Riwaya: Machinga mimi Masikini

Riwaya: Machinga mimi Masikini

KAZI YA TATU; Starehe na Ubudurishaji
Katika mji huu watu tunalipwa vizuri ujira unaotosha mahitaji yetu yote na kubakia na ziada, ukizingatia muda wa kufanya kazi ni mchache, watu wana muda mwingi wa kustarehe na kufurahia maisha yao, ndugu na rafiki zao, hivyo sekta ya kuburudisha na starehe ni muhimu sana kuhakikisha watu wanaburudika.

Mambo ya michezo, burudani, mziki, utalii, vyakula, maeneo ya burudani, michezo n.k. vipo kwa wingi kwenye huu mji. Vilevile mji unajipatia kipato kutokana na uwepo wa haya maeneo na shughuli za starehe kwa watu kutumia pesa zao za ziada ambapo jiji linafaidika na kupata uwezo wa kuendelea kutoa huduma kwa wakazi.

Kwahio pamoja na kuwafanya watu wasichoke na kukosa cha kufanya hii sekta inawafanya watu wawe na furaha na vilevile mji unajipatia kipato.

Katika shule na chuo watu wanafundishwa mambo ya sanaa na mara kwa mara wanatoa kazi kama maigizo na sanaa tofauti ambazo zinawekwa sokoni ili wakazi waweze kuburudika.

Mji wetu una timu za mpira wa miguu, timu hizi huwa zinategemea kwa wakati husika kuna vipaji kiasi gani. Mfano sasa tuna timu tatu sababu tuna vijana kama 150 wenye vipaji kwahio kuliko kuwa na timu moja na wengine kucheza na wengine kukaa bench, tuliamua tutakuwa na timu nyingi kadri ya vipaji kwa wakati husika.

Hawa wachezaji wote 150, uchezaji wao pia unahesabika kama ajira, na wao wanalipwa kama wengine kwa mwezi ujira wao wa dollar 500, ambayo tayari ipo katika gharama ya mishahara kwa mwezi. Huwa tuna michezo kama minne kila mwezi, na ticket ya mpira huwa ni kama Dollar Tano, kwahio mtu akiangalia mechi nne kwa mwezi ni dollar 20 hivyo kama watu 4,500 kutoka kwenye watu elfu hamsini wakiangalia kila mechi tayari hizi timu zinakuwa zimejilipa mishahara, na hapo bado faida nyingine za watu kununua nguo zenye nembo ya timu n.k, kwahio hizi timu zinaongezea kipato sana mji wetu na pia kuleta umoja na kujivunia, kwa sasa timu zetu mbili kati ya hizi tatu zipo kwenye ligi kuu.

Nakumbuka Busara aliwahi kuniambia, tunataka kutengeneza jamii yenye furaha…. Nakumbuka nilikuwa nimechoka hio siku, nikamuuliza kwa dhihaka Aahh, kwani furaha ni nini Bwana….

Busara alinijibu furaha inaletwa na kuridhika, mafanikio ya kile ambacho mtu amekianzisha au amepanga akifanye, amani ya nafsi, kutokuwa na wasiwasi….

Na mji wetu utaleta yote hayo?, Nilimuuliza kwa mshangao.

Busara aliniangalia kwa sekunde kadhaa, akaniuliza, ni kitu gani kwa sasa kitakufanya uwe mwenye furaha?

Ingawa lilikuwa swali jepesi nilifikiri wa dakika kadhaa…, nadhani nikiwatimizia mahitaji wanangu, nikahakikisha wanapata elimu nitakuwa mtu mwenye furaha…, ila nadhani mimi furaha ilishanikimbia, nilikuwa na ndoto za kutimizia familia yangu, watoto na wazazi mahitaji yao, badala yake nimekuwa kama kupe wa kuwanyonya na kuwasababishia umasikini, nimesababisha mpaka kifo cha mama yangu.

Ni kweli haya yote yasingetokea kama ungekuwa na uhakika wa mahitaji yako, badala ya kuishi kwa kuhangaika kuhusu kesho yako ungekuwa unahangaika kutimiza malengo binafsi..., kuumwa kwako kusingelazimisha watu wauze mali ili utibiwe kama kungekuwa na matibabu ambayo unaweza kumudu gharama zake. Ungekuwa haukosi uzingizi kuhusu karo za watoto wako kama elimu yao ungekuwa na uhakika wa kuweza kuimudu.

Busara aliendelea, unaweza kuona matajiri ukadhani wao wanafuraha sababu wanapesa na wanamudu gharama za hapa na pale. Lakini kijana nakwambia kwa mimi ambaye nilishakuwa tajiri fikra hizo sio kweli. Uoga wa kuweza kupata hasara, uwezekano wa biashara yangu kufilisika na watu wanaokufanyia kazi kukosa ajira, mzigo wa kuendesha biashara na chuki toka kwa wasionacho kukuona wewe ni beberu na myonyaji nina uhakika usingependa kabisa kuwa kwenye viatu vyangu.

Ni kweli nilimjibu Busara, kila mtu na mzigo wake, kuna wanaokosa usingizi kwa kufikiri ni vipi wanaweza kuwafurahisha wachumba zao, na wengine hawalali kwa wasiwasi wa kutokupata chakula, makazi na kutokujua kama wataendelea kuishi mpaka mwisho wa wiki…, ni ukweli usiopingika hatuwezi kujaribu kulinganisha shida za hao wawili.

Busara alitabasamu akaendelea, ni kweli siwezi nikasema kwamba mji utakuwa na dawa ya mapenzi ya kumfanya mtu ampende au apendwe, lakini kuwa na uhakika wa makazi, elimu, huduma za afya, burudani, uwepo wa huduma na bidhaa, mafao ya uzeeni kwa kila mstaafu, na kuwa na ziada ya kipato itasaidia sana furaha kwa wakazi.

Nakumbuka hapo nilimuuliza Busara vipi kuhusu chakula, unawezaje kuhakikishia watu watabaki na ziada ya ujira wao kama gharama za chakula zikipanda?

Busara alinijibu kwa upole, jibu lako linanipeleka kwenye kazi namba nne; Chakula Bora kwa kila Mmoja.

Nakumbuka jibu alilonipa kabla sijaelewa vizuri zile hatua kumi lilinifanya nione kama amechanganyikiwa, Utahakikisha kila mtu ana pesa za kununua chakula bora? Unajuaje kama pesa hizo watu hawatatumia kwenye kamari au ulevi

Hapana kijana, tutahakikisha kila mtu anapata milo mitatu kwa siku, na sio bora chakula, bali chakula bora na cha kuvutia.
 
KAZI YA NNE; Chakula Bora kwa Wote
Nakumbuka ile siku kama jana wakati Busara ananielewesha…, tunaishi kipindi ambacho kina mama ni wafanyakazi, enzi za fikra kwamba kina mama sehemu yao ni jikoni imepitwa na wakati. Watu hawana muda wa kufanya kazi na vilevile kutayarisha chakula hali hii inafanya maisha kuwa ya usumbufu hivyo kupelekea familia nyingi kutafuta wafanyakazi wa ndani, jambo ambalo ni gharama, hususan kwenye mji wetu itakuwa ni vigumu sababu huyo mfanyakazi wa ndani atakuwa na fursa / uwezo wa kupata ajira yenye malipo ya kumtosheleza kuishi katika mji, hivyo hatakubali kufanya kazi za ndani kwa ujira mdogo.

Nilimwangalia Busara na kumuuliza utawezaje kubadilisha hayo.

Mji utahakikisha kila mtu anapata chakula bora bila usumbufu wa kupika wala utayarishaji, na wakati huo huo kudumisha umoja na urafiki, hilo litawezekana iwapo kula chakula nje (yaani kwenye migahawa na mahoteli) itakuwa bei rahisi kuliko kujipikia, na faida ya ziada itakuwa ni kuokoa muda ambao ungetumika katika utayarishaji wa chakula. Hayo tulikuwa tunayaongea baada ya kutayarisha chakula na kula kwa pamoja kipindi hicho tulikuwa familia mbili, mimi, mke wangu, rafiki yangu na mke wake, na Mzee Busara.

Nilimwangalia Busara usoni nione kama anatania!!, Mzee labda kama unapika mabaki na vyakula vya kuokoteleza, iweje mlo wa kwenye mgahawa au hoteli uwe gharama sawa na mtu kujipikia, unajua kabisa mgahawa ili upate faida unaongezea asilimia kadhaa kwenye chakula wanachouza, unalipia huduma, urahisi na burudani, watu wanakula kwenye migahawa kama burudani, starehe na kujifurahisha na kupumzika kutoka kwenye maisha ya mihangaiko, mara nyingi chakula cha kwenye migahawa ni kama mara tatu zaidi ya mtu kujipikia na hapo ni kama unakula kwa kina Ashura na sio kwenye migahawa ya wachache wenye uwezo.

Busara aliendelea kunijibu huku akiendelea kula pole pole, ni kweli usemayo watu hawali kwenye migahawa na mahoteli sababu ya kuepuka gharama, lakini kwa kuzalisha chakula wenyewe, uhakika wa wateja na hivyo kujua kiasi gani cha chakula na aina gani kutayarisha, na uwepo wa soko yaani wateja wengi itasaidia sana kwa mji wetu kupunguza gharama hata kupelekea kupata faida. Vilevile itapunguza sana upotevu wa chakula, bila kusahau hata nishati itakayotumika kupikia hicho chakula itakuwa ni gesi asilia ambayo nayo itakuwa inazalishwa hapa hapa kijijini ambapo baaade patakuwa mji.

Nilianza kuwaza huenda Busara asemayo yana maana, ingawa tulikuwa familia mbili tu na yeye lakini tulishaanza kutumia gesi asilia kutoka kwenye mabaki ya mifugo yetu ingawa kwa sasa mtambo ulikuwa mdogo tu tuliotengeneza kutoka kwenye mapipa, niliwaza yale mapipa tofauti na sasa mtambo wa Biogas ni mkubwa sana unaochukua uchafu wa mji mzima na tunapata gesi ya kutosha kwa mahitaji yote ya kupikia na kubaki na ziada, kweli tumetoka mbali…, mawazo yangu yalirudi tena kwenye yale maongezi yetu na Busara siku ile…

Busara aliendelea, na kama tutaweka utamaduni wa watu kujihudumia yaani self service tutapunguza sana gharama za nguvu kazi.

Kupunguza nguvu kazi? Aliuliza rafiki yangu, nilidhani lengo ni kuongeza ajira na sio kuzipunguza…, aliongezea.

Busara kwa masikitiko alisema, nasikitika ulikuwa hausikilizi, hatutengenezi kazi ili watu wapate cha kufanya, kama kuna uwezekano mashine zitafanya kila kitu, lengo ni kazi zinazohitajika kufanyika (kumbuka neno muhimu hapa ni hitajika)…, kazi zinazohitajika kufanyika zitafanywa na watu waliopo…, lengo ni kuwa na kazi chache iwezekanavyo ili watu wawe na muda mchache wa kufanya kazi kama inavyowezekana, ili muda unaobaki utumike kwa mambo mengine kama starehe, kuongeza ujuzi, uchunguzi n.k.

Kwahio mji utakuwa na ajira za upishi na kazi zote zinazohusiana na utayarishaji na huduma za chakula, na kama nilivyosema hapo mwanzo kupunguza nguvu kazi jiji litahamasisha watu kujihudumia (self service), buffet na vilevile kwa wale wanaotaka huduma ya take away pia itakuwepo.

Nimekuelewa Busara, umeweka Chakula Bora kwa kila Mmoja kama kazi sababu pamoja na kutoa huduma ya chakula hii pia itatoa ajira kwa watu hivyo kujipatia kipato.

Wakati nakumbuka hayo nilikuwa hapa kwenye moja kati ya migahawa kama mia mbili hamsini katika huu mji, migahawa hii ilikuwa na chakula bora na vyakula tofauti tofauti vya kuvutia.

Kati ya wakazi elfu hamsini wazee wastaafu takriban elfu kumi wanapata milo yao mitatu kwa siku bure, waliobaki wote kila mtu alikuwa ana haki ya kupata milo mitatu kwa siku kwa kuchangia kutoka kwenye mshahara wake dollar themanini kwa mtu kwa mwezi, hivyo kwa familia ya wazazi wawili na watoto wawili yenye jumla ya kipato cha dollar elfu moja na mia mbili walikuwa wanachangia kama dollar 320 kwa ajili ya chakula bora kila siku, kinachopatikana kwenye migahawa, mahoteli, au take-away. Kwa huduma hii jiji linakusanya kutoka kwa watu elfu arobaini kila mmoja elfu themanini jumla ya milioni 3.2 kila mwezi kwa ajili ya kuwalisha watu elfu hamsini. Vyakula karibia vyote vinazalishwa na wakazi wenyewe kwenye sehemu ya viwanda, kwahio kwenye vyakula kuna nyama, matunda, kuku, samaki, mbogamboga n.k., vile vyakula ambavyo vinahitajika na havizalishwi jijini huwa vinaagizwa kwa bei ya jumla wakati wa msimu na kuhifadhiwa ili vitumike kwa ajili ya wakazi.

Unaweza ukashangaa kwa kuona kwamba pesa mtu anayotoa ya dollar 80 kwa mwezi ambayo ukigawa kwa thelasini ni kama dollar 2.7 kwa siku, kuwa itakuwa ni vigumu kwa kiasi hicho mtu kupata chakula bora kinachojumuisha vitu vitamu na vya gharama kama kuku, nyama, maziwa, matunda na mapochopocho mengine. Ingawa ni kweli kwa mtu mmoja huenda isiwezekane, ila kwa kundi la watu kutokana na wingi wao pesa hii inatosha na bado kunapatikana faida, bila kusahau kuwa vyakula vingi vinazalishwa hapahapa, na nishati ya kupikia pia inapatikana kwenye gesi asilia inayozalishwa kutokana na mabaki ya uchafu unaopatikana mjini, na mwisho kabisa hata wapishi na watoa huduma pia ni sehemu ya ajira ya wakazi wa huu mji.

Ukitembelea nyumba nyingi katika huu mji utakuta kuna fridge, microwave na vitu vidogo vidogo vya kupashia chakula, watu wengi katika huu mji wana utamaduni wa kula kwenye migahawa na kwenye hizi hoteli na sio kujipikia majumbani, ingawa wakitaka pia wanaweza kufanya hivyo, ila kulingana na faida na kuokoa muda wengi hawafanyi hivyo.

Pamoja na Chakula Bora kwa Wote mji pia una chakula cha ziada ambacho wakazi wanaweza kununua au watu kutoka nje ya mji wakija kutembelea mji huwa wananunua ingawa bei hio huwa inakuwa ni kubwa kuliko gharama za ile milo mitatu kwa siku.

Kwa matumizi ya Camera CCTV na uhamasishaji wa watu kujihudumia huu mji unafanya kazi masaa ishirini na nne (yaani mji ambao haulali) na ukizingatia kuna shifts tofauti na wengine wanafanya kazi usiku baadhi ya sehemu za starehe huwa hazifungwi na zinafanya kazi mida yote.

Maendeleo mengi katika huu mji yalitokea polepole na yalijengwa hatua kwa hatua kulingana na uhitaji ila vitu kama chakula bora kwa wote na utumiaji wa teknolojia katika malipo bila kutumia pesa (miamala yote kufanyika kieletroniki) yalifanyika tokea mwanzo. Vilevile mambo ya burudani yalikuwepo tangia mwanzo mfano hata kabla ya kuwa na timu za mpira kila mwisho wa wiki kulikuwa kuna mashindano ya timu za watoto wetu ambapo watu walijumuika, kushangilia na kuburudika… yaani nadhani tangia mwanzo huu mji umekuwa ni wa furaha, sherehe na kustarehe.
 
KAZI YA TANO: Huduma za Afya
Nakumbuka tulipoanzia tulikuwa hatuna hospitali wala zahanati, ilikuwa ukiugua zaidi ya kutumia mitishamba n.k. ilibidi kusafiri mpaka mjini kupata matibabu, hali hio ilibadilika polepole kwa kupata zahanati ndogo na kukodi daktari na nesi kutoka mjini, ingawa baadae tulipata madaktari wetu na manesi ambao walikubali kujiunga na jiji letu.

Tangia mwanzo lengo lilikuwa ni kuimarisha, na kuhakikisha afya za wakazi zinakuwa bora kwa kushirikiana na hospitali nyingine ambazo zipo nje ya mji.

Nguvu kubwa tuliiweka kwenye kuhakikisha afya zetu zinakuwa imara ili sio tu tuishi maisha marefu bali tuishi maisha yenye afya na yenye nguvu kwa muda mrefu iwezekanavyo. Badala ya kuwekeza kwenye kutibu magonjwa, uwekezaji zaidi tunauweka kwenye kuzuia magonjwa na kuelimisha watu kuhusu afya bora. Kwa lugha ya kigeni tunaweza kusema (focus on proactive care rather than reactive care).

Tuna hospitali ya mji ambayo kuna kila takwimu za matatizo au shida ambazo anazo kila mkazi, hii inasaidia pindi shida ikitokea au kama mtu akiugua inakuwa rahisi kwa hospitali kujua wapi pa kumpeleka au jinsi ya kumsaidia. Na sababu huu mji ni SMART ni rahisi sana kuzuia magonjwa mengine hata kabla hayajaripuka, hii inatokana na kuwa na habari na ufahamu kuhusu afya za wakazi hivyo jambo lolote likitokea inakuwa rahisi kulisimamisha kabla halijaleta maafa.

Utumiaji wa teknologia umesaidia sana na kupunguza uhitaji wa wataalamu wa afya wengi na kazi nyingi katika sekta yetu ya afya zinafanywa na watu ambao kazi yao ni ya kuwaangalia wagonjwa (social care) hususan wazee, na hii imepelekea watu wengi zaidi kuweza kufanya kazi kwenye sekta hii ya afya. Kuwa na hospitali katika mji kumehakikisha kila mtu anaweza kupata huduma za afya wakati wowote.

Nakumbuka kabla ya kuongezea familia tatu kwenye kijiji chetu ambazo zilikuwa na daktari na manesi wawili, nilikuwa na mjadala na Busara, nilimuuliza Busara hivi kwanini nchi kama Japan watu wanaishi zaidi kuliko nchi nyingine, huko Japan wastani wa mtu kuishi ni miaka 85.3, lazima kuna jambo wanalifanya sawa, kwanini nchi nyingine zisiige wanachokifanya? Kwa kuwa na jamii yenye afya tutaokoa gharama kubwa sana inayotumika katika kutibu watu na kukosa nguvu kazi ya watu kufanya kazi au kustarehe sababu ya kuwa na afya mbovu.

Busara alitabasamu na kunijibu, kuna mji upo Japan unaitwa Nagano, mpaka miaka ya ’80 walikuwa na matatizo sana ya magonjwa ya moyo, hata wakati uchumi wa Japan unapanda na watu kuishi maisha marefu, Nagano bado hali ilikuwa mbaya na watu wengi walikufa kwa magonjwa ya moyo, husasan wanaume.

Lakini sasa hivi mji huo huo Nagano ni kati ya miji duniani inayoongoza kwa watu kuishi maisha marefu, wanawake wastani wao ni miaka 87.2 na wanaume 80.9, na huwezi amini Nagano ndio inatumia gharama ndogo zaidi katika afya kuliko sehemu nyingine Japan, hivyo utaona inpunguzia walipa kodi mamilioni ya pesa kila mwaka ambazo zingetumika kama huduma za afya. Utakubaliana na mimi kwa watu kuwa na afya na kuendelea kuzalisha ndio njia pekee ya kuepuka gharama za afya.

Nilimuuliza Busara walifanyaje hadi kutoka kwenye sehemu yenye maisha mafupi kuliko zote Japan hadi kuwa kati ya sehemu zenye maisha marefu duniani?

Chakula bora, mazoezi na kuongeza miaka ya kufanya kazi. Baada ya uchunguzi serikali iligundua kwamba tatizo lilikuwa kwenye chakula chao cha asili, (mboga zilizosindikwa), sababu ya hali ya hewa ya Nagano ili kuhifadhi vyakula walikuwa wanasindika mboga zao, na moja ya kiungo walichokuwa wanatumia ilikuwa ni chumvi nyingi sana, kwahio wakazi wa Nagano walikuwa wanakula chumvi kupita kiasi. Kwahio hatua ya kwanza ilikuwa ni kurekebisha chakula chao kwa kupunguza matumizi ya chumvi.

Nilimwambia Busara kwa utani…, kwahio na sisi tukihakikisha watu wanakula chakula bora chenye afya tutapunguza gharama za matibabu…

Aliendelea kama vile hajanisikia, pia walihamasisha maisha ya ukakamavu, waliwashauri watu watembee kwa kutengeneza njia za watu kutembea, pia waliwashauri watu wasistaafu mapema bali waongeze miaka ya kufanya kazi kabla ya kustaafu au wakistaafu wachague kazi nyingine hivyo waishi maisha yenye afya kwa muda mrefu.

Hayo maongezi yalikuwa kama miaka ishirini iliyopita lakini matokeo yake nayaona sasa, watu wana afya katika huu mji, watu wanafanya mazoezi kwenye viwanja vya michezo na wengine wanatembea kila siku au kuendesha baiskeli ingawa hospitali zipo ila ni kama majengo tu ya watu kwenda kucheki afya zao. Watu kuugua ugua katika huu mji sio jambo la kawaida.
 
KAZI YA SITA; Urembo na Mitindo
Mahitaji na matamanio yote ya wakazi yanafanywa na wana jamii wenyewe, hii inajumlisha na vinyozi, saluni n.k. Vitu vyote vinavyohusu urembo na mitindo vinafanyika katika mji, na fursa ya kuyafanya hayo ipo wazi kwa yoyote mwenye ujuzi ili aweze kujipatia kipato kwa kufanya masaa yanayotakiwa katika mwezi husika.

Mfano mimi huwa nina appointment ya kumuona kinyozi wangu na mara nyingi upendelea kuweka kabisa miadi kabla, ingawa hata hapa nikiangalia kwenye simu naweza kuona ni lini au saa ngapi naweza kupata kinyozi, ingawa ni bora nikifanya appointment kabla inakuwa rahisi kazi hio kujulikana mapema ili wanaofanya hio kazi waweze kujipanga.

Kwahio mji huwa unajua kabisa kutokana na order au kutokana na uhalisia wa siku kwa siku, kwamba ni watu wangapi kwa kawaida huwa wananyoa au kusuka, pia kuna wale wanaopenda kusukwa au kunyolewa na Fulani mara nyingi huwa wanatoa appointment ili kinyozi au msusi ajipange. Au ijulikane kama atakuwa tayari kufanya kazi kipindi hicho au atakuwa anafanya jambo lingine au kupumzika.

Hii pia ilikuwa ni kati ya kazi mama tulizoanza nazo tangia huu mji ulivyokuwa kijiji. Watu walikuwa wanasukana, kunyoana, kurembeshana n.k., ingawa baada ya muda jiji liliamua kuweka na hizi shughuli kama ajira ili watu wajipatie kipato kwa kufanya hayo na jiji liweze kupata faida. Hizi kazi na zenyewe huwa zipo kwenye mtandao wa kazi kwa siku, wiki na mwezi ili watu waweze kujisajili kuzifanya au kuchagua kuzifanya

KAZI YA SABA; Usafi na Ukarabati wa Mji
Majengo, nyumba, maeneo ya wazi, na sehemu zote za jamii zinahitaji usafi wa mara kwa mara na sehemu za bustani na maeneo yote ya jiji yanahitaji uangalizi.

Tulijua kuanzia awali, ili mji uweze kuvutia na watu wapende kuishi na kufurahia unahitaji uangalizi ili kuhakikisha haupotezi mvuto wake. Tangia mwanzo tulihakikisha kwamba kila uchafu na mabaki ya uzalishaji mmoja ni malighafi ya uzalishaji mwingine, yaani mabaki na bidhaa zikishatumika zinatumika kama malighafi ya uzalishaji mwingine (recycling) hivyo watu wa usafi na ukarabati wanasaidia sana katika kuhakikisha mabaki na uchafu unakusanywa na kupelekwa sehemu husika ili kufanya uzalishaji mwingine.

Kile mahali kuna sehemu za kutupia taka tofauti sehemu tofauti, hivyo hata wakazi wanasaidia katika kuweka mji safi kwa kutokufanya uchafuzi, utamaduni wa usafi wa wakazi umepelekea mji kuwa msafi na kwa matumizi ya uchafu/mabaki kama malighafi kumesaidia sana sababu kila uchafu na mabaki ni malighafi hivyo unakusanywa kwenda kuzalisha kitu kingine.

Ili kuweza kutumia mabaki kama malighafi, uzalishaji wote na ununuzi wa bidhaa unazingatia kwamba kila kinachozalishwa hakina madhara kwa mazingira na ni rahisi kutumika tena au kutumiwa kama malighafi ya kitu kingine, kwahio matumizi ya vitu kama plastiki au chupa za plastiki hazitumiki kwenye huu mji bali chupa ambazo zinaweza kutumika tena na tena bila kuhitaji utengenezaji kila wakati.

Na ili kurahisisha usafi kuna vifaa vya kusafishia sehemu mbalimbali na sababu mji huu unafanya kazi masaa 24, kuna baadhi ya usafi unafanyika usiku wa manane watu wakiwa wachache ili kutokusababisha kero au kusimama kwa shughuli nyingine.

Ili kufanikisha usafi huu kila mwezi kila nyumba inatoa dollar 10, hivyo jiji linakusanya dollar laki moja kwa ajili ya usafi na ukarabati.
 
kiongozi tupo tunafatilia bado, hivyo endelea kushusha nondo.
Nipo najitahidi kuendelezea si unajua nakimbizwa kimbizwa na hizi hamisha hamisha, mimi Machinga Masikini ?
 
KAZI YA NANE; Usafiri na Usafirishaji
Kwenye miji mingi usafiri na usafirishaji una athari sana katika jamii kwa kuchafua mazingira, ajali, gharama za mafuta na watu kupoteza muda kwenye foleni. Duniani usafiri ni moja kati ya vitu vinavyotumia nishaji nyingi zaidi na kuharibu mazingira kwa kutoa hewa ya ukaa (carbon dioxide emission).

Matumizi mengi ya usafiri ni ya watu kutoka na kwenda makazini na kwenye shughuli zao za kila siku. Kwa ufahamu huu kuanzia mwanzo tuliamua kuweka mji wetu karibu sana na sehemu za uzalishaji (viwanda / eco industial park) na kuhakikisha sehemu hiyo inafikika kwa urahisi na usafiri wa jamii, hivyo kuondoa haja ya watu kuwa na magari binafsi, hii imepelekea kupunguza uchafuzi wa mazingira na gharama kubwa ambayo ingetumika kwenye matumizi ya mafuta, na ukizingatia mabasi yetu ya jamii yote ni ya umeme hii imetusaidia zaidi kupunguza gharama na kutokuwa na uhitaji mwingi wa mafuta.

Pia kutokana na huu usafiri wa jamii mambo ya kuchelewa na kupoteza muda kwenye mji wetu hayajawahi kutokea na sikumbuki kama tumeshawahi kuwa na ajali yoyote ya magari tangia mji huu uanzishwe, tofauti na miji mingine ambayo ajali ni jambo la kila siku.

Miundombinu bora ya huu mji ni pamoja na kituo karibu na kila jengo la watu wanapoishi hivyo mabasi ya jamii ni kama mtu kupaki gari lake mlangoni sababu akilihitaji kila baada ya dakika tano kuna basi linapita hii inasaidia kuwapeleka watu makazini pamoja na kwenye mahitaji yao ya kila siku.

Vilevile kuna magari ya usafirishaji yanayohakikisha bidhaa zinatolewa sehemu ya uzalishaji mpaka sokoni zinapohitajika.

Kwa magari yetu yote ya mjini kutumia umeme, imetusaidia sana, sababu pamoja na kuwa na nishati ya kutosha ya solar inayokusanywa kwenye kila paa la nyumba, pia magari ya umeme hayahitaji matengenezo kama magari ya Mafuta, hivyo gharama za uendeshaji katika usafiri imepungua sana.

Tulipanga kuanzia mwanzo kwamba mji uwe rafiki kwa watembea kwa miguu na waendesha baiskeli, maegesho ya magari yote (car parks) yanapatikana sehemu ya kuingilia na kutokea katika mji, usafiri wa jamii pekee ndio unapatikana ndani ya mjini na unapita kwenye makazi ya watu. Kwa wale wanaotaka magari yao binafsi au magari ya kutumia ili kwenda sehemu nyingine nje ya mji kuna huduma ya kukodisha magari.

Nakumbuka wakati tunajadiri na Busara kuhusu suala la kukodi usafiri, tulikubaliana kabisa kwamba watu wanapenda kumiliki zaidi ya kukodi, lakini tulitambua kama mji ukiwa na mpango wa kukodisha magari kwa gharama nafuu na kuhakikisha katika magari yake kuna gari nzuri na zinazoendana na wakati, vilevile wateja kuweza kuchagua aina tofauti, huenda ikasaidia kufanya watu wapende kujiunga na mpango huu, ukizingatia pia magari haya hayataruhusiwa kupaki kwenye mitaa bali kwenye maegesho ya magari sehemu ya kuingia kwenye jiji ili wanaokuja wayapaki huko au wanaotoka mjini wayapitie huko itasaidia sana kufanikisha mpango huu.

Na sababu hii ya magari kupaki nje ya mji, umesaidia sana kuhakikisha mji wetu hauna kabisa msongamano sababu usafiri wa jamii, watu kutembea na kuendesha baiskeli ndio usafiri pekee ndani ya mji. Kwa ufupi ndani ya mji kuna aina tatu za usafiri, usafiri wa jamii (mabasi n.k.), waendesha baiskeli na watembea kwa miguu…, maegesho ya magari yote ni nje ya mji.

Nakumbuka siku moja wakati tunaongelea hili suala tukiwa watano mimi, mke wangu, rafiki yangu, mke wake na Busara, rafiki yangu alimuuliza Busara…, “Lakini Mzee kwanini watu wapende kukodi kuliko kumiliki magari”

Nilijikuta namjibu kwa kumshangaa…, hivi unaongelea watu gani hao? Sisi ambao hatuna hata baiskeli wala mkokoteni alafu unaongelea kupenda kumiliki? Kwetu sisi lolote ni bora kuliko hiki tulichonacho leo….

Busara alinijibu kwa upole…, kijana kumbuka hali zenu hazitaendelea kuwa hivi…, pili zaidi ya faida za kimazingira za kukodi badala ya kumiliki, mji utatumia njia zifuatazo ambazo zitakuwa na faida na kuleta hamasa kwa watu kuvutiwa na kupenda kukodi badala ya kumiliki…

Ni zipi hizo niliuliza kwa shauku!!!

Moja; uwezo wa kuchagua mipango tofauti ya kukodi; muda mfupi, mrefu au siku baada ya siku.

Mbili; Aina nyingi za magari ya kuweza kuchagua, na vilevile uwezo wa kubadilisha uchaguzi mara kwa mara (leo unaweza ukawa unaendesha Ferrari, kesho Lamborghini na keshokutwa Bugatti…. Na hayo yote utayafanya bila gharama ya ununuzi wala ukarabati.

Mhh niliuliza kwa mshangao!!!, kutoka kuwa machinga mzururaji mpaka dereva ndani ya Bugatti!!!, Hata ingekuwa kupata Punda tu kwangu ningeridhika.... Nilisema kwa kukata tamaa....

Tatu; kutokuwa na wasiwasi wa kukarabati wala gari kuharibika, hivyo kuingia gharama…, sababu mji utawajibika kuhakikisha gari linabakia katika ubora na kushughulikia ukarabati wa aina zote.

Nne; Kwa wale wasiopenda matumizi ya pamoja wana uwezo pia wa kukodi kwa muda mrefu au kuamua gari fulani walitumie peke yao kwa muda wote…, ingawa kama wakipenda vilevile wanaweza kununua yao ingawa wakikodi watapata faida zote ambazo wangezipata kwa kununua bila kero nyingine.

Tano; kupunguza gharama za ununuzi, ukarabati na matengenezo ambavyo vyote vitafanywa na jiji.

Sita; Mji utafanya umiliki wa magari usiwe na umuhimu / sababu ukizingatia maegesho ya magari binafsi ni nje ya mji na magari ya abiria yanafika mpaka mlangoni kwa mkazi. Hivyo kwa suala la usafiri mjini litafanywa vyema na magari ya abiria.

Na hayo ndio tuliyofanya, pamoja na magari ya abiria kuwepo kila wakati, masafi na ya kuvutia vilevile tunaokoa mazingira na hakuna msongamano kabisa ndani ya jiji. Na watu hawapotezi muda wakiwa kwenye usafiri

Na ili kufanikisha yote haya kila mtu isipokuwa wazee anachangia dollar kumi kwa mwezi kwa ajili ya usafiri na usafirishaji, kwa mchango huo kila mkazi anatumia usafiri wa ndani ya jiji yaani mabasi kwa mwezi mzima…. Hivyo jiji linakusanya kutoka kwa watu takriban elfu arobaini kila mmoja dollar kumi; kiasi cha dollar laki nne kila mwezi kinakusanywa kwenda kwenye sekta ya usafiri na usafirishaji.

Na ukizingatia mabasi ya umma ni ya umeme na hayahitaji gharama kubwa za ukarabati na vilevile uvunaji wetu wa nishati ya umeme gharama za uendeshaji zinazidi kupungua.
 
Hatua ya Sita (na Kazi ya Tisa) Nyumba Bora kwa Wote

Unaweza ukajiuliza Nyumba Bora kwa Wote inawezeje ikawa ni kazi…, lakini nitakuelewesha punde. Kama nilivyosema awali katika huu mji kila familia ina makazi bora kabisa, hatuna watu ambao hawana nyumba au wapangaji kwenye nyumba za wengine.

Haikuwa hivyo hapo mwanzo, familia ya kwanza mimi na mke wangu tulikaa kwenye kajumba ka udongo na baada ya hapo tulihamia kwenye mabanda yaliyokuwepo karibu na mifugo yetu ili tuweze kuiangalia kwa ukaribu na kuilinda.

Tuliendelea vivyo hivyo na kwa familia zilizokuwa zinakuja tuliendelea kujenga mabanda ya muda ili na wao weweze kuishi. Baada ya miaka kadhaa tuliamua kuanza kujenga kulingana na ramani ambazo tulikuwa tumepanga kuanzia mwanzo.

Nyumba ambazo zinakusanya nishati, nyumba ambazo zinasaidia mazingira kwa kufanya recycling na nyumba ambazo zinapendeza na kujengwa kwa mpangilio bila kuchukua nafasi kubwa na kufikika kwa urahisi kwa usafiri mpaka mlangoni. Kuanzia mwanzo ujenzi wa nyumba ulifanyika kutokana na mahitaji na sio kujenga ilimradi tu ili kukusanya kodi, yaani ujenzi unazingatia mahitaji ya watu ambao idadi yao inazingatia uwepo wa shughuli za kujipatia kipato na uzalishaji uliopo wa mahitaji yao.

Ujenzi wa nyumba haukuwa mgumu sababu kutokana na idadi ya nyumba tulizohitaji (economy of scale) yaani ukihitaji vitu vingi vya aina moja ni rahisi gharama ya kila kimoja kupungua. Tulianza kwanza na nyumba 100, ingawa mkataba wa tender na kampuni ya ujenzi walijua kabisa mwisho wa siku tutakuwa na nyumba za kuishi yaani maghorofa 833 na mahoteli, migahawa, shule na majengo mengine mengi.

Nakumbuka wakati familia zimeongezeka kidogo na watu bado wanaishi kwenye mabanda kuna siku jamaa mmoja mtata sana…, alitufuata mimi mimi na Busara tulipokuwa tumepumzika baada ya kazi nzito ya siku…, kipindi hicho tulikuwa tunapiga kazi kwelikweli na sio masihara….., basi bwana huyu akauliza hivi kwanini tusiwajengee watu nyumba za gharama nafuu ?

Busara alijibu baada ya muda mrefu sana, jamaa alidhani labda hajasikia, alivyokuwa anataka kuuliza tena Busara alianza kujibu…, “Nadhani huu ni muda muafaka wa kutambua kwamba nyumba za gharama nafuu sio nafuu…, kwa lugha nyepesi kuwajengea nyumba za gharama nafuu watu wasio na kipato haiwezekani.

Niliona jamaa amepigwa na butwaa, nilijua kabisa kwenye fikra zake alikuwa anaanza kujuta kuja kwake kwenye hiki Kijiji kama Maisha yake yake yote yataishia kwenye hayo mabanda tunayoishi.

Busara aliendelea, narudia tena kama nilivyowahi kumwambia mwenzako, hapa duniani hakuna cha bure…. Vilevile nyumba za gharama nafuu sio nafuu…, Kwenye hizi tunazoita nyumba za gharama nafuu, kuna tofauti kubwa sana baina ya gharama za ujenzi na kodi ambazo watu wengi wanaweza kulipa. Hivyo basi bila kupata ruzuku au misaada kutoka sehemu, ujenzi wa nyumba hizi hauwezekaniki.

Nilijikuta naamuliza Busara, sababu nilijua kabisa nyumba bora ni hatua moja katika hatua zile kumi…, Sasa umepanga mikakati gani ya kuhakikisha sisi tunajenga hizo nyumba?

Busara aliendelea kama vile hajanisikia…, ujenzi unatumia gharama kubwa sana, na makampuni ya ujenzi na wakandarasi wanategemea mikopo na njia nyingine za kupata pesa ili kugharamia ujenzi kabla ya wakazi ambao watakuwa wapangaji wataweza kuishi na kuanza kulipa kodi.

Kwahio utaona kwa ufupi wakandarasi na wajenzi watashiriki iwapo tu kama wakazi watakaoishi kwenye hizo nyumba watakuwa na uwezo wa kulipa au ujenzi huo utaleta pesa ya kulipia mikopo na kuzalisha faida kwa hao wawekezaji.

Kwahio kwa ufupi kama ujenzi hauna uhakika wa mkandarasi / mwekezaji kulipa mikopo hakuna uwezekano wowote wa mwekezaji huyo kupata fedha za huo mradi.

Nilianza kumuelewa Busara…, Naam niliongezea kwa furaha kwahio kwa sisi wakazi tukiwa na kipato hivyo kuwa na uwezo wa kulipa, kununua na kukarabati hizo nyumba mradi wote utakuwa unawezekana?

Naam…, alijibu Busara, kama nilivyokwambia siku ya kwanza tulivyokutana kwamba sisi masikini na wabangaizaji kwa nguvu na umoja wetu tutaweza kufanikisha kubadilisha Maisha yetu toka umasikini na kuwa matajiri bila kuhitaji msaada wa mtu yoyote, na mwisho wa siku gharama zote tutazilipia…

Hio ilikuwa miaka kadhaa kabla hatujakutana na wakandarasi wa kujenga nyumba zetu. Baada ya kufanya uchunguzi tuliongea na wachina ili watujengee kwa mkataba wa kuwalipa polepole. Tulichagua wachina sababu nyumba tulizoamua kujenga ni zile kwa lugha ya kigeni zinaitwa Pre-Fabricated Houses (yaani hizo nyumba kuta na sehemu nyingine zinatengenezwa kiwandani alafu kwenye site ni kuja kuziunganisha. Ujenzi huu ni wa gharama nafuu, rahisi kujenga, salama, hauharibu mazingira na ujenzi unafanyika kwa haraka bila kuharibu au kuchafua maeneo ambayo ujenzi unafanyikia.

Na kuwachagua wachina na si wengine ni baada na kuvutiwa na ujenzi waliofanya wa kujenga hoteli ya ghorofa thelasini kwa muda wa siku kumi na tano tu! Kwa kweli hilo lilituvutia sana… tuliwasiliana nao ili watusaidia kutengeneza kiwanda kwenye Kijiji chetu cha kuweza kutengeza hizo nyumba ukizingatia tulijua ujenzi utakuwa endelevu na baada ya kumaliza kutakuwa na ukarabati wa mara kwa mara hivyo tulionelea kuliko kuangiza hizo malighafi kutoka Uchina ni bora zikitengenezewa mjini kwetu.

Tuliingia mkataba wa kujenga nyumba hizo ambapo malipo yalikuwa ni ya muda mrefu na sababu walitufundisha na nguvu kazi na malighafi tulikuwa tunatoa kwetu gharama ya ujenzi ilipungua maradufu.

Kwa wakazi nyumba hizi za ghorofa nne zenye nyumba nne kwenye kila sakafu ni za ubora wa hali ya juu, na kila mtu anaweza kulipia sababu tulimpa kila mmiliki mpango wa malipo ya muda mrefu bila kulipia riba yoyote…, kwahio kila mkazi alipewa fursa ya kununua nyumba kwa malipo ya muda mrefu bila riba, na pesa hiyo ilikuwa inakatwa kutoka kwenye mshahara.

Na kwa kuhakikisha hakuna mtu atakayekosa makazi hata kama mnunuzi katika familia akifa waliobaki katika familia hiyo wanaweza kuendelea na malipo ya nyumba ili kumalizia deni na mwisho wa siku nyumba kuwa ya kwao.

Ili kuhakikisha hakuna watakaotumia mpango huu vibaya kwa kununua hizi nyumba na baadae kutaka kupangisha wengine au kuwauzia wengine, tuliweka sheria kwamba yoyote atakayetaka kuuza nyumba anaweza kuuza nyumba hiyo kwa jiji pekee kwa gharama ya uhitaji wa nyumba wa wakati huo na si vinginevyo! Tulijua tukiachia holela kutaleteleza bei za nyumba kupanda na kushuka na vilevile kutakuwa na nyumba nyingi au chache kulinganisha na mahitaji. Kwa maana hiyo mtu aliyenunua nyumba au anayelipia nyumba ili ije kuwa yake, anaweza wakati wowote ule akiamua kuuza akauza nyumba hiyo na jiji litanunua hiyo nyumba kwa bei husika ya wakati wa kuuza. Na hii imepelekea wengine kuona nyumba kama mafao yao ya uzeeni, yaani wakizeeka wanaweza kuuza hio nyumba na hizo pesa kutumia katika uzee wao na wenyewe wakitaka wanaweza kuamia kwenye nyumba za wazee.

Mji wetu unajenga nyumba kulingana na mahitaji, uwezo wa mji na nguvu kazi inayohitajika katika uzalishaji, na hii imepelekea kutokuwa na idadi ya watu zaidi ya uwezo wa mji…, ingawa bado tunapata maombi ya watu kuhamia katika mji wetu ila kuna mpango wa kuwasaidia na wenyewe wajenge mji wao pengine ili ufanisi usipungue, ukizingatia na wenyewe kuwa na mji wao tutakuwa tumeongezea nguvukazi na idadi ya wanunuzi wa uzalishaji.

Kama nilivyosema awali hizi nyumba zetu pia ni vituo vya kukusanyia nishati, kila jengo kwenye huu mji limewekewa solar panels kwahio kwa nyumba zetu 833 ambazo kila jengo lina ukubwa wa futi za mraba 4,000; zinatoa jumla ya zaidi ya ekari 76 za solar panels. Na kupunguza matumizi ya battery, nishati hii inayokusanywa inawekwa moja kwa moja kwenye grid / umeme wa mji, hii imesaidia sana kutokuwa na battery kila nyumba hivyo kupunguza gharama za ukarabati na ununuzi wa battery mpya.

Nyumba hizi pia zinatumika kama vituo vya recycling. Kila mkazi amewekewa sehemu za kutupia taka tofauti, na vilevile uchafu wa chooni wote kutoka kwenye majengo kukusanywa mpaka sehemu ya mbali na baada ya muda kutumika kama mbolea ya kuoteshea mazao ambao siyo ya chakula kwa ajili ya kuzalishia nishati.

Maji ya kuoshea na kuongea hayo pia yanakusanywa na kutumika katika umwagiliziaji.

Na kama nilivyosema kila mkazi mwenye nyumba amepewa fursa ya kumiliki nyumba kwa malipo ya muda mrefu bila riba, makato hayo ya nyumba yanakatwa kila mwezi kwenye mshahara; kila nyumba inalipia dollar 100 inayokusanywa ili aje awe mmiliki, kwahio kwa mwaka kila nyumba inatoa dollar 1,200.

Kwahio kama ulijiuliza kwanini hizi nyumba pia nimesema ni kazi, ingawa ujenzi utakuwa ni wa mara moja tena huenda ukachukua siku chache, ila ukarabati wa nyumba hizo utakuwa ni wa Maisha. Hii ikimaanisha kwamba watu wataajiriwa ili kuangalia, kukarabati na kuhakikisha nyumba hizo zinakaa katika ubora.
 
HATUA YA SABA – UHAKIKA WA MAHITAJI MUHIMU KWA WOTE

Ni jambo la kushangaza kwa dunia ya leo kuwa na sehemu ambayo kila kiumbe sio tu kuwa na uhakika wa chakula, malazi, na mavazi..., bali kubaki na nyongeza ya kula raha!!!, na hayo yote sio kwa kutegemea hisani ya fulani au kuomba kwa fulani ni kwa kila mtu kutumia jasho lake kadri ya uwezo na mapenzi yake. Na mahitaji hayo anayapata sio kwa kuwa mtumwa wa kazi bali kwa kufanya kazi chache na kwa muda mchache iwezekanavyo, huku akibakiwa na muda wa kutosha kustarehe na kutumia kipato chake..., Ndio maana starehe na burudani ni moja ya nguzo muhimu sana kwenye mji wetu....

Hayo yameweza kufanikiwa kutokana na mji kuhakikisha kila mtu ana nyumba (makazi bora), yanayodumishwa kila wakati (kuna watu ambao ni kazi zao kuhakikisha yanasafishwa na kila ukarabati unapohitajika unafanyika).

Makazi hayo kuwa bora na kudumishwa kila wakati kumewezekana kwa kuwa mji ulihakikisha kila mtu ana ujuzi wa kuweza kufanya kazi zilizopo katika eco-industrial park iliyopo, na hivyo mwanajamii huyu kuweza kujipatia kipato cha kuweza kustahimili maisha ndani ya mji, ikiwemo chakula, matibabu, elimu kwa watoto wake, na kama mtoto ni yatima jamii inahakikisha mtoto huyu anaelimika ili mwisho wa siku aweze kuwa na mchango chanya kwa jamii.

Kila mtu ana Mpango Mzuri wa Uzeeni, baada ya kustaafu jamii imehakikisha kila mtu anazawadiwa kwa kuangaliwa anapozeeka, (nyumba za wazee, na uangalizi wa masaa 24 kila unapohitajika kutoka kwa wauguzi)

Sababu kuu ya mji wetu kufanikiwa ni kwa kuzingatia aliyosema Busara, "Duniani hakuna kitu cha bure"..... Na kwa misingi hiyo badala ya kutoa misaada au vitu vya bure ambavyo mwisho wa siku watu hawavijari au kuvifuja au kuwa duni sababu ya kukosa fedha na mitaji, tulihakikisha hakuna kitu cha bure bali kila kitu kina bei nafuu inayolingana na kipato cha wanajamii, na hilo liliwezekana kutokana na kwamba mji wetu kigezo cha kwanza sio kutengeneza faida kubwa iwezekanavyo bali ni kutoa huduma kwa gharama ndogo iwezekanavyo na kwa kuzalisha huduma kwa ufanisi na gharama ndogo iwezekanavyo. na kwa uwepo wa wateja wakutosha hata zile bidhaa ambazo hazitengenezwi kwenye mji zinanunuliwa kwa jumla hivyo uwezo wa mji kupata bei ndogo kwa bidhaa hizo.

Kwa ufupi mji umehakikisha kila mwanajamii ana fursa ya kupata kipato cha kumuwezesha kupata mahitaji yake yote muhimu. Kipato hicho anakipata kwa kufanya kazi zinazopatikana ndani ya mji na kazi hizo mji umehakikisha ni kazi tofauti zenye ujuzi tofauti. Kila mwanajamii (ambaye kwenye mji wetu ana ujuzi tofauti tofauti - multi skills) hawezi kukosa kazi yenye ujira ya kufanya pindi anapohitaji pesa....., na ukizingatia kazi zote ngumu tumeweza kuzirahisha na kuwa nyepesi hakuna mtu yoyote katika huu mji anayekosa shughuli ya kufanya ili kujipatia ujira.

Nakumbuka Busara alikuwa anapenda sana msemo wa "Looking after People from Cradle to the Grave),na katika kijitabu chake kulikuwa na mchoro ufuatao
cradle to the grave.png
Nakumbuka zamani wakati wa mlo wa mchana, tukiwa tunapanga mikakati ya muda mrefu mimi, Busara, Mke wangu, rafiki yangu na mke wake..., Busara alisema Mji wa kwenye fikra zangu ni mji unaoangalia watu wake from Cradle to the Grave...., Yaani tangia mtoto anazaliwa, kuhakikisha anapata elimu na ujuzi wa baadae kuweza kufanya shughuli na kupata ujira na hata siku akifa...., Mji utahakikisha hata mazishi yake yanashughulikiwa na mji....

Nini ?!!!!...., Nilijikuta ninapaliwa na tonge ugali na kumuangalia Busara huenda kinywaji alichokuwa anakunywa kilikuwa na kilevi....

Busara aliendelea, tunaona kwa sasa hata kitu kama kifo kinavyogharimu ndugu wa marehemu, yaani mazishi yamekuwa gharama sana katika maisha ya Mwanajamii...

Na wewe unataka kulipia yote hayo ?!! Rafiki yangu alimuuliza Busara kwa mshangao...

Sio moja kwa moja....., lakini kama imani itaruhusu na sababu ardhi imekuwa malighafi kubwa sana na matumizi ya ardhi ni ya manufaa makubwa kwa mji na vizazi vijavyo basi mji utatoa huduma ya Cremation..., na kwa kutoa motisha kwa watu kukubali cremation badala ya kuzika mji utatumia baadhi ya majivu yanayobaki kutengenezea almasi.., jambo ambalo litakuwa ni zuri kwa watu kuwakumbuka wapendwa wao walioaga dunia....

Ingawa nitapenda kungaa kama Almasi nitakapokufa ila hii inawezekana vipi..., alisema mke wa rafiki yangu.

Busara aliendelea kama vile hajasikia swali..., Gharama ya kutengeneza almasi kwenye maabara imeshuka sana, kuna sehemu nilisoma hapo zamani iligharimu USD 4000 kwa carat moja ingawa sasa hivi imeshuka hadi USD 300 kwa carat, kwahio kwa mji kuchangia gharama hizi itakuwa imeokoa ardhi ambayo ingetumika kwa makaburi....

Haya nayawaza nikiwa hapa kwenye Jengo la Makumbusho ambalo wachache walioamua kuwa - cremated kuna almasi zao na taarifa za maisha yao naangalia Almasi inayoitwa Busara, na nyingine chache....., sio nyingi sana mpaka sasa sababu vifo katika mji wetu ni vichache sana life expectancy ya watu ni miaka 90 mpaka mia na ushee... Busara mwenyewe alikufa akiwa na miaka mia na kitu...

Kwahio Almasi moja inakaa makumbusho na nyingine kadri wanajamii wanavyotaka wanapewa ili wazitunze au hata wakitaka wazivae; mwisho wa siku unaweza ukawa na almasi ya vizazi na vizazi, tokea babu mzaa mababu mpaka wajukuu na vitukuu...
 
HATUA YA SABA – UHAKIKA WA MAHITAJI MUHIMU KWA WOTE

Ni jambo la kushangaza kwa dunia ya leo kuwa na sehemu ambayo kila kiumbe sio tu kuwa na uhakika wa chakula, malazi, na mavazi..., bali kubaki na nyongeza ya kula raha!!!, na hayo yote sio kwa kutegemea hisani ya fulani au kuomba kwa fulani ni kwa kila mtu kutumia jasho lake kadri ya uwezo na mapenzi yake. Na mahitaji hayo anayapata sio kwa kuwa mtumwa wa kazi bali kwa kufanya kazi chache na kwa muda mchache iwezekanavyo, huku akibakiwa na muda wa kutosha kustarehe na kutumia kipato chake..., Ndio maana starehe na burudani ni moja ya nguzo muhimu sana kwenye mji wetu....

Hayo yameweza kufanikiwa kutokana na mji kuhakikisha kila mtu ana nyumba (makazi bora), yanayodumishwa kila wakati (kuna watu ambao ni kazi zao kuhakikisha yanasafishwa na kila ukarabati unapohitajika unafanyika).

Makazi hayo kuwa bora na kudumishwa kila wakati kumewezekana kwa kuwa mji ulihakikisha kila mtu ana ujuzi wa kuweza kufanya kazi zilizopo katika eco-industrial park iliyopo, na hivyo mwanajamii huyu kuweza kujipatia kipato cha kuweza kustahimili maisha ndani ya mji, ikiwemo chakula, matibabu, elimu kwa watoto wake, na kama mtoto ni yatima jamii inahakikisha mtoto huyu anaelimika ili mwisho wa siku aweze kuwa na mchango chanya kwa jamii.

Kila mtu ana Mpango Mzuri wa Uzeeni, baada ya kustaafu jamii imehakikisha kila mtu anazawadiwa kwa kuangaliwa anapozeeka, (nyumba za wazee, na uangalizi wa masaa 24 kila unapohitajika kutoka kwa wauguzi)

Sababu kuu ya mji wetu kufanikiwa ni kwa kuzingatia aliyosema Busara, "Duniani hakuna kitu cha bure"..... Na kwa misingi hiyo badala ya kutoa misaada au vitu vya bure ambavyo mwisho wa siku watu hawavijari au kuvifuja au kuwa duni sababu ya kukosa fedha na mitaji, tulihakikisha hakuna kitu cha bure bali kila kitu kina bei nafuu inayolingana na kipato cha wanajamii, na hilo liliwezekana kutokana na kwamba mji wetu kigezo cha kwanza sio kutengeneza faida kubwa iwezekanavyo bali ni kutoa huduma kwa gharama ndogo iwezekanavyo na kwa kuzalisha huduma kwa ufanisi na gharama ndogo iwezekanavyo. na kwa uwepo wa wateja wakutosha hata zile bidhaa ambazo hazitengenezwi kwenye mji zinanunuliwa kwa jumla hivyo uwezo wa mji kupata bei ndogo kwa bidhaa hizo.

Kwa ufupi mji umehakikisha kila mwanajamii ana fursa ya kupata kipato cha kumuwezesha kupata mahitaji yake yote muhimu. Kipato hicho anakipata kwa kufanya kazi zinazopatikana ndani ya mji na kazi hizo mji umehakikisha ni kazi tofauti zenye ujuzi tofauti. Kila mwanajamii (ambaye kwenye mji wetu ana ujuzi tofauti tofauti - multi skills) hawezi kukosa kazi yenye ujira ya kufanya pindi anapohitaji pesa....., na ukizingatia kazi zote ngumu tumeweza kuzirahisha na kuwa nyepesi hakuna mtu yoyote katika huu mji anayekosa shughuli ya kufanya ili kujipatia ujira.
Swala la ulinzi nalo, lilizingatiwa katika huo mji?
swala la uongozi je lilibaki kwa mzee busara na machinga?
 
Swala la ulinzi nalo, lilizingatiwa katika huo mji?
Swala la ulinzi nadhani lipo kwenye hatua kadhaa vilevile ukizingatia huu mji ni Smart; Self Managed Transparency community kama (Hatua ya Kwanza inavyosema) Kuwa na Mji unaojiendesha kwa Uwazi - Hatua ya Kwanza "Miundo Mbinu Sahihi" Kwahio ukiwa na CCTV Cameras kila mahali hata kwenye maduka na supermarkets hauhitaji hata wauzaji ni mtu kuchukua bidhaa kuscan barcode na pesa automatically inakuwa deducted kwenye salio lako....
swala la uongozi je lilibaki kwa mzee busara na machinga?
Self Managed Transparent Community; Hakuna uhitaji wa kiongozi mmoja, bali jamii nzima inajiongoza kulingana na misingi iliyojiwekea..., kila changamoto ikitokea kuna fursa ya mikutano na kubadilishana mawazo (online na offline) mtu yoyote anatoa dukuduku na wadau kwa ujumla kulishughulikia ingawa wazee wapo na wanafanya kazi ya Thinktanks na ushauri..., Kila Tatizo na suluhisho lake ambalo lilishafanyika nyuma linajulikana likitokea tena inajulikana ni nini cha kufanya.

Nadhani Step Number Tisa: Continuous automation and Innovation from All itajibu vizuri hili suala
 
HATUA YA NANE: UFANISI - (Kila Uchafu ni Malighafi na kila Nishati inakusanywa) - Every Waste Recycled and every Energy Collected)

Kama tulivyoona katika Hatua ya Tano; Fursa ya Kupata Kipato, kama umechagua kwa kipindi hicho kufanya shughuli ya usafi (yaani kuhakikisha mji ni msafi) moja ya kazi hizo za usafi ni kukusanya uchafu / mabaki ya bidhaa ili yawe recycled (kutengeneza bidhaa mpya au kutumika kuzalisha nishati).

Mtambo wa Biogas uliopo katika eneo la Eco Industrial Park linakusanya mabaki yote kutoka kwenye makazi ya watu, migahawa viwanda, sehemu za ufugaji na sehemu zote za mji. Yaani kila mabaki ambayo yanaweza kubadilishwa na kuwa Biogas mtambo huu unafanya hivyo.

Kama nilivyosema hapo awali nyumba sio makazi ya watu pekee bali pia ni viwanda na vyanzo vya malighafi, yaani hata unapokwenda chooni ule uchafu unakusanywa na kupelekwa kwenye mabomba sehemu ya mbali na mji na baada ya muda uchafu huo unabadilika kuwa mbolea inayotumika kwenye miti na mimea ambayo inatumiwa kuzalisha nishati.

Tuliamua kutokea mwanzo kwamba mji lazima ujitosheleze kwa nishati na hata ziada ambayo inaweza kupelekwa kwenye miji jirani kama itakuwa na uhaba. Kila chanzo cha nishati kilichopo kinatumika, hii ni pamoja na hekari kama 75 za solar panels ambazo zipo kwenye kila paa la majengo ya huu mji.

Kwenye huu mji hakuna tone la maji linalopotea bure au kufanya kazi mara moja, hata maji yanakuwa recycled !

Water Recycling kwenye Mji; Kwenye mji wetu kuna Matumizi Makubwa ya Maji ya Aina Tatu:-
1: Maji yanayotumiwa kwenye Vyoo: Haya maji yanakusanywa kutoka kwenye kila choo cha kwenye nyumba za makazi na vyoo vingine vyote vilivyopo kwenye mji na kupelekwa sehemu moja na kuwa composted (kutengeneza mboji) itakayotumika kwenye mazao yasiyo ya chakula (misitu na mazao mengine ya kuzalisha nishati)

2: Grey Water (Maji yanayotumika kuogea, kufulia na kuoshea vyombo): haya yanakusanywa na kupelekwa kwenye eco industrial park tayari kutumiwa kwa umwagiliziaji, bustani zote za kwenye mji zinamwagiliziwa kwa kutumia haya maji.

3: Dark Water (Maji Machafu yenye Vinyesi vya Watu): haya yanakusanywa katika sehemu maalumu na kutengeneza mboji tayari kwa kutumika kama mbolea kwenye mazao yasio ya chakula ya muda mfupi yanayotumika kuzalisha nishati.

Pia mji huu tangia mwanzo nguzo yake kubwa ilikuwa ni ciricular mode of production; nakumbuka mchoro uliokuwepo kwenye kile kitabu alichonipa Busara siku ile nikutane nae enzi za umachinga wangu

recycle.png
Nakumbuka maneno ya Busara wakati ananielewesha kuhusu tunavyoishi kwa kukosa ufanisi...., Busara alisema kwenye Uchumi wa sasa ambao ni Linear Economy; Malighafi zinachukuliwa kutoka kwenye mazingira, zinabadilishwa kuwa bidhaa, zinatumiwa na mwisho wa siku zinatupwa kama uchafu hivyo kuchafua mazingira. Wakati kama tungebadilika na kutumia mfumo wa Circular Economy kwanza kabisa bidhaa zingetengenezwa ili zidumu na kila bidhaa inayotengenezwa ingezingatia kwamba bidhaa hio inazingatia Re-Use; Re-Pair; Re-Furbish na Re-Cycle bila kusahahu kutumia bidhaa nzee au zilizoisha kama malighafi ya bidhaa nyingine, yaani kutupa bidhaa ni hatua ya mwisho kabisa na kama hakuna uwezekano wa bidhaa hio kutumika tena basi ni bora isitengenezwe...

Na hayo ndio tunayofanya sasa na kwa ufanyaji huu tumepunguza upotevu kwa hatua kubwa sana na kuongeza ufanisi.

Hata kwa zile bidhaa ambazo hazitengenezwi na mji wetu tunafanya kazi na makampuni ambayo tunahakikisha yanakidhi..., yaani bidhaa zao zinadumu na zinaweza kuwa recycled au kutumika tena kama malighafi ya bidhaa nyingine. Na kwa kufanya hivi kumetusaidia kutokutegemea malighafi chache ambazo nyingine ni shida kupatikana hivyo kuepuka kupanda kwa bei kwa kutegemea malighafi hizo.
 
swala la uongozi je lilibaki kwa mzee busara na machinga?
Hii ni Post namba 13 inaongelea Uongozi...

Mji unaojiendesha kwa Uwazi
Kwa mgeni mjini anaweza kushangaa jinsi mambo yanavyojiendesha vizuri, wengi huwa wanashangaa ni nani anayepanga nini kifanyike. Ufanisi huu hauna kiongozi wala mpangaji, hauna bosi wa kupanga wala Muelekezaji.

Yote yanafanyika kwa uwazi na kwa kutumia teknolojia. Kazi zote zinazohitajika kufanywa kwa mwezi mzima zipo wazi kwenye mtandao, kila bidhaa zikipungua mfano kuna juice inayopendwa sana na inapatikana kwenye supermarket na kwenye migahawa kila inaponunuliwa idadi inapungua kwenye takwimu, taarifa hii inapelekwa kwa wazalishaji ili kujua kiasi gani zaidi kinahitaji kuzalishwa na wasambazaji ili kujua ni idadi gani inabidi ipelekwe kwenye mgahawa husika au supermarket. Na uzalishaji huo unaotakiwa unapelekea kupanga ni idadi gani ya wazalishaji wanatakiwa.

Miamala yote ya pesa inafanyika kwenye mtandao, malipo na mishahara yote ni kwenye mtandao, ingawa malipo haya yanasaidia shughuli za ndani na kuwezesha wakazi, ila kuna pesa inayotakiwa kununua bidhaa zinazohitajika na hazizalishwi ndani, hivyo bidhaa zote zinazozalishwa na kuuzwa nje pesa huwa inahifadhiwa ili iweze kutumika kununua bidhaa kutoka nje.

Mji huu ingawa hauna kiongozi, bali kuna mikutano ya mara kwa mara ya kupanga mikakati ambayo mtu yoyote anaweza kuhudhuria na katika kila uamuzi wa uwekezaji wazo linaweza kutoka kwa yoyote baada ya kufanya upembuzi yakinifu lakini kabla ya kufanya uwekezaji huo mijadala huwa inafanyika kuona kama uwekezaji huo unafaida za kiuchumi na kimazingira. Na ili kutumia busara na ujuzi wa wazee wetu huwa tunawatumia sana kwenye mambo ya ushauri.

Kwahio utaona kuwa katika mji wetu hakuna uwezekano wa ufujaji wala ufisadi, kila kitu kipo wazi na yoyote yule anaweza kuangalia na kuona ustawi wetu kama jamii.

Tuliamua kila kitu kiwe kwa uwazi na kutumia teknolojia ili mji ujiendeshe kuepuka ufujaji na lile lililomtokea Busara na Kampuni yake lisijirudie tena.
 
HATUA YA NANE: UFANISI - (Kila Uchafu ni Malighafi na kila Nishati inakusanywa) - Every Waste Recycled and every Energy Collected)

Kama tulivyoona katika Hatua ya Tano; Fursa ya Kupata Kipato, kama umechagua kwa kipindi hicho kufanya shughuli ya usafi (yaani kuhakikisha mji ni msafi) moja ya kazi hizo za usafi ni kukusanya uchafu / mabaki ya bidhaa ili yawe recycled (kutengeneza bidhaa mpya au kutumika kuzalisha nishati).

Mtambo wa Biogas uliopo katika eneo la Eco Industrial Park linakusanya mabaki yote kutoka kwenye makazi ya watu, migahawa viwanda, sehemu za ufugaji na sehemu zote za mji. Yaani kila mabaki ambayo yanaweza kubadilishwa na kuwa Biogas mtambo huu unafanya hivyo.

Kama nilivyosema hapo awali nyumba sio makazi ya watu pekee bali pia ni viwanda na vyanzo vya malighafi, yaani hata unapokwenda chooni ule uchafu unakusanywa na kupelekwa kwenye mabomba sehemu ya mbali na mji na baada ya muda uchafu huo unabadilika kuwa mbolea inayotumika kwenye miti na mimea ambayo inatumiwa kuzalisha nishati.

Tuliamua kutokea mwanzo kwamba mji lazima ujitosheleze kwa nishati na hata ziada ambayo inaweza kupelekwa kwenye miji jirani kama itakuwa na uhaba. Kila chanzo cha nishati kilichopo kinatumika, hii ni pamoja na hekari kama 75 za solar panels ambazo zipo kwenye kila paa la majengo ya huu mji.

Kwenye huu mji hakuna tone la maji linalopotea bure au kufanya kazi mara moja, hata maji yanakuwa recycled !

Water Recycling kwenye Mji; Kwenye mji wetu kuna Matumizi Makubwa ya Maji ya Aina Tatu:-
1: Maji yanayotumiwa kwenye Vyoo: Haya maji yanakusanywa kutoka kwenye kila choo cha kwenye nyumba za makazi na vyoo vingine vyote vilivyopo kwenye mji na kupelekwa sehemu moja na kuwa composted (kutengeneza mboji) itakayotumika kwenye mazao yasiyo ya chakula (misitu na mazao mengine ya kuzalisha nishati)

2: Grey Water (Maji yanayotumika kuogea, kufulia na kuoshea vyombo): haya yanakusanywa na kupelekwa kwenye eco industrial park tayari kutumiwa kwa umwagiliziaji, bustani zote za kwenye mji zinamwagiliziwa kwa kutumia haya maji.

3: Dark Water (Maji Machafu yenye Vinyesi vya Watu): haya yanakusanywa katika sehemu maalumu na kutengeneza mboji tayari kwa kutumika kama mbolea kwenye mazao yasio ya chakula ya muda mfupi yanayotumika kuzalisha nishati.

Pia mji huu tangia mwanzo nguzo yake kubwa ilikuwa ni ciricular mode of production; nakumbuka mchoro uliokuwepo kwenye kile kitabu alichonipa Busara siku ile nikutane nae enzi za umachinga wangu

Nakumbuka maneno ya Busara wakati ananielewesha kuhusu tunavyoishi kwa kukosa ufanisi...., Busara alisema kwenye Uchumi wa sasa ambao ni Linear Economy; Malighafi zinachukuliwa kutoka kwenye mazingira, zinabadilishwa kuwa bidhaa, zinatumiwa na mwisho wa siku zinatupwa kama uchafu hivyo kuchafua mazingira. Wakati kama tungebadilika na kutumia mfumo wa Circular Economy kwanza kabisa bidhaa zingetengenezwa ili zidumu na kila bidhaa inayotengenezwa ingezingatia kwamba bidhaa hio inazingatia Re-Use; Re-Pair; Re-Furbish na Re-Cycle bila kusahahu kutumia bidhaa nzee au zilizoisha kama malighafi ya bidhaa nyingine, yaani kutupa bidhaa ni hatua ya mwisho kabisa na kama hakuna uwezekano wa bidhaa hio kutumika tena basi ni bora isitengenezwe...

Na hayo ndio tunayofanya sasa na kwa ufanyaji huu tumepunguza upotevu kwa hatua kubwa sana na kuongeza ufanisi.

Hata kwa zile bidhaa ambazo hazitengenezwi na mji wetu tunafanya kazi na makampuni ambayo tunahakikisha yanakidhi..., yaani bidhaa zao zinadumu na zinaweza kuwa recycled au kutumika tena kama malighafi ya bidhaa nyingine. Na kwa kufanya hivi kumetusaidia kutokutegemea malighafi chache ambazo nyingine ni shida kupatikana hivyo kuepuka kupanda kwa bei kwa kutegemea malighafi hizo.
popote pale changamoto hazikosekani, mji huu unakumbwa na changamoto zipi?
 
Back
Top Bottom