Six Man
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 253
- 892
- Thread starter
- #81
RIWAYA; MTOTO WA RAIS
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU 0652 212391
SEHEMU YA KUMI NA TISA
"Sipendi kukutesa Salum. Sitaki Aisha akakosa baba pia. Aisha hastahili kuwa yati.." Daniel hakumaliza alichotaka kusema.
"Nooo! Usiseme chochote kuhusu Aishaaa.." Salum aliongea huku akidondosha machozi.
"Salum, niambie ulifata nini nyumbani kwa Donald Tengo?" Daniel hakujari kama Salum alikuwa analia.
"Sijui nianzie wapi Daniel kukueleza" Salum aliongea huku machozi yakimdondoka.
"Ni kweli mimi ninaitwa Salum Taiwan. Nilikuwa meneja wa tawi la benki la LDB huko Muheza. Nilikuwa meneja nzuri sana katika benki hiyo. Na mara kadhaa nimepewa tuzo ya mfanyakazi bora. Pengine uchapakazi wangu ndio ulioniponza. Maana kama miezi miwili hivi nyuma nilipokea barua ya kuhamishwa kutoka Muheza, na kuletwa katika tawi letu la Mlimani city. Mimi niliukataa uteuzi huo. Na sababu ikiwa ni moja tu, sikutaka kuwa mbali na mke wangu, Merina!.
Nilikuwa nampenda sana Merina. Nilimpenda kuliko kitu chochote kile hapa duniani. Nilimpenda kwasababu alinipa sababu milioni za kumpenda. Barua ile ya uhamisho, kwangu ilikuwa sawa na kutenganishwa na Merina, mkewangu.
Unaweza ukasema si ningehama na Merina na kuhamia jijini Dar es salaam? Hiyo ilikuwa ngumu, na kama tungetaka iwe hivyo ilimpasa Merina aache kazi! Kwa maana Merina alikuwa ni katibu muktasi katika shamba la miti huko Longuza. Nilipeleka hoja hiyo kwa afisa rasilimali wetu wa mkoa, lakini wala haikusikilizwa. Ilikuwa ni lazima mimi nihame Muheza. Na nilipoonekana mbishi kuhama Muheza kwa sababu ya Merina, ndiposa walipoamua kumuua Merinaaa!" Salum aliangua kilio kikubwa.
Daniel alimwangalia Salum kwa huruma. Aliujua uchungu wa mke ingawa yeye alikuwa hajaoa.
"Pole sana Salum. Ninajaribu kuvaa viatu vyako lakini havinitoshi. Walimuua mkeo kwa sababu ndogo kama hiyo?" Daniel aliuliza kwa wahka mkubwa.
"Ndio, walimuua Merina! Vijana wa Bahari nyekundu walimuua Merina! Ili tu lengo lao litimie la mimi kuhama Muheza"
"Bahari nyekundu walimuua Merina, ni kina nani hao vijana wa Bahari nyekundu?" Daniel aliuliza. Kwa mara nyingine tena alisikia kuhusu Bahari nyekundu.
"Nitakueleza. Nitakuekeza kila kitu Daniel. Baada ya Merina kuuwawa sikuwa na sababu ya kukaa Muheza. Kumbukumbu za Merina zilikuwa haziishi kunijia ndani ya mji ule. Nilikubaliana na matakwa yao ya kuhamia Dar es salaam.
Wiki moja iliyopita ndio niliingia hapa mjini, jumatatu niliwasili kazini, ndipo nilipokutanishwa na meneja Hashim. Mambo niliyoyakuta Dar es salaam ni tofauti kabisa na kazi yangu. Kitaaluma mimi ni afisa mikopo, ambapo kule Muheza nilipanda cheo na kuwa Meneja. Lakini jukumu alilonipa meneja Hashim halikuwa la uafisa mikopo na wala halihusiani na mambo ya kibenki" Salum alisema.
"Ulipewa kazi gani?" Daniel aliuliza kwa hamu kubwa sana.
"Nilipofika hapa, kazi yangu kuu ilikuwa ni kila siku jioni kupeleka pesa katika duka moja la Kilimo.
Mwanzoni niliikataa kazi hii, nikisema sicho nilichosomea. Sicho nilichokuja kufanya Dar es salaam. Sicho kilichonitoa Muheza. Lakini sikusikilizwa hata kidogo. Nilitishiwa kuuwawa kama mke wangu Merina. Hapo ndipo nikajua kwamba ajari ya Merina ilikuwa ni ya kupangwa. Pamoja na hivyo bado nilikataa kuwa mtumwa kwa kutishiwa kifo. Hapo ndipo walipomteka mwanangu, Aisha..." Salum alianza kulia tena.
"Pole sana Salum. Mimi sijabahatika kupata mtoto lakini najua maumivu unayoyapitia.."
"Daniel, hawa watu ni wabaya sana. Bahari nyekundu sio watu hata kidogo. Walimrudisha kwangu Aisha, lakini hakuwa Aisha yule. Wamemtia Aisha ugonjwa wa ajabu sana. Ugonjwa ambao inampasa Aisha anywe vidonge maalum kila siku. Bila hivyo vidonge basi Aisha naye naenda kumpoteza.
Atakufa mwanangu!!!"
"Pole sana Salum. Hivyo vidonge maalum unavitoa wapi?" Daniel aliuliza.
"Wanavyo wao. Wao tu. Mimi wananipa vidonge vya kutumia kwa wiki moja kwa malipo ya kwenda kuwachukulia kemikali zao kila siku jioni"
"Wapi unapoenda kuchukua hizo kemikali?"
Huwa nafungwa kitambaa usoni nikielekea lilipo hilo duka. Meneja Hashim hunipa mkoba wenye hela kutoka benki. Nafunguliwa mita chache kabla sijafika dukani. Lakini nikipelekwa sasahivi au nikipita karibu na hilo duka, nitalikumbuka"
"Ushaenda mara ngapi katika hilo duka?"
"Kila siku jioni, na jana ni siku ya sita"
"Unahisi wanataka kufanyia nini hizo kemikali?"
"Kwakweli sifahamu. Lakini ninavyoamini wanataka kufanya kitu kikubwa sana. Maana wanatumia gharama kubwa sana kununua hizo kemikali"
"Na pale kwa Donald Tengo ulifata nini?"
"Inavyoonesha jana ndio ilikuwa siku ya mwisho kuchukua hizo kemikali. Na leo asubuhi tulipokea ujumbe kuwa tunatakiwa tukapewe shukrani, tukielekezwa tuende kwenye nyumba ile. Lakini cha kushangaza haikuwa shukrani, tumepewa kazi nyingine"
"Kazi gani mliyopewa?"
"Tumepewa kazi ya kumuua Mtoto wa Rais!"
"Mumue nani, Aneth au Moses?" Daniel alishangaa.
"Yule mzee alisema anaitwa Aneth.."
"Mpango wao wa kumuua Aneth, ukoje?" Daniel aliuliza.
"Najua unajua kuwa Aneth ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu ya sheria katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Aneth ni mwanafunzi mahiri sana katika uga huo. Aneth amekuwa makini katika masomo pia katika mambo yake binafsi. Maisha yake ameyafanya kuwa siri ijapokuwa yeye ni Mtoto wa Rais. Lakini cha kushangaza maisha ya Aneth sio siri kwa watu wale. Wanajua kila kitu kuhusu Aneth. Wanajua analala saa ngapi?, anaamka saa ngapi? anakula nini? Na atavaa nini?. Kitu walichotuambia leo ni kuwa Mh. Rais ana mpango wa kumuachia madaraka Aneth pindi muda wake utakapokwisha. Sote tunajua kuwa Rais Mark amebakisha miaka mitatu ili muda wake wa kukaa madarakani uishe. Hivyo Rais anamtengeneza Aneth aje kuwa mrithi wake. Jambo hilo linapingwa kwa nguvu zote na wale watu. Hawataki Aneth aje kuwa Rais!!"
"Kwanini hawataki Aneth awe Rais? Kwa sababu ni mtoto wa Rais?"
"Hapana, sababu sio hiyo. Hata mimi niliuliza swali hilo, yule jamaa alikataa kwa kichwa. Lakini pamoja na kumdadisi sababu, katu hakutuambia sababu ya wao kupinga Aneth arithi madaraka ya baba yake" Salum alisema.
"Na mpango wa kumuua Aneth upoje?"
"Jamaa alinambia kuwa Aneth ni mteja wa benki ya LDB pale Mlimani city. Na kila jumatatu asubuhi amekuwa akienda pale ofisini kupeleka marejesho ya mkopo wake. Na hapo ndipo mimi nilipangwa niwe kama Mhudumu wa kupeleka kahawa yenye sumu wakati Aneth akiwa katika ofisi ya afisa mikopo"
"Wana uhakika angekunywa hiyo kahawa? Na je isingegundulika kama pale benki ndio mliomnywesha hiyo sumu Aneth?"
"Kama nilivyokwambia awali. Jamaa wanajua kilakitu kuhusu Aneth. Wanajua kwamba Aneth ni mpenzi mkubwa sana wa kahawa. Na amekuwa na utaratibu wa kunywa kahawa kila anapofika katika ofisi ile. Afisa mikopo na Aneth wana urafiki tangu zamani, hivyo huwa hana wasiwasi wowote kutumia chochote mle ofisini. Kuhusu kugundulika hata mimi nilimuuliza yule jamaa, alinambia kwamba sumu hiyo ingemuua taratibu. Ingemchukua mwezi mzima ndipo afe, hivyo isingekuwa rahisi watu kuitilia shaka benki ya LDB kuhusika na mauaji ya Aneth"
"Unadhani mpango wa kumuua Aneth utaendelea hata baada ya nyinyi kukamatwa?" Daniel aliuliza.
"Wale jamaa wana dhamira ya kweli kumuua Aneth. Naamini mpango wa kumuua Aneth utaendelea. Ingawa sina hakika kama wataendelea na namna hiihii waliyoipanga ya kumuua Aneth" Salum alisema.
Daniel alitafakari, kisha akasema "Salum ninashukuru sana kwa ushikiriano wako. Kwa ushirikiano huu ulionipa ninakuahidi nami nitakusaidia. Nitahakikisha mwanao hafi kwa kupata hizo dawa maalum siku zote utakapokuwa hapa, kisha tutampeleka nje ya nchi kumtibu kabisa"
"Kweli Daniel?" Salum alikuwa analia.
"Chukua maneno yangu. Utakuwa salama, na mwanao atakuwa salama!" Daniel alisema kwa kujiamini.
Salum alinyanyuka kwenye kiti na kumkumbatia Daniel.
"Usijari, ni katika jukumu langu. Haya twende ukumbini tukaungane na wenzetu" Daniel alisema.
Daniel na Salum waliongozana hadi ukumbini. Waliwakuta wakina Amini wakiongea mambo mbalimbali. Wakati Hannan akichezea tarakilishi yake. Alipofika Daniel, wote walikaa kimya.
Daniel akashika usukani. Akawasimulia kila kitu alichoambiwa na Salum. Wote pale ukumbini walisikitika sana, walimpa pole Salum kwa madhila yaliyomkuta.
"Sasa tuna kazi mbili mbele yetu" Daniel alisema. Ukumbi ukachukua tena utulivu wake. Kazi ya kwanza tutaifanya kuanzia sasahivi, hadi usiku iwe imekamilika. Kuhakikisha tunapata dawa maalum za mtoto wa Salum!" Daniel alinyamaza akiwaangalia wote mle ukumbini kwa zamu. "Tuna njia moja tu ya kupata hizo dawa maalum, ni kumteka yule jamaa aliyewapa kazi wakina Salum ya kumuua Aneth! Yule ndiye atakuwa funguo yetu wapi hizo dawa maalum zinawekwa. Kazi yetu ya pili tutaifanya kesho asubuhi, nayo ni kufatilia nyendo zote za Aneth, na endapo ataenda katika benki ya LDB ni lazima tuhakikishe usalama wake." Daniel alisema. Huku vijana wote walikubaliana naye.
"Daniel," Hannan aliita. Daniel akamwangalia Hannan
"Wakati ukiwa unamhoji Salum, kuna vitu viwili vimetokea. Kwanza nimegundua kwamba simu za kina mzee Rwekwaza zimetoka katika orodha yangu ya simu ninazozifatilia. Hii ni ishara kwamba wamegundua kwamba simu zao zilikuwa zimedukuliwa" Hannan alimeza mate huku akihakikisha taarifa hizo zinapenya vizuri katika masikio ya kina Daniel.
"Jambo la pili, kuna meseji mbili zimeingia katika simu ya Robin. Namshukuru Mungu kwani niliweka mfumo maalum wa kuhifadhi meseji zote zitakazoingia katika simu hii. Kwani baada ya meseji hizo kuingia simu ya Robin ilipoteza taarifa zake zote. Na kwasasa hatuwezi tena kunasa meseji zozote zitakazoingia. Nina imani nao wamegundua kwamba simu ya Robin haipo katika mikono salama" Hannan alinyamaza kidogo. Ukumbi ulikuwa kimya, masikio yote walimpa Hannan.
"Meseji ya kwanza ilisema hivi 'Ukimya wako inamaanisha kwamba ZAK amekunyima mzigo. Na amechukua mzigo wako'. Meseji hiyo ilifatiwa na meseji nyingine iliyoandikwa 'Nenda kwa balozi wa 21.19.1 kama kuna tatizo' na baada ya meseji hiyo ndipo simu ikazimwa" Hannan alimaliza.
Itaendelea...