Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Hapa kuna utata.
Ila Kwa mujibu wa mada, kosa la Rose lipo wapi?
Tuanzie hapa kwanza... Rose ni nani kwenye ile zahanati mpaka kutoa amri vipimo vilivyo expire vitumike kwa wajawazito?
Bila shaka rose anamajukumu fulani yanayohusiana na store ya dawa ndio maana labarotory Technologist alienda kwake kutoa hiyo taarifa.

Lab tech hawezi kunyenyuka na kwenda kwa nurse kusema "situmii vifaa vimexpire"?
Kwanini taarifa iende kwa rose? Jibu rahisi Rose alikuwa responsible kwenye hicho kipimo.
 
Mtu ukimuambia Jambo kama haelewi wewe unafanyaje?

Hapo Rose alikuwa anamjibu mfanyakazi mwenzake kulingana na Muktadha wa mazungumzo Yao.
Huyo James Getogo alichokuwa anatafuta ni Shari tuu. Na kaipata. Na ndivyo inavyotakiwa.
Wewe ndio huelewi kabisa taratibu kazini tena huna weledi wowote nafikiri. Au umefunzwa na wakufunzi wababaishaji. Huwezi toa lugha kama hizo za rose shirima ofisini eti ikubaliwe kama ni sawa.
 
Hapo mimi siangalii nani anakosa hayo watayajua wenyewe... Kikubwa nimejua mwenendo mzima wa hospitali zetu zinavyofanya mambo yake...
Na huo usiri unaosema wewe ukizingatiwa ndio mambo hayo hushika hatamu zaidi...

Na kwakugundulika jambo hili ambalo mtaalamu huyo amevujisha kwa sababu anazo zijua yeye...
Najua wakubwa huko watajitafakari na kuanza kuchukua hatua stakihiki kuliko kungeendelea kuwapo huo usiri unao usema...

Mimi sijui kama hospitali hiyo ni ya serikali au private... Japo kwa hisia zangu nahisi 70℅ hiyo ni hospital ya government... Bwana maskini Tunalindwa na Mungu Wallah.
 
Wewe ndio huelewi kabisa taratibu kazini tena huna weledi wowote nafikiri. Au umefunzwa na wakufunzi wababaishaji. Huwezi toa lugha kama hizo za rose shirima ofisini eti ikubaliwe kama ni sawa.

Hizo Lugha zipo mbona kila Siku maofisini,
Nafahamu sio utaratibu lakini yapo mazingira Lugha hizo zinatumika hasa Kwa mambo ya kipuuzi au Watu wapuuzi wasioelewa wanachoambiwa.

Kumbuka hao Wawili ni wafanyakazi, huyo kijana hajatumia hizo Lugha Kwa sababu tayari anajua anarekodi video.
Lakini amini nakuambia,
Kama hiyo video ingerekodiwa alafu Wawili hao wote hawajui wanarekodiwa sio ajabu ungeshangaa huyo James ndio Mbaya zaidi.
 
Wewe ndio huelewi kabisa taratibu kazini tena huna weledi wowote nafikiri. Au umefunzwa na wakufunzi wababaishaji. Huwezi toa lugha kama hizo za rose shirima ofisini eti ikubaliwe kama ni sawa.
Huyu jamaa(ROBERT HERIEL) thread zake nyingi anaandika kinyume na uhalisia ili kupata umaarufu hapa JF.
Anajitahidi kuandika ukweli kwa baadhi ya thread... Lakini nyingi anapinga uhalisia kwa makusudi ili alete mjadala mkubwa target yake ni umaarufu usio na tija.
ROBERT HERIEL
 
Hapo mimi siangalii nani anakosa hayo watayajua wenyewe... Kikubwa nimejua mwenendo mzima wa hospitali zetu zinavyofanya mambo yake... Na huo usiri unaosema wewe ukizingatiwa ndio mambo hayo hushika hatakmu zaidi...
Na kwakugundulika jambo hili ambalo mtaalamu huyo amevujisha kwa sababu anazo zijua yeye...
Najua wakubwa huko watajitafakari na kuanza kuchukua hatua stakihiki kuliko kungeendelea kuwapo huo usiri unao usema...
Mimi sijui kama hospitali hiyo ni ya serikali au private... Japo kwa hisia zangu nahisi 70℅ hiyo ni hospital ya government... Bwana maskini Tunalindwa na Mungu Wallah.

😂😂😂
Wewe ndio unajua Leo Jambo Hilo.

Niliwahi andika hapa👉👉Kwa hawa Madaktari huko mbeleni tutapata tabu
 
Huyu jamaa(ROBERT HERIEL) thread zake nyingi anaandika kinyume na uhalisia ili kupata umaarufu hapa JF.
Anajitahidi kuandika ukweli kwa baadhi ya thread... Lakini nyingi anapinga uhalisia kwa makusudi ili alete mjadala mkubwa target yake ni umaarufu usio na tija.
ROBERT HERIEL

Kwa uelewa wako majibizano katika maofisi yapo au hayapo?

Ninyi ndio mnataka mkifanya upuuzi mjibiwe Kwa upoleupole.
Watakaojibiwa Kwa upole ni wateja tuu, tena Wateja wenye nidhamu, lakini wateja/wagonjwa wasio na nidhamu watajibiwa vikali vile wanavyojionyesha na kujieleza.
 
Kwanini majibizano kati yao wawili? By any chance mmojawapo anafanya kinyume au hatimizi majukumu yake...
 
Kwanini majibizano kati yao wawili? By any chance mmojawapo anafanya kinyume au hatimizi majukumu yake...

Kwa mujibu wa hiyo video Nani hatimizi wajibu wake?

Aliyesababisha majibizano ni James Getogo, Kwanza yeye ndiye kamfuata mwenzake,
Pili licha ya mwenzake kumuambia kuwa Aende Kwa incharge lakini bado anang'ang'aniza majibizano, Wakati ishu ilikuwa ndogo Mno.

Kama vifaa vime-expire Rose keshamuambia asitumie. Sasa tatizo ni lipi?

Makosa ya James
1. James kachafua hicho kituo cha afya
2. James kaichafua serikali.
3. James kafanya kosa kumrekodi mwenzake pasipo idhini yake.
4. James kapost na kusambaza mtandaoni au kawatumia wenzake video ya MTU mwingine akilenga kumchafua, Jambo ambalo ni kosa kisheria.
5. James hajafuata maadili ya Kazi katika kushughulika na majibu mabaya aliyojibiwa na Rose.

Makosa ya Rose
1. Kutoa maneno ya shombo na kashfa Kwa mfanyakazi mwenzake.
 
Ofisi nyingi zina taratibu za kusainisha wafanyakazi wote confidentiality form...

Kwa namna yoyote hupaswi kutoa mambo ya kazini nje ya ofisi...

Ngoja tuone... Though kafichua maovu...
 
Mbona sijaona kuandika hata kosa moja la rose Ina maana Yuko sawa... ukiangalia vizuri hio video sekunde mwanzoni James anasema dawa zime expire situmii lakini huyo rose anamjbu " mbona unakihelehele , unataka uwe mfanyakazi Bora"

Sasa wewe mkuu unataka kusema haujaona tatizo la rose hapa kweli?
 
Kwa mujibu wa hiyo video Nani hatimizi wajibu wake?

Aliyesababisha majibizano ni James Getogo, Kwanza yeye ndiye kamfuata mwenzake,
Pili licha ya mwenzake kumuambia kuwa Aende Kwa incharge lakini bado anang'ang'aniza majibizano, Wakati ishu ilikuwa ndogo Mno.

Kama vifaa vime-expire Rose keshamuambia asitumie. Sasa tatizo ni lipi?

Makosa ya James
1. James kachafua hicho kituo cha afya
2. James kaichafua serikali.
3. James kafanya kosa kumrekodi mwenzake pasipo idhini yake.
4. James kapost na kusambaza mtandaoni au kawatumia wenzake video ya MTU mwingine akilenga kumchafua, Jambo ambalo ni kosa kisheria.
5. James hajafuata maadili ya Kazi katika kushughulika na majibu mabaya aliyojibiwa na Rose.

Makosa ya Rose
1. Kutoa maneno ya shombo na kashfa Kwa mfanyakazi mwenzake.
Ungeandika hivi ungeonekana wa maana na unaipenda nchi yako.

1. James ni shujaa aliye fichua uozo wa hicho kituo unaotetewa na watu wengi rose na afisa utumishi.

2. James amesaidia serikali kujua majukumu yake nakwamba ina wajibu wa wakupeleka dawa sahihi na kuondoa dawa zote zisizo sitahili sokoni kwa wakati... Si kwenye hospital za serikali pekee bali kuanzia maduka ya dawa muhimu hadi pharmacy kubwa nchini.

3. James kafanya vizuri kurekodi kwani video inatumika kama ushahidi kuonesha uozo uliopo katika kituo husika na probably vituo vingi hapa nchini.

4. "Akilenga kumchafua" haya ni mawazo yako. Inawezekana lengo lake siyo kumchafua bali kufichua uovu wake wa kutaka vipimo vilivyo expire vitumike kwa wajawazito.

5. Utazishawishije ngazi za juu kuwa umejibiwa majibu mabaya na mtumishi mwenzio bila ushahidi. Hivyo, James alikuwa katika hatua ya mwanzo ya kukusanya ushahidi kwa ajili ya kushughulikia mdomo mchafu wa mtumishi mwenzie.

MAKOSA YA ROSE
1. Majibu mabaya kwa mtumishi... Hivyo kinyume na maadili ya kibinadamu.

2. Kukumbatia uozo wa Zahanati. Hivyo anaficha uovu kwa maslahi yake binafsi au kwa maslahi ya group la watu... Hivyo apishe uchunguzi.

3. Kuhatarisha maisha ya wajawazito na watoto watakao zaliwa... Maana nyepesi ni kuhatarisha maisha ya jamii ijayo kwa ujumla kwani inaweza pelekea kuzaliwa kwa watoto wasio na akili. - Hili amelitenda baada ya kusikika akisema "katumie hivyo vipimo kwa wajawazito"

4.....

HITIMISHO.
Nampongeza James kwa kukataa kutumia vipimo vilivyo expire kufanya hivyo amedhihirisha upendo halisi kwa wagonjwa na kwamba amewatendea yale ambayo hata yeye akiwa mgonjwa au mzima angependa kutendewa.
 
Mbona sijaona kuandika hata kosa moja la rose Ina maana Yuko sawa... ukiangalia vizuri hio video sekunde mwanzoni James anasema dawa zime expire situmii lakini huyo rose anamjbu " mbona unakihelehele , unataka uwe mfanyakazi Bora"

Sasa wewe mkuu unataka kusema haujaona tatizo la rose hapa kweli?
Hoja zake anaandika kwa ajili ya kupinga uhalisia... Kwa kutumia point za kufikrika.
 
Unaweza ibua Makosa ya familia yako? Badala ya kutafuta namna ya kuyatatua?

Hivi Mkeo akiibua Makosa yako Mbele ya umma ni halali Kwa muono wako?
Au wewe unakampuni na ndio boss alafu mfanyakazi mmoja anaibua Mbele za umma Makosa ya kampuni yako ni Sawa?

Hapo angefanya MTU wa nje ingekuwa Sawa Kabisa.
Sio kama nakataa Watu wasifichue Makosa au maovu, lakini waangalie nafasi zao na majukumu yao
Taasisi za serikali ni mali za umma. Na umma ni sisi wananchi. Je hutaki kujua yanayoendelea kwenye taasisi unayomiliki?
 
Ni kweli hii taarifa ingekua ya third party ingekua credible, otherwise sjaona issue ya kumwajibisha mtu, then huyo dada alimshauri mrekodi aende kwa in charge akapate ufafanuzi ambacho kilikua kitu sahihi .kama aliyerekod ni mtumishi WA serikali basi ashughulikiwe kwa kupeleka taarifa za serikali mahali pasipo sahihi.
 
Mdada ana majibu mabaya,ila ukiangalia wale watu wanaopenda kujibujibu hovyo,hasa kukiwa hakuna kamera,wanamtetea huyo dada.
Kwanini ajibu hovyo?
Kwanini asiwe HALISI,na ajulikane kua huwa yuko namna flani?
Huyo jamaa aliyerekodi kataka kuonyesha jamii hali ilivyo kwenye baadhi ya taasisi zinazotoa huduma za afya.
Sidhani kama trafiki au mwalimu angetoa majibu ya hivyohovyo,jamii ingechukuliaje.
 
Kwa mujibu wa hiyo video Nani hatimizi wajibu wake?

Aliyesababisha majibizano ni James Getogo, Kwanza yeye ndiye kamfuata mwenzake,
Pili licha ya mwenzake kumuambia kuwa Aende Kwa incharge lakini bado anang'ang'aniza majibizano, Wakati ishu ilikuwa ndogo Mno.

Kama vifaa vime-expire Rose keshamuambia asitumie. Sasa tatizo ni lipi?
Kaangalie tena video bila kuifoward James hapo anaktaa kutumia kifaa kilicho expire huyo rose unayemtetea anamjbu jamaa aache kiherere tena kamuuliza "unataka ufanyakazi Bora au" yaani kufuata utaratibu ni kiherere kwa mjubu wa rose
Makosa ya James
1. James kachafua hicho kituo cha afya
2. James kaichafua serikali.
Kama kufichua uovu wa serikali au taasisi ni kuichafua basi inanifanya nikushangae kwa ulichokiandika ,
James kafanya kosa kumrekodi mwenzake pasipo idhini yake.
Hauitaji ruhusa mtu kufichua uovu
 
Back
Top Bottom