Ripoti za CAG: Itungwe sheria wale wote wanaotajwa au kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha katika ripoti za CAG wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Huu ndio ushauri wangu, vinginevyo ubadhirifu huu wa kila mwaka hautaishi kwani wanajua hata wakituhumiwa, hakuna kitachofanyika, na kama ni kuchukua hatua basi, itategemea na utashi wa Raisi.

Binafsi siku hizi sina hata hamu tena ya kufuatilia ripoti za CAG kwasababu naona ni kama kutufanya watanzania wajinga kwani tuhuma huibuliwa kila mwaka huku hakuna jambo serious linalofanyika iwe ni kufanya uchunguzi, watu kusimamishwa kazi au kufanya special auditing katika maeneo yanayotajwa hasa yale yanayohusu ubadhirifu mkubwa au uhujumu uchumi.

Ripoti teyari zinaonyesha madudu,halafu vyombo kama TAKUKURU vinasubiri Raisi au Makama Mwenyekiti wa CCM Bara atoe tamko ndio hatua zichukuliwe!! Bora hizi ripoti wasitusomee na wakae nazo, na kama ni kutosomea, basi watusomee tukishapata Tume Huru ili wananchi waje wachukue hatua uchaguzi unapofika kwa kuondoa watawala au chama kinacholea ufisadi.

Tusichoshane, teyari inflation inatutesa, hivyo msituongezee mauzauza. Kaeni na maripoti yenu.
 
Afu tukisha simamishwa kazi sisi tuendelee kula wapi. Fanya mkuu na wewe uingie kwenyw chain ya kula hizi pesa ni tamu
 
Chadema pia wametajwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma, nani atatoka pale? Mbowe na Mnyika na Lissu?
 
Nilikuwa napewa maneno kipindi cha Magufuli kuwa yeye shujaa katika rushwa , kumbe ni shujaa katika kutafuna hela zetu.
Kabisa JPM alikuwa Fisadi haswaaaa lakini sijui hizo pesa za kujenga barabara, flyovers, viwanja vya ndege vya kimataifa, stendi mpya za mabasi, Umeme wa bwawa la Nyerere, bandari za maji na kavu, vivuko, madaraja, Mahospitali, na kutuweka uchumi wa kati TZ alizitoa wapi nakati hakuwa na diplomasia kabisa "Dikteta" hadi alinyimwa misaada na mabeberu [emoji848]

Tukafukue pesa Chato atakuwa kazichimbia ndani mwake [emoji23]
 
Afu tukisha simamishwa kazi sisi tuendelee kula wapi. Fanya mkuu na wewe uingie kwenyw chain ya kula hizi pesa ni tamu
Naona na huyu ana Justify posho za Marekani.

Nchi hii bwana.
20220428_192338.jpg
 
Kabisa JPM alikuwa Fisadi haswaaaa lakini sijui hizo pesa za kujenga barabara, flyovers, viwanja vya ndege vya kimataifa, stendi mpya za mabasi, Umeme wa bwawa la Nyerere, bandari za maji na kavu, vivuko, madaraja, Mahospitali, na kutuweka uchumi wa kati TZ alizitoa wapi nakati hakuwa na diplomasia kabisa "Dikteta" hadi alinyimwa misaada na mabeberu [emoji848]

Tukafukue pesa Chato atakuwa kazichimbia ndani mwake [emoji23]
China wangekuwa na akili kama zenu, wasingefika hapo walipo leo hii.
 
Kagame kachota sana Tanzanate zetu, now dayz hawataki hata hasogee.
 
China wangekuwa na akili kama zenu, wasingefika hapo walipo leo hii.
Si huwa mnawaita CHINA "Madikteta" kwa upumbavu mliopumbazwa nao "democracy" na mabeberu [emoji848]

Nakati China hawajui na wala hawataki kabisa kusikia "democracy" lakini wameendelea mbali mno kiuchumi hadi kuwa nafasi ya pili duniani [emoji16]
 
Huu ndio ushauri wangu, vinginevyo ubadhirifu huu wa kila mwaka hautaishi kwani wanajua hata wakituhumiwa, hakuna kitachofanyika, na kama ni kuchukua hatua basi, itategemea na utashi wa Raisi.

Binafsi siku hizi sina hata hamu tena ya kufuatilia ripoti za CAG kwasababu naona ni kama kutufanya watanzania wajinga kwani tuhuma huibuliwa kila mwaka huku hakuna jambo serious linalofanyika iwe ni kufanya uchunguzi, watu kusimamishwa kazi au kufanya special auditing katika maeneo yanayotajwa hasa yale yanayohusu ubadhirifu mkubwa au uhujumu uchumi.

Ripoti teyari zinaonyesha madudu,halafu vyombo kama TAKUKURU vinasubiri Raisi au Makama Mwenyekiti wa CCM Bara atoe tamko ndio hatua zichukuliwe!! Bora hizi ripoti wasitusomee na wakae nazo, na kama ni kutosomea, basi watusomee tukishapata Tume Huru ili wananchi waje wachukue hatua uchaguzi unapofika kwa kuondoa watawala au chama kinacholea ufisadi.

Tusichoshane, teyari inflation inatutesa, hivyo msituongezee mauzauza. Kaeni na maripoti yenu.
Katiba mpya ndio dawa ya haya yote
 
Mbaya zaidi wezi huwa ni walewale wa siku zote,
Wanachofanya ni kuhamishana tu, wa huku anapelekwa kule wa kule analetwa huku, nchi ngumu sana hii
 
Back
Top Bottom