibu Bunge linaongozwa kwa kuzingatia Kamati ya Uongozi ambayo katika Kamati hiyo Serikali ina mwakilishi wake na walikuwepo tumekutana na kuamua ripoti hii ijadiliwe kabla ya kipindi cha maswali kuisha,?alisema.


Alisema kama tukio la Jumapili la wabunge kususia semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati isingetokea taratibu za Bunge zingeendelea kama kawaida, lakini hali imechafuka na moto mkubwa unafukuta Bungeni kutokana na ripoti hiyo.


Kauli hiyo ya Spika ilishangiliwa na wabunge wote na kushindwa kujizuia kwa kupinga meza zao kuonyesha kufurahishwa na uamuzi huo uliotolewa na Spika huyo.


Hatimaye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Mwakyembe alienda mbele ya Bunge hilo na kuanza kusoma muktasari wa ripoti hiyo huku wabunge wakiwa wametulia kimya kumsikiliza kwa makini na wakishangilia katika sehemu kadhaa zilizowataja watuhumiwa hao kuhusika moja kwa moja kitendo hicho.


Hata hivyo, Dk Mwakyembe muda wa kuwasilisha hoja hizo ambao kwa taratibu za Bunge

ni saa moja, uliisha hivyo Mwenyekiti huyo aliomba muongozo wa Spika kuomba asome

mapendekezo kutokana huo kuisha jambo lililopingwa vikali na wabunge.


Spika wa Bunge ilibidi kuingilia kati na kusema kuwa kwa taratibu za Bunge hoja inapaswa kuwasilishwa kwa muda wa saa moja hivyo kama wanataka hoja hiyo iendelee ni lazima wabadili kanuni za Bunge hilo ambapo hata hivyo taratibu zinaruhusu kuongezwa kwa dakika 30 pekee.


Dk Willibrod Slaa aliomba muongozo wa Spika na kutaka hoja hiyo iendelee kwakusema kuwa

ripoti hiyo ni muhimu kwa maslahi ya wananchi na kwamba ilitumia pesa nyingi za walala hoi hivyo ni muhimu kuongezewa muda jambo lililokubaliwa na Spika.


Mara baada ya kumaliza kusoma ripoti hiyo, Spika wa Bunge alihairisha shughuli za Bunge na kutangaza kuwa ripoti hiyo itajadiliwa kwa siku mbili yaani leo na kesho hivyo ni vyeme kupeana nafasi ya kusoma akisisitiza kuwa mambo hayo ni mazito.


Hata hivyo, mara baada ya kuharishwa shughuli za Bunge watuhumiwa wote wa ufisadi

huo wakiongozwa na Waziri Mkuu, walishindwa kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge kwa

zaidi ya dakika 10 huku wakikaa kikao kujadili.


Hata hivyo, haikujulikana nini walichokuwa wakijadili watuhumiwa hao, lakini walionekana kuwa wanyonge na kuishiwa nguvu kutokana na matokeo ya ripoti hiyo.


mwananchi
 
Napenda kuwa taarifu kwamba baada ya kile kikao cha kwanza kumalizika sasa kikao cha Wabunge wote wa CCM ndiyo kimeanza . Kimya kimetawala hofu imetanda . Kikao kina anza bila ya waziri Mkuu kuwepo Ukumbini . Habari nilizo nazo na za uhakika kwamba Lowasa kaitwa Ikulu na hatujui nini kinaendelea huko Ikulu .Nitaendelea kuwapa maendeleo ama mwana JF mwingine tafadhali tupe yanayo jiri kama una habari ama upo hapa Dodoma kama mimi .
 
mpaka kieleweke,

Unajua duniani kuna mengi- pia kuna kulipiza visasi, kukumoana, au to represent reality!

Kwa hiyo hii reporti yawezekana kuna mengine yamefichika- sisi hatujui! Unajua ni mara ya kwanza kupata ripoti kama hii tena toka Mwkiti wa kamati akiwa mwana CCM!

Pia yawezekana Mwakyembe amesema ukweli kama inavyopasa! I just want to look into the matter in a larger picture!

yaani una maana watu wazungumze ukweli pale tu wanapolipiziana kisasi??
Mwakyembe hakumtuma mtu afanye uovu huu.Tuondokane na mawazo haya potofu kuwa mpaka watu wawe wanalipiziana kisasi ndo waseme ukweli.Mtu huamua kusema uongo kwa makusudi sio kama anakuwa hajui ukweli.Alichofanya Mwakyembe na kamati yake ni kuvunja ule mwiko wa kuficha ukweli kwa kutumia bunge, lakini hakuna ambacho watu walikuwa hawafahamu kabla ya hapo.JF imeripoti kila kitu ila watu walikuwa wanadharau kuwa ni redio mbao.
 
EL is toast na hatarudi tena,swali vipi zile 152M per day tunaendelea kulipa au tayari tumesimamisha?
 
Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi wamesema kamati hiyo haikuwatendea haki kwa kuwa haikuwapa nafasi ya kutoa maoni yao kama Watanzania wengine. Akizungumza na Mwananchi jana mara baada ya ripoti hiyo kusomwa Bungeni, Waziri Karamagi alisema anasikitishwa na Kamati hiyo kwani haikumtendea haki kwa kuwa haikumpa nafasi ya kumuita na kumuhoji juu ya ufisadi huo hivyo Kamati hiyo ilitoa matokeo yake kwa hisia tu.

MZEE wa Buzwagi naona anachanganya mambo hapa, yeye ni wa Richmond au yeye ni wa Buzwagi? Mbona kuna wengine walikwenda bila kuitwa inakuwaje yeye atake kuitwa, au alikuwa amelala wakati Harrison anasema kuna wengine wanne walikwenda bila kuitwa, yeye inabidi asubiri ya Buzwagi ataitwa tu! huenda nayo inakuja!
Chenge naye anaongea uozo, sijui anataka nini, yaana anataka aamibiwe ku\osa lilikuwa hapo halafu aseme tutarekebishe, halafu yaishe, no way!
 
Napenda kuwa taarifu kwamba baada ya kile kikao cha kwanza kumalizika sasa kikao cha Wabunge wote wa CCM ndiyo kimeanza . Kimya kimetawala hofu imetanda . Kikao kina anza bila ya waziri Mkuu kuwepo Ukumbini . Habari nilizo nazo na za uhakika kwamba Lowasa kaitwa Ikulu na hatujui nini kinaendelea huko Ikulu .Nitaendelea kuwapa maendeleo ama mwana JF mwingine tafadhali tupe yanayo jiri kama una habari ama upo hapa Dodoma kama mimi .

Ningeomba Edward Kesho Afikishwe Mahakamani kujibu tuhuma za kufanya biashara akiwa kwenye Ofisi za Umma na kutumia madaraka vibaya (FISADI MKUBWA)
 
Huyu naye anajidharaurisha tuu,yaani tangu umafia wa Buzwagi na hili la richmond bado anataka kutuambia nini,si bora ajiuzuru tuu? huyu si alitishia kwenda mahakamani...haha ahahaha ahaha ahah,mzee wa rushwa huyu nasikia na kule bandarini ana kamkono kake kwenye ile kampuni iliyoongezewa mkataba kabla haujaisha,fisadi kweli kweli huyu!
 
mzeee lunyungu hata mie mzee mwenzio nnaomba uniwie radhi ni kweli kikao hakiongozwi na mzee ambaye mnamwita mimvi

nisameheeee eeh mzee mwenzangu ukija zenji nitakuchunjia bata si unampenda(jokes)
 
Spika wa Bunge ilibidi kuingilia kati na kusema kuwa kwa taratibu za Bunge hoja inapaswa kuwasilishwa kwa muda wa saa moja hivyo kama wanataka hoja hiyo iendelee ni lazima wabadili kanuni za Bunge hilo ambapo hata hivyo taratibu zinaruhusu kuongezwa kwa dakika 30 pekee.

Dk Willibrod Slaa aliomba muongozo wa Spika na kutaka hoja hiyo iendelee kwakusema kuwa

Huyu Spika (Mr. Standard) hata hajui maslahi ya nchi ndio maana aliona mafisadi na akataka kukimbilia Marekani.
 
Waziri Karamagi alalamika kamati ya Richmond haikumtendea haki

Alisema wanachotakiwa kukifanya wabunge, ni kutumia sasa mamlaka yao kufuta ajira ya Lowassa waliyoithibitisha baada ya rais kuwasilisha jina lake bungeni.Vilevile alishauri wote waliohusika na kashfa ya Richmond wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo ili kudhibiti wasitoroke nchini, ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zao
mwanachi

Maneno yenye hekima haya ...wasije enda tibiwa US bure...
 
mzeee lunyungu hata mie mzee mwenzio nnaomba uniwie radhi ni kweli kikao hakiongozwi na mzee ambaye mnamwita mimvi

nisameheeee eeh mzee mwenzangu ukija zenji nitakuchunjia bata si unampenda(jokes)

Mtu wa Pwani, bata una maana gani ?
 
Hii ripoti nimeipenda kwa vipengele hivi viwili:

[I]....Serikali kuizuia TANESCO isivunje mkataba na kampuni hiyo licha ya sababu zote kisheria kuwepo, ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyo juu ya Wizara ya Nishati na Madini kutumika katika suala hili na Kamati Teule kutokana na ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa mdomo, inaiona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu. [/I]

Na hitimisho hili:

.....Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge
 
Politics is a dirty game.JK haikuwa choice yake EL kuwa PM bali CCM mtandao walimlazimisha.

Natabiri EL atajiuzulu come kesho...MR Pinda will be our new PM..watch this space friday
 
mwaka huu ni mwaka mwema kwa watanzania.

unajua ukitaka kupona lazima upate machungu mazito, haya ni machungu ya kupona haya ni machungu ya mzazi kupata mwana mwema.

tuvumilie maumivu haya kwa matarajio mema.
 
Napenda kuwa taarifu kwamba baada ya kile kikao cha kwanza kumalizika sasa kikao cha Wabunge wote wa CCM ndiyo kimeanza . Kimya kimetawala hofu imetanda . Kikao kina anza bila ya waziri Mkuu kuwepo Ukumbini . Habari nilizo nazo na za uhakika kwamba Lowasa kaitwa Ikulu na hatujui nini kinaendelea huko Ikulu .Nitaendelea kuwapa maendeleo ama mwana JF mwingine tafadhali tupe yanayo jiri kama una habari ama upo hapa Dodoma kama mimi .

Lunyungu,

Ina maana JK hahudhurii hicho kikao cha wabunge wa CCM? Sasa kama Lowassa hajaenda kwenye hicho kikao, kweli kitafanyika? Au itabidi wamsubiri.

Ni kama yeye ndio kiongozi wa wabunge wa CCM kwahiyo ni muhimu kuwepo kwenye huo mkutano mpaka pale wabunge wakiamua asiwe mwenyekiti kwasababu ni mtuhumiwa.
 
Back
Top Bottom