Tetesi: Ripoti za uchunguzi wa uhalali wa shahada ya uzamivu (PhD) ya hayati Magufuli pamoja na wengine zimefichwa

Nimeona umeweka kifungu cha Prospectus ya UDSM cha 2007, ndani yake kinazungumzia time frame kuhusu muda wa kumaliza, 3-5 years respectively.

Hata kama Magufuli alikuwa kiongozi wa serikali, nimeshamjibu mwenzako, alikuwa mchapakazi, hakuwa mvivu na mzembe kama wengine, hivyo kwake kufanya jambo kinyume na huo muda uliowekwa hapo juu sishangai.

Kuhusu kupewa cheo Dr. aliyekuwa Supervisor wake, hiyo pia sio kigezo cha Magufuli kupendelewa, tumeshazoea huko CCM vyeo hutolewa kwa kujuana, na kama Magufuli alifahamiana na huyo Dr. kutokana na kusimamiwa paper yake, kutoa cheo sio fumbo la siri.
 
Nakushauri utulie kwenye hoja yako usitoke nje ya hapo, jitahidi uwe na consistence.

Kuhusu Magufuli kuwa "exception" au vinginevyo inategemeana na anayejiuliza, wewe kwa chuki na hasira zako kwake huwezi kuliona hilo.

Kama wewe hukumuona hivyo, wengine walimuona alikuwa exception kwa namna alivyo set standard kwenye utendaji serikalini, mpaka leo tunawaona kina Samia wanajitutumua kuifikia, bahati nzuri naye ameshakiri hilo.
 
Hoja nzuri hii.

ila kupotea kwa huyu kijana kunasikitisha sana, hivi hakuna watu waliojaribu kumshawishi hatari ya alichokuwa anakifanya?... hata chama chake hakikuona hiyo hatari?
Bahati mbaya ukishakuwa mwenyekiti wa CCM, and above all President, hakuna wa kukuhoji, unageuka kama mungu mtu.
 
We unasema Phd ? G.P.A nyingi ni za kustruggle kwa kukesha usiku na za kupewa tu.

Wakati nachukua Masters yangu chuo (unknown) kuna siku kulikuwa na UE. Basi nikawakuta wadada wazuri wanajisomea nikawatania, 'Jamani sijasoma hata kidogo jana nilikuwa maji' Wakanicheka, kisha wakanipa maswali 5 nijisomee. Aisee kuingia kwenye pepa nayaona yote. Nikaupelekea moto huo mtihani vizuri nikalamba A+

Nilijitafakari sana. Kumbe wengine wanajua ya leo na ya kesho. Mambo ya chuo yana siri nyingi jamani bora tuyaache tu.

Muacheni mzee wetu Magu apumzike
 
Mtu ambaye aliiba PhD tunamzungumzia kwenye maeneo yote. Alianza kwa kuiba elimu na kufanya udanganyifu ambao ukaendelea na kuwa udanganyifu wa chanzo cha fedha za miradi ya serikali na hatimaye ikawa wizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa na ule mkuu wa 2020.

Mtu huyu akawa hataki tena kufuata sheria wala katiba. Akaendelea mbele na kutaka kuendesha nchi kwa matamko. Akawa anatoa maelekezo kwa spika na jaji mkuu. Chanzo cha yote ni elimu feki aliyoiba.
 
Mkuu tunaomba wewe na hao wadada mripoti sentro kesho asubuhi mkiwa na hizo masters mkononi.🤣🤣
 
Una mihemko sana, na nilishakuona toka mwanzo; naona sasa umeshajigeuza judge na kuamua kwamba Magufuli aliiba PhD.

Wakati kule juu uzi wako uliuanzisha kama tetesi, nakuona hujielewi, g9t..!!
 
Una mihemko sana, na nilishakuona toka mwanzo; naona sasa umeshajigeuza judge na kuamua kwamba Magufuli aliiba PhD.

Wakati kule juu uzi wako uliuanzisha kama tetesi, nakuona hujielewi, g9t..!!
Mrudisheni Ben Saanane kwanza ndio tutakuwa na uhakika kwamba PhD sio fake.

Halafu mimi nakusamehe kwa personal attacks zako.
 
Mrudisheni Ben Saanane kwanza ndio tutakuwa na uhakika kwamba PhD sio fake.

Halafu mimi nakusamehe kwa personal attacks zako.
Nakuona tena unatafuta "public sympathy" ili kutafuta uungwaji mkono wa hoja yako nyepesi uliyoianzisha kama tetesi.

Narudia tena, suala la PhD ya Magufuli kuwa fake, au kutokuwa fake, halina uhusiano wowote na kupotea kwa Ben. Nimeshakuonesha kule juu tabia za Magufuli ambazo ziliwa-cost wengi waliokwenda kinyume nae, lakini unajidai hutaki kuelewa.

Hakuna personal attacks hapo, jisome maandiko yako yalivyo ujitambue, nimekwambia una chuki na hasira nikiwa na sababu, coz unatumia theory za kufikirika kufanya judgement which to me is unfair.

Mfano unaandika PhD ya Magufuli is fake, but kule juu umeandika tetesi, which is which...?! basi kama una ushahidi wa ufeki wa PhD ya Magufuli tuwekee hapa tuione na sababu zako tumalize mjadala.

Lakini sio kusema tu muda aliotumia ulikuwa mfupi, au wengine sijui nini ..... kwangu mimi, mtu yeyote anayejitambua hawezi kutumia sababu za jumla kuhukumu kitu specific, kwasababu vitu hutofautiana, sijui unanielewa?!

Haya mambo naona yamekuzidi kimo, huujui udhaifu wako wewe unauona strength, na bahati nzuri kwako kuna wenye mihemko ya kishabiki kama yako huku watakuunga mkono, lakini wewe bado sana.
 
Anangisye pia ana familia inamtegwmea.wakimpoteza nazina utamtunzia familia
 
Kwa
Kwa uwezo alikuwa nao JPM nadhani hata huo Udactari hamtoshi alipaswa awe professor kabisa
 
PhD ya Magufuli ni FEKERO, hilo hakuna ubishi. Wenyewe UDSM wameitoa kwenye maktaba, nakushangaa wewe unakomaa kusema mchapakazi.

Hivi unajuwa Haiba za wezi na mafisadi? Hujifanya wachapakazi na watu wa kukemea wenzao. Endelea kuamini upuuzi kuwa Magufuli alijuwa mchapa kazi wakati alikuwa anafunika wizi wake
 
Nakushagaa pia unavyolazimisha bila ushahidi, mleta mada anawapenda kama wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…