TANZIA Rose Nyerere, Mtoto wa Mwisho wa J.K Nyerere afariki dunia

TANZIA Rose Nyerere, Mtoto wa Mwisho wa J.K Nyerere afariki dunia

Umuofia Kwenu wana JF,

Kheri ya Mwaka Mpya!

Mtoto wa mwisho wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Rose Nyerere amefariki leo mjini Dar es Salaam.

Taarifa za duru za uhakika zinaarifu kuwa Rose amefariki katika hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam ambako alilazwa kwa muda mrefu. Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.

View attachment 1665226

KK,
MINJINGU.

Dar es Salaam. Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imepata msiba wa mtoto wao Rosemary Nyerere aliyefariki jana jioni jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wanafamilia aliyejitambulisha kwa jina la Sophia Nyerere ameandika katika mtandao wa Instagram kuwa shangazi yake amefariki.
Mwananchi limewatafuta baadhi ya wanafamilia akiwemo Manyerere Jacton aliyethibisha kuwa ndugu yao amefariki.

"Ni kweli dada amefariki jioni hii, lakini taarifa rasmi itatolewa," amesema Manyerere.

Rosemary alikuwa miongoni mwa watoto saba wa Mwalimu Nyerere
Alikuwa mzee kuliko mama Yake
 
Kuna thread nyingine humu pia imemtaja JOHN NYERERE kuwa amefariki dunia Muhimbili na kuwa kaka yake Madaraka Nyerere amethibitisha kifo hicho. Ndio kusema watoto wawili wa Mwl. Nyerere wamefariki wakati mmoja au ni misinformation mahali?
Ww Masundi ni mkongwe humu.....
umeshindwaje kutofautisha thread mpya na ya zamani!!??
 
Kulikuwa kuna haja gani ya kutaja Jina la Hospitali ?
Wacheni Unafiki...!!
Angefia kwenye Hospital kubwa India hata ingetajwa isingekua shida....
Angefia Muhimbili pia hata ingetajwa isingeleta shida....

Kafia alipofia Unaumia Hospital iliyojaribu kuokoa Maisha yake kutajwa, au Kwa vile ni Hospital ndogo!!?

Acha Unafiki!
 
Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani ya milele. AMINA
 
yalikuwa ya chini kivipi wakati alikuwa na degrees na mkufunzi wa hadi chuo kikuu?
Labda analinganisha maisha yake na ya Mh. Zitto! Bwana alitoa Bwana ametwaa jina lake na liabudiwe!
 
Labda analinganisha maisha yake na ya Mh. Zitto!
Mkuu hili jina lako la Ndebile ni la asili ya wapi? Na maana yake ni nini?

Kuna kabila moja wao hutoa jina la ndebile kwa watu wenye mapungufu fulani...nikawa curious kidogo kujua khs wewe
 
Kulikuwa kuna haja gani ya kutaja Jina la Hospitali ?
Siku zote hospitali zimekua zikitajwa. Sijawahi kuona taarifa ikisema mtu amefariki baada ya kulazwa hospitali kwa muda bila kutaja jina la hospitali. Mleta taarifa hajakosea lolote, ingekua kosa kama angetaja ugonjwa. Umri wako ukiongezeka utajua hilo ni jambo la kawaida.
 
Conclusion ninayoiona Ni kuwa Kuna kilio Cha Muda mrefu Cha watanzania kutaka familia hii ipewe heshima ya kipekee kabla hawajatoweka wote tunaasili ya ki monarch hivyo tunawatazama Kama ma Prince lakini sivyo wanavyo chukuliwa, vyeo wanalimbikiziwa watoto wa wakuja that is not Honour
 
Mkuu hili jina lako la Ndebile ni la asili ya wapi? Na maana yake ni nini?

Kuna kabila moja wao hutoa jina la ndebile kwa watu wenye mapungufu fulani...nikawa curious kidogo kujua khs wewe
Watoto
Mkuu hili jina lako la Ndebile ni la asili ya wapi? Na maana yake ni nini?

Kuna kabila moja wao hutoa jina la ndebile kwa watu wenye mapungufu fulani...nikawa curious kidogo kujua khs wewe
Ndebile (kisukuma) = watoto njiti
Kuna member kasema maisha ya marehemu yalikuwa ya chini (material things kama nyumba, magari nk) nami nikatoa mfano wa mwanasiasa ambaye ana vitu hivyo lakini bado maisha yake bado ni ya ovyo! Wenye akili wameelewa!
 
Back
Top Bottom