Ronaldo pamoja na kuwa na hela nyingi mpaka leo hajaoa (ana mchumba tu), lakini wewe Pangu Pakavu ushajitwisha majukumu

Ronaldo Ni Ronaldo mimi ni mimi kwahiyo kisa Ronaldo hajaoa na wengine tusioe? Zuckerberg na Ronaldo Nani tajiri? Ila Zuckerberg mbona ameoa? Warren buffet na Ronaldo nani tajiri? Mbona buffet ameoa? Steve job mpaka anafariki alikuwa ana mke! Acha kupangia maisha kila mtu ana choice yake kwenye maisha hatujaja dunia kuigana hapa kila ashinde mechi zake
 
Kabla ya hao uliwataja kuwepo hapa chini ya jua,walikuwepo wengine wa namna hiyo?
Je ni dhambi sisi wengine kutowaiga?
 
Mimi nilihisi ukiwa na pesa utapata furaha ila baada ya kuzipata nimegundua pesa haiwezi leta furaha japo ni muhimu
Sahihi % 💯. Una pesa ila ndani huna hata mtu wa kukujulia hali. Unapishana na makolokolo ya billions of money yasiyoongea. Unakufa unaacha mali kwa taasisi za ugawaji mali. Mhubiri 2:11. "Kisha nitaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu katika kazi yangu yote na taabu yote niliyotaabikia katika kuzitenda , na tazama yote ni ubatili na kujilisha upepo, Wala faida hakuna chini ya jua."
 
Kama ilivyo kwako kuwa na ronaldo kama role model wako bila kuchaguliwa na mtu yeyote, vivyo hivyo waliooa kuna kitu/watu waliwainsipire kuoa.

Ishi na useja wako, wao waishi kwenye ndoa zao. Usiwapangie wala usitake mfanane
 
Hii dozi inaweza kuuaa 😁😁😁 wengine hata hizo nyumba za tope hawana labda wakifa wake zao warithi mashati yao ya oversize
 
Hii dozi inaweza kuuaa 😁😁😁 wengine hata hizo nyumba za tope hawana labda wakifa wake zao warithi mashati yao ya oversize
Hebu na wewe shangaa!! Eti mali 🤣🤣

Hiyo mishati yenyewe oversize unakuta ni mkewe alimsuprise nao… 😹
Hebu waje na utetezi wenye uzito ila sio kurithi mali, hivi wanazijua mali kwanza mbwa Hawa.!??
 
Tatizo lenu 'bendera fuata upepo' huangalia maisha ya nje ya mtu ama kitu zaidi na kukitengenezea conclusion.

Ni kuulize: ulishamchunguza ukamilifu wake wa kiume na kisha ukaongea naye juu ya mustakabali wa maisha yake akaja na jibu zuri juu ya unayoyatolea ushuhuda, tuchambulie alisemaje?

Je kama jongoo lake halipandi mtungi na anapakatwa, ukishalijua hilo baadaye utakuja kurekebisha topic, ama utaendelea kumchukulia kama role model wako?

Maisha ya mtu hayatolewi mfano kwa sababu kila mmoja ana njia zake za maisha na kwamba maisha hayana formula.
 
Kila mtu anaeoa ana lengo lake 1 ni zinaa anaeoa Ili asizini 2 ni awe mke wake Halali hata kikitokea chochote awe na pakuanzia 3 haki za msingi zinazowatambua wanandoa Kila Moja apate haki yake 4 watoto kuwa na baba ndani ya ndoa. Ronaldo ni nani mpaka tumfanye wakumuiga? Tuache mafundisho ya Allah tumfate to Dolnaro?
 
Hebu na wewe shangaa!! Eti mali 🤣🤣

Hiyo mishati yenyewe oversize unakuta ni mkewe alimsuprise nao… 😹
Hebu waje na utetezi wenye uzito ila sio kurithi mali, hivi wanazijua mali kwanza mbwa Hawa.!??
Ila wewee 🤣🤣🤣 mishati ya surprise
 
Mimi nilihisi ukiwa na pesa utapata furaha ila baada ya kuzipata nimegundua pesa haiwezi leta furaha japo ni muhimu
Mama yangu alistaafu mwaka 2020 akapewa 85 millions ya kiinua mgongo kisha akakimbia kutoka Dar akarudi kijijini kwao Dodoma. Pesa zimemuisha anaanza kunitafuta kwenye simu ananijulia hali. Wakati hakunipa hata shilingi 50.

Nimemwambia, kila mmoja ashinde mechi zake.

Nimemwambia akinitatuta tena kwenye simu nitamtukana..
 
Mwanaume kamili, rijali , timamu, mpambanajj anaona fahari kuzaa, kutunza na kunidhamisha (discipline) Haogopi. Mtoto wa mama, shoga, na mfuasi/mtetezi wa wazungu atapiga miayo, na blaa blaa na kulia lia. Africa tusipozaa nani akae na kuishi.
 
Huyo ni mzazi wako, kala chake nawe tafuta chako. Mheshimu daima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…