Waafrika wengi bado tuna colonial mentality, ni ngumu sana kumtambua mwafrika alielimika na ambae hajaelimika!! Anae jiita msomi utamkuta kwenye foleni ya babu wa loliondo akisubiri apewe kikombe kilichojaa maji, akiamini eti hayo maji yanatibu na kumaliza kabisa magonjwa ya kansa,ukimwi,kisukari na mengine yote sugu!!! Ambae hajaelimika utamkuta anakata mauno kwenye viwanja vya mikutano akishangilia na kuamini porojo za yule "msomi" alietoka kunywa maji ya kikombe loliondo!! kuwa atamletea neema na kumaliza matatizo yake yote aliyonayo!!! Wengine utawakuta wakilia makanisani wakimlilia Mungu, wanatafuta wanaume wa kuwaoa,na maisha mazuri kwa njia za kimiujiza!!! Ni ngumu sana kumuelewa mwafrika,huyo waziri ni sample tu,huoni mwingine anajiona katika watu milioni zaidi ya hamsini yeye peke yake ndio mwenye akili kuliko wote,hao Wakoloni hawakuondoka hivi hivi waliacha wamepanda mbegu kichwani mwetu,sasa wanavuna taratibu wakiwa uko kwao.