Rombo: Kuyumba kiuchumi na kushindwa kulea familia vyasababisha Wanaume kupigwa na Wake zao

Rombo: Kuyumba kiuchumi na kushindwa kulea familia vyasababisha Wanaume kupigwa na Wake zao

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Kuyumba kiuchumi na kushindwa kuwajibika katika malezi ya familia kwa baadhi ya wanaume, kumetajwa kuwa moja ya sababu za kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya kikatili na wake zao.

Hayo yalibainishwa jana na ofisa Mtendaji wa Kata ya Kingachi, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Issa Maringo wakati wa kikao cha kamati ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili wa Kijinsia kwa watoto na wanawake (Mtakuwa) cha kata hiyo.

Kikao hicho kilichoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu na kutoa msaada wa kisheria (Ajiso) kilikuwa na lengo la ufuatiliaji wa matukio ya kikatili katika kata hiyo.

Maringo alisema kumekuwepo na vikundi vingi vya kuwezesha wanawake kiuchumi, ikiwemo vicoba, hivyo kumiliki uchumi na kuwaacha wanaume nyumbani. “Kutokana na hili baadhi ya wanaume wamejiingiza kwenye ulevi wa kupindukia na kuambulia vipigo kutoka kwa wake zao, pindi wanaporudi nyumbani,” alisema Maringo.

Aliongeza kuwa baadhi ya wanaume hunyanyaswa katika familia lakini wanaogopa kusema.

Kwa upande wake, mjumbe wa kamati hiyo, Erenia Kimaro alisema ipo haja sasa kwa Serikali na mashirika yanayotetea wanawake, kuwatazama wanaume na kuona namna ya kuwawezesha kiuchumi kupitia vikundi, ikiwemo vicoba ili kuondokana na manyanyaso.

“Wanawake wamekuwa wakipewa kipaumbele sana, leo wamewezeshwa kiuchumi kupitia vicoba na hata fedha za Serikali, hawakai nyumbani wanatoka kwenda sokoni kutafuta, baba ndiye anabaki nyumbani kulisha mifugo, hili linawaathiri wanaume wengi na kuishia kunywa pombe kupunguza msongo wa mawazo,” alisema.

Naye Kaimu mratibu wa Mtakuwa Wilaya ya Rombo, Lightness Msemo alikiri kuwepo vitendo vya kikatili dhidi ya wanaume wilayani humo na kueleza kuwa matukio hayo kwa sasa yameibuka kutokana na elimu ambayo imekuwa ikitolewa kwenye jamii na Ajiso na kamati ya Mtakuwa.

“Matukio ya kupigwa kwa wanaume kwa sasa yameibuka kwa wingi kutokana na elimu inayotolewa na shirika la Ajiso linalofanya kazi kwa kushirikiana na kamati za Mtakuwa.

“Hata hivyo, siyo wengi wanaoripoti, bado wapo wengi wanahofia kutoka hadharani kutoa taarifa za kupewa kipigo na wake zao kwa kuona watakuwa wanaaibika kwa jamii,” alisema.

Akilizungumzia hilo, ofisa ufuatiliaji wa shirika hilo, Yolanda Kimwangana alisema wamekuwa wakifanya kazi Rombo na kamati za Mtakuwa na kupitia mafunzo ambayo wamekuwa wakiyatoa kwenye kamati, jamii imepata uelewa na kushiriki kwa karibu kukomesha matukio ya ukatili kwa jamii.

Alisema katika ufuatiliaji, wamebaini uwepo wa matukio ya migogoro ya ndoa na ardhi, vitendo vya ulawiti na ubakaji, pamoja na utoro wa wanafunzi mashuleni unaochangiwa na changamoto ya malezi duni.

Chanzo: Mwananchi
 
“Matukio ya kupigwa kwa wanaume kwa sasa yameibuka kwa wingi kutokana na elimu inayotolewa na shirika la Ajiso linalofanya kazi kwa kushirikiana na kamati za Mtakuwa.

“Hata hivyo, siyo wengi wanaoripoti, bado wapo wengi wanahofia kutoka hadharani kutoa taarifa za kupewa kipigo na wake zao kwa kuona watakuwa wanaaibika kwa jamii,” alisema.
Hao warombo wa kiume si riziki🙄
Wanaaibisha jinsia ya Me!
 
Tatizo vijana walobaki kijijini wanaendekeza pombeee

Zao la kahawa lilikuwa likiwabeba sana na kwa sasa halipoo, shughuli mingine za kujipatia kipato ni za msimu, hata huku mjini wapo wanaume wananyanyuka kwenda kutembea popote ilimradi anaweza okota chochote. Mwenda bure sio sawa na mkaa bure huenda akaokota chochote
 
Wanaume wa rombo hela yao ni ya bia na gongo tu hata muda wa kula hawana. Hivyo wanadhoofika mno. Wamama wanalima, wanafanya vibarua, wanauza ndizi, wanakula chakula hivyo wana nguvu. Sasa vicoba si waanzishe vya wanaume na wao?
 
Ndo ilivyo hiyo siku zote na ndio sababu hata ndani ya nyumba Me ndo akiwa anafanya kazi mke hajishughulishi manyanyaso, masimango, maneno madogo madogo yasiyo na kichwa wala miguu kuwepo ni lazima.

Ni wachache waelewa.

Hivyo hao Me wa Rombo wasipotafuta njia za kujitafutia kipato wataendelea sana kula mbata.
 
Huko ndo kulipoanza tatizo la nguvu za kiume🤣🤣🤣
Wakahamia dar Kuna kipind wanawake walikuwa wanaenda mpaka Kenya kukidhi haja zao za kimwili
 
Back
Top Bottom