Roho inaniuma nimetimiza miaka 35 sina mtoto wala maisha

Uko Kama Mimi mdogo wangu...tuliza boli utapata Kama uliandikiwa...kikubwa uhai na ibada....mtaani kwetu kuna Jamaa Ana hela maisha ya kifahari lakini hazai kabisa Bora hata wewe hujasema Kama unamatatizo ya uzazi...yeye kapewa pesa kanyimwa watoto lakini anayafurahia maisha Yake kwake anaishi na ndugu tu..shukuru kwa kila jambon uzidishe ibada.
 
pole sana mkuu lakini pia hongera kwa kushtuka na kujutia, hiyo ni ishara tosha wewe ni mpambanaji na mpambanaji siku zote hakati tamaa,wengine hushtukia washashika mkongojo.endela kupambana mkuu, kwani kuna mahali uliona pameandikwa kila mtu atafanikiwa ndani ya miaka yake 35 ?, jibu ni hapana.
kila mtu ana muda wake mkuu. pambanaa pambanaa na tena pambanaa. ushauri wangu ni huu, sali sana na pia jitathmini wewe mwenyewe ujue wapi unakosea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We tafuta tu hela mkuu hata ukiwa na miaka hamsini Bora kuzeeka ukiwa na ela sio watoto
 
USIKATE TAMAA USIOGOPE, KUHUSU MTOTO UKIPATA MTU WA KUBEBA MIMBA YAKE AU KUMPA MIMBA MPE TU...
KUHUSU MAISHA ENDELEA KUMTUMAINIA MUNGU IPO SIKU YAKO VERY SOON KIKUBWA USIJIFUNGIE NDANI...
 
Na waliokuwa hospital wanataman angalau wangekuwa na afya kama yako wasemeje?
 
Mungu akubariki sana kwa shuhuda ulizotoa hapa Chifu.
Binadamu tunataabika sana kwa kujifanyia ulinganifu katika maisha na watu wengine. MUNGU kila mja amempangia mapito yake.Wakati yeye anasikitika hana watoto na maisha yanayoeleweka, kuna mtu anapigania walau apone tu na dalili haipo! Tushukuru kwa kila jambo mkuu
 
Hongera kwa uhai ulionao
 
Maisha ndio haya haya. Magumu alafu atunywi sumu kujiua. Kilicho mbele ndio tunafanya. Usitake kuishi maisha ya mipango ya ndotoni kumbe huna, imenitesa Sana hii hali ya kutamani maisha ya mtu. Soma vitabu vingi vinavyofundisha kutunza pesa na kutumia pesa japo ikiwa ndogo.
 
Ushauri bora wa Mwaka huu!!
 
Mkuu sio kweli kwamba jamaa "kamchamba" .. ila kaanua kuchangia tu maoni yake kama wewe unavyochangia sasa...
 
Hapo kWa kusema hana mtoto ndo anakosea.watu wana miaka 30 kwenye ndoa Sasa na hawana hata mtoto wa ngama.
Anaweza aoe na asipate hao watoto anaowawaza.
Kila sehemu mitihani. Au Unaweza uwapate na wa kaondoka wote kama yule maza Akiondoka na watoto wote 4 kwenye msiba wa magufuli.
We shukuru Mungu u yu hai... Hayo mengine yatajiseti.
Jua wakati u napanga na Yeye anapanga.
Na ya kwake ndio mara zote yanatimia.
Au uanweza ukawapata na wote wakawa mateja... Kama jirani yangu hapa... Mpk alikuwa analaamika kwamba Yeye ndio mtu Mwenye mkosi Dunia nzima. Haiwezekani Ana watoto 5 wa kiume na wote mateja/bangi mpk wanamshikia kisu Yeye.
 

Moja kati ya ushauri wa hovyo kuwahi kutolewa JF
 
Ndiyo hivyo yule mama wawili walikuwa wakwake na wawili washeji yake na mdada wa kazi naye akifariki pia piga picha kama hiyo mmewe kabaki na shemeji yake na mkewe wamebaki hawana watoto, mambo mengine nikumshukuru MUNGU tu ukiwa na afya mengine MUNGU anafanya mwenyewe, watu tuna misiba ila unamwachia MUNGU tu akusaidiye.
 
Mkuu ulifanikiwa kuhama kwa baba Mkubwa..? Kitu unapaswa kushukuru Mungu ni kua na Afya njema. Hayo mengine yanakuja tu ukipambana. Shukuru Mungu kwa zawadi ya maisha, badili mitazamo na misimamo yako kaa pekeyako au tafuta mtu (mentor) akuongoze katika kujua nn unapaswa kufanya. Wakati mwingine haufanikiwi kwasababu unafanya sana kazi bali kwa kufanya kazi sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…