Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Leo Jumapili hatujaambulia chochote kweli....!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii simulizi inatoa fundisho kwa wale Manabii uchwara.Hii kitu nimeichukia mana ina hamasisha sana ushoga na kusagana, imagine ichezwe movie hii, itakuaje
🔥🔥SIN 74
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Tafadhali Jery usitulazimieshe kutumia nguvu”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akimzuia Jery kwa kumshika kifuani mwake. Jery akautazama mkono wa mlinzi huyo na kumfanya autoe.
“Nina mtoa sasa ole wake mtu aniguse, huo ugeni wenu leo wote uta vurugika na muta jua kama mimi ni kishaa au nina akili timamu”
Jery alizungumza na kuwafanya walinzi hao kutazamana huku wakijuliza ni kitu gani ambacho Jery amekidhamiria kukifanya kwao.
ENDELEA
“Kama leo muna mfanyia mwenzenu hivi ambaye amjitoa maisha yake yote kwa ajili yangu. Kumbukeni huyo huyo ambaye alimfanya awe hivi ipo siku nanyi ata wafanya kuwa hivi. Ana stahiki kuishi ana mtoto wa kike ni mdogo na ana miaka mitatu ana stahili maleze ya baba yake. Nina mjua baba yangu sio mtu mwenye utu kabisa.”
Jery alizungumza maneno ambayo yaliwaingia walinzi hao wawili mioyoni mwao.
“Ana hitaji kuishi mwenzenu”
“Sawa ila daktari aletwe hapa hatutoa hitaji atoke hapa ndani kwa maana na sisi hatuhitaji kupata adhabu kama hiyo”
“Sawa nita mtibu mimi mwenyewe. Nisubirini nina kuja”
Jery akatoka ndani hapo kwa haraka, akaingia chumbani kwake na kuchukua kibegi chake kidogo chenye vifaa vya kidaktari kisha akarudi eneo hilo na kuanza kumpatia matibabu ya siri mlinzi wake huyo.
***
Ulinzi ukazidi kuimarishwa katika kiwanja cha ndege cha mwalimu Jk Nyerere na majeshi ya nchi za pande mbili, Marekani na Tanzania. Umakini haukuwa tu kwenye maeneo ya ardhini, bali hata eneo la anga, ndege za kijeshi aina ya Jet zipatazo kumi zime uzingira uwanja huo huku zikisubiria ndege kubwa ya raisi wa Marekani, ali maarufu kwa jila la Air Force One itue katika kiwanja hicho.
Raisi Chinas, mke wake pamoja na viongozi wengine wa kitaifa, wamekusanyika katika kiwanja hicho kuusubiria ugeni huo ambao kwa nchi ya Tanzania ni ugeni mmoja mkubwa sana. Hazikupita dakika kumi na tano ndege hiyo ikaanza kuonekana kwenye anga la uwanja huo wa taifa. Wananchi wengi walio jitokeza wakaanza kushangilia huku kila mmoja akiwa na hamu kubwa sana ya kumuona raisi wa Marekani. Taratibu ndege hiyo ikaanza kutua na kupunguza mwendo wake wa kasi, ilipo kaa sawa, ikaendeshwa hadi katika zulia jekundu lililo wekewa ngazi maalimu kwa ajili ya raisi wa Marekani na timu yake kushuka. Raisi Chinsa Mtenzi mpamoja na mke wake wakasogelea katika eneo hilo la ngazi huku kukiwa na vitoto viwili vya kike vikiwa vime beba maua ambayo wata mpatia raisi huyo ambaye naye ameambatana na mke wake pamoja na mtoto wake wa kike.
Raisi Minler Thomas akaanza kushuka na mke wake katika ngazi hizo huku wakiwa wame jawa na furaha kubwa sana. Wakapeana mikono na raisi Chinas Mtenzi huku wakiwa na furaha kubwa snaa. Wakatambulishana wake zao kisha wakaeleka kwenye kijukaa maalumu. Ukaanza kupigwa wimbo wa Taifa wa nchi ya Tanzania kisha ukafwatia wimbo wa taifa wa nchi ya Marekani. Baada ya hapo, wakakagua kikosi cha jeshi kilichopo hapo uwanjani kisha wakaelekea katika eneo la wacheza ngoma. Wakatazama ngoma hizo kwa dakika tano kisha wakaingia kwenye gari maalumu ambalo lina tumiwa na raisi wa Marekani.
“Nchi yako ina watu wakarimu sana”
“Nashukuru sana ndugu yangu. Karibu sana Tanzania”
“Nashukuru sana ndugu yangu. Nime jawana furaha sana kufika hapa. Kipindi chote cha misha yangu nime kuwa na hamu kubwa sana ya kufika nchini hapa na leo ndoto yangu ime kamilika”
“Nafurahi kusikia hivyo ndugu yangu”
Msafara huo moja kwa moja ukafika ikulu. Raisi Mtenzi akamuagiza mmoja wa walinzi wake waende kumuita Jery kw amaana na yeye ana paswa kutambulishwa kwa familia ya raisi Minler. Mlinzi huyo akaanza kuulizia ni sehemu gani aliyopo na akaelezwa kwamba yupo katika gereza alilo fungwa mlinzi wake. Akafika katika gereza hilo na kumkuta Jery akimalizia kumuhudumia mlinzi huyo.
“Jery baba yako ana kuita”
“Wameshafika?”
“Ndio”
“Ndugu yangu hii sindano niliyo kuchoma ita saidia sana katika kukausha majeraha ya vidonda.”
Jery alizungumza kisha akaondoka eneo hilo, moja kwa moja akaelekea chumbani kwake, akaoga haraka haraka ana kuvaa suti nzuri kisha akeleeka katika eneo walipo wazazi wake. Jery akasalimia na riaisi Minller, mkewe pamoja na mwanaye wa kike.
“Huyu ni mwanangu wa mwisho”
“Ohoo nashukuru sana kumfahamu”
“Jery una weza kumtembeza mwanangu na muka zungumza mambo mawili matatu”
Raisi Minler alizungumza na kumfanya Jery atabasamu. Wakatoka eneo hilo pamoja na mtoto huyo wa kike wa raisi Minler ambaye ana umri mmoja na Jery.
“Una itwa nani?”
“Naitwa Godliver”
“Wao ni jina zuri sana”
“Nashukuru hata na wewe pia jina lako ni zuri sana.”
Jery akampeleka msichana huyo kwenye bwawa kubwa ambalo lime zungukwa na maua mazuri pamoja na bata mzinga wengi ambao wame kuwa ni kivutia kizuri sana kwa Godliver.
***
“Nimejarubu kumpigia Julieth simpati hewani vipi wewe ume mpata?”
Mrs Sanga alimuuliza mume wake ambaye amekaa sebleni akisoma biblia yake.
“Hawezi kuwa hewani, leo ikulu kuna ugeni mkubwa hivyo ni lazima simu yake itakuwa off. Si unajua jinsi wezetu Wamarekani wanavyo jali sana kwenye mambo ya usalama”
“Ahahaa….Nilijawa na wasiwasi mwingi, nikihisi labda ule mpango wetu ume julikana”
“Hapana, yule dokta yupo vizuri sana”
“Mume wangu, haya sasa tuna nafasi ya ukaribu na raisi, ehee je tuna fanyaje juu ya mipango yetu?”
“Subiri kidogo muda uta amua. Unajua inabidi tuvumilie hadi pale utakapo ingia bungeni na mambo yakiwa vizuri basi kila jambo tutakalo lipanga litakwenda poa”
“Sawa mume wangu mimi nina kusikiliza wewe. Vipi leo una kwenda kwenye ibada?”
“Yaa nina hamu sana ya kurudi mazabahuni.”
“Mungu akutangulie”
“Vipi hutaki kwenda na mimi?”
“Mmmm hapana kuna mahala nina kwenda mara moja kisha nina rudi nyumbani. Nahitaji kuwandalia chakula kizuri kwa leo usiku”
“Sawa mke wangu”
Mrs Sanga akambusu mume wake mdomoni kisha akaondoka nyumbani hapo. Nabii Sanga alipo hakikisha ameandaa somo zuri la kwenda kuhubiri kanisani akajiandaa na kuanza safari ya kuelekea kanisani kwake. Wingi wa watu walio kusanyika kanisani hapo, uka zidi kumfanya nabii Sanga aamini nguvu alizo nazo zina zidi kufanya kazi. Kila muumini aliye muona nabii Sanga alizidi kujawa na wa furaha kwa maana ni kipindi kirefu hawajamuona mtumishi wao huyo. Shangwe na nderemo zikazidi kupambam moto kanisani hapo huku wana kwaya wakizidi kutumbuiza kisawa sawa. Nabii Sanga akaanza makeke yake ya kuhubiri huku waumini wake wakizidi kujawa na imani mioyoni mwao pasipo kufahamu kwamba siri ya mambo yote nyuma ya nabii wao huyo ina tokana na nguvu za giza na wala si kwa nguvu za Mungu.
***
Kadri muda unavyo zidi kusonga mbele ndivyo jinsi Julieth anavyo jawa na wasiwasi.Hatambu lengo la yeye kuweka ndani ya chumba hicho ambacho kina kila aina ya huduma. Kitu kibaya zaidi ni simu yake ameicha alipo kuwa ana ingia ofisini kwa raisi. Akasimama na kugonga mlango huo. Mlango ukafunguliwa na akachungulia mlinzi mmoja wa kike.
“Ndio”
“Nahitaji kumuona Jery”
“Kwa sasa Jery yupo na wageni”
“Tafadhali nin kuomba umuombe aweze kuja humu”
“Hapana dada. Raisi wa Marekani yupo hapa hivyo kila mmoja yupo busy”
“Sasa kwa nini nime fungiwa humu ndani kama mfungwa?”
“Haujafungiwa kama mfungwa ndio maana hauna pingu mkononi mwako.”
“Ila nina kuomba unisaidie kumuita yule ni mume wangu mtarajiwa na nina kila haki ya kumuona”
Mlinzi huyu kidogo akastuka baada ya kusikia kwamba Julieth ni mke mtarajiwa wa Jery. Wakashauriana walinzi hao na mmoja wapo akaondoka na kuanza kumtafuta Jery. Akafanikiwa kumuona Jery, akamsogelea na kumgong’oneza sikioni mwake.
“Sawa muambie nina kuja”
Mlinzi huyo akaondoka na kumuacha Jery akiendelea kuzungumza na mgeni wake.
“Ana kuja”
“Sawa”
Kidogo Julieth akaanza kujawa na furaha kwa maana ana weza kupata fumbo la yeye kuwekwa ndani hapo. Baada ya nusu saa Jery akaingia ndani hapo. Wakakumbatiana kwa nguvu huku kila mmoja akiwa na hisia kali za kimapenzi kwa mwenzake.
“Jery nime choka kukaa peke yangu humu ndani”
“Usijali twende chumbani kwangu. Unajua kuna ugeni mkubwa sana wa raisi kutoka Marekani”
“Ahaa kumbe ni leo”
“Yaa ni leo. Pia si una jua kwamba wewe ni mke wangu mtarajiwa hivyo baba haja penda uwe una onekana onekana kwa watu hadi pale tutakapo oana”
Jery alimuomgopea Julieth ili mradi ajawe na amani ambayo anatambua kwamba ilisha mtoweka.
“Nime kuelewa mume wangu”
“Nashukuru kusikia hivyo. Twende”
Jery akatoka na Julieth na walinzi hao wakashindwa kuwazuia, walicho kifanya ni wao kufwata kwa nyuma. Jery akamuingiza Julieth chumbabi kwake.
“Kila kitu kipo humu ndani mke wangu. Ukihitaji games zipo kuwa na furaha”
“Simu yangu”
“Ohoo simu nita mtafuta yule mlinzi kisha nita kuletea”
“Sawa mume wangu”
“Vipi una jihisi njaa?”
“Kwa mbali?”
“Basi nita muagiza mpishi akuletee. Ila nisamehe sana mke wangu kwa maana kuna baadhi ya wageni ambao baba ame nikabidhi niwe nao hivyo sipaswi kuwa nao mbali”
“Usijali mume wangu, huo ndio wakati wa wewe kuji funza baadhi ya mambo. Huwei jua huko mbele nawe ukaja kuwa raisi”
“Hahaa sawa mke wangu. Nina kupenda sana”
“Nakupenda pia”
Jery akambusu Julieth mdomoni mwake kisha Jery akatoka ndani hapo. Akamuaagiza mpishi wa familia ya kumuandalia Julieth chakula, kisha yeye akaelekea alipo muacha mtoto wa raisi wa Marekani.
***
“Mkuu gari ina elekea kukata mafuta na huku tulipo ni porini”
Dereva alizugumza huku akimtazama mkuu wake aliye kaa siti ya pembeni.
“Daa na huku hakuna hata dalili ya mtu kuishi?”
“Yaaa”
“Dogo endapo mafuta yatatuishia, damu yako ita kuwa ndio mafuta yetu”
Jamaa huyo alizugumza huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Kwa nini jamani mume niteka?”
“Wewe una kulaje sahani moja na wenye nchi. Hili ndio linalo kutokea”
Mkuu huyo alizungumza huku akimtazama Evans kwa macho ya dharau. Evans machozi yakaanza kumlenga lenga na hapa ndipo akaanza kupata picha kwamba mateso haya yote anayo yapitia kwa sasa ni kutokana na kuwa na mahusiano na Julieth.
‘Wanawake kweli ni wauaji’
Evans alizungumza kimoyo moyo huku akiwatazama wanaume hawa watano alio kaa nao ndani ya gari hilo linalo elekea asipo pajua.
“Naombeni kujisaidia haja ndogo”
Evans alizungumza huku akijaribu kutazama maporomoko yaliyopo pembezoni mwa hii barabara.
‘Una zingua una jua?”
“Ni kweli naombeni sana nijisaidie”
Kwa ishara mkuu wa kikosi hicho akamuomba dereva huyo kusimamisha gari hilo pembezoni mwa barabara.Vijana wawili walio kaa siti ya nyuma na Evans waka shuka ndani ya gari hilo, walipo hakikisha kwamba ulinzi upo vizuri wakamshusha Evans ambaye ni kweli ame banwa na haja kubwa.
“Mkuu una jua kwamba tuna songa tu mbele na hatujui ni wapi tunapo elekea?”
“Huku mbele kuna kijiji ana ishi babu yangu, nina imani tuna weza kukaa pale hadi mkuu atakapo kuja”
“Ila mkuu tume poteza sana wezetu. Sisi tulio baki hatujui tuna ishi vipi, hatuelewi familia zetu zita kuwa kwenye hali gani”
“Ni kweli nina wasiwasi hata mimi, Ila hii ndio njia tuliyo ichagua. Hatuna namna ya kurudi nyuma tena”
“Daa kazi kweli kweli kaka. Ila huyu dogo sijui ata fanywa nini na Jery?”
“Atamuu “
“Ila mapenzi ni mambo ya kijinga sana. Sisi tuna hangaika ila wao wakipatana mambo yana endelea”
“Tuta fanyaje sasa ikiwa ndio kazi yetu”
Evans akasogea pembezoni kabisa kwa barabara hiyo, akafungua zipu ya suruali yake na kuanza kujisahidia haja ndogo huku macho yake yote yakitazama katika eneo hilo lenye bonde kubwa. Chini kabisa ya hilo bonde ambalo ni refu sana akaona mto mkubwa sana una tirisha maji. Akageuka nyuma na kuwatazama watu hao walio mteka. Wawili alio shuka nao kwenye gari wame simama eneo moja huku wakipiga stori zao na kucheka. Wengine watatu wapo ndani ya gari wakiendelea na mazungumzo yao.
‘Ni heri kufa kuliko kuendelea kushikiliwa na hawa watu ambao sijui hatima ya maisha yangu itakuwa ni nini mikononi mwao’
Evans alizungumza huku akiifunga zipu ya suruali yake. Akarudi hatua mbili nyuma kisha akakimbia kwa kasi na kujirusha kuelekea chini katika bonde hilo kubwa na kuwafanya walinzi hao wote kustajabu kwa maana hakuna hata mmoja wao aliye tarajia kuona Evans akifanya tukio kama hilo.
ITAENDELEA
Haya sasa, Evans ameamua kujitosha kwenye bonde hilo kubwa, je atafanikiwa kutoka hai ikiwa walinzi hao wamepewa agizo la kuhakikisha wana mshikilia Evans hadi pale atakapo onana na Jery.? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 75.
Hatari🔥🔥🔥SIN 76
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Usione nime kaa kimya ukahisi nina kuogopa tafadhali nina kuomba uweze kutoka ndani hapa”
Joseph akamtazama Magreth kuanzia usoni hadi katika mkono wake ulio mshika.
“Niachie mkono wangu kabla sija kuvuruga sura yako”
“Nitakuachia mkono wangu pale utakapo kubali kutoka ndani hapa”
Joseph kwa nguvu akamashika Magreth shingoni mwake na kuanza kumkaba. Kitendo hicho kika muashiria Magreth kwamba mwanaume huyo hataki amani na analo lihitaji kwa sasa ni fujo. Magreth kwa mikono yake miwili akaupiga kwa nguvu mkono wa Joseph, akampiga kigoti cha tumboni na kumfanya Joseph kuanza kugugumia kwa maumivu makali sana kwa maana hakutegemea kamaa ana weza kupigwa na Magreth ambaye ana mchungulia ni mnyonge kama mpenzi wake Josephine.
ENDELEA
“Toka humu ndani na usidhubutu kurudi tena kwa maana ukirudi nita hakikisha nina kufanya kitu amacho hujawahi kufanywa kwenye maisha yako”
Magreth alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasri, Joseph taratibu akaanza kutoka ndani hapo huku akiwa amejikunja kwa maana maamivu anayo yahisi kwenye tombo lake si ya mchezo mchezo.
“Na jambo jengine. Ole wako nione siku una mtukana rafiki yangu au kumdhalilisha kwa aina yoyote ile, nakuapia haki ya Mungu sinto kuacha salama wewe. Umenielewa?”
Joseph akatingisha kichwa, akafungua mlango na kutoka ndani hapo. Taratibu akamsogelea Josephine na kumkumbatia.
“Japo tume umbwa kusikiliza amri ya mwanaume na kufwata yale anayo yahitaji ila haitupasi kuendelea kukaa chini yamanyanyaso yao na kejeli kama hizi. Nimuda wako sasa Josephine kusimama wewe kama wewe na si kumtegemea mwanaume. Sawa”
Magreth alizungumza kwa sauti ya upole huku akimwagikwa na machozi usoni mwake.
“Nashukuru kusikia hivyo rafiki yangu. Nina kupenda sana”
“Nina kupenda pia Josephine”
Wakakumbatiana huku wote wakimwagikwa na machozi mengi kwenye nyuso zao.
***
Walinzi hao wakazidi kujitahidi kuogelea ila kila aliye jaribu kushika jabali alilo kalia Evans, hakuweza kumruhusua na alicho kifanya ni kuikanyaga mikono yake, kutokana na wingi na nguvu ya maji hayo wakajikuta wakisombwa na kuzidi kupelekwa mbali sana. Evans akaendelea kukaa ju ya jabali hilo kwa muda mrefu huku mwili wake wote ukitetemeka kwa baridi kali pamoja na maumivu ya kujibamiza katika baadhi ya majabali yaliyomo ndani ya mto huo. Masaa yakazidi kusonga mbele na giza likaanza kutawala anga. Baridi kali ikazidi kuutesa mwili wa Evans ambaye hapo alipo ana tisheti na suruali yake tu.
‘Ehhee Mungu kwa nini nina pitia mateso yote haya. Ni nini nilicho kukosea mimi?’
Evans alizungumza huku akiendelea kujikunyata kwa baridi hiyo. Maji ya mto huo hayakuweza kutulia kabisa, matone ya mvua yaliyo anza kumdondokea taratibu yaka zidi kumpa wasiwasi na woga mwingi sana. Hazikuisha hata dakika ishirini mvua kubwa ikaanza kunyesha na kumfanya Evans azidi kuteseka katika eneo hilo. Maji yakazidi kujaa mara dufu, maji hayo sasa yakaanza kufika kimo cha jabali hilo na kuzidi kumfanya Evans kupagawa.
‘Ehee Mungu niokoe’
Evans alizungumza huku akiendelea kung’ang’ania jabali hilo. Wimbi kubwa likamkumba na kujikuta akishindwa kabisa kushikilia jambali hilo. Akasombwa na maji hayo na kujikuta akianza kupiga kelele huku akilia kwa jinsi anayo zungushwa zungushwa na maji hayo yanayo mfanya ashindwe hata kuogelea. Evans naye akaanza kubamizwa kwenye baadhi ya majabali yaliyomo katika mto huo na kumsababishia maumivu makali sana. Maumivu hayo yakazidi kuutesa mwili wake na mwishowe akajikuta akipoteza fahamu.
Sauti za watu wanao zungumza lugha ambayo Evans hakuweza kuitambua kwa uharaka kwa maana ni lugha ya kikabila. Akafumbua macho yake na kujikuta akiwa amelazwa k
wenye kitanda chakavu fulani. Chumba alicho lala kime tengenezwa na matofali ya kuchomwa na juu kime ezekwa na nyasi. Mwanga wa jua unao pitia dirisha dogo, ukamfanya Evans kutambua kwamba kume pambazuka japo hakumbuki ni jinsi gani alivyo weza kufika katika eneo hilo.
Akanyanyuka kitandani taratibu, ila maumivu makali ya mwili mzima yakamfanya aweze kurudi tena kitandani na kulala. Akaingia msichana aliye valia kaniki nyeusi huku kichwani mwake akiwa amenyoa nywele zote. Msischana huyo akamuita baba yake, naye akaingia ndani hapo huku naye akiwa amejifunga kaniki nyekundu huku mkononi mwake akiwa ameshikilia mkia wa Simba. Mzee huyo akazungumza kilugha huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Baba yangu ana uliza una jisikiaje?”
Msichana ali tafsiri lugha hiyo ya kiruguru.
“Nasijisikia maumivu mwili mzima. Hapa nipo wapi?”
Msichana huyo akamuambia baba yake huyo ambaye ni mzee sana na wala hafahamu lugha ya kiswahili.
“Baba ana sema uta pona tu”
“Sawa, hapa nilipo nipo wapi?”
“Upo kwenye milima ya Ukaguru”
Binti huyo alijibu na kumfanya Evans kujawa na mshangao mkubwa sana.
“Nimefikaje fikaje hapa?”
“Leo asubuhi tulipo kuwa tuna tafuta samaki kwenye bwawa tuliweza kukuokota wewe ukiwa ume nasa kwenye moja ya jiwe kubwa. Tulipo gundua kwamba upo hai tulikuleta hapa”
Evans akamtazama msichana huyo kisha macho yake akayahamishia kwa mzee huyo na akakutana na tabasamu pana la mzee huyo.
“Nina shukuru kwa kunisaidia”
Msichana huyo akamtafsiria baba yake. Kisha baba yake huyo amampa maagizo ya kuleta dawa walio kuwa ana ichemsha. Baada ya muda msichana huyo ambaye ukimchunguza kwa sana, ana urembo ulio fichika katika dibwi kubwa la umasikini, akaingia ndani hapo huku mkononi mwake akiwa ameshika kikombe cha plastiki ambacho kime jaa dawa.
“Hii ni dawa ya kuponyesha maumivu ya ndani kwa ndani”
Msichana huyo alizungumza huku akimkabidhi Evans kikombe hicho. Taratibu Evans akachukua kikombe hicho, akakitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kunywa. Uchungu wa dawa hiyo ukamfanya Evans kusitisha kwanza kunywa dawa hiyo huku akisikilizia jinsi inavyo mkereketa kwenye kinywa chake.
“Kunywa, ita kusaidia”
“Mbona chungu sana?”
“Ndio dawa kaka”
Msichana huyo aliendelea kumsisitizia Evans, hakuwa na jinsi yoyote zaidi ya kujikaza na kunywa dawa hiyo. Kwani kitendo cha watu hao mkusaidia na kumleta nyumbani hapo basi wana onekana ni watu wema sana hivyo hakuwa na wasiwasi na dawa hiyo.
“Ohooo khragrahaaa!!!”
Evans alilalama huku uso wake ukiwa umejikunja kisawa sawa. Baada ya kumaliza dawa hiyo, binyo huyo akamkabidhi Evans kipande cha sukari guru.
“Ni nini hii?”
“Sukari, lamba ina maliza uchungu wako mdomoni”
Evans akatazama kipande hicho,akakilama kidogo na alipo gundua kweli ni kitambu basi akaanza kukilamba kwa fujo ili mradi kutoa uchungu wote mdomoni.
“Una itwa nani?”
“Mimi?”
“Ndio”
“Naitwa Evans”
“Sawa”
Binti huyo akamtafsiria jinsi alivyo zungumza na Evans.
“Baba ana kuambia ukaribie hapa nyumbani”
Mzee huyo akatoka ndani hapo na kumuacha binti yake huyo na Evans. Taratibu Evans akamtazama binti huo jinsi alivyo jazia maeneo ya kiunoni mwake. Hispi zake kwa kweli zime weza kubeba makalio makubwa kiasi cha kumfanya Evans kuingiwa na tamaa ya ngono. Mbaya zaidi kaniki aliyo ivaa kidogo ina onyesha maumbilie yake ya ndani.
“Mbona una nichunguza sana?”
“Aha….hapana”
“Usinitamani kwa maanaa mwanaume yoyote anaye jaribu kufanya hivyo basi ni lazima afe”
Msichana huyo ambaye haja jitambulisha jina lake alizungumza kisha akatoka ndani hamo na kumuachia Evans maswali ya sinto fahamu ya kwani msichana huyo ame weza kuzisoma hisia zake haraka sana tofauti na alivyo mdhania kwa maana amekaa kishamba shamba.
***
“Ehee jana ilikuwaje?”
Nabii Sanga alimuuliza Julieth mara baada ya kukutana naye sebleni.
“Ahaa katika siku zangu zote za maisha nilizo ishi hapa duniani, jana ilikuwa ni siku yangu ngumu baba”
“Kwa nini ilikuwa ni siku ngumu?”
“Daa wee acha tu. Yaani baba yangu mkwe ni mkali kisawa sawa. Ile nina kutana naye akanionyesha picha za walinzi walio uwawa mkono Morogoro. Weee niliogopa sana, baada ya hapo akaagiza nipelekwe kwa dokta nipimwe kila kitu. Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba nimekutwa nipo salama kila idara”
“Yule mzee ni mkali sana. Ila mwishoni ilikuwaje?”
“Nimepita jaribio hilo na amekubali niolewe na mwanaye”
Nabii Sanga akatabasamu kidogo kisha aka mkumbatia Julieth kwa maana uwepo wake uta leta faidi kubwa sana kwenye familia yake.
“Sasa kuna mambo nina bidi kukueleza kama mwana familia uliye kuwa na una kwenda kuolewa sasa mwanangu”
Nnabii Sanga alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akimtazama Julieth kwa umakini sana usoni mwake.
“Ni nini baba”
“Niandalie kahawa nzuri na uje huku kwenye bustani.”
“Sawa”
Nabii Sanga akaondoka sebleni hapo na Julieth akaandaa kahawa hiyo ambayo yeye na mama yake tu ndio watu wa pekee wanao weza kuandaa kahawa nzuri na inayo mpendeza mzee huyo. Julieth akamuandalia baba yake kikombe hicho cha kawaha kisha akaa kiti cha pembeni katika kijibanda hicho cha kupumzikia, kilichopo katika bustani hiyo yenye majani mazuri sana.
“Ndio baba”
“Kwenye maisha yangu kuna mambo mengi sana sikuweza kukueleza kama mwanangu mpendwa. Japo kuna baadhi ulisha wahi kuyaona na yaka kuumiza ila sasa ni wakati wa wewe kuweza kutambua kila jambo”
Nabii Sanga baada ya kuzungumza hivyo, akapiga fumba moja la kahawa kisha akaendelea kuzungumza.
“Natambua hivi karibuni una kwenda kuwa mkwe wa raisi Mtenzi. Uwepo wake kwenye familia yake si kumzalia wajukuu tu na akafurahi, bali nasi kwa upande wetu ni lazima tuweze kunufaika katika kipindi hichi ambacho yeye ata kuwa ana nufaika na wewe”
“Nahitaji ukiingia kwenye familia yake kuna baadhi ya majukumu uweze kuyafanya”
“Majukumu gani baba?”
“Moja nina hitaji uweze kumshawishi Jery kubaki hapa nchini Tanzania na kama ata rudi nchini Marekani basi akamalizie kusoma tu kisha arudi Tanzania”
“Hilo ni jambo rahisi halina shaka baba”
“Jambo jengine nina hitaji utengeneze uaminifu na uweze kupata nafasi ndani ya ikulu ya raisi Mtenzi, si kama mkwe tu bali uwe kama sekretari au uwe na nafasi yoyote ambayo itakusaidia katika kujua kila jambo linalo endelea ndani ya ikulu ile”
“Kwa nini baba una taka niajiriwe ikiwa una fahamu kabisa kwamba mimi ndoto zangu ni kuwa mfanya biashara mkubwa?”
“Nalielewa hilo mwangu, ila kazi yako utakayo ipata ikulu, ita zitimiza kwa haraka ndoto zako za kuwa mfanya biashara mkubwa sana ndani na nje ya Tanzania. Moja uta weza kuhakikisha kwamba biashara zako zote zina pita bandarini pasipo usubumbu wa aina yoyote na wala huto weza kuchukuliwa kodi ya aina yoyote ila. Nina imani una tambua ni jinsi gani kodi zinavyo waumiza wafanya biashara”
“Yaa ni kweli baba”
“Pili nahitaji tuingie kwenye biashara ya giza”
“Biashara ya giza? Kivipi baba?”
“Biashara ya giza ni biashara ambazo zina tuingizia kipato kikubwa. Mimi na mama yako tulikuwa tuna ifanya biashara hiyo kwa siri sana na wewe ndio uta kuwa mtu wa pekee ambaye una weza kufahamu siri hiyo”
“Ni biashara gani hiyo baba?”
“Tuna uza madawa ya kulevya”
“BABAAAAAAA!!!”
Julieth alishangaa sana huku akimtazama baba yake.
“Usishangae mwanangu. Una hisi kanisa kama kanisa lina weza kutuingizia pesa nyingi kiasi cha nyinyi akaunti zenu kuwa na mabilioni of money? No hii biashara ndio ima wafanya na nyinyi leo mukipangwa kwenye orodha ya vijana matajiri basi na nyinyi wanangu wote watatu muta kuwepo”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Julieth kushusha pumzi nyingi.
“Muna muda gani muna ifanya hiyo biashara?”
“Kabla hata wewe hujazaliwa”
“Hee hamjawahi kukamatwa?”
“Hakuna aliye weza kutugusa wala kufahamu au kuhisi. Trust ndio kitu pekee kilicho tufanya tukae zaidi ya miaka ishirini na nane kwenye hiyo biashara. Ni hivi juzi juzi tu ndio tuli simama kama miaka miwili, kuangalia nguvu ya raisi Mtenzi ipo vipi ila kwa sasa tuna yaka kurudi rasmi na tuna hitaji kuingiza kiasi kikubwa sana cha pesa kutokana na mahusiano yetu haya tunayo kwenda kuyajenga”
Julieth akashusha pumzi taratibu huku akimtazama baba yake usoni kwa maana mtihani alio pewa ni mkubwa sana.
“Ila baba ni kazi hatari?”
“Ndio ni hatari ila hakuna ambaye ata fahamu juu ya wahusika wake”
“Ila baba nikiwa ndani ya ikulu, muda wote ita nipasa kuwa karibu sana na raisi. Nina imani kwamba simu zangu zita kuwa zina rekodiwa. Je hapo itakuwaje baba?”
“Kuna mfumo maalumu ambao tuta kuwa tuna utumia kuwasiliana”
“Mfumo gani huo baba?”
“Nita kuamabia ni mfumo gani ila jina lako utakuwa una litumia kwenye uongozi wa biashara hiyo ni BLACK GHOST. Kwa maana mimi baba yako nina kwenda kukurithisha jina hilo”
Nabii Sanga alizungumza huku akitabasamu na kumfanya Julieth naye kutabasamu huku kwa maana mtoto wa nyoka naye ni nyoka.
ITAENDELEA
Haya sasa, nabii Sanga ana hitaji kumuachia mwanaye Julieth biashara ya madawa ya kulevya je ita kwenda salama vizuri kama alivyo ipeleka yeye mwe nabii Sanga.? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 77.