Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
- Thread starter
- #21
KAZI YA TATU; Starehe na Ubudurishaji
Katika mji huu watu tunalipwa vizuri ujira unaotosha mahitaji yetu yote na kubakia na ziada, ukizingatia muda wa kufanya kazi ni mchache, watu wana muda mwingi wa kustarehe na kufurahia maisha yao, ndugu na rafiki zao, hivyo sekta ya kuburudisha na starehe ni muhimu sana kuhakikisha watu wanaburudika.Mambo ya michezo, burudani, mziki, utalii, vyakula, maeneo ya burudani, michezo n.k. vipo kwa wingi kwenye huu mji. Vilevile mji unajipatia kipato kutokana na uwepo wa haya maeneo na shughuli za starehe kwa watu kutumia pesa zao za ziada ambapo jiji linafaidika na kupata uwezo wa kuendelea kutoa huduma kwa wakazi.
Kwahio pamoja na kuwafanya watu wasichoke na kukosa cha kufanya hii sekta inawafanya watu wawe na furaha na vilevile mji unajipatia kipato.
Katika shule na chuo watu wanafundishwa mambo ya sanaa na mara kwa mara wanatoa kazi kama maigizo na sanaa tofauti ambazo zinawekwa sokoni ili wakazi waweze kuburudika.
Mji wetu una timu za mpira wa miguu, timu hizi huwa zinategemea kwa wakati husika kuna vipaji kiasi gani. Mfano sasa tuna timu tatu sababu tuna vijana kama 150 wenye vipaji kwahio kuliko kuwa na timu moja na wengine kucheza na wengine kukaa bench, tuliamua tutakuwa na timu nyingi kadri ya vipaji kwa wakati husika.
Hawa wachezaji wote 150, uchezaji wao pia unahesabika kama ajira, na wao wanalipwa kama wengine kwa mwezi ujira wao wa dollar 500, ambayo tayari ipo katika gharama ya mishahara kwa mwezi. Huwa tuna michezo kama minne kila mwezi, na ticket ya mpira huwa ni kama Dollar Tano, kwahio mtu akiangalia mechi nne kwa mwezi ni dollar 20 hivyo kama watu 4,500 kutoka kwenye watu elfu hamsini wakiangalia kila mechi tayari hizi timu zinakuwa zimejilipa mishahara, na hapo bado faida nyingine za watu kununua nguo zenye nembo ya timu n.k, kwahio hizi timu zinaongezea kipato sana mji wetu na pia kuleta umoja na kujivunia, kwa sasa timu zetu mbili kati ya hizi tatu zipo kwenye ligi kuu.
Nakumbuka Busara aliwahi kuniambia, tunataka kutengeneza jamii yenye furaha…. Nakumbuka nilikuwa nimechoka hio siku, nikamuuliza kwa dhihaka Aahh, kwani furaha ni nini Bwana….
Busara alinijibu furaha inaletwa na kuridhika, mafanikio ya kile ambacho mtu amekianzisha au amepanga akifanye, amani ya nafsi, kutokuwa na wasiwasi….
Na mji wetu utaleta yote hayo?, Nilimuuliza kwa mshangao.
Busara aliniangalia kwa sekunde kadhaa, akaniuliza, ni kitu gani kwa sasa kitakufanya uwe mwenye furaha?
Ingawa lilikuwa swali jepesi nilifikiri wa dakika kadhaa…, nadhani nikiwatimizia mahitaji wanangu, nikahakikisha wanapata elimu nitakuwa mtu mwenye furaha…, ila nadhani mimi furaha ilishanikimbia, nilikuwa na ndoto za kutimizia familia yangu, watoto na wazazi mahitaji yao, badala yake nimekuwa kama kupe wa kuwanyonya na kuwasababishia umasikini, nimesababisha mpaka kifo cha mama yangu.
Ni kweli haya yote yasingetokea kama ungekuwa na uhakika wa mahitaji yako, badala ya kuishi kwa kuhangaika kuhusu kesho yako ungekuwa unahangaika kutimiza malengo binafsi..., kuumwa kwako kusingelazimisha watu wauze mali ili utibiwe kama kungekuwa na matibabu ambayo unaweza kumudu gharama zake. Ungekuwa haukosi uzingizi kuhusu karo za watoto wako kama elimu yao ungekuwa na uhakika wa kuweza kuimudu.
Busara aliendelea, unaweza kuona matajiri ukadhani wao wanafuraha sababu wanapesa na wanamudu gharama za hapa na pale. Lakini kijana nakwambia kwa mimi ambaye nilishakuwa tajiri fikra hizo sio kweli. Uoga wa kuweza kupata hasara, uwezekano wa biashara yangu kufilisika na watu wanaokufanyia kazi kukosa ajira, mzigo wa kuendesha biashara na chuki toka kwa wasionacho kukuona wewe ni beberu na myonyaji nina uhakika usingependa kabisa kuwa kwenye viatu vyangu.
Ni kweli nilimjibu Busara, kila mtu na mzigo wake, kuna wanaokosa usingizi kwa kufikiri ni vipi wanaweza kuwafurahisha wachumba zao, na wengine hawalali kwa wasiwasi wa kutokupata chakula, makazi na kutokujua kama wataendelea kuishi mpaka mwisho wa wiki…, ni ukweli usiopingika hatuwezi kujaribu kulinganisha shida za hao wawili.
Busara alitabasamu akaendelea, ni kweli siwezi nikasema kwamba mji utakuwa na dawa ya mapenzi ya kumfanya mtu ampende au apendwe, lakini kuwa na uhakika wa makazi, elimu, huduma za afya, burudani, uwepo wa huduma na bidhaa, mafao ya uzeeni kwa kila mstaafu, na kuwa na ziada ya kipato itasaidia sana furaha kwa wakazi.
Nakumbuka hapo nilimuuliza Busara vipi kuhusu chakula, unawezaje kuhakikishia watu watabaki na ziada ya ujira wao kama gharama za chakula zikipanda?
Busara alinijibu kwa upole, jibu lako linanipeleka kwenye kazi namba nne; Chakula Bora kwa kila Mmoja.
Nakumbuka jibu alilonipa kabla sijaelewa vizuri zile hatua kumi lilinifanya nione kama amechanganyikiwa, Utahakikisha kila mtu ana pesa za kununua chakula bora? Unajuaje kama pesa hizo watu hawatatumia kwenye kamari au ulevi
Hapana kijana, tutahakikisha kila mtu anapata milo mitatu kwa siku, na sio bora chakula, bali chakula bora na cha kuvutia.