Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Baada ya Waziri fulani kujitumumua na kujimwambafai mbele ya waandishi wa habari kuwa msanii fulani hawezi kumkosoa kwa kuwa yeye ana degree 4, hizo insults nahisi zina-hold for all na tumedharauliwa wote wenye tuelimu tudogo kwamba eti tulioishia darasa la 7 kamwe hatuwezi kuwaonya na kuwakosoa wenye degree 4.

Wale wote tulioishia la saba tuungane tuone ni jinsi gani tunaweza ku-rise nguvu ya kuweza kuwakosoa wale waliopotoka kwa kuwa wana madrigrii mengi mengi zinazokaribia zile za thermometer.
Rudi shule.Wenzako walipokuwa wakomaa kusoma wewe ulikuwa unashida club eti saizi tukuonee huruma.Nakuambia tena Ukiona mwenye PHD amejeruhiwa sehemu ujue wewe mwenye kadigirii kamoja ungekufa na kusagika.
 
Wazazi wake bwana mkubwa naamini hawana PhD kama yeye je ina maana wakiona kuna mambo fulani anafanya ndivyo sivyo hawawezi kumuita na kumshauri kufanya lililo jema.
 
Ana degree 4 lakini gari lake likiharibika analipeleka gereji na anashauriwa ili lipone nini kifanyike.. pumbavu
 
Kama kweli kayasema hayo, basi hayo ndio tunaita matumizi mabaya ya akili.

Hua najiuliza kama hii ndo aina ya viongozi tunaowaamini kufanya maamuzi ya nchi. Je, nchi yetu iko salama kweli?
Natamani huu uzi uwe ni propaganda na isiwe kayasema hayo kweli .
Kayasema hayo.... unahitaji clip?
 
Mtume Muhammad (S.A.W) hakuwa na elimu hata ya chekechea.. lakini leo hii hata wenye digriii 200 wanafuata matendo yake na maamrisho yake..
 
Haya mambo ya kujimwambafai kisa elimu yako na kuwaona wengine hawana uwezo wa kukueleza jambo lolote pia ni ukiazi
 
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"

Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
Waziri anayumba sana, wakiiimba mambo ya Sodoma na Gomora hawataki, wakiimba mambo yenye akili hawataki au wanataka nyimbo za cheichei
 
IMG_4051.JPG
 
Mpaka sasa kati ya wawili hawa mwenye akili zaidi ameshajulikana

Waswahili husema debe tupu haliishi kutika.
 
Digree nne! Anajua kutengeneza Simu? anajua IC inavyotengenezwa? Hawa ndiyo wale wanaotoswa kwenye maji na Waendesha Ngalawa wanapovuka mito.

Mimi msomi...
Ogelea basi..
Hahahahaa naikumbuka hii kitu pale Ifakara kuna jamaa alileta ujinga wake watu wakamzabika mtoni kumbe hata kupiga mbizi hajui.
 
Waweza kuwa na degree sabini ila moja ndio inafanya kazi..Mzee JK alisema kuhusu KUJIMWAMBAFY lakini yawezekana watu wengi haka kaugonjwa kanawatesa sana..ni bora kusikiliza na kufanyia kazi wazo au kulipuuza kwa kutokujibu kuliko kutoa jibu la kijigamba kusikomsaidia mwanachi ambaye Baba wa Taifa anatambua na alisema anahitaji ukombozi na kusaidiwa na aliyepewa dhamana (Kiongozi).
 
Back
Top Bottom