Roho yangu imeumia kumuona Mugalu kwenye msafara

Roho yangu imeumia kumuona Mugalu kwenye msafara

Bado Mugalu ni mchezaji mzuri. Sioni sababu ya kupoteza hela kumsajili Manzoki ambaye anafanana Kila kitu na Mugalu.
 
Kwa jinsi watu wanavyochangia hapa juu ya usajili wa Simba inabidi bodi ya Simba ikutane haraka irekebisha mambo kungali bado mapema na dirisha la usajili lipo wazi. Inaonekana mashabiki na wanachama walivumilia msimu ulioisha wakitegemea uongozi wao utarekebisha mambo kwenye dirisha hili la usajili kuelekea msimu mpya lakini inaonekana wala uongozi haujali. Lakini wakumbuke tarehe 13/08/2022 si zaidi sana ya wiki tatu zijazo sijui hao viongozi wataangalia mpira wakiwa wapi. Na usiku wa deni haukawii kukucha.

Kwenye dirisha hili Simba ilitakiwa ifanye "ovehaul" kabisa lakini wao wamefanya "repair" ndogo kama wenzao Yanga wakati wenzao timu yao ipo tayari toka msimu ulioisha. Na tangu Hersi awarudishe watu wa mpira karibu yake walau sasa Yanga imeanza kusajili kiufundi kwa kiasi fulani.

Lakini jambo ambalo linashangaza sana kwenye bodi ya Simba kumejaa watu wazoefu sana na wanoujua mpira na ndani na wa kimataifa na fitina zake kweli kweli. Watu kama Magori, Kaduguda na Kasim Dewji wanauzoefu wa zaidi ya miaka 30 kwenye mpira wa nchi hii. Je kimejiri nini huko ndani ya bodi kiasi kuruhusu baadhi ya wachezaji waendelee kuwepo Simba wakati kabisa wanaonekana uwezo wao umeshuka? Kwa haraka haraka wachezaji kama Mugalu, Mhilu, Kagere, Mwenda na Gadiel walitakiwa msimu ujao wasiwepo kabisa pale Simba.

Haya makosa yanayofanyika sasa timu ikifanya vibaya huko mbele ya safari zigo lote ataangushiwa kocha. Na kwa jinsi nchi hii ilivyo na mashabiki wengi maandazi tena hoya hoya viongozi watapongezwa kwa uamuzi wa kumtimua kocha kama ilivyotokea kwa Pablo.
Ahmed Ally alishasema hawasajili Kwa matakwa ya mashabiki. Na sijasikia mashabiki wakikemea Hilo tamko.
 
Unachangia shilingi ngapi hadi utukane watu,Swala la mchezaji kufanya vizuri au kutofanya vizuri ni kawaida kwasababu soka ni kazi kama zilivyo zingine.Au wewe ofisini kwako siku zote unafanyaga vizuri.Mugalu alishacheza simba kwa kiwango kikubwa tu swala lakutofanya vizuri msimu ulioisha haimaanishi kua ni mbaya.Au wewe unajua sana kuliko uongozi wa simba na bench la ufundi?.Nyie ndo wale mashabiki wapuuzi wanaotaka kuingiza mihemko kwenye soka.
 
Katika kikosi chote cha simba mchezaji mbovu kuliko wote pale ni Gadiel Michael uyo apelekwe hta kitayosa kwa mkopo hana hadhi ya kukaa kwenye benchi la simba
Huyu aliniharijia carrier yake Kwa tamaa ya mil.5, alikuwa mfalme Yanga akapiga vibaya hesabu na washauri wa ovyo akapotea. Hivi kweli Gadiel aliamini anakwenda kumnyang'anya namba Shabalala?
 
Ndugu yangu nilikuwa hapa nasubiri utambulisho wa manzoki na beki huyo wa kati ila moyo wangu umeingiwa na simanzi sana kwa kuwaona hao watu
Acha kujipa matumaini makubwa wakati hao wachezaji hawajacheza simba hata nusu msimu.
 
Kizer Chief wenyewe walifagia wazee wote na wale wasiofanya vizuri kama Kambole na yule Samir Nuckovich, tena kwa kuwavunjia mikataba ila sisi tunakumbatia tu magarasa.

Mugalu na kagere hamna kitu pale kwasasa, yani ni bora ucheze na Kyombo kuliko hao wasenge wawili.
Kagere uwezo wa kufunga bado anao,tatzo msim uliopta katkat palikuwa pabovu
 
Simba wangekubali hasara kwa kuvunja mikataba tu...
Bocco
Mugalu
Kagere
Gadiel
Mhilu
Nyoni
Mzamiru

Hawa hawakutakiwa kuwepo kwenye timu

Muhilu Tayari ameshakatwa kichwa baba jeni bye bye
 
Bado Mugalu ni mchezaji mzuri. Sioni sababu ya kupoteza hela kumsajili Manzoki ambaye anafanana Kila kitu na Mugalu.

Kufanana sura ama nini mkuu [emoji2955]?acha kufananisha manzoki na vitu vya ajabu
 
Nasikia eti kwenye mkataba wa Mugalu kuna kifungu kuwa Simba inatakiwa kumnunulia bigijii za 3400 kila siku Je ni kweli?
 
1.mugalu
2.kagere
3.nyoni
4.mhilu
5.gadiel
Hawa viumbe kubaki simba ni sawa na kusema umeokoka wakati tunguli bado unazo ndani
 
Kwa taarifa yako wakati Simba wanamsajili alikuwa ametoka kwenye majeruhi ya muda mrefu. Halafu kaja hapa ndani ya misimu miwili ni majeruhi tu kama gari la mkaa tripu shamba tripu gereji. Kwa kifupi ni kuwa kwa namna usajili ulivyoendeshwa haihitaji utaalamu kujua Simba haina fedha kwa sasa ndio maana Adebayor, Sylla, Aziz Ki na wengineo wakaota mbawa. Na hata Luis jurudi itakuwa ndoto za mchana.
Luis hawezi kurudi yule, ataenda team zilizo level ya Al Ahly.
 
Bado Mugalu ni mchezaji mzuri. Sioni sababu ya kupoteza hela kumsajili Manzoki ambaye anafanana Kila kitu na Mugalu.
Usimfananishe Manzoki na Mugalu tafadhari, muheshimu Manzoki wa watu.
 
Unachangia shilingi ngapi hadi utukane watu,Swala la mchezaji kufanya vizuri au kutofanya vizuri ni kawaida kwasababu soka ni kazi kama zilivyo zingine.Au wewe ofisini kwako siku zote unafanyaga vizuri.Mugalu alishacheza simba kwa kiwango kikubwa tu swala lakutofanya vizuri msimu ulioisha haimaanishi kua ni mbaya.Au wewe unajua sana kuliko uongozi wa simba na bench la ufundi?.Nyie ndo wale mashabiki wapuuzi wanaotaka kuingiza mihemko kwenye soka.
Nawee ni shabiki wa mpira? Unajua unachokizungumza??
 
Back
Top Bottom