TANZIA Rose Nyerere, Mtoto wa Mwisho wa J.K Nyerere afariki dunia

TANZIA Rose Nyerere, Mtoto wa Mwisho wa J.K Nyerere afariki dunia

Lala salama Rose
Pole kwa familia na wote walioguswa na msiba
 
Umuofia Kwenu wana JF,

Kheri ya Mwaka Mpya!

Mtoto wa mwisho wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Rose Nyerere amefariki leo mjini Dar es Salaam.

Taarifa za duru za uhakika zinaarifu kuwa Rose amefariki katika hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam ambako alilazwa kwa muda mrefu. Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.

View attachment 1665226

KK,
MINJINGU.
Kwa muonekano wa picha inaonekana kabla hata ya kuumwa alikuwa anaumwa.
R.i.p rozi.
 
Kafanana na Mwalimu mpaka meno.
R.I.P mtoto wa Nyerere.
 
Pole sana mama yetu mama Maria, Mwenyezi Mungu awe nawe na familia nzima ya mwalimu katika kipindi hiki kigumu
 
R.I.P mdogo wangu Rose!
Hukuwa na makuu - Mungu akupokee ktk falme isiyoisha
 
Kuna thread nyingine humu pia imemtaja JOHN NYERERE kuwa amefariki dunia Muhimbili na kuwa kaka yake Madaraka Nyerere amethibitisha kifo hicho. Ndio kusema watoto wawili wa Mwl. Nyerere wamefariki wakati mmoja au ni misinformation mahali?
 
Sana, na alikua anasaidia sana watu,niliwahi kwenda kwake,Upanga huko,Loan Board walikua wanazingua,akanipeleka kwa Mwenyekiti wa Loan Board enzi hizo alikua Nimrord Mkono,Mkono akapiga simu tukaenda kwa Mkurugenzi wa HESLB,tukaenda hadi kule,siku hiyo hiyo mkopo wangu ukawa fresh,nikaambiwa baada ya siku tano mzigo utajaa! Kweli bwana,ilikua jumanne,ijumaa mzigo huo! Mother was very humble,na still akanipa number yake,na bado akanipa na pesa kidogo kabla ya mzigo wa bodi hujazama
Nenda msibani....
 
Back
Top Bottom