Rombo: Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Kushirikiana na Mpenzi wake Kumuua Mama yake

Rombo: Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Kushirikiana na Mpenzi wake Kumuua Mama yake

Wadad wa chuga nawagwaya sana.

Wao kuua ni jambo dogo sana.
Rombo sio chuga...anyway ishu ya mauaji hayo ipo sio huko tu japo kwa huko ni kama matukio ni mengi japo sijajua ni kwamba report znafika sana kwenye media kuliko maeneo mengine/mikoa mingine au ishu ikoje.
 
Rombo sio chuga...anyway ishu ya mauaji hayo ipo sio huko tu japo kwa huko ni kama matukio ni mengi japo sijajua ni kwamba report znafika sana kwenye media kuliko maeneo mengine/mikoa mingine au ishu ikoje.
Najua hilo mkuu.
Kwa watu tulio nje ya kanda ya kaskani imezoeleka kua kila mtu wa huko ni mchaga kama ilivyozoeleka kila mtu kutoka mbeya ni mwaisa.
 
Wanawake wa Kilimanjaro kukuua kwa sababu ya mali ni jambo la kawaida na kwenye mali hawaangalii kama huyu ni mama ama baba ama mume wanakushughulikia vizuri sana.

Sio uongo watu wa huko ni wa kuogopa kama ukoma.
Hivi shida ni nini hadi wanakuwa wanahusudu mali na pesa kuliko chochote unajua hadi sasa bado natafuta majibu sijapata?

Au kuna kitu kiliingia kwenye maji kikaenda kuwaharibu ubongo hadi wanakuwa ni mazombie kwenye pesa kiasi hicho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapenzi wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumuua bibi kizee wa miaka 100 kwa kumpiga na kitu kizito kichwani wakati wakigombea ardhi.

Bibi huyo, Felister Silayo, mkazi wa Kijiji cha Kirongo juu, Kata ya Kirongo Samanga, Wilaya ya Rombo alifikwa na umauti Agosti 13 akiwa nyumbani kwake baada ya kuvamiwa na watu hao na kupigwa na kitu kizito kichwani wakati akiingiza ndani majani ya mbuzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema juzi kuwa wapenzi hao walikamatwa juzi na sasa wanaandaa jalada kwa ajili ya kupeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro tunawashikilia watu wawili ambao ni wapenzi kwa tuhuma za mauaji ya bibi kizee. Baada ya tukio tulifanikiwa kumkamata mwanamke na kwa bahati mbaya mpenzi wake alitoroka, lakini jana tumemkamata na wote wawili tunao,” alisema.

Kamanda Maigwa alisema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa ardhi uliokuwepo muda mrefu tangu mwaka 1990 kati ya bibi huyo na mtoto huyo a kike.

Kutokna na tukio hilo, kamanda Maigwa aliwasihi wananchi kupata hati miliki ya ardhi, ili kuepuka migogoro ya ardhi inayosababisha uvunjifu wa amani na mauji kama hayo. Bibi huyo alizikwa Agosti 20 nyumbani kwake kijiji cha Kirongo juu, kata ya Kirongo Samanga.

Awali, ndugu wa bibi huyo, Plasidi Constantine (60) alidai bibi huyo alikuwa na watoto wawili--- mmoja wa wa kiume na mwingine wa kike na kila mmoja alimpa shamba lake, baada ya mgawanyo wa mashamba mtoto huyo wa kike aligoma kuondoka nyumbani akitaka kuchukua maeneo yote, jambo ambalo lilileta mgogoro.

Aliekeza kuwa hali hiyo ilisababisha mtoto huyo wa kiume kutoroka nyumbani.

“Cha kushangaza huyu mtoto wa kike baada ya kupewa eneo laake hakutaka kuondoka hapa nyumbani kwa huyu bibi akawa anang’ang’ania kukaa.

Alitaka kuchukua maeneo yote mawili...mwisho wa siku ndio hivyo huyu bibi ameuawa. Kwa kweli tunasikitika,” alisema.

Source: Mwananchi
Huyo dada anatokea maeneo gani; Machame, Rombo, Kibosho, au Marangu?
 
Hivi shida ni nini hadi wanakuwa wanahusudu mali na pesa kuliko chochote unajua hadi sasa bado natafuta majibu sijapata?

Au kuna kitu kiliingia kwenye maji kikaenda kuwaharibu ubongo hadi wanakuwa ni mazombie kwenye pesa kiasi hicho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wote wanahusudu pesa hasa wasichana wenye sura nzuri na maumbo ya kuvutia.
Style tu ya kuzipata inatofautiana ila wengi wako radhi kufanya ushetani ili wapate pesa
 
Back
Top Bottom