Ronaldo pamoja na kuwa na hela nyingi mpaka leo hajaoa (ana mchumba tu), lakini wewe Pangu Pakavu ushajitwisha majukumu

Kila mtu anaeoa ana lengo lake 1 ni zinaa anaeoa Ili asizini 2 ni awe mke wake Halali hata kikitokea chochote awe na pakuanzia 3 haki za msingi zinazowatambua wanandoa Kila Moja apate haki yake 4 watoto kuwa na baba ndani ya ndoa. Ronaldo ni nani mpaka tumfanye wakumuiga? Tuache mafundisho ya Allah tumfate to Dolnaro?
Kilichomkuta Bill Gates na Abromovic unakijua?? Wanawake wa sasa ni business oriented, sasa wee jifanye Mr. Lover man, utakuja kusimulia hapa..
 
Huyo ni mzazi wako, kala chake nawe tafuta chako. Mheshimu daima.
Sawa nitatafuta changu hata kwa kuuza karanga, yeye pia aache kuwasiliana na mimi.
Kwanini ananitafuta baada ya pesa kumuisha sasa?? Mimi kapuku ananitafuta wa nini??

Akiendelea kunitumia SMS au kunipigia simu, nitamtukana matusi ya nguoni. Aniache na kazi zangu za kuuza Uji..
 
Kwamba Ronaldo ndio SI Unit ya Maisha ? Kama hutaki kuoa hata kama Dunia Nzima wakioa sio lazima wewe upate mke.., Na kama unataka Mke hata kama Dunia nzima wakiamini Mke ni laana wewe fanya roho inapenda.... You are the Best Judge of Yourself...

Kilichomkuta Bill Gates na Abromovic unakijua?? Wanawake wa sasa ni business oriented, sasa wee jifanye Mr. Lover man, utakuja kusimulia hapa..
Kuachana kwa matajiri uliowataja ni mfano kuwa kutafuta pesa na kuchelewa kuoa sio suluhisho la ndoa wala kuzaa watoto wachache. Ukiamua na sio shoga na unamudu kuwatunza zaa wengi tu.
 
Kama ilivyo kwako kuwa na ronaldo kama role model wako bila kuchaguliwa na mtu yeyote, vivyo hivyo waliooa kuna kitu/watu waliwainsipire kuoa.

Ishi na useja wako, wao waishi kwenye ndoa zao. Usiwapangie wala usitake mfanane
Mada inataka utaje faida za ndoa ambazo mseja hazipati
 
Kuachana kwa matajiri uliowataja ni mfano kuwa kutafuta pesa na kuchelewa kuoa sio suluhisho la ndoa wala kuzaa watoto wachache. Ukiamua na sio shoga na unamudu kuwatunza zaa wengi tu.
Bila shaka haujaelewa mantiki yangu. Hao jamaa walipokonywa Mali zao baada ya divorce. Ni bora kuishi nao kuliko kufunga ndoa..
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Hata mzee Slaa bado anaishi na mchumba wake Josophin kama sijakosea
Huwa mnapotosha maana ya maneno ya kiswahili saazingine bila kujua.

Hauwezi kuishi na mchumba hata siku moja, mchumba huishi kwa wazazi wake na hauruhusiwi kumgusa hadi mfunge ndoa.

Partner unayeishi naye ni mke/mme ama kimada inategemeana na vigezo vya kisheria.

Kama mmefunga ndoa huyo ni mme/mke.

Kama hamjafunga ndoa mnaishi tu huyo ni kimada.

Kwa hiyo Dr. kama anaishi bila ndoa, anaishina kimada wake.
Mama yangu alistaafu mwaka 2020 akapewa 85 millions ya kiinua mgongo kisha akakimbia kutoka Dar akarudi kijijini kwao Dodoma. Pesa zimemuisha anaanza kunitafuta kwenye simu ananijulia hali. Wakati hakunipa hata shilingi 50.

Nimemwambia, kila mmoja ashinde mechi zake.

Nimemwambia akinitatuta tena kwenye simu nitamtukana..
Huyo ni mama gani, mamako mzazi au mama wa kambo yaani mke wake baba?
 
Je kama jongoo lake halipandi mtungi na anapakatwa, ukishalijua hilo baadaye utakuja kurekebisha topic, ama utaendelea kumchukulia kama role model wako?
Hiki kichaka unachotaka kulitumia kujifichia ni kidogo sana. Kwa taarifa yako tu ni kwamba Ronaldo ana mtoto ambaye alizaa na mchumba wake wa kwanza. Yuko kwenye aoademi za mpira hivi Sasa.
 
Sikia, siyo kila baba unayesikia kazaa ni baba.
Na mama anayezaa bila uangalizi wa haki aweza asiwe mama.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Bila shaka haujaelewa mantiki yangu. Hao jamaa walipokonywa Mali zao baada ya divorce. Ni bora kuishi nao kuliko kufunga ndoa..
Kupokonywa mali sio sababu ya kutooa. Hata ukizaa bila ndoa utaandamwa na kanuni za kisheria kutunza au kulea. Kilicho nyuma ya mjadala wa kukataa ndoa ni ukisasa au ushoga. Tuoe na kuzaa na kuwatunza. Utamaduni, lugha, na asili vipo kwa kuwa tuliozaliwa, tulilelewa na kutunzwa. Tusiige yasiyotuhusu.
 
Kila mtu anaeoa ana lengo lake 1 ni zinaa anaeoa Ili asizini 2 ni awe mke wake Halali hata kikitokea chochote awe na pakuanzia 3 haki za msingi zinazowatambua wanandoa Kila Moja apate haki yake 4 watoto kuwa na baba ndani ya ndoa. Ronaldo ni nani mpaka tumfanye wakumuiga? Tuache mafundisho ya Allah tumfate to Dolnaro?
Dhambi haipo kwenye zinaa tu. Dhambi inapatikana kwa kuwaza, kunena na kutenda.

Mna usafi gani hadi useme mmeoa kukwepa kumuudhi mwenyezi Mungu?
 
Sawa nitatafuta changu hata kwa kuuza karanga, yeye pia aache kuwasiliana na mimi.
Kwanini ananitafuta baada ya pesa kumuisha sasa?? Mimi kapuku ananitafuta wa nini??

Akiendelea kunitumia SMS au kunipigia simu, nitamtukana matusi ya nguoni. Aniache na kazi zangu za kuuza Uji..
Kuna shida sehemu, nahisi si mzazi wako.
 
Kupokonywa mali sio sababu ya kutooa. Hata ukizaa bila ndoa utaandamwa na kanuni za kisheria kutunza au kulea. Kilicho nyuma ya mjadala wa kukataa ndoa ni ukisasa au ushoga. Tuoe na kuzaa na kuwatunza. Utamaduni, lugha, na asili vipo kwa kuwa tuliozaliwa, tulilelewa na kutunzwa. Tusiige yasiyotuhusu.
Kwisha hiyo.
 
Kuitunza na kulea watoto wangu kwani kuna ubaya gani?? Siwezi kugawana Mali zangu na toto la mtu mwingine eti kisa ndoa..
 
Kustaarabika?
Kwangu ni tofauti kidogo,
Kitendo cha huyo Mjaluo kuvuta sigara tu kwangu ni upumbavu uliokithiri.

Mimi nadhani masikini wa mali waliowengi ndio wanamuona huyo OBAMA kama role model wao kwa kudhani kuwa wale binti zake watashindwa kutumia mali za baba yao kikamilifu na kuwapatia wao kama msaada.

Haya mawazo hata mtoa mada anayo sana.
Acheni utegemezi!
Mtu unaishi kwa shemeji yako,utaoa ili iweje?
Dada yako akifukuzwa wewe na mkeo mtabaki?
Hakuna hoja inayostahili kujibiwa hapa, a lot of jokes in here.
 
Nani alikuambia kuoa ni dili wewe mwanaume mlalahoi? Kipato chako cha mwezi Ronaldo anakipata kwa sekunde 1 tu, lkn mpk leo hajaoa.

Sasa wewe Choka Mbaya kwann unajitafutia stress?

Hebu taja faida za kuoa ambazo asiyeoa kamwe hawezi kuzipata.

View attachment 3188558
Huyu ndiye mchumba wa Ronaldo.
Kataa ndoa tunaumaliza mwaka 2024 kwa ushindi wa 3-0
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Nani alikuambia kuoa ni dili wewe mwanaume mlalahoi? Kipato chako cha mwezi Ronaldo anakipata kwa sekunde 1 tu, lkn mpk leo hajaoa.

Sasa wewe Choka Mbaya kwann unajitafutia stress?

Hebu taja faida za kuoa ambazo asiyeoa kamwe hawezi kuzipata.

View attachment 3188558
Huyu ndiye mchumba wa Ronaldo.
Hana nguvu za kiume huyo ndio.maana wanawake hawataki kuolewa naye wanabaki urafiki tu
 
  • Kicheko
Reactions: G4N
Back
Top Bottom