Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

SEHEMU YA 47



Wote wale sita walikuwa wamevaa nguo zilizochafuka. Wawili wao walivaa viatu vya mpira na wengine walikuwa miguu wazi. Hii ilikuwa ni ajabu kubwa kwa Kijakazi. Maisha yake yote, tangu uhai wa Bwana Malik, hakupata kuona watu kama wale wakiingia ukumbini mle mlimopambwa kwa mapambo ya kila aina. Miguu ya wale watu ililichafua lile zulia zuri lililotandikwa juu ya sakafu ya ukumbi huo.

Baada ya kukaa vitini wale wageni wasiojulikana kwa yule waliyemtembelea, kwanza walitazamana na mara mmoja wao akaanza kusema.

“Nafikiri unaelewa kuhusu sheria mpya ya ardhi?”

“Sheria ya ardhi? Sheria gani?” Fuad aliuliza huku roho ikimwenda mbio.

“Sheria inayosema kwamba ardhi yote ni mali ya serikali.”

“Naam! Nimeisikia, Bwana!” Fuad alijibu, wakati umemgeukia na sasa naye anajua kuita ‘Bwana’.

“Basi sisi tumekuja kukujuvya kwamba, ijapokuwa wewe mwenyewe utakuwepo hapa, inakupasa ujue kwamba ardhi yote ile iliyokuwa chini ya milki yako ni mali ya serikali. Kwa hivi sasa unaweza kuendelea na kazi zako mpaka tutakapokuletea taarifa nyingine,” alieleza yule mtu.

“Nimesikia, Bwana! Nimesikia!”

“Basi sisi tumekuja kukuarifu tu tunakwenda zeut.”

Wale watu walitoka na kuingia ndani ya magari yao wakaondoka.

Baada ya kuondoka tu. Fuad alitoka nJe ya nyumba. yake amekasirika sana, uso umemwiva mwekundu kama papai akinung’unika peke yake.

“Wezi wakubwa!” alijisemea.

Ilikuwa wakati wa asubuhi kiasi ya saa nne. Kijakazi alikuwa anafagia uwanja ulioko mbele ya jumba la Fuad. Fuad alikuwa chumbani mwake amelala na mara ilifika gari moja mbele ya nyumba yake.

Ilikuwa ni moja katika zile gari mbili zilizokuja siku ile. Baada ya kufika tu gari hiyo, alishuka mtu mmoja na kumwuliza Kijakazi, “Fuad tumemkuta?”

“Bwana? Si ... sijui, ngojea nikamtazame ndani.” Kijakazi alijibu.

Fuad aliyekuwapo chumbani mwake alimsikia yule mtu alipokuwa akiuliza na mara alitoka nje mbio.

“Nipo! Nipo Bwana! Je mnataka kuonana na mimi?” Fuad aliuliza huku akijifunga vizuri kikoi cha Jabir alichokuwa amevaa wakati ule.

“Tuna haja ya kuonana na wewe kidogo,” alisema yule mtu.

“Karibuni, piteni ndani!” Fuad alijibu huku akijidai kucheka kama mtu aliyefurahi kweli kufikiwa na wageni wale.

Watu wengine wawili waliteremka kutoka kwenye lile gari na wote watatu waliingia ukumbini kwa Fuad pamoja na Fuad mwenyewe.

Kijakazi hakuwa mbali na aliweza kusikia wazi wazi yaliyokuwa yakizungumzwa.

“Je, khabari za toka siku ile?” aliuliza mmoja wa wageni wale.

“Nzuri! Nzuri Bwana!” Fuad alijibu.

“Tumekuja kuonana na wewe kuhusu ile habari tuliyozungumza siku ile. Je unakumbuka tulizungumza nini?”

“Nakmbuka! Nakumbuka vizuri!”
 
SEHEMU YA 48



“Basi tunapenda kukueleza hivi,” alianza yule kijana, “kama unavyojua, serikali ya Ki-Sultani tumeipindua na siasa ya serikali ya kimapinduzi ni kujenga ujamaa. Tunajua kwamba hiki ni kitu kipya kwako ambacho hukupata hata kukisikia. Au je, unaelewa maana ya ujamaa?”

“Sielewi, Bwana, na itakuwa vizuri ukinifahamisha!” Fuad alijibu.

“Hayo ndiyo madhumuni ya kaja hapa,” aliendelca yule kijana. “Sisi tutakuzungumza wewe kuhusu ardhi tu. Siku ile tulikwambia kwamba ardhi yote imechukuliwa na serikali lakini hii baina maana kuwa ardhi ni ya serikali tu, basi. La! Ardhi ni ya serikali lakini itagawiwa miongoni mwa wakulima. Katika sehemu nyingine jambo hili limekwishatendeka na sasa ni zamu ya sehemu hii. Kila mkulima anayeishi katika eneo hili atagawiwa ardhi na baada ya hapo kuna mipango ya kuanzisha ukulima wa kijamaa, yaani kuanzisha mashamba ya ushirika. Maana yake m kwamba shamba lako pia itabidi ligawiwe na wewe mwenyewe utapewa sehemu yako ili nawe uwe na kitu cha kukuendeshea maisha yako. Utapatiwa ardhi inayokutosha, lakini itakubidi uilime wewe mwenyewe kwani hutapata mtu wa kukutumikia tena.”

“Mimi niko tayari! Niko tayari kabisa! Wako majirani hapa naweza kushirikiana nao katika kazi kama hiyo. Wapo akina Pandu, Haji, Makame na majirani wengine chungu nzima ambao naweza kushirikiana nao. Mimi mwenyewe nitafanya kazi bila shaka; kwani nyinyi mnafikiri mimi siwezi kushika jembe?. Naliweza vizuri” Fuad alisema huku akijidai kucheka na kufanya masihara.

Kutoka alipokuwa amesimama Kijakazi aliyasikia vizuri yaliyokuwa yakizungumzwa, lakini hakuna alichokielewa Mambo ya ujamaa hakuyaelewa hata kidogo. Aliona yote yale hayakumhusu yeye. Jambo lililomshangaza ilikuwa kule kumsikia Fuad akiwataja watu kama Pandu, Haji na Makame - kama majirani zake; watu ambao, hapo zamani, hakuwa na mahusiano nao yo yote. Watu hao walikuwa wakiishi hapo Koani lakini walikuwa m katika mafukara wa kutupwa.

Baada ya mazungumzo yao kumalizika wale watu walitoka nje wakaingia ndani ya gari lao na kuondoka. Kama kawaida baada ya kuondoka tu, Fuad alikuwa mkali kama moto.

Siku nyingi zilipita; Kijakazi hakujua kinatokea nini pale walipokuwa na katika nchi kwa jumla. Taabu na wasiwasi wake ilikuwa kule kumwona Bwana wake alivyokasirika siku wale watu walipokuja.

Siku moja Kijakazi alikuwa amekaa peke yake chini ya mti nyuma ya nyumba ya Fuad. Hapo alianza kujiuliza maswali, “Jamani huu ujamaa ndiyo nini hasa? Hawa watu wanataka nini hasa kwa Bwana Fuad. Haweshi kuja kumkera maskini.”

Ijapokuwa hakuweza kupata jawabu lo lote katika maswala aliyokuwa akijiuliza, alitia shaka kwamba lazima kuna jambo linataka kutendeka.

Vuguvugu la mapinduzi ya kumiliki ardhi lilianza kutapakaa katika kila sehemu ya Unguja. Mabwana sbamba walishikwa na wasiwasi mkubwa. Kila njia za kutaka kuharibu mipango ya serikali ya kimapinduzi walizifanya.

Fuad alikuwa amekaa ukumbini pamoja na mabwana shamba wengine watatu ambao walikuja kumtembelea siku ile, Khalfan, Swelum na Khator.

“Hapa pako washakuja?” Khator aliuliza.

“Washakuja! Ati wanataka kuligawa shamba langu madhalim wale!” Fuad alijibu hamaki zimemjaa moyoni mwake.

“Hata mimi walipokuja shambani kwangu walinambia maneno hayo hayo! Hawa watu wana wazimu? Hawajui kama ni dhambi kubwa kumnyang’anya mtu mali yake?” Swelem naye aliingia kati.

“Ati wanataka kujenga ujamaa; ujamaa, ujamaa, hawana lao moja wanaloliweza hawa!” Khalfani naye alisema.

Mazungumzo baina ya Fuad na mabwana shamba wenzake yalichukua muda mrefu na baada ya kuzungumza kila mmoja alishika njia na kwenda zake.
 
SEHEMU YA 49



Kila siku iliyopita, wasiwasi ulimzidi Fuad. Kijakazi aliyaona haya na mara alikuwa akimwona Fuad akificha vitu. Mara humwona akificha mbatata, mara akificha sukari, mara akificha vitunguu. Almuradi alikuwa ni mtu aliyejaa wasiwasi.

Kijakazi hakuweza kuelewa nani aliyekuwa akifichwa vitu hivi lakini alihisi kama kuna maadui kutoka mbali wanataka kumnyang’anya Fuad shamba lake zuri. Tena alihisi kuwa maadui hao ni watu wenye nguvu. Alistaajabu kuona hakuambiwa chochote kuhusu mambo yaliyokuwa yakitokea lakini aliamini kwamba huu ujamaa na kuishi kijamaa ni mambo ya laana kubwa kwa vile alivyomwona Fuad akighadhibika anapozungumza habari hiyo......

Ilikuwa wakati wa jioni, Fuad ametoa kiti chake cha kulala uwanjani mbele ya nyumba yake anapunga upepo. Alikuwa akivuta sigara moja baada ya moja huku kichwa chake kinatazama juu. Mara alipita Mkongwe. Alipomwona tu, Fuad hakuweza kujizuia na mara alimwita.

“Mkongwe hebu njoo nikwambie!”

“Unambie nini?” Mkongwe aliuliza.

“Wewe njoo tu halafu utasikia nini nataka kukwambia!” Fuad alisema huku sigara yake iko mkononi.

“Usinishughulishe mimi, sasa hivi n’na kazi,” Mkongwe alijibu.

‘Njoo mara moja tu,” Fuad alimwomba Mkongwe.

“Eh! Husikii nakwambia n’na kazi; sitaki basi!” Mkongwe alijibu na hapo hapo alielekea kule kwenye banda la ng’ombe na kwenda zake.

“He! Hata Mkongwe naye siku hizi amekuwa jeuri. Ama kweli mambo yamebadilika!” Fuad alisema peke yake huku amej nyosha juu ya kile kiti cha kulala.

Mkongwe alikuwa hashughuliki tena na kazi. Alikuwa akipuuza kila kitu. Hata huyo Fuad alikuwa hampi heshima kama ile heshima anayotaka apewe - heshima ya bwana shamba mwenye kumiliki ardhi na kila kinachoishi katika ardhi hiyo, tokea mimea mpaka watu. Yeye al’elewa vizuri nini kinatokea kwani Umari alikwisha mdokeza kuhusu mipango mipya ya serikali ya kimapinduzi.

Wafanyakazi wa shambani kwa Fuad walikuwa wakisubiri tu lini wao watagaiwa ardhi ili wao pia wapate kuishi kijamaa kwani hii ilikuwa ndio njia ya pekee itakayoweza kuwaokoa kutoka katika ule unyonge waliokuwa nao kwa muda mrefu.

Fuad alimtilia shaka kila mfanyakazi katika shamba lake kwani siku hizo hakuna tena hata mmoja aliyemjali.

Mabwana shamba kutoka sehemu mbalimbali waliendelea kuja kumtembelea Fuad. Walikuja kutaka nasaha lakini hakuna aliyeweza kutoa nasaha zo zote kwa mwenzake, na kwa hiyo, mazungumzo yao yalikuwa ni yale yale ya kulaani ujamaa na kuutemea mate chini. Waliwaita wakuu wa serikali mpya kila jina baya, wajinga, wahuni watu wasiosoma, wezi na kadhalika.

Wajumbe wa serikali ya kimapinduzi walikuja tena kuonana na Fuad. Kama kawaida, Fuad aliwakaribisha ukumbini na mara hii aliwatengenezea kahawa. Alitoa pakti ya sigara na kuizungusha duru na kila aliyekuwa mvutaji alichukua moja. Mazungumzo yalikuwa yale yale - ardhi - kilio cha wakulima kwa miaka. IIlkuwa ni siku ya, furaha kwa wafanyakazi wa shambani kwa Fuad kwani kila walipokuja wajumbe wale, wafanyakazi hao walikuwa wakifurahi sana wakiwa na matumaini ya kukombolewa kutokana na mateso ya siku zote za nyuma.

Kinyume na wafanyakazi wenzake, Kijakazi alikuwa akielemewa na unyonge mkubwa alipowaona watu wale ambao hakujua walitoka wapi au walitaka nini. Alihisi walimlctea bwana wake kero na hili hakulipenda. Alipowaona wale watu alikuwa akizunguka huku na kule akitafuta kazi ya kufanya karibu na ukumbi wa nyumba ya Fuad ili alau asikie nini kinazungumzwa.
 
SEHEMU YA 50

Katika kupitapita pale alisikia sauti ya mmoja wa wale wageni ikisema,

“Sasa Fuad unasemaje? Sisi tumekwisha anzisha kilimo cha pamoja, na tunataka kukiendeleza mpaka sehemu hii ya shamba lako.”

“Fikra nzuri!” Fuad aliruka na kusema. “Mimi nakubaliana moja kwa moja na fikra hizo. Najua vizuri kwamba hilo ni jambo zuri na naliunga mkono kwa moyo wangu wote. Niko tayari kabisa kuishi kijamaa.”

Hiyo ilikuwa ni sauti ya Fuad na Kijakazi aliweza kuitambua hata kama ingelikuwa miongoni mwa sauti elfu nyinginezo. Kijakazi alisita hapo chini ya dirisha ili aweze kusikia zaidi yaliyokuwa yakizungumzwa. Aliyoyasikia yalikuwa ni maneno ya ajabu. Hakupata kumsikia Fuad hata siku moja kusema kwamba yeye anataka kuishi kijamaa. Alilojua yeye m kwamba hao waliozungumza habari hizo za kuishi kijamaa ni makafiri wakubwa na ilikuwa ni mara yake ya kwanza kusikia Fuad akisema maneno kama yale.

“Hivyo haya maneno aliyoyasema Bwana mimi nimeyasikia vizuri au masikio yangu yananidanganya? Au huyu Bwana, masikini, amekwishatekwa akili na hawa watu wanaokuja hapa?”

Kijakazi alisimama kusikiliza zaidi mazungumzo yale yaliyomshitua.

“Si muhimu ikiwa wewe unaunga mkono au huungi mkono, sisi tumekuja kukwambia tu ikiwa m katika mipango yetu, tusije tukafanya jambo halafu ukasema, ‘eh, wamefanya hivi wamefanya vile!” Mbaruku alisema.

Wenzaka wote walinyamaza kimya wakivuta sigara tu na kila walipomaliza basi Fuad alikuwa tayari kuwakaribisha nyingine.

Mbaruku aliendelea na mazungumzo yake na kusema, “Basi wapo vijana hapa, watoto wa wakulima, washaanza kazi hiyo ya kulima pamoja na wanaelekea huu upande wako, ukiona wamefika sehemu hii nd’o ujue tena, wamo kazini.”

Kijakazi aliyekuwa amejibanza pale dirishani alimsikia Fuad akisema tena, na mara hii kwa sauti ya juu zaidi.

“Vijana? Walete hapa kwangu, mimi nitawafahamisha kila kitu, mana’ke nankiri wao bado vijana hawana ujuzi wa kazi hizi za kulima.”

“Wao hawana haja ya kufundishwa kulima, wao ni wakulima tokea babu wa babu zao,” Mbaruku alisema.

“Sisi tunachotaka ni kwamba tutakapofika sehemu hii utuonyeshe kila kilichomo ndani ya shamba,” aliendelea Mbaruku.

“Msitie wasiwasi mimi nitakuonyesheni kila kitu na mimi mwenyewe nitachukua dhamana ya vitu hivyo!” Fuad alisema, amehamaki, lakini hawezi kuonyesha, akijidai kucheka anaposema kitu, ingawa ukweli ni kwamba hana kicheko. Joto la hamaki lilikuwa likifukuta ndani ya kiwiliwili chake na alikuwa akitoka kijasho chembamba ilhali ya kuwa upepo mzuri ulikuwa ukiingia ukumbini humo.

Mazungumzo ya Fuad na wale watu yalimshangaza Kijakazi na hasa yaliyomshangaza zaidi ni maneno ya bwana wake Fuad. Kule kusema kwa Fuad kwamba yuko tayari yeye mwenyewe kushiriki na kuwafunza hao vijana wakulima ilikuwa ajabu kubwa. Zamani watoto kama hao Fuad hakutaka hata kukaribiana nao acha kushirikiana nao na kuwafundisha cho chote. Kijakazi alifikiri labda bwana wake amepotelewa na akili.
 
SEHEMU YA 51



Mara Kijakazi alimsikia Fuad akiagana na wale watu naye akaondoka pale alipokuwa amejibanza.

“Basi mnaweza kuja siku yo yote ile, mimi mtanikuta tu hapa,” alisema Fuad alipokuwa anaagana na akina Mbaruku, amesimama mlangoni.

“Mambo makubwa haya!” Kijakazi alinong’ona peke yake, “Masikini Bwana! Lakini nafikiri atabadili fikra zake!”

Kwanza Kijakazi aliyaamini aliyoyasema Fuad kwa kuhisi kuwa akili zake zilikwisha tekwa. Lakini hakumwona na furaha yo yote na hii ilimfanya awe na wasi wasi kwamba huenda Fuad anayasema yale kwa kuzidiwa nguvu. Kila alipofikiri hivyo alifurahi kidogo kwani hakutaka Fuad achanganyike na watu wale.

Baada ya kwisha kuagana na akina Mbaruku Fuad alibaki pale pale mlangoni jasho linamtoka, hamaki zimemjaa. Mara Kijakazi alipita na mtungi kichwani anaelekea kisimam kuteka maji. Kumwona tu, mnyonge wake alianza kumfokea kama kwamba yeye ndiye aliyefanya mapinduzi.

“We, wewe, kazana! Unakwenda kama huna miguu! Kwanza nani aliyekutuma maji? Basi kazi kwenda kuchezea maji tu huko kisimani?”

“Nakwenda kuwapa ng’ombe maji haya!” Kijakazi alijibu.

Kwa kweli Fuad hakuwa na haja yo yote ya kumhimiza Kijakazi lakini hakuwa na mwingine ye yote wa kuweza kumhamakia isipokuwa yeye tu. Kijakazi alikaza mwendo na kwa ajili ya uzee wake atikuwa akiyumba njiani ungedhani ataanguka wakati wo wote.

Fuad hakuwa na la kufanya. Hakuwa na njia yo yote ya kuyazuia yaliyokuwa yakitokea. Kila siku akisikia matangazo ya mapinduzi katika redio, matangazo ya kuohukuliwa mali za mabepari, kudhibiti biashara ya nje na ya ndani na matangazo mengine mengi ambayo yalidhamiria kuzuia kabisa unyonyaji wa mabepari na mabwana shamba. Yeye hakuwa na la kusema isipokuwa kulaani na kutukana tu na hayo hayakumsaidia cho chote. Kila siku hatua zaidi za kimapinduzl zilichukuliwa.

Siku nyingi kidogo zilipita kabla ya Fuad kusikia. cho chote kuhusu ile mipango aliyoambiwa na Mbaruku. Jambo hili lilimpa moyo mkubwa akifikiri yamekwisha au labda wale watu wamemsahau.

Halafu bila ya kutumaini, siku moja aliona watu wawili waliovaa nguo zilizochakaa wakija nyumbani kwake. Alipowaona tu alinong’ona peke yake, “Hao washakuja tena, sijui wanataka nini? Mungu awashinde!”

Lakini mara aliigeuza sura yake iliyokuwa imekasirika. na kujifanya kama aliyefurahi kuwaona.

“Je, nini khabari za siku nying’? Naona mmenitupa siku hlzi hamnipiti kabisa?” Fuad aliuliza.

Wale watu hawakutaka kujijulisha, na Fuad mwenyewe alikwisha tambua wanapokuja wageni kwake huwa wametoka wapi.

Fuad aliamkiana na wale watu na kuwapa mkono lakini wao hawakumwambia kitu cho chote. Mmoja wao alitia mkono mfukoni na kumpa barua. Fuad aliisoma ile barua na mara aliruka.

“Mnataka lile trakta? Kachukueni! Kachukueni! Hapana wasiwasi wo wote; tena ile ni mashine nzuri sana, mali ya M’ngereza ile!”

Fuad aliwachukua wale watu mpaka lilipokuwa lile trekta na mmoja katika wale watu wawili alilipanda na kulitia moto.

“Barabara!” alisema yule dereva.

Fuad alipeana mikono na wale watu wakaagana na hata aliwasindikiza kidogo, wao wakiwa juu ya trekta na yeye akitembea kwa miguu.

Kabla ya lile trekta halijafika njia kuu, Kijakazi ambaye umbea wa kutaka kujua nini hasa kinachotokea ulikuwa umemshika alimwona Fuad akirejea ameghadhibika. Aliivua kofla aliyokuwa ameivaa na kuitupa chini halafu akaikanyagakanyaga kwa miguu huku akisema kwa sauti kubwa,
 
SEHEMU YA 52


“Basi huu si wizi huu? Huu ni wizi dhahiri. Wanaiba kimacho macho!” Alipiga makelele huku akilaani na kutukana. Makelele yalikuwa makubwa hata ng’ombe waliokuwa wakila majani bandani walisituka.

Kijakazi hakujua lililokuwa likitokea. Alipigwa na mshangao kuona watu wanakuja na kuanza kuchukua vitu vya bwana wake. Lilikuwa trekta jipya alilonunua siku zile zile aliponunua liIe gari lake la aina ya Rambler.

Alisimama karibu ya Fuad na kukunja mikono yake huku akimwonea huruma. Puad alipomwona tu Kijakazi amemsimamia mbele yake alimrushia teke kali lakini Kijakazi alijirusha upande na teke hilo halikumpata. Hata hivyo, kwa ajili ya kutokuwa na nguvu kwake kuliko sababisbwa na utu uzima, Kijakazi alianguka chini lakini mara alijizoazoa na kusimama.

“Mbuzi we! Unataka nini hapa? Kwani huna kazi ya kufanya?” Fuad alimpigia makelele Kijakazi.

Kijakazi alijiburura hivyo hivyo, mbio na kukimbilia bandani kwa ng’ombe.

Kutoka pale, Fuad alifutuka moja kwa moja mpaka kwenye banda la matrekta na magari na alipofika hapo alisimama kati kati na kuanza kupiga kelele kama mtu aliyepandwa na wazimu, “Wezi wakubwa, wallahi ntayaharibu.” Alilitazama gari lake la kupelekea karafuu mjini ambalo kwa muda wa miezi miwili lilikuwa limelala kwa kukosa mipira ya nyuma.

Aliranda huku na buku halafu alisimama mbele ya trekta lake moja lililobakia, “Na hili hawalipati ng’o,” aliendelea kupiga kelele huku jasho linamtoka kwa hamaki zilizochanganyika na joto la bandani mle.

Alitazama huku huku na halafu alitoka bandani mle na kurejea nyumbani kwake na kuingia katika vyumba vyote kama mtu asiyejua la kufanya na mwisho aliingia ndani ya ghala yake ya chakula. Alifungua gunia la sukari na kuijaza sukari hiyo ndani ya kikapu tele, halafu akarejea tena kule kwenye banda la magari na kikapu chake cha sukari mkononi.

“Hawalipati; na hata wakilichukua litakuwa halina faida yoyote. kwao,” aliendelea kusema huku akifungua kifuniko cha tangi la petroli la gari lile. “Na atakayekuja kulitia moto injini itampasukia,” aliendelea huku akimimina ile sukari ndani ya tangi lile la petroli.

Fuad alimimina sukari nyingine ndani ya tangi la petroli la trekta halafu alifungua pale penye mashine na kukatakata waya.

Alipoondoka bandani hapo hakusimama mpaka bandani kwa ng’ombe na kufungua mlango kwa vishindo vikubwa na kumsitua Kijakazi ambaye alikuwa amekaa amejinamia, mnyonge, kama aliyefiwa na baba yake. “Toka mbele ya macho yangu kisirani mkubwa we!” Fuad alimpigia kelele, na baada ya ukelele huo Kijakazi aliinuka na kuanza kukimbia mbio huku akisepetuka na kushikilia viguzo asije akaanguka.

Bandani humo Fuad alianza kuvunjavunja mabao na vitu vingine na vishindo vilivyokuwamo bandani humo viliwasitua hata ng’ombe wakaanza kupiga kelele ovyo kama walioingiliwa na chui zizini mwao. Fuad aliangaza huku na huku na halafu aliuvuta ubao uliokuwa karibu naye na kushangaa nao mkononi halafu akamrembea nao ng’ombe mmoja na kumpigia kelele, “Na nyinyi nyote nitakufungulieni mtokomee huko mkatafute huo ujamaa wanaojenga ng’ombe wenzenu.”

Alipotoka bandani humo alifululiza mpaka nyumbani kwake, akajitupa chali juu ya kitanda huku akipumua kama mtu aliyeshikwa na ugonjwa wa pumu kwa ghafla. “Mungu atawalaani! Mungu atawashinda makafir hawa!” alipiga makelele.

Fuad tafrani zilimzidi. Asubuhi baada ya kwisha kunywa chai tu alivalia kwa safari ya mjin’. Alitia gari lake moto na kuondoka mbio. Hakusimama po pote mpaka Shangani kwa rafiki yake Nasoor. Alipofika nyumbani kwa Nassor hakushuka ndani ya gari ila alibakia humo humo na kupiga honi ya gari. Nassor, ambaye alijua vizuri sauti ya honi ya gari ya Fuad, alichungulia dirishani.

“Vaa twende!” Fuad aliamuru.
 
SEHEMU YA 53



“Wapi?” Nassor aliuliza.

“Twende zetu tukaupige!” Fuad alijibu.

Bila ya kuchelewa Nassor alival’a na waliondoka pamoja mpaka bar ya marikiti. Walipofika tu walianza kwa ‘vikali’. Hapakuwa na mazungumzo yo yote isipokuwa yale ya Fuad kutaka kuchukuliwa shamba lake. Ijapokuwa Fuad alikuwa na nishai, hakuweza kuzungumza kwa kelele kwa kuchelea asije akasikika akiisubu serikali ya kimapinduzi ambayo wananchi wote waliikaribisha kwa mikono miwili.

Walilewa mpaka usiku na walipomaliza walianza kutafuta panapo starehe.

“Sasa leo wapi?” Fuad aliuliza.

“People’s” Nassor alijibu.

“People’s nd’o wapi?” Aliuliza Fuad.

“Densini hapo Mnazimmoja!” Nassor alijibu.

“Densini? Twende zetu!” Fuad alisema.

Waliingia ndani ya gari mpaka mnazi mmoja hapo People’s Club.

Ndani humo mlikuwa na kivumbi. Mziki ulikuwa umekolea na wananchi walikuwa wakicheza densi huku nyoyo zao zimejaa furaha. Zamani fursa kama ile walikuwa hawawezi kuipata kwani kabla ya mapinduzi klabu ile ilikuwa m ya mabwenyenye tu; wafanyakazi na wakulima waliiona kwa nje tu. Wakati huo ilijulikana kwa jina la Karimjee Club. Baada ya mapinduzi jumba hilo zuri lilichukuliwa na serikali na pakawa ni pahala maarufu ambapo wafanyakazi na wakulima huenda kujipumzisha baada ya kazi.

Fuad hakupendezwa na mandhari ya humo ndani. Aliona waliomo humo wote ni kama wale watumishi wake ambao zamani akiwatuma kama anavyotaka yeye mwenyewe.

“Hawa wanajuaje kustarehe hawa? Mimi nakwenda zangu. Siwezi fujo kama hii!” Fuad alimwambia Nassor.

Alitoka nje peke yake na kumwacha Nassor anastarehe na mziki. Aliingia ndani ya gari lake na kuondoka. Alikuwa amelewa sana na alipofika hapo Mikunguni aliligonga gari kwenye mti. Katika ajali hiyo pale pale fahamu zikampotea.

Kijakazi alijawa na wasiwasi mkubwa. Siku zote Fuad al pokwenda mjini basi Kijakazi hakupata usingizi mpaka alipolisikia gari la Bwana wake limerudi. Lakini siku hiyo mpaka saa sita ya usiku Fuad alikuwa bado hajarudi. Alikaa, macho muda mrcfu lakini Fuad hakutokea.

“Sijui amefikwa na maafa gani maskini?” Kijakazi alijiuliza huku amekaa juu ya kitanda chake cha mayowe.

Kucha Kijakazi hakupata usingizi na kila usiku ulipozidi kuwa mwingi bila ya kumwona bwana wake wasiwasi ulimzidi. Alitoka usiku ule mpaka kibandani kwa Mkongwe na kubisha hodi.

“Mbona saa hizi, Kijakazi, kumezidi nini?” Mkongwe aliuliza.

“Bwana Fuad hajarudi mpaka saa hizi sijui amefikwa na nini” Kijakazi alisema kwa sauti ya unyonge.

“Na wewe nawe na Fuad wako? Mimi nikifikiri umefikwa na jambo gani sijui; kumbe hujalala mpaka saa hizi kwa sa’oabu Fuad hajarudi?”

“Maana yake si kawai...”
 
SEHEMU YA 54



Kabla Kijakazi hajamaliza kusema Mkongwe alimkatiza maneno yake na kusema:

“Sikiliza shoga; kama lililokuleta hapa ndilo hilo basi bora ondoka uniwache mimi nipumzike, mana’ake nimejichokea hapa niiipo.”

Kijakazi hakuwa na ‘a kusema. Aliondoka na kwenda zake, wasiwasi umemjaa.

Asubuhi iliingia, Fuad hakutokea. Kijakazi alikaa mbele ya mlango wa nyumba ya Fuad ameshika tama hajui la kufanya. Mara gari la hospitali liliingia na Kijakazi aliruka kutoka pale alipokaa. Kwa hakika hakujua ni gari gani lile alifikiri Fuad amenunua gari jingine kubwa zaidi lakini alishtushwa alipoona nyuma ya gari hilo ukifunguliwa mlango na watu wanne wakitoka na machera wamcmbeba Fuad.

“Jamani niwahini! Niwahini jamani! Masikini Bwana wangu!”

Kijakazi aliangusha kilio; alilia na huku akiomboleza kama mwanamke aliyefiwa na mumewe. Wafanyakazi wenzake wote walifika pale lakini hapana aliycouyesha majonzi wala huruma. Wote walikuwa wakimtazama Kijakazi alivyokuwa akimiminikwa na machozi.

Aliwaongoza wale waliochukua machera mpaka chumbani kwa Fuad na walipofika humo walimlaza juu ya kitanda.

“Usilie mama hakuumia sana,” mmoja katika wale waliokuwa wamechukua machera alimwambia Kijakazi. Alimbembeleza kidogo na baada ya kumwona yumo katika kupiga makelele tu alimpuuza. Waliingia ndani ya lile gari la hospitali na kurejea mjini.

Kijakazi alimwonea huruma Fuad mfano wa mama anavyomwonea huruma mtoto wake mchanga wakati akiwa mgonjwa. Kila Fuad alipoondoka na gari lake dua ya Kijakazi ilikuwa “Mungu mrejeshe salama” lakini leo amerejea hali ile, majeruhi.

Fuad aliumia kichwa na mguu wa kulia. Kichwa kilizungushiwa kitambaa cheupe na mguu ulikuwa ndani ya gamba la chokaa.

Ajali hii ilimlaza Fuad kitandani muda wa miezi miwili. Mguu ulianza kupona lakini Fuad alikuwa mkaidi hatulii; wakati mwingi alifanya mambo ya kitoto labda kwa ajili ya athari ya kichwa aliyoipata.

Siku moja jioni Kijakazi alikuwa anakwenda jikoni kuchukua kigongo cha kusukumia mkate. Fuad alikuwa chumbani amejinyosha kitandani na alipomwona Kijakazi alimwita bila ya kufikiri.

“Kijakazi! Kijakazi! Njoo unikande mguu!”

Fuad alionyesha mguu wake uliovikwa gamba la chokaa. Kijakazi alisita na kupigwa na mshangao. Alitazama chumbani kwa Fuad kwa hofu kwani hakupata hata siku moja kufikiri kwamba iko siku Fuad atamwita chumbani mwake.

“Kijakazi!” Fuad aliita tena kwa sauti ya upole, “nimekwambia uje unikande mguu.”

Kijakazi aliingia chumbani taratibu huku akinyemelea pale kitandani alipolala Fuad kama paka anavyomnyemelea panya anapotaka kumkamata.

“Na hebu usindike huo mlango!” Fuad aliamuru lakini si kwa hamaki kama kawaida yake.

Baada ya kuusindika mlango Kijakazi alikwenda mpaka penye pembe ya kitanda alipolala Fuad na kusimama hapo.

“Kaa! Kaa! Usiogope,” Fuad alimwambia Kijakazi.

Kijakazi alikaa pembeni mwa kitanda kwa hadhari kubwa huku akiupakata mguu wa Fuad uliokuwa ndani ya gamba la chokaa. Alianza kuukanda na kuutikisatikisa.

“Hivyo hivyo!” Fuad alisema kwa sauti ya chini.
 
SEHEMU YA 55



Kijakazi aliukanda na kuutikisa mguu wa Fuad kama mama anapombembeleza mtoto wake. Kijakazi alijiona amefanikiwa pakubwa kuitwa na Fuad kuja kumkanda mguu. Fursa kama hii hakuipata tokea alipokatazwa kumbeba Fuad na Bi. Maimuna wakati Fuad alipokuwa bado mdogo. Kijakazi aliukumbatia mguu wa Fuad huku furaha imemjaa moyoni. Aliona kama anambembeleza mtoto na huku mtoto huyo anapata usingizi kidogo kidogo.

Kijakazi aliukanda mguu wa Fuad kama alivyoweza. Alijikusanya nyuma akawa mdogo mwisho wa uwezo wake.

“Ah! Kijakazi” Fuad alianza kusema kwa sauti ya mtu aliyekuwa akiona raha kwa kukandwa, “Tokea leo wewe ndiye utakayekuwa mwuguzaji wa mguu wangu. Wewe ni bora kuliko daktari yo yote yule; wewe cdie ulicnilea nilipokuwa mdogo,” Fuad alisema huku Kijakazi amelikumbatia guu lake.

“Hayo ni kweli Bwana,” Kijakazi alijibu mbio mbio huku machozi yanammiminika kwa huruma aliyokuwa nayo kwa Bwana wake. “Muni nimekulea tokea udogo wako na ilikuwa ni mimi tu niliyeweza kukunyamazisha wakati unapoanza kulia, hapana mtu yo yote aliyeweza kufanya hivyo; hata mama yako Bi. Maimuna alikuwa akishindwa kukunyamazisha. Ulikuwa kitoto kizuri,” Kijakazi aliendelea kusema.

“Haya Kijakazi, wewe ni mtumishi wangu mtiifu. Nyimbo gani vile ulikuwa ukiniimbia nilipokuwa mdogo?” Fuad alimwuliza Kijakazi.

“Hebu niimbie kidogo,” Fuad alimwomba Kijakazi.

Kijakazi alipata furaha kubwa kuambiwa maneno kama yale na Fuad, hakupala hata siku moja kuambiwa maneno kama yale. Alihisi kazi yake ya utiifu kwa Bwana wake ilikuwa si ya bure kwani Bwana leo amcfurahi naye, na kumwambia kwamba ni mtumishi mtiifu. Alipata furaha isiyokuwa na mfano.

“Bwana! Sijui kama nitaweza kuimba kama nilivyokuwa nikikuimbia!” Kijakazi alijibu huku akiogopa, bado ameupakata mguu wa Fuad.

Mara Kijakazi alianza kuimba kwa sauti yakc nenc yenye kukwaruza kama debe bovu na Fuad alionyesha kufurahi. Kijakazi aliona kama anaota kwa furaha aliyokuwa nayo. Aliendelea kuimba:

Lala mtoto tala, katika kitanda lala,
baba ni mtukufu, mama ni mtukufu,
Lala mtoto lala, katika kitanda lala...
“Funga mdomo wako!” mara Fuad upole aliokuwa nao ulimwisha. “Sauti kama ng’ombe! Unatikiri huo ndio wimbo uliokuwa uldniimbia?” Kwa hamaki Fuad aliuliza.

“Huu ndio ule wimbo Bwana! Huu ndio wimbo uliokuwa ukiutaka kila siku! Huu ndio wimbo niliokuwa nikikuimbia; ndio uliokuwa mzuri kuliko zote, nina hakika nasema kweli!” Kijakazi alijibu huku akitetemeka kwa hofu kwa kumkera Bwana na pia akiogopa asije akamtonesha mguu wake kwa kutetemeka kwake.

“Sitaki kusikiliza sauti yako mbovu! Hufai pesa moja! Washenzi wale wananikera na wewe huwezi kuniliwaza hata kwa kuimba tu! Toka hapa! Mungu akulaanini nyote!” Fuad alipiga kelele huku akitaka kuinuka lakini alishindwa.

“Itanibidi niondoke Bwana?” Kijakazi aliuiiza kwa hofu akijihisi amefanya makosa makubwa.

“Ondoka! Toka nenda zako!” Fuad alipiga kelele.

Kijakazi aliulaza mguu wa Fuad uliokuwa na maumivu juu ya kitanda kwa hadhari kubwa halafu akasimama.

“Haya toka hapa nenda kawape ng’ombe maji! Upesi” Fuad alisema.

Kijakazi alitoka chumbani mle mbio huku akishusha pumzi.

Kijakazi alikwenda bandani kwa ng’ombe na kuwapa maji kama alivyoamrishwa na Fuad.

“Ah! N’nastahili haya!” Kijakazi alisema peke yake huku anawapa maji ng’ombe. Alihisi anastahili yale kwa kutaka makubwa.

Hazikupita siku nyingi, Fuad alimwita tena Kijakazi chumbani. Mara hii Fuad alikuwa amekaa juu ya kitarida huku ameegemea mto uliokuwa nyuma ya mabega yakc. Kijakazi, kama mara ya kwanza, alikwenda na kuketi pembeni mwa kitanda huku akiunyanyua mguu wa Fuad kwa hadhari kubwa na kuuweka taratibu juu ya mapaja yake. Kijakazi alimtazama Fuad kwa macho makali kama kwamba ndiyo kwanza amwone.

Kijakazi alikuwa ameupakata mguu wa Fuad anaukanda na mara Fuad alianza kumsaili.

“Hebu niambie Kijakazi,” alianza, “unaionaje dunia ya leo? Unayaonaje haya mambo mapya ya siku hizi?”

Kijakazi hakujua nini la kujibu kwani yeye hakuwa na lo lote alilolijua. Aliogopa hata kusema asije akafurushwa kama mara ya kwanza. Alijibabaisha na kujidai kumkanda Fuad mguu huku akiimba:
 
SEHEMU YA 56


“Lala mtoto lala; lala mtoto lala ...”
“Ebo! Mimi nasema na wewe, unaniona kama mwenda wazimu? Nakuuliza haya mambo unayapenda au huyapendi?” Kwa hamaki Fuad aliuliza tena.

“N-n-nayapenda Bwana! Nashukuru kwa yote!” Kijakazi alijibu.

“Unasemaje?” Fuad alimkodolea macho Kijakazi “Wewe unawapenda wale wahuni wale! Washenzi wale! Wezi! Wajinga! Unayapenda mambo wanayoyafanya makafiri wale? Oh! Hivyo na wewe pia uko pamoja nao?” Fuad alitoa maneno kwa hamaki kubwa.

Kijakazi alibabaika; hakujua aseme nini kwani alikuwa hata hakufahamu aliulizwa nini na Fuad. Hakuyaelewa hayo mambo mapya aliyoulizwa na Fuad. Kichwa kilimduru na mara alisema.

“Sijui unakusudia nini Bwana! Mimi mambo haya siyaelewi!”

Kijakazi khofu ilimshika; alikuwa akitetemeka.

“Naona sasa wewe ushakuwa unashirikiana nao wale, eh? Sikujua kama nilikuwa mkimlea nyoka ndani ya nyumba yangu!’’ Fuad alipiga kelele.

“Ah! Bwana wangu! Mimi nimemtumikia baba yako kwa utiifu kabisa na nitakutumikia wewe vile vile kikomo cha uwezo wangu.” Kijakazi alisema huku akila viapo.

Mara Fuad alikunja matao ya chini na kuanza kuzungumza na Kijakazi kwa upole, “sikiliza Kijakazi, sherti ujue kama sisi tunakuona kama wewe m mmoja wetu ndani ya nyumba hii, wewe ni kama bibi yangu, ni sawa sawa na ye yote katika ukoo wangu. Wewe wakati wote ulikuwa mtumisbi mtiifu. Kijakazi sherti ufahamu kwamba wewe ni kama mzee wangu kwani wewe ndiye uliyenilea. Nakuahidi kwamba utakapofariki nitakufanyia mazishi makubwa yasiyowahi kufanywa hapa Koani, nami nakwambia wazi wazi kama wewe umekuwa kama mama yangu wa pili.”

Kijakazi alikuwa ameshughulika kuukanda mguu wa Fuad huku akimsikiliza kwa makini.

Fuad aliendelea na manemo yake na kusema, “Lakini sikiliza Kijakazi, hawa washenzi hawa, mijitu hii siku hizi imekuwa kama mizimwi. Ati hivi vijitu vifukara katika kijiji hiki vimejikusanya na ati vinajidai vinataka kuanzisha kilimo cha pamoja na kuishi kijamaa! Unafikiri vijitu hivi, visivyojua kitu, vinaweza kufanya kitu cho chote. Wao kila wakija hapa wananiletea haban za kutaka kulichukua shamba langu. ati nijiunge pamoja na vijitu vile. Wao hawaelewi jambo moja; wanafikiri wanauhodari kuliko mimi Fuad, Fuad bin Malik.”

Fuad aliendelea kuropoka, akiutukana na kuufanyia stihizai mpango wa ujamaa na serikali ya mapinduzi.

Alisita kidogo na kutikisa kichwa akaendelea kusema:

“Sikiliza Kijakazi: mimi nakwambia yote haya kwa sababu nakuamim. Tena kitu kimoja; napenda kukutahadharisha na Mkongwe. Tafadhali siku hizi usichanganyike naye. Usichanganyike naye hata kidogo kwani yeye amekwisha tutoka na karibu namwona atatukimbia hapa nyumbani. Siku hizi amezidi, hafanyi kazi, amekuwa mvivu kama kunguni na amekuwa mjeuri. Hana adabu tena. Juzi nilimwita na mara alinitolea ujuvi; lakini mwache aondoke. Atakapoondoka itakubidi wewe Kijakazi ufanye kazi zaidi.”

Kijakazi aliyasikia maneno ya Fuad kwa mbali na wakati Fuad alipokuwa akisema Kijakazi hakuamini kwamba maneno hayo alikuwa akiambiwa yeye. Kijakazi alianza kujiuliza.

“Amesema nini vile? Mimi ni sawa sawa na mama yake wa pili? Vipi vile? Mimi ni sawa sawa na yo yote ndani ya nyumba hii. Oh! Bwana amenambia maneno mazuri leo, haijambo kazi yangu si ya bure. Sasa nitafanya kazi zaidi ili bwana afurahi na m’mi zaidi.”

Kijakazi aliendelea kumkanda mguu Fuad mpaka akapata usingizi na baada ya hapo aliulaza mguu huo taralibu juu ya kitanda. Alitoka nje na kuufunga mlango akamwacha Fuad amelala.

Siku ya pili ilifika na Kijakazi alitamani aitwe na Fuad kwenda kumkanda mguu ili amsikie akisema kuwa amekuwa kama mama yake wa pili. Maneno haya yalimpa Kijakazi furaha maalum. Lakini siku ile ilipita, kesho ikapita, leo ilikuwa jana, na jana ikawa juzi, na taratibu siku zilipita bila ya Kijakazi kuitwa tena kwenda kuuguza mguu wa Fuad.

Kijakazi alikuwa amejinyosha juu ya kitanda cha mayowe na ghafla Mkongwe akaingia chumbani kwake. Kwa namna Mkongwe alivyoingia ilikuwa dhahiri alikuwa na kitu muhimu alichotaka kumwambia Kijakazi. Mkongwe alikuwa amechukua kifurushi chepesi mkononi mwake.
 
SEHEMU YA 57



“Nimekuja kukuaga Kijakazi. Nimekata shauri kuacha kazi na kesho asubuhi naondoka hapa. Nimechoka kutumwa na kusumbuliwa na Fuad. Mtu huyu hana wema wala ihsani. Hata fadhila na mtovu wa adabu. Roho yangu imechoka, nakwenda zangu.”

“Unakwenda wapi mwanangu? Umekaa hapa huna wasiwasi wo wote. Unataka kwenda wapi?” Kijakazi aliuliza.

“Sina wasiwasi? N’na wasiwasi, tena wasiwasi mkubwa.”

“Wasiwasi gani ulio nao, mwanangu?”

“Naujua mwenyewe,” Mkongwe alijibu.

Pale pale Kijakazi aliyakumbuka maneno ya Fuad aliyomwambia kuhusu Mkongwe kama sasa amekuwa haaminiki na anaweza kuondoka saa yo yote ile. Aliyaona maneno ya Fuad yote ni ya kweli, sio kuhusu Mkongwc tu bali yote aliyoambiwa na Fuad kuhusu wale watu na mipango yao mipya.

Kijakazi alimkodolea macho Mkongwe na kumtazama na, mara alimwambia, “Mkongwe, nakuomba usiondoke; usiwafuate wale wabaya!”

“Nani hao walo wabaya?” Mkongwe aliuliza.

“Wale watu wanaokuja hapa kila wakati kumkera Bwana!”

“Wale?” Mkongwe alisema, “Wale watu wazuri sana, tena nawaombea dua Mungu awasaidie katika wanayotaka kuyafanya. Nani aliyekwambia kama wale ni watu wabaya?”

“Bwana. Bwana Fuad, ameniambia kuwa wale ni wahuni, wezi na makafiri.”

“Wale si wezi si wahuni. Wale ni watu na heshima zao, tena wana heshima kuliko huyo Fuad wako. Fuad ndiye mwizi, mwizi wa nguvu za watu, mtovu wa adabu tena hana heshima hata kidogo. Katuweka hapa anatutuma kama ng’ombe na hatuna lo lote tunalolipata kutoka kwake!” Mkongwe alisema huku hamaki zimemjaa.

“Oh! Mkongwe unasema hivyo mwanangu? Unamwita Bwana hivyo?”

“Ndiyo namwita mwizi, mtovu wa adabu, hana wema wala ihsani. Na wewe Kijakazi utakuja kukubaliana na mimi siku moja kama utakuwa bai!”

“Basi unanikimbia Mkongwe mwanangu? Sasa kazi zote zitanielemea mimi; nitakuwa sina wa kunisaidia,” Kijakazi alisema huku akipumua kama mtu aliyekimbia masafa marefu. Mara Kijakazi alianza kusema tena kumnasihi Mkongwe:

“Lakini, Mkongwe, unaelewa unalolifanya? Umefikiri vizuri kabla ya kukata shauri ya kuacha kazi? Nakwambia, Mkongwe. halafu utakuja kujuta na kama unavyojua, majuto mjukuu. Inakupasa ufikiri vizuri kwani halafu utakuja taka kurejea na Bwana hatokukubali tena.”

“Nani? Mimi, nirejee tena hapa kwa mnyonyaji huyu anayetutesa bila ya hata kutuonea huruma? Nastahabu kufa na njaa kuliko kurejea hapa. Mimi nimeshafikiri barabara na nimeshaamua kwenda kujiunga na wenzangu katika shamba la ushirika. Nitakwenda huko kuishi kijamaa pamoja na wakulima wenzangu. Huko mambo ni mazuri kabisa. Huko wana ng’ombe kiasi ya hamsini na mpaka hivi sasa wanawake walioko huko hawatoshi kwa kazi za ufugaji. Kuna kuku, kuna mbuzi; shamba hilo ninalokwambia ni zuri sana,” Mkongwe alimweleza Kijakazi.
 
SEHEMU YA 58


“Shamba hilo ni zuri kuliko la Bwana?”

“Eh, Kijakazi shoga! Bwana wako hana shamba tena. Wewe uko wapi siku zote hizi?”

“Na hao ng’ombe wote wa nani?”

“Ni wa kila mtu aliye mfanyakazi wa shamba hilo.”

“Lakini vipi ng’ombe hao wanaweza kuwa wa watu wote? Vipi kila nunoja ataweza kuyajua maziwa yake?”

Mkongwe alikaa vizuri akiona huu sasa ndio wakati wa kumfahamisha Kijakazi.

“Hebu sasa Kijakazi nisikilize vizuri,” Mkongwe alianza. “Maziwa yote hutiwa ndani ya madebe na kupelekwa madukani kwa ajili ya kuuzwa. Pesa zinazopatikana hugawiwa kwa mujibu wa kazi aliyofanya kila mmoja katika shamba hilo na zinazobakia hutengwa na kuwekwa katika mfuko wa akiba wa shamba hilo. Mpango huu huu ndio unaofuatwa kuhusu mazao mengine kama vile mpunga, muhogo na kadhalika. Ukifanya kazi zaidi unapata pesa zaidi; umefahamu?”

Kwa wakati ule Mkongwe alijihisi kama ni mwalimu anayemfahamisha mwanafunzi jambo ambalo hakupata kulisikia. Kijakazi alishangazwa na maneno ya Mkongwe kwani yale yalikuwa lu mengine mapya ambayo hakupata kuyasikia katika maisha yake.

“Nani mkubwa huko? Nani kama Bwana Fuad?”

“Sikiliza Kijakazi; wewe umekwishazoea kila wakati uwe unachungwa na kuamrishwa. Wewe unataka kila wakati awepo mtu na fimbo nyuma yako huku anakupigia makelele kaina mnyama asiye na thamani.” Mkongwe alimweeleza Kijakazi huku akimsogelea karibu.

“Sikiliza Mkongwe mwanangu, hayo ndiyo majaaliwa yangu. Kuna wengine Bwana Mungu amewajaalia na kuwatukuza mabwana wakubwa na wengine amewajaalia umasikini. Lazima ufahamu Mkongwe kama kila mtu na majaaliwa yake. Hivi ndivyo ulivyo ulimwengu.”

“Hivyo sivyo ulimwengu wa leo ulivyo,” Mkongwe alisema kama kutaka kumsuta Kijakazi.

“Sivyo?”

“Sivyo,” alijibu Mkongwe. “Ni kweli hivi sasa kuna matajiri na masikini lakini nakuahidi kwamba matajiri hawataendelea kuwa matajiri na masikini hawatakufa masikini. Mambo yamebadilika,” Mkongwe alisema.

“Kayabadilisha nani?” Kijakazi aliuliza kama kutaka kufanya stihizai.

Kwa hamaki Mkongwe alijibu, “Watu! Watu wenyewe ndio. walioyabadilisha. Wale unaowaona wakija na kuondoka hapa pamoja na wenziwao wengi ndio waliyoyabadilisha mambo!”

“Sikiliza mtoto; hutobadilisha kitu cho chote kwa kunipigia makelele. Jitulize na useme taratibu,” Kijakazi alimwambia Mkongwe huku akiwa na hofu Fuad asiyasikie waliyokuwa wakizungumza.

Mkongwe, ambaye alijawa na hamasa, alianza tena kuzungumza kwa sauti ya chini. Alihisi kwamba alifanya makosa kumpigia makelele Kijakazi wakati wajibu wake ulikuwa m kumfahamisha kwa utaratibu mpaka aelewe.

“Kijakazi! Najua kwamba wewe unamwogopa Fuad. Najua kuwa wewe m mtumishi wake mtiifu, tena mtiifu wa kutolewa mfano...”

“Ah! Kweli?” Kijakazi aliukunjua uso kwa furaha kwa kuambiwa vile na Mkongwe.

“Wacha upumbavu wako unisikilize ninavyokwambia!” Mkongwe alihamaki tena na kumpigia makelele Kijakazi.
 
SEHEMU YA 59



“Ninajua kuwa Fuad anakuamini sana wewe na siku hizi anakwita chumbani kwake ukamwuguze. Pia najua kakwambia usishirikiane na mimi. Ndiyo maana siku hizi unanikimbia kama shetani anavyoukimbia Msahafu. Lakini Kijakazi jifikirie nawe. Kwa nini ufanyisbwe kazi kama punda kwa pesa mbili tu?”

“Siyo suala la pesa shoga yangu!”

“Nini basi?”

“Ni utiifu wa kazi tu,”

“Utiifu wa kazi! Utiifu kwa nani? Kwa bakhili yule, mtu ambaye anaweza kuitafuna hata shahamu yake mwenyewe? Mimi siwezi tcna kuvumilia mateso yake.”

“Mkongwe mwanangu,” Kijakazi alianza kusema huku akimpiga piga bega Mkongwe, “hili ni jambo usiloweza kulielewa. Mimi si kama nipo hapa kwa ajili ya Bwana Fuad tu bali kwa kila kilichomo ndani ya shamba lake. Mama yangu amemaliza maisha yake hapa na mimi nimedhamir’a kufuata unyanyo wa mama yangu. Mimi nipo hapa kwa yote yaliyopo hapa; Bwana Fuad, kuku wake, ng’ombe wake na kila kilichomo ndani ya shamba hili mimi nakipenda. Nimeazimia kutum’ka hapa mpaka kufa kwangu.”

Mkongwe alinyamaza kimya. Alitaka kumwuliza Kijakazi kama huyo Bwana wake alipata kumnunulia ijapokuwa gwanda la kaniki lakini hata hivyo alinyamaza kimya akijua kwamba maneno aliyoyasema Kijakazi yalitoka ndani ya moyo wake na kwamba hilo ni jambo linalopasa kuheshimiwa. Lakini hata hivyo hakuacha kuzipinga fikra za kipumbavu za Kijakazi, fikra za kitumwa, utumishi wa upofu, utumishi unaomdhalil’sha binaadamu.

Kwa sauti ya chini Mkongwe alianza tena kumweleza Kijakazi.

“Kijakazi! Wewe kweli ni mtiifu na katika maisha yangu sijapata kumwona mtu mtiifu kukushinda wewe. Lakini kuna faida gani kumtii mtu huyu. Wewe umepoteza maisha yako yote katika shamba hili na bado huna cho chote cha kuonyesha ulichopata kutokana na jasho lako. Shamba hili limekunyonya nguvu na damu na kukuunguza kama taa inavyounguza mafuta. Shamba hil’ limekuvunja miguu yako na baada ya miaka yote hiyo ya kazi na utiifu kvva Fuad huna hata kipande cha kaniki cha kujitanda. Ni kweli shamba la Fuad ni kubwa na zuri. Laldni hata ukuti mmoja katika shamba hili si wako wewe. Hakuna cho chote kilicho chako. Wewe mwenyewe hujimiliki. Binaadamu unamilikiwa na mwenye shamba kama anavyomiliki kuku na ng’ombe. Hata hao kuku na ng’ombe wana afadhali kuliko wewe kwani wao walau hupata chakula oha kutosha. Wewe hupati chakula cha kukutosha. Habidhi yule hakuthamini wewe hata kidogo. Hata mimi nilikuwa nikiishi haijambo kidogo kuliko wewe. Kwa muda mrefu watu wote hapa wamekuwa wakikuepuka kwa kuchelea usije ukamwambia Fuad yale waliyokuwa wakizungumza. Lakini sasa unaelewa kila kitu, sikuweza kukuficha tena yaliyokuwemo ndani ya kifua changu. Mimi ninaondoka hapa.”

Kijakazi alikuwa na wasiwasi alipokuwa akizungumza na Mkongwe. Alihisi kama Bwana wake aliyasikia yote yaliyosemwa na Mkongwe. Alimtumbulia macho Mkongwe na ghafla akaanza kulia.

“Mkongwe! Mkongwe! Tafadhali nyamaza upuuzi wako na niondokee mbele ya macho yangu. Tafadhali ondoka uende zako. Wewe huwezi hata kunionea huruma!” Kijakazi alipiga kelele huku machozi yakimmiminika.

“Kijakazi shoga yangu, tafadhali nyamaza kulia. Usilie namna hiyo, mimi sikukwambia jambo lo lote lililo baya; tafadhali nyamaza kulia namna hiyo. kwani ukiendelea utaweza kuniliza na mimi. Basi naondoka nenda zangu takini nakuomba ukipata nafasi uje unitembelee siku moja na tutazungumza zaidi habari hizi,” Mkongwe alisema.
 
SEHEMU YA 60


Pale pale alitoka chumbani kwa Kijakazi na hakungojea tena siku ya pili ifike kama alivyokusudia mwenyewe. Alichukua kile kifurushi alichokifunga na bila ya kumuaga mtu ye yote isipokuwa Kijakazi alishika njia kulikimbia na kulihama shamba la Fuad. Alimwacha Kijakazi kwikwi imemshika kwa namna alivyokuwa akilia.

Siku nzima ile Kijakazi alifanya kazi huku akiwa na majonzi makubwa. Mkongwe amemtukania Bwana wake; amemwita mwizi, hana adabu, bakhili na sifa nyingi nyingine mbaya. Kwa Kijakazi Fuad alikuwa m mtu aliyetimilia; hakuna mwenye heshima na adabu kumshinda yeye, hakuna mzuri wa kumshinda yeye; hana dosari hata kidogo. Na tazama leo, Mkongwe amekuja kumchamba mbele yake.

“Sitomsahau mtoto yule. Ama kweli watoto wa siku hizi hawana adabu!” Kijakazi alisema peke yake.

Kijakazi alifanya kazi hii na ile. Mara kwa mara alijipitisha mbele ya chumba cha Fuad ili apate kuitwa asifiwe kwa utiifu wake, lakini hakuitwa tena. Fuad alikuwa amepata nafuu kidogo na lile gamba la chokaa lilikwisha tolewa mguuni mwake.

Mara moja, Kijakazi alipokuwa akijipitisha hapo, Fuad alimwita.

“Kijakazi! Njoo hapa!”

Kijakazi alisita kidogo, amefurahi, ile fursa aliyokuwa akiitaka kwa muda mrefu sasa ameipata. Alitabasamu lakini punde alimpigia makelele na kumsitua.

“Unacheka nini? Jambo gani linalokuchekesha? Nakwambia njoo hapa!”

Fuad alikuwa amekwisha kuyasahau yote yale aliyomwambia siku ile alipokuwa ameupakata mguu wake mgonjwa. Si mama yake wa’ pili tena. Wala si sawa na yeyote yule ndani ya nyumba ile. Ni Kijakazi tu kama kawai. da.

“Yuko wapi Mkongwe?”

Kijakazi alitaka kujibu kwamba amekwenda zake lakini alikuwa na hofu ya kujibu hivyo asije akaambiwa na yeye alikuwa akishirikiana naye kwani alikwisha onywa asifanye hivyo.

“Sijui Bwana!”

“Hujui? Ebo! Nenda kamtafute aje kunisafishia viatu vyangul” Fuad aliamuru kwa makolele kama kawaida yake.

“Sijui nitamwona wapi, Bwana!”

“Hujui utamwona wapi? Neoda kamtafute mpaka umwone!”

Sasa Kijakazi alifikwa na kazi kubwa. Kazi ya kumtafuta Mkongwe ambaye alikuwa na hakika hayupo tena shambani mwa Fuad. Hakujua alikokwendea na alilolijua ni kwamba amekwenda kujiunga na wale ambao Fuad anawaita wahuni. Kijakazi alikuwa na hofu ya kumwambia Fuad hivyo kwani pindi akimwambia basi lazima atakabiliwa na swali la “ulijuaje isipokuwa na wewe unashirikiana nao?” Wasiwasi ulimjaa wala hakujua la kufanya.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 61


Alihangaika kumtafuta kwenye kila pembe ya shamba la Fuad huku akijua hakika hawezi kumwona.

Baada ya muda mrefu Kijakazi alirejea kwa Fuad akamkuta amekaa ukumbini.

“Sikumwona Bwana!”

“Hukumwona? Ng’ombe we! Nimekwambia usirejee hapa mpaka umwone!”

“Lakini, Bwana......”

“Lakini, lakini, lakini nini?”

“Lakini, Bwana, nimemtafuta kila pahala sikumwona!”

“Umekwenda kibandani kwake?”

“Nimekwenda kila pahala, Bwana! Hakuna pembe ya shamba hili niliyoibakisha, lakini sikumwona!”

“Ahaa! Hukumwona sio? Mwachilie mbali! Lazima amekimbia hapa na mimi nitakwenda kumwona baba yake. Mzee Sharwan, nimuhadithie kila kitu,” Fuad alisema, lakini sasa kwa sauti ya chini.

“Umari je, umemwona po pote?”

“Umari nimemwacha kule bondeni anapalilia mpunga,” Kijakazi alijibu.

“Nenda kamwite basi!”

Kijakazi alikuwa amechoka lakini, ndio yumo katika utiifu; kumtii Bwana wake. Bila ya kupoteza wakati alikwenda mpaka kule alikokuwa Umari.

Alimkuta Umari ameshughulika, tumbo wazi. anapalilia mpunga.

“Umari, Bwana anakwita.”

Umari aliinuka na kujiuyosha, kijasho kinamtoka. Ali mtazama Kijakazi na halafu akatikisa kichwa.

“Kwani Kijakazi hunioni kama mimi nina kazi mkononi?” Umari aliuliza.

“Nimemwambia kuwa unapalilia mpunga lakini kanituma nije nikwite,” Kijakazi alijibu.

“Nenda kamwambie sitaki,” Umari alisema.

“Ah! Mimi sitoweza kumjibu hivyo!” Kijakazi alisema.

“Usiogope, Kijakazi, nenda kamwambie hivyo hivyo. Usimwogope yule, Kijakazi: wakati wake umekwisha, na sote hapa tunangojea siku ifike tuondoke. Labda utabakia wewe peke yako hapa, Kijakazi.” Umari alisema huku akitabasamu,

Mbio, Kijakazi alirudi na alipofika alimkuta Fuad amekaa pale pale ukumbini.

“Yuko wapi?” Fuad aliuliza kwa hamaki.

“Anasema... anasema...” Kijakazi hakuweza kusema kama alivyoambiwa.

“Anasema nini?” Fuad aliuliza huku amesimama baada ya kuondoka kwa ghafla juu ya kiti alichokuwa amekalia. “Anasema nini?”

“Arasema hataki!” Kwa khofu Kijakazi alijibu.

“Hataki? Anathubutu. kujibu hivyo? Mwachilie mbali; leo ndio mwisho wake ndani ya shamba hili.”

“Basi, wewe Kijakazi nenda ukafanye kazi zako na huyo Umari akija tutaonana mimi na yeye.”

Kwa hakika Fuad mwenyewe alikwisha kuelewa kwamba siku zake zimekwisha ila alijikaza kisabuni tu. Kila mmoja katika watanyakazi wake alikwisha yajua hayo isipokuwa Kijakazi.
 
SEHEMU YA 62



Kijakazi aliendelea na kazi zake tangu asubuhi mpaka magharibi. Usiku ulipofika alijitia chumbani mwake na kujinyosha. Alijitupa na kulala chali, macho yake yakiangalia boriti za dari. Taa ya kibatari iliyokuwamo humo ilitoa mwangaza mdogo uliomwezesha kuona bali duni ya maisha yake lakini haukutosha kumwonyesha jinsi gani atokane nayo. Zlimjia fikra nafflna kwa namna na katika jambo lililozidi kumharibu akili yake lilikuwa ni mazungumzo yake na Mkongwe. Alijaribu kujikurupusha ili zimtoke fikra alizokuwa nazo lakini hakuweza.

Hata usingizi ulimruka. Alijihisi kama mtu aliyefikwa na msiba mkubwa. Mazungumzo ya Mkongwe yalimchafua moyo wake. Alihisi Mkongwe anataka kumfarakanisha na Bwana wake mpenzi Fuad.

Aligaragara, mara ageuze ubavu huu mara ubavu ule lakini usingizi hakuupata kamwe. Mara zilimjia fikra za Fuad. Alifikiri jinsi alivyokuwa ameupakata mguu wake huku akizungumza naye taratibu. Hakupara kusemeshwa taratibu na Fuad hata siku moja isipokuwa siku ile aliyomwita akamwuguze. Lakini sasa hata mawazo haya hayakuweza kumletea Kijakazi furaha kwani pale pale zilimjia fikra za jinsi alivyotukanwa kabla hata’ hajawahi kuimba ule wimbo aliotakiwa na Fuad auimbe.

Mara aliyasikia kichwani mwake maneno aliyoambiwa na Umari, “Usimwogope yule, zake” zimekwisha.” Aliyafikiri maneno haya lakini kwake yeye havakuwa na maana yo yote. Hakufahamu Umari alikusudia nini.

Baada ya kufurukuta huku na huku kwa muda mrefu usingizi ulimchukua. Katika huo usingizi alitoa ndoto ya ajabu. Aliota anamnyonyesha mtote mchanga na mtoto huyo alikuwa akizivuta chuchu zake kwa nguvu kwa ajili ya njaa aliyokuwa nayo. Kijakazi alishindwa kuvuta pumzi kwa namna mtoto huyo alivyokuwa akizivuta chuchu zake. Mwisho Kijakazi aliweza kumgandua mtoto huyo kifuani na kupata nafasi ya kuvuta pumzi. Mara ndoto ilibadilika na badala ya kitoto kile kilichokuwa kikinyonya aliuona uso wa bwana shamba unamulika; amemsimamia mbele yake anampigia kelele. Kijakazi alishtuka na kuzindukana.

Kijakazi aliamka mapema na kama kawaida yake alisafisha uwanja, akawalisha ng’ombe na kuwapa maji. Alifanya kazi zake zote. Baada ya kumaliza, alikusanya taka akazitia ndani ya debe na kulichukua debe hilo kwenda kulimwaga.

Wakati anapita mbele ya nyumba ya Fuad na pipa lake la taka kichwani, Fuad alichungulia dirishani pa mara alimwona na kumpigia makelele, “Kijakazi! We Kijakazi! Njoo!”

Bila ya kufikiri, Kijakazi alitua pipa la taka alilokuwa amelichukua na kukimbilia chumbani kwa Fuad. Hakujua anakwenda kuambiwa nini tena la kheri au shari.

Alimkuta Fuad amelala kitandani.

“Njoo univue viatu!” Fuad aliamrisha.”

Kijakazi alikaa pembeni ya kitanda na mara Fuad alintupa mguu wake juu ya mapaja yake. Fuad alikuwa amekula amevimbiwa hata hawezi kufurukuta. Kijakazi aliweza kuona namna gani Fuad alikuwa anahisi joto kwa namna uso wake ulivyomwiva.

“Fanya upesi na wacha kunipotezea wakati wangu!” Fuad aliamuru.

Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, Kijakazi alimwangalia Fuad kwa karibu. Macho ya Fuad yalikuwa yamedidimia ndani ya uso wake na matone ya majasho yanang’aa juu ya kipaji chake. Kijakazi alikuwa akimvua viatu Fuad na wakati huo ilimjia huruma kubwa kumhurumia Bwana wake, Fuad mpenzi. Alimhisi kama ni mateka asiyekuwa na silaha. Hapo hapo Fuad alichukuliwa na usingizi na Kijakazi alimvua viatu taratibu ili asije akamwamsha. Hapo hapo Kijakazi ilimjia fikra nyingine na kufikiri labda kuna mtu anamhadaa. Alijiuliza moyoni, “Nani hasa anayejaribu kunihadaa? Nani? Nani hasa?” Na baada ya hapo mara kwa mara Kijakazi aHkuwa anajiuliza swali hili. Kulikuwa kumekwisha pambazuka, lakini Fuad hakuinuka kitandani ijapokuwa alikuwa yu macho. Hewa nzuri ya upepo wa umande uliokuwa ukivuma alfajiri ulimtia uvivu Fuad na kumfanya abakie hapo hapo kitandani akiwa amejifunika shuka.
 
SEHEMU YA 63


Hakuwa na raha ya moyo hata kidogo licha ya kuwa kila alichokitaka katika raha za maisha aliweza kukipata. Pesa alikuwa nazo, tena nyingi, lakini maisha hakujua yanaendea wapi. Kila alilotaka kulifanya aliona silo. Khofu na wasiwasi vilimjaa moyooi.

Alihisi mambo yamebadilika. Heshima aliyokuwa akipewa ilikuwa inapungua, kwani hata Umari naye huitwa na kuthubutu kujibu “staki”. Aliiona dunia imempa kisogo na mambo yamembadilikia.

Fuad alikuwa amejinyosha hapo kitandani fikra namna kwa namna zikimjia kichwani mwake. Alifikiri labda mambo huenda yakabadilika. Alijigeuza huku na huku pale kitandani alipokuwa amejinyosha na mara alisikia sauti ya mtu ikiita kutoka nje, “Hodi! Hodi!”

“Karibu!” Fuad aliruka kutoka pale kitandani kidogo aanguke. Alijizoazoa na kujifunga sbuka aliyokuwa ameivaa kiunoni uzuri, na bila ya hata kunawa uso Fuad alitoka nje kwenda kumsikiliza aliyebisha hodi.

Hapana aliyewahi kujibu. Mara Fuad alifika mlangoni huku akijipangusa tongo zilizokuwa zimemjaa machoni.

“Je, kumezidi nini tena; mbooa leo asubuhi na mapema?” Fuad aliuliza.

‘Tumekuja tunataka kuonana na wewe mara moja, alijibu mmoja katika wale vijana.

Wote wanne walikuwa wamevaa mashati na suruali, viatu virefu vya mpira na makofia makubwa ya ukuli. Walikuwa wamechukua vijiti vifupi vilivyochongwa katika ocha moja na kamba ndefu iliyozongwazongwa. Walikuwa ni watu wapya ambao Fuad hakupata kuwaona - sio wale waliokuja kila siku. Hata hivyo alihisi kuwa hata wao ni katika kundi la wale wale wanaokuja kumkera kila mara.

“Piteni ndani. Karibuni ukumbini; lakini tafadhalini nisubirini kidogo nikajitie maji, “ Fuad aliwaambia wageni wake ambao hakujua walilolijia.

“Hapana kitu, fanya kazi zako kwa utulivu. Sisi tutakusubiri hapa nje.”

“La! Kwa nini mkae nje? Piteni ndani. Karibuni... nyumba, nyumba yenu,” Fuad alisema.

Bila ya kupoteza wakati katika kujadiliana ama waingie au wasiingie, wote waliingia ndani na walifululiza moja kwa moja mpaka ukumbini. Walikaa juu ya makochi mazuri yaliyokuwamo ukumbini hapo na kila mmoja katika wao alianza kutazama huku na huku baada ya Fuad kwenda msalani. Walishangazwa na mapambo waliyoyaona ukumbini hapo na mara mmoja katika wao alisema kwa sauti ya kunong’ona, “Hadi amestarehe kijana huyu!”

Hakuna aliyejibu katika wale wenzake, walinyamaza kimya wakitazamana macho. Walikaa kwa kituo hapana aliyekuwa na wasi wasi, wote wanamngojea Fuad kwa hamu kubwa.

Fuad alifanya haja zake zote na alipomaliza aliingia chumbani na kuvalia nguo zake. Baada ya kumaliza alikuja pale ukumbini ili kuwasikiliza wageni wake na kujua nini lililowaleta pale

“Naam, mnasemaje?” Fuad aliuliza huku wasi wasi umemwingia.

“Sisi ni watumishi wa Idara ya Ugawaji wa Ardhi,” alisema mmoja katika wale wageni wa Fuad.

Fuad roho ilimpiga na moyo ukaanza kumwenda mbio. Aliona sasa kweli imedhihiri.

“Idara ya Ugawaji wa Ardhi?” Fuad aliuliza, macho yamemtoka.

“Ndiyo”.

“Ehe! Mna shida gani n’nayoweza kukusaidieni?” Fuad aliuliza, uso umemwiva, midomo inamcheza.

“Tunataka utuonyeshe mipaka ya shamba lako,” alisema yule mtu.

“Kwani mna...” Fuad alitaka kusema kwa hamaki. Kabla hajamaliza aliyotaka kuyasema alikuja matao ya chini na kuzizuia hamaki zake za “hayati Bwana”.
 
SEHEMU YA 64


“Mipaka ya shamba langu siyo?” Fuad aliuliza.

“Ndiyo,” alijibu yale kijana.

“Kaskazini limepakana oa shamba la Ruwehi, kusini nashambala...”

Kabla hajamaliza yule mtu alimkatiza maneno yake “Sisi hatutald maelezo, tunataka ukatuonyeshe wewe mwenyewe.”

“He! Itakuwa kazi kubwa, kazi ya kutwa; pengine hata tusiimalize,” Fuad alisema.

Tunajua.”

Fuad aliinama chini na kufikiri. Hakujua la kufanya Mara aliinua kichwa na kusema, “Basi nisubirini kidogo.”

Aliingia ndani bila ya hata kuwa na haja yo yote na mara akatoka nje.

“Haya twendeni.”

Safari ya kwenda kukagua mipaka ya shamba la Fuad ilianza; nayo ilikuwa ndefu. Walikwenda kaskazini na kusini, mashariki na magharibi huku wakipima kila sehemu waliyokuwa wakiikagua kwa kamba zao. Baada ya kila marefu waliyoyataka walichomeka kijiti katika vile vijiti walivyokuwa navyo. Fuad alikuwa amechoka taabani, anakwenda aldpepesuka kama mtu aliyekunywa chupa nzima ya tende. Hakupata maishani mwake kwenda masafa marefu kwa miguu kama siku ile. Hapana aliyekula kitu isipokuwa matunda mbali mbali waliyoyaangua kutoka kwenye miti ya matunda iliyokuwa shambani mle.

Huku nyuma Kijakazi alijawa oa wasi wasi. Kutwa nzima hakumwona bwana wake wala hakujua ameendea wapi. Alitaagatanga kila pembe lakini hakufanikiwa kumwona bwana wake mpenzi Mwishowe aliangukia kibandani kwa Umari ambaye siku ile alikuwa hakwenda kazini kupiga majalbe.

“Umari mwanangu! Hukumwona Fuad?”

Umari aliyekuwa amekaa juu ya kigogo cha mnazi nje ya kibanda chake alimtazama Kijakazi kwa jicho la humma kama kutaka kumwambia “masikini roho yako.”

“Kwani unamtafutia nini? Umari aliuliza.

“Leo kutwa sijamwona; sijui amefikwa na masahiba gani!” Kijakazi alijibu na kuuliza huku akionyesha ni mtu mwenye wasi wasi mkubwa.

“Mimi pia sijamwona; sijui yuko wapi?” alisema Umari.

“Masikini! Sijui yuko wapi tena? Anajitabisha ilhali mguu wake hata haujapona uzuri” alisema Kijakazi.

Hapo hapo Kijakazi aliondoka na kuendelea na msako wake wa kumtafuta Fuad.

Umari hakushughulishwa na cho chote. Alikuwa amekwisha pata fununu kwamba shamba la Fuad karibu litachukuliwa lakini hakujua lini. Yeye alikuwa anangojea siku ifike tu.

Fuad na wageni wake waliendelea kulipima shamba mpaka jua lilipokuchwa. Kazi yote ilimalizika magharibi na. baada ya kumaliza wakaanza safari ya kurejea nyumbani kwa Fuad. Lilikuwa shamba kubwa lililojaa miti ya kila aina. Baada ya masafa marefu walifika nyumbani kwa Fuad na hapo mmoja katika wale watu alimwomba Fuad wazungumze kidogo.

Kijakazi alikuwa amekaa nje ya nyumba ya Fuad amejikunja lakini unyonge wote ulimwisha alipomwona Fuad anarejea. Alifurahi kama vile anavyofurahi mtoto mchanga anapomwona baba yake baada ya kutomwona kwa muda mrefu. Alitabasamu na kushusha pumzi

“Si bora tukenda ukumbini kwa mazungumzo yetu?” Fuad alitoa shauri.
 
Back
Top Bottom