Riwaya: Mwanamke Kama Mama Yangu

Riwaya: Mwanamke Kama Mama Yangu

RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)

TEMBELEA: riwayatakatifu.weebly.com

ILIPOISHIA…

Basi nikawa mwenyewe pale tena nikimtazama kwa hasira mke wangu kwani namhesabia kama ni mtu aliyeniharibia maisha yangu. Nilitamani nimuue pia ili aone uchungu ambao wameupata wanangu kwa kutokwa na roho zao.
Yeye hakuthubutu hata kunyanyua uso wake kunitazama. Nikajikuta nimesimama huku nikiendelea kumtazama kana kwamba kuna jambo nataka kumueleza.

ENDELEA………

"Vuta picha ungekuwa umezaliwa mwanaume. Je, ungethubutu kuoa mwanamke wa sampuli yako?"nilijikuta nimemuuliza hivyo lakini wala sikusubiri jibu lake bali nilimuacha pale nikaelekea zangu chumbani na kujifungia mlango.

Nilipanda kitandani na kulala tena kwa kujifunika shuka gubi gubi nikiamini huenda nitakapoamka nitukuwa nimepata jibu kati ya kuachana naye ama kuendelea kuishi naye.
Lakini hadi napanda kitandani kichwa changu kilikuwa kinanituma niachane naye ingawa sikutaka kufanya maamuzi wakati huo ambao nilikuwa na hasira, kwani katika maisha wanaofanya
maamuzi wakiwa wamekasirika siku zote hutoa maamuzi mabovu.

**********************
Niliamka masaa nane baadae, nikanyanyuka toka kitandani na kwenda kufungua mlango. Hasira bado nilikuwa nazo kwahiyo hata na muda huo nisingeweza kutoa maamuzi juu ya mke wangu.
Nikatoka hadi sebuleni lakini nilichokutana nacho sikukiamini.
Nilijikuta nimeduwaa nisijue la kufanya, miguu ikawa mizito ghafla na hata nikakosa nguvu ya kujongea kwa takribani sekunde thelathini.

Lakini ghafla nilijikuta nimechomoka niliposimama na kusogea pale kwenye kile ninachokitazama.
Ni mke wangu--Ashura, nilimkuta amelala kwenye kochi, ulimi nje, macho yamemtoka kama mtu aliyekabwa kooni lakini kubwa zaidi ni povu lililokuwa limeganda mdomoni mwake ambalo bila shaka lilimtoka kwa muda mrefu uliopita.

Kwa akili ya haraka nikagundua kwamba amejiua lakini ili kuthibitisha hilo nilimpima mapigo ya moyo wake kwa kutumia kiganja cha mkono wangu. Nikagundua kuwa moyo umesimama, hiyo ina maana ya kwamba damu haitembei mwilini mwake na kitaalamu mtu anayefikia hali hiyo anakuwa ni mfu.
Ndiyo hivyo, Ashura alikuwa amekata roho. Hapumui na bila shaka sitazungumza naye tena labda kama tutakutana huko kwa Mungu.

Nilijikuta natokwa chozi, nikamkumbata na kuangua kilio cha uchungu, sikupenda kuona anafariki mapema namna hiyo ingawa alinifanyia ubaya. Nahisi bado alikuwa na nafasi kwangu, nafasi ya kuniomba msamaha mimi na hata Mungu wake na bila shaka angesamehewa.
Nilijikuta naangua kilio tu ambacho hata sijui nilikitoa wapi lakini baadae niliacha baada ya kugundua kwamba pembeni ya pale alipolala palikuwa na karatasi yenye maandishi, nikanyoosha mkono wangu na kuichukua ili niisome kwani bila shaka itakuwa yenye maelezo kuhusu kifo cha Mke wangu.

"Nitangulize SAMAHANI kwa yote niliyokufanyia Mume wangu Jamal, kisha nikueleze ukweli tu kwamba NAKUPENDA tena sana zaidi ya udhaniavyo" yalisomeka hivyo maandishi ya mwanzoni mwa karatasi hiyo ambayo mimi naweza kuiita barua.
Ikanivutia kwani niliamini itakuwa imebeba mambo mengi sana hata ya siri, nikaendelea kuisoma.

"Yote niliyoyafanya yalikuwa nje ya uwezo wangu, nisengeweza kujizuia labda tu kwa uwezo wa Mungu aliyeniumba.
Najua unanichukia, tena si peke yako bali wanadamu wengi msioufahamu ukweli na kinagaubaga cha mambo. Pengine nyote mtafurahi baada ya kupata taarifa ya kifo changu huku mkimwomba Mungu aniadhibu vilivyo kwa moto mkali wa Jahanamu.
Hamfahamu lakini mtakapomaliza tu kusoma barua hii nyote mtabadilisha dua zenu na kuniombea niwe mmoja kati ya wachache watakaopata bahati ya kumgusa Mungu.

Mbegu ya matatizo yote yaliyotokea ilipandawa tangu nilipokuwa mtoto mdogo wa miaka saba tu. Nilipokuwa na umri huo alikuja mgeni nyumbani kwetu. Ni mdogo wake Mama ambaye alikuwa wa mwisho kuzaliwa katika familia yao. Alikuja kuishi nasi kwa lengo la dada yake yaani mama yangu kumtafutia shule ya ufundi Magari ili ajifunze ufundi na hatimaye kutafuta ajira ya kuanzisha maisha yake.

Tuliishi na mjomba huyo ambaye alikuwa akiitwa Mubah kwa takribani mwaka mzima akiwa hajapata shule kwani hali ya kifedha nyumbani haikuwa nzuri kwa wakati huo.
Watoto wote tukamzoea pale nyumbani, tukawa mabingwa wa kumtania naye wala hakuwa mtu mwenye kuchukia masihara yetu kwani alikuwa na sifa ya kupenda watoto.
Ulipoanza mwaka mpya mjomba Mubah alipata nafasi ya kuanza chuo na ule uwepo wake nyumbani ukawa si kwa muda mwingi. Alikuwa akishinda huko gereji na kurejea nyumbani jioni.
Siku moja Baba yangu alisafiri pamoja na wadogo zangu wawili na nyumbani nikabaki mimi, Mama pamoja na Anko Mubah tu. Niliogopa kulala peke yangu chumbani kwani wenzangu niliokuwa nikilala nao ndiyo hao waliosafiri na Baba.

Nilimtaka Mama nikalale kwake lakini alikataa kwani Baba alishatupiga marufuku na hata kuingia ndani ya chumba hicho ilikuwa ni kwa ruhusa zao, huwezi ukakurupuka tu.
Basi mama akaamua kwamba nikalale chumbani kwa Anko Mubah. Ikawa hivyo, nikaenda kulala kwa Anko Mubah kwa siku ya kwanza, ya pili na ya tatu pia.
Siku ya nne Baba alirejea lakini akiwa mwenyewe, ndugu zangu aliwaacha huko huko alipokwenda nao. Alikwenda nao kijijini kuwafanyia matambiko ya kimila kwani tangu wazaliwe hawakuwahi kufika.

Alikaa nyumbani siku moja tu kisha kesho yake akageuka kwenda tena ambapo alitarajiwa kukaa huko kwa wiki nzima kabla ya kurejea nyumbani.
Nami nikaendeleza ile tabia yangu ya kuendelea kulala chumbani kwa Anko Mubah.
Usiku mmoja nikiwa nimelala nilihisi kupapaswa, nikasituka na kumkuta ni Anko Mubah anayenifanyia hivyo.
"Shiii, nyamaza kuna kitu nataka kukuonesha" akanambia nami nikatulia kweli, nilikuwa namuuamini na si peke yangu tu bali hata Mama na ndiyo maana hata aliniruhusu kulala humo.
Akawa anashika vi-jimatiti vyangu ambavyo ndiyo kwanza vilikuwa vikiota.
"Sitaki Anko Mubah" nikawa namwambi lakini naye alinitaka niache kuongea.
Alinizidi ujanja na nilipotahamaki alikuwa ameingiza kidole chake ukeni mwangu.
Nilihisi maumivu lakini alinitaka nitulie, nikatulie na pengine ni kwasababu nilikuwa mtoto hivyo nilikosa uwezo wa kufurukuta kwenye laghai ya Anko Mubah.
Akanivua gauni langu la kulalia kabisa na akanigeuza, akaanzaa kunichezea nyuma........

Siwezi kuendelea kuusimulia usiku huo kwani ulikuwa ni usiku wenye kuumiza sana katika maisha yangu lakini kwa kifupi Anko Mubah alinilawiti.
Nilipata maumivu sana lakini Anko Mubah alinibembeleza na kuniomba nisimueleze mtu yeyote kuhusu tukio hilo na kweli likawa siri ingawa ilikuwa nusura ibumburuke kwani nilikuwa nikipata maumivu muda mwingi hasa wakati wa kutembea, nilijitahidi kuficha hali hiyo kila nilipokuwa na Mama na hakunigundua hata kidogo.

Haikuishia hapo, Anko Mubah alinifanyia tena kitendo hicho na hiyo ikawa mara ya pili. Niliendelea kuficha siri hiyo bila kufahamu kwamba madhara yake ni makubwa sana.
Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo nami nilivyozidi kuharibika, maumivu yakazidi na hatimaye nikashindwa kujizuia. Muondoko wangu ulianza kubadilika kutokana na maumivu niliyokuwa nikipata na hatimaye Mama aligundua kwamba nina tatizo na aliponichunguza ndipo alipogundua kwamba nimeharibika vibaya sehemu ya haja kubwa.

Shida aliipata pale alipotaka kujua ni nani aliyehusika kunifanyia unyama huo. Sikutaka kumwambia kwani Anko Mubah alishanizuia kufanya hivyo. Mama naye akaning'ang'aniza kweli kweli na kunitishia kwa namna nyingi ili tu nimueleze ukweli.
Nilijikuta nashindwa kuhimili vishindo vya Mama vya kunishinikiza nimtaje shetani aliyenifanyia vile. Nikamtaja, nikamueleza Mama kwamba Anko Muba ndiye aliyefanya yote hayo.
Kwanza Mama alipoteza fahamu nilipomueleza hivyo, hakutaka kuamini kama ndugu yake wa damu anaweza kinidhuru. Alipozinduka ikaanza ng'we nyingine ya maswali, Mama akawa anataka kujua mengi zaidi kuhusu kila kitu nami nikawa huru kumsimulia yote.

Jioni Anko Mubah alirejea na hapo nikitegemea kwamba lingezuka varangati la nguvu kutokana na jinsi Mama yangu alivyoonesha kuumizwa na kitendo nilichofanyiwa.
Lakini mambo yalikuwa tofauti na nilivyodhani kwani nilimuona Mama akiingia chumbani kwetu pamoja na Anko Mubah, bila shaka walikuwa na mazungumzo kuhusu kile kilichotokea na walitumia dakika zaidi ya kumi kabla ya kutoka.
Walipotoka Mama alinichukua na kunipeleka hospitali ya binafsi na huko nilisafishwa na kupewa matibabu kwenye nyeti zangu huku mambo yakifanyika kisirisiri ili jambo hilo lisije kuvuja na kufika kwenye vyombo husika.

Kisha tuliporejea nyumbani Mama alinambia mambo ya ajabu ambayo kwa wakati ule sikuwa nikifahamu kwamba Mama alikuwa akinipotosha.
"Kufanya hivyo mbele ni hatari zaidi, tena ni bora alivyokufanyia nyuma kuliko mbele. Usithubutu hata siku moja kufanya tena hasa mbele. Huko ni kwa mume wako atakayekuoa... Lakini usimwambie mtu yeyote kuhusu hili hata Baba yako" alinambia hivyo Mama.
Lakini nimekuja kugundua kuwa Mama alinambia vile ili kumlinda Kaka yake (mdogo wake). Alikuwa akimpenda zaidi ya anipendavyo mimi na ndiyo maana aliona ni heri mimi nipotee kuliko ndugu yake kuangamia kwani bila shaka kama siri hii ingebumbuluka Anko Mubah angehukumiwa.
Kutokana na umri wangu mdogo niliyaamini maneno ya mama kwamba ni heri niwe nafanywa nyuma kuliko mbele, nikakaua na imani hiyo na mbaya zaidi mwananaume wa kwanza kuwa na mahusiano naye alinitaka nifanye hivyo pia.
Mume wangu nasikitika kukwambia kwamba kwa kipindi chote nilichokuwa naishi na wewe nilikuwa najihusisha na mapenzi ya kinyume na maumbile.

Sikuwahi kukwambia hata siku moja lakini ukweli ndiyo huo.
Nasadiki kwamba mapenzi ya aina hiyo ni jambo ninalolichukia kweli, nilikuwa natamani niache kabisa lakini nimeshindwa kwani tayari nilikuwa nimeshazoea. Ni hali ambayo inaponijia huja na hamu ya juu ya kuingiliwa na ni lazima nimtafute wa kunisaidia.
Najua hili litakuumiza pia lakini maji nimeyavulia nguo sina budi kuyaoga; kwa kuwa tayari nimeshaamu kukueleza ukweli basi wacha nikueleze kila kitu.

Nilipojifungua mtoto wa kwanza nililazimika kwenda kujifungulia nyumbani ili kuficha aibu ambayo ningeipata kwani wanawake wanaoshiriki mapenzi ya kinyume na maumbile hupata tabu kwenye kujifungua, kwani hulegea kwa misuli husababisha kushindwa kusukuma mtoto.

Kama ningelijifungulia hospitali za kawaida basi bila shaka ungefahamu siri yangu ambayo mimi na mama tu ndiyo tuliokuwa tukiitunza na ndiyo maana hata ilibidi tuwazuie nyote hata ndugu zangu ili msije kujua kinachoendelea.
Tulifanikiwa lakini huo haukuwa mwisho wa mimi kuendelea na huo mchezo mchafu unaopingwa na Mungu.

************************

BADO WEWE, BARUA IMEBEBA MENGI SANA AMBAYO HATA MWENYEWE SIKUWA NIKIYAFAHAMU, USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA SITA NA HIYO NDIYO ITAKUWA YA MWISHO KWA RIWAYA HII.

WAWEZA WASILIANA NA MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU HILI KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI KWA HALAKA ZAIDI.
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA KUMI NA SITA (MWISHO)

ILIPOISHIA…

Nilipojifungua mtoto wa kwanza nililazimisha kwenda kujifungulia nyumbani ili kuficha aibu ambayo ningeipata kwani wanawake wanaoshiriki mapenzi ya kinyume na maumbile hupata tabu kwenye kujifungua, kwani kulegea kwa misuli husababisha kushindwa kusukuma mtoto.
Ndiyo maana hata ilibidi tuwazuie nyote ili msije kujua kinachoendelea.
Tulifanikiwa lakini huo haukuwa mwisho wa mimi kuendelea na huo mchezo mchafu huu mchafu unaopingwa na Mungu.

ENDELEA….

Pia Mume wangu naomba unisamehe katika hili ambalo pengine hukuwa ukilifahamu. Nilikuwa na mahusiano na rafiki yako Maige ambaye naye alikuwa akishiriki ngono ya aina hii.
Tena maige ndiyo ameathirka kabisa kiasi cha kwamba uume wake hausimami anapotaka kumuingilia mwanamke kwa njia iliyosahihi na ndiyo maana yeye na mke wake hawana hata mtoto hadi leo hii; wote wanashiriki uchafu huo.

Nilipata tabu sana alipofariki Maige, sikuwa na mtu wa kunitimizia hitaji langu hasa ukizingatia si kila mwanaume ni mshiriki wa vitendo hivyo. Ilibidi nitumie uume wa Bandia ili angalau kukata kiu ya tatizo langu.
Kama nilivyopata kukuomba samahani mwanzo naomba na hapa nirudie tena Mume wangu.
Samahani sana kwani baada ya kifo cha Maige na matumizi ya muda mrefu ya uume bandia nilianza mahusiano na Mwalimu Makoronjo ambaye naye alikuwa ni mpenzi wa ngono ya kinyema na maumbile.

Na ni yeye ambaye amesababisha vifo vya wanangu kwani ilinishauri tutoke nje ya Dar es salaam ili tupate uhuru wa kufanya uchafu wetu na pia alikuwa na mpango wa kunitorosha kwenda nyumbani kwao Kenya ili akanione kabisa.
Mimi na mwalimu Makoronjo tulitoka Dar es Salaam na kwenda Zanzibar. Tukachukua chumba hotelini na kupanga kukaa huko kwa wiki nzima. Najua ungeniacha pindi nitakaporudi lakini sikujali kwani kilichokuwa kinaniongoza hapo si hizi akili zangu hizi za kibanadamu, bali za kiasherati na kishetani. Nilikuwa tayari kwa lolote lile ili mradi tu niridhishwe hitaji langu.

Lakini mpango wetu wa kuburudika ulishindikana baada ya Mwalimu Makoronjo kupigiwa simu na kuitwa Dar es Salaam kikazi. Ikanibidi mimi nay eye turudi kwa pamoja; kwahiyo naomba ufahamu kwamba sikurudi kwasababu ya ile simu mliyonipigia.
Niliumia sana nilipogundua kuwa mzuwanda wangu Ally amekwenda bado mdogo hali kadhalika na Dada yake pia, yote ni makosa yangu lakini ni makosa ya Mama yangu pia. Hakunipenda na alitaka niishi maisha haya yasiyo ya kiungwana kwani mzizi wa tataizo uko pale alipoamua kuficha siri ya ndugu yake.

Unadhani ingekuwaje kama angelimfikisha Anko Mubah kwenye vyombo vya dola. Je, ningeendelea kuamini kwamba mapenzi ya kinyume na maumbile ni sahihi zaidi na kuamua kushiriki? Bila shaka hapana.
Namuombea Mungu amchome moto mkali ingawa ni Mama yangu, nasadiki kusema simpendi kuliko kitu chochote duniani. Aliamua nipotee kwasababu anipendi basi na hata kwangu ni hivyo.

Mungu walaze pahala pema peponi wanangu wapenzi lakini pia wanangu wanisamehe kila kitu kwani kila nilichokifanya kilikuwa nje ya akili yangu, nililazimika.
Pia mume wangu naomba unisamehe tena sana, zile dharau nilizokuwa nakufanyia na kutojali wanangu ilikuwa ni kwasababu sikuwa naona umuhimu wako kwangu. Wewe ulikuwa ukifanya mapenzi na mimi lakini sikuwa nikiridhika. Nilikuwa nakuona ni kituko tu na ndiyo maana hata nilipojaribu kujirudi sikufanikiwa. Nilikuwa mwema kwa muda mfupi tu lakini nabadilika ghafla hamu ya kutaka kuingiliwa inaponijia.
Mwisho nakuombea upate mwanamke mwingine na umuoe lakini asiwe MWANAMKE KAMA MAMA YANGU"

Nilijikuta nimeilowanisha barua yote kwa machozi, barua ilibeba mambo ya kuumiza sana, yaliyo nyuma ya pazia ambayo sikuwahi hata kuyafikiria. Niliumia kwa kweli, nililia sana siku hiyo huku nikimuomba Mungu amsamehe Ashura wangu.
Sitaki kurudia kuzungumzia chochote kati ya yale mengi yaliyo ndani ya barua hiyo lakini nahisi nimemuelewa sana Ashura wangu. Nimegundua kwamba mzigo wote wa dhambi tuliombebesha haukuwa wake.

Pia jambo kama lililomkuta mke wangu ni jambo linalotokea sana katika maisha yetu ya kila siku, watoto wadogo siku hizi wamekuwa ni watu wa kuchungwa kweli kweli kwani wamezungukwa na majangiri waliokosa haya wala hiyana kwa kuwatamani watoto wadogo.
Na inapotokea mtenda dhambi anakuwa ni mwana falimia mwenzetu huwa tunayamaliza mambo kimya kimya yaani tunatumia ile “system” ya Ng’ombe wa Bwana Heri na shamba la Bwana Heri kwahiyo hakuna kesi hapo lakini haya ndiyo matokeo yake.

Lakini kingine nilichogundua ni kwamba Mwanamke ana nafasi muhimu sana katika jamii yetu. Mwanamke ndiyo mwenye uwezo wa kui-shape jamii, anaweza kuumba jamii ya watu wabaya, watenda dhambi na waliolaaniwa na Mungu na mfano mfupi ni Mama yake Ashura.
Yeye aliamua kutengeneza mtoto wa aina ya Ashura bila kujali kwamba baada ya miaka kadhaa mbele mtoto huyo angelikuwa ni mama na kiongozi wa familia. Je, unadhani angeiongoza vipi familia yake ikiwa yeye ni mdhambi mashuhuri?

Ndiyo maana mke wangu hakuwa akijali familia yake, alinidharau mimi na kila nilichokifanya. Hakutambua hadhi ya kuwa mama wa familia tena mwenye watoto. Si kosa lake bali hakuandaliwa.
Lakini pia Mwanamke anaweza kuunda jamii katika umbo la watu wenye hofu ya Mungu, wachakalikaji, wapenda maendeleo na watakatifu na mwanamke wa mfano huo ni Mama yangu.
Bila shaka ni malezi yake yaliyonifanya niwe mvumilivu kwa muda wote wa miaka zaidi ya nane niliyoishi na mke wangu kwa visa, misukosuko na vituko. Malezi yake ndiyo yaliyonifanya nitambue thamani ya kuwa Baba tena mwenye watoto.

Niliipigania familia yangu hadi ukomo wa nguvu zangu ulipofikia na Mungu akaamua kuwapumzisha wanangu na mke wangu pia.
Funzo kwako wewe kijana mwenye ndoto za kuolewa, hakikisaha unaolewa na mwanaume kama mimi. Niliyetayari hata kuwa bwege kwasababu ya kupigania familia yangu.
Na kwako wewe unayepanga kuoa nakushauri hakikisha unapotaka kuoa, unaoa MAWANAMKE KAMA MAMA YANGU.

MWISHO

PIA WAWEZA PATA RIWAYA NYINGINE ZA MAISHA KAMA HII KWA KUWASILIANA NA MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU.

AHSANTENI KWA KUWA NAMI KWANZIA MWANZO HADI HIVI LEO MWISHO WA RIWAYA HII.
 
Shukran sana mkuu, hii barua ya Ashura Ina funzo kubwa sana
 
jibwa Mkuu mie ilinitokea baada ya kumtokea demu mmoja tulikubaliana tukaanzisha kudinyana daily, ajab nikitaka kufanya dog style anazingua, mikwara mingi na janja janja! Pia nikianza kumpapasa kuelekea makalioni anawahi kunidaka mikono na kuirudisha maskioni! Eti anavunga kupapaswa maskio ndo anapata mzuka kuliko sehem zote za mwili! Duh! Ila haikupita hata wiki nkaja gundua anavidonda vikubwa kwenye kifereji! Nadhani stori ilibadilika papo hapo!
 
jibwa Mkuu mie ilinitokea baada ya kumtokea demu mmoja tulikubaliana tukaanzisha kudinyana daily, ajab nikitaka kufanya dog style anazingua, mikwara mingi na janja janja! Pia nikianza kumpapasa kuelekea makalioni anawahi kunidaka mikono na kuirudisha maskioni! Eti anavunga kupapaswa maskio ndo anapata mzuka kuliko sehem zote za mwili! Duh! Ila haikupita hata wiki nkaja gundua anavidonda vikubwa kwenye kifereji! Nadhani stori ilibadilika papo hapo!
Yah af pia hawa wa2 ukitangaza kuoa wanakuwa wagumu sana kukwambia kama wanaruka ukuta wanaona utamuona malaya kumbe wanajiaribia mwishoe wanachepuka...
 
Back
Top Bottom