RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU
MTUNZI: KELVIN KAGAMBO
SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)
TEMBELEA: riwayatakatifu.weebly.com
ILIPOISHIA…
Basi nikawa mwenyewe pale tena nikimtazama kwa hasira mke wangu kwani namhesabia kama ni mtu aliyeniharibia maisha yangu. Nilitamani nimuue pia ili aone uchungu ambao wameupata wanangu kwa kutokwa na roho zao.
Yeye hakuthubutu hata kunyanyua uso wake kunitazama. Nikajikuta nimesimama huku nikiendelea kumtazama kana kwamba kuna jambo nataka kumueleza.
ENDELEA………
"Vuta picha ungekuwa umezaliwa mwanaume. Je, ungethubutu kuoa mwanamke wa sampuli yako?"nilijikuta nimemuuliza hivyo lakini wala sikusubiri jibu lake bali nilimuacha pale nikaelekea zangu chumbani na kujifungia mlango.
Nilipanda kitandani na kulala tena kwa kujifunika shuka gubi gubi nikiamini huenda nitakapoamka nitukuwa nimepata jibu kati ya kuachana naye ama kuendelea kuishi naye.
Lakini hadi napanda kitandani kichwa changu kilikuwa kinanituma niachane naye ingawa sikutaka kufanya maamuzi wakati huo ambao nilikuwa na hasira, kwani katika maisha wanaofanya
maamuzi wakiwa wamekasirika siku zote hutoa maamuzi mabovu.
**********************
Niliamka masaa nane baadae, nikanyanyuka toka kitandani na kwenda kufungua mlango. Hasira bado nilikuwa nazo kwahiyo hata na muda huo nisingeweza kutoa maamuzi juu ya mke wangu.
Nikatoka hadi sebuleni lakini nilichokutana nacho sikukiamini.
Nilijikuta nimeduwaa nisijue la kufanya, miguu ikawa mizito ghafla na hata nikakosa nguvu ya kujongea kwa takribani sekunde thelathini.
Lakini ghafla nilijikuta nimechomoka niliposimama na kusogea pale kwenye kile ninachokitazama.
Ni mke wangu--Ashura, nilimkuta amelala kwenye kochi, ulimi nje, macho yamemtoka kama mtu aliyekabwa kooni lakini kubwa zaidi ni povu lililokuwa limeganda mdomoni mwake ambalo bila shaka lilimtoka kwa muda mrefu uliopita.
Kwa akili ya haraka nikagundua kwamba amejiua lakini ili kuthibitisha hilo nilimpima mapigo ya moyo wake kwa kutumia kiganja cha mkono wangu. Nikagundua kuwa moyo umesimama, hiyo ina maana ya kwamba damu haitembei mwilini mwake na kitaalamu mtu anayefikia hali hiyo anakuwa ni mfu.
Ndiyo hivyo, Ashura alikuwa amekata roho. Hapumui na bila shaka sitazungumza naye tena labda kama tutakutana huko kwa Mungu.
Nilijikuta natokwa chozi, nikamkumbata na kuangua kilio cha uchungu, sikupenda kuona anafariki mapema namna hiyo ingawa alinifanyia ubaya. Nahisi bado alikuwa na nafasi kwangu, nafasi ya kuniomba msamaha mimi na hata Mungu wake na bila shaka angesamehewa.
Nilijikuta naangua kilio tu ambacho hata sijui nilikitoa wapi lakini baadae niliacha baada ya kugundua kwamba pembeni ya pale alipolala palikuwa na karatasi yenye maandishi, nikanyoosha mkono wangu na kuichukua ili niisome kwani bila shaka itakuwa yenye maelezo kuhusu kifo cha Mke wangu.
"Nitangulize SAMAHANI kwa yote niliyokufanyia Mume wangu Jamal, kisha nikueleze ukweli tu kwamba NAKUPENDA tena sana zaidi ya udhaniavyo" yalisomeka hivyo maandishi ya mwanzoni mwa karatasi hiyo ambayo mimi naweza kuiita barua.
Ikanivutia kwani niliamini itakuwa imebeba mambo mengi sana hata ya siri, nikaendelea kuisoma.
"Yote niliyoyafanya yalikuwa nje ya uwezo wangu, nisengeweza kujizuia labda tu kwa uwezo wa Mungu aliyeniumba.
Najua unanichukia, tena si peke yako bali wanadamu wengi msioufahamu ukweli na kinagaubaga cha mambo. Pengine nyote mtafurahi baada ya kupata taarifa ya kifo changu huku mkimwomba Mungu aniadhibu vilivyo kwa moto mkali wa Jahanamu.
Hamfahamu lakini mtakapomaliza tu kusoma barua hii nyote mtabadilisha dua zenu na kuniombea niwe mmoja kati ya wachache watakaopata bahati ya kumgusa Mungu.
Mbegu ya matatizo yote yaliyotokea ilipandawa tangu nilipokuwa mtoto mdogo wa miaka saba tu. Nilipokuwa na umri huo alikuja mgeni nyumbani kwetu. Ni mdogo wake Mama ambaye alikuwa wa mwisho kuzaliwa katika familia yao. Alikuja kuishi nasi kwa lengo la dada yake yaani mama yangu kumtafutia shule ya ufundi Magari ili ajifunze ufundi na hatimaye kutafuta ajira ya kuanzisha maisha yake.
Tuliishi na mjomba huyo ambaye alikuwa akiitwa Mubah kwa takribani mwaka mzima akiwa hajapata shule kwani hali ya kifedha nyumbani haikuwa nzuri kwa wakati huo.
Watoto wote tukamzoea pale nyumbani, tukawa mabingwa wa kumtania naye wala hakuwa mtu mwenye kuchukia masihara yetu kwani alikuwa na sifa ya kupenda watoto.
Ulipoanza mwaka mpya mjomba Mubah alipata nafasi ya kuanza chuo na ule uwepo wake nyumbani ukawa si kwa muda mwingi. Alikuwa akishinda huko gereji na kurejea nyumbani jioni.
Siku moja Baba yangu alisafiri pamoja na wadogo zangu wawili na nyumbani nikabaki mimi, Mama pamoja na Anko Mubah tu. Niliogopa kulala peke yangu chumbani kwani wenzangu niliokuwa nikilala nao ndiyo hao waliosafiri na Baba.
Nilimtaka Mama nikalale kwake lakini alikataa kwani Baba alishatupiga marufuku na hata kuingia ndani ya chumba hicho ilikuwa ni kwa ruhusa zao, huwezi ukakurupuka tu.
Basi mama akaamua kwamba nikalale chumbani kwa Anko Mubah. Ikawa hivyo, nikaenda kulala kwa Anko Mubah kwa siku ya kwanza, ya pili na ya tatu pia.
Siku ya nne Baba alirejea lakini akiwa mwenyewe, ndugu zangu aliwaacha huko huko alipokwenda nao. Alikwenda nao kijijini kuwafanyia matambiko ya kimila kwani tangu wazaliwe hawakuwahi kufika.
Alikaa nyumbani siku moja tu kisha kesho yake akageuka kwenda tena ambapo alitarajiwa kukaa huko kwa wiki nzima kabla ya kurejea nyumbani.
Nami nikaendeleza ile tabia yangu ya kuendelea kulala chumbani kwa Anko Mubah.
Usiku mmoja nikiwa nimelala nilihisi kupapaswa, nikasituka na kumkuta ni Anko Mubah anayenifanyia hivyo.
"Shiii, nyamaza kuna kitu nataka kukuonesha" akanambia nami nikatulia kweli, nilikuwa namuuamini na si peke yangu tu bali hata Mama na ndiyo maana hata aliniruhusu kulala humo.
Akawa anashika vi-jimatiti vyangu ambavyo ndiyo kwanza vilikuwa vikiota.
"Sitaki Anko Mubah" nikawa namwambi lakini naye alinitaka niache kuongea.
Alinizidi ujanja na nilipotahamaki alikuwa ameingiza kidole chake ukeni mwangu.
Nilihisi maumivu lakini alinitaka nitulie, nikatulie na pengine ni kwasababu nilikuwa mtoto hivyo nilikosa uwezo wa kufurukuta kwenye laghai ya Anko Mubah.
Akanivua gauni langu la kulalia kabisa na akanigeuza, akaanzaa kunichezea nyuma........
Siwezi kuendelea kuusimulia usiku huo kwani ulikuwa ni usiku wenye kuumiza sana katika maisha yangu lakini kwa kifupi Anko Mubah alinilawiti.
Nilipata maumivu sana lakini Anko Mubah alinibembeleza na kuniomba nisimueleze mtu yeyote kuhusu tukio hilo na kweli likawa siri ingawa ilikuwa nusura ibumburuke kwani nilikuwa nikipata maumivu muda mwingi hasa wakati wa kutembea, nilijitahidi kuficha hali hiyo kila nilipokuwa na Mama na hakunigundua hata kidogo.
Haikuishia hapo, Anko Mubah alinifanyia tena kitendo hicho na hiyo ikawa mara ya pili. Niliendelea kuficha siri hiyo bila kufahamu kwamba madhara yake ni makubwa sana.
Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo nami nilivyozidi kuharibika, maumivu yakazidi na hatimaye nikashindwa kujizuia. Muondoko wangu ulianza kubadilika kutokana na maumivu niliyokuwa nikipata na hatimaye Mama aligundua kwamba nina tatizo na aliponichunguza ndipo alipogundua kwamba nimeharibika vibaya sehemu ya haja kubwa.
Shida aliipata pale alipotaka kujua ni nani aliyehusika kunifanyia unyama huo. Sikutaka kumwambia kwani Anko Mubah alishanizuia kufanya hivyo. Mama naye akaning'ang'aniza kweli kweli na kunitishia kwa namna nyingi ili tu nimueleze ukweli.
Nilijikuta nashindwa kuhimili vishindo vya Mama vya kunishinikiza nimtaje shetani aliyenifanyia vile. Nikamtaja, nikamueleza Mama kwamba Anko Muba ndiye aliyefanya yote hayo.
Kwanza Mama alipoteza fahamu nilipomueleza hivyo, hakutaka kuamini kama ndugu yake wa damu anaweza kinidhuru. Alipozinduka ikaanza ng'we nyingine ya maswali, Mama akawa anataka kujua mengi zaidi kuhusu kila kitu nami nikawa huru kumsimulia yote.
Jioni Anko Mubah alirejea na hapo nikitegemea kwamba lingezuka varangati la nguvu kutokana na jinsi Mama yangu alivyoonesha kuumizwa na kitendo nilichofanyiwa.
Lakini mambo yalikuwa tofauti na nilivyodhani kwani nilimuona Mama akiingia chumbani kwetu pamoja na Anko Mubah, bila shaka walikuwa na mazungumzo kuhusu kile kilichotokea na walitumia dakika zaidi ya kumi kabla ya kutoka.
Walipotoka Mama alinichukua na kunipeleka hospitali ya binafsi na huko nilisafishwa na kupewa matibabu kwenye nyeti zangu huku mambo yakifanyika kisirisiri ili jambo hilo lisije kuvuja na kufika kwenye vyombo husika.
Kisha tuliporejea nyumbani Mama alinambia mambo ya ajabu ambayo kwa wakati ule sikuwa nikifahamu kwamba Mama alikuwa akinipotosha.
"Kufanya hivyo mbele ni hatari zaidi, tena ni bora alivyokufanyia nyuma kuliko mbele. Usithubutu hata siku moja kufanya tena hasa mbele. Huko ni kwa mume wako atakayekuoa... Lakini usimwambie mtu yeyote kuhusu hili hata Baba yako" alinambia hivyo Mama.
Lakini nimekuja kugundua kuwa Mama alinambia vile ili kumlinda Kaka yake (mdogo wake). Alikuwa akimpenda zaidi ya anipendavyo mimi na ndiyo maana aliona ni heri mimi nipotee kuliko ndugu yake kuangamia kwani bila shaka kama siri hii ingebumbuluka Anko Mubah angehukumiwa.
Kutokana na umri wangu mdogo niliyaamini maneno ya mama kwamba ni heri niwe nafanywa nyuma kuliko mbele, nikakaua na imani hiyo na mbaya zaidi mwananaume wa kwanza kuwa na mahusiano naye alinitaka nifanye hivyo pia.
Mume wangu nasikitika kukwambia kwamba kwa kipindi chote nilichokuwa naishi na wewe nilikuwa najihusisha na mapenzi ya kinyume na maumbile.
Sikuwahi kukwambia hata siku moja lakini ukweli ndiyo huo.
Nasadiki kwamba mapenzi ya aina hiyo ni jambo ninalolichukia kweli, nilikuwa natamani niache kabisa lakini nimeshindwa kwani tayari nilikuwa nimeshazoea. Ni hali ambayo inaponijia huja na hamu ya juu ya kuingiliwa na ni lazima nimtafute wa kunisaidia.
Najua hili litakuumiza pia lakini maji nimeyavulia nguo sina budi kuyaoga; kwa kuwa tayari nimeshaamu kukueleza ukweli basi wacha nikueleze kila kitu.
Nilipojifungua mtoto wa kwanza nililazimika kwenda kujifungulia nyumbani ili kuficha aibu ambayo ningeipata kwani wanawake wanaoshiriki mapenzi ya kinyume na maumbile hupata tabu kwenye kujifungua, kwani hulegea kwa misuli husababisha kushindwa kusukuma mtoto.
Kama ningelijifungulia hospitali za kawaida basi bila shaka ungefahamu siri yangu ambayo mimi na mama tu ndiyo tuliokuwa tukiitunza na ndiyo maana hata ilibidi tuwazuie nyote hata ndugu zangu ili msije kujua kinachoendelea.
Tulifanikiwa lakini huo haukuwa mwisho wa mimi kuendelea na huo mchezo mchafu unaopingwa na Mungu.
************************
BADO WEWE, BARUA IMEBEBA MENGI SANA AMBAYO HATA MWENYEWE SIKUWA NIKIYAFAHAMU, USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA SITA NA HIYO NDIYO ITAKUWA YA MWISHO KWA RIWAYA HII.
WAWEZA WASILIANA NA MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU HILI KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI KWA HALAKA ZAIDI.