Rostam Aziz anunua asilimia 31.5 ya Williason Diamonds (Mwadui)

Rostam Aziz anunua asilimia 31.5 ya Williason Diamonds (Mwadui)

na tukiendelea kusubiri huko mbele almasi nayo inaweza kuwa haina dili pia..tukabaki nayo tunacheza mdako...
Unajua diamond kazi yake sio tu decoration bali ina kazi nyingine...., Issue ni kwamba Tanzania ina resources kibao kuhakikisha tuna-exhaust zote katika kizazi hiki na tunachofanyia hizo pesa hakionekani ni upeo mfupi..., unaongelea mitaji na mashine za kuchimba n.k. unaonaje kama faida ya kwenye diamonds ingetusaidia kuwekeza kwenye madini mengine na kufanya uchimbaji angalau hisa / faida iwe 80 / 20 kwa in our favor ? Hizi ni commanding heights na zingetumika vizuri tungekuwa hatukabani mitaani na vi-tozo vya kwenye miamala (win / win for all)
 
Caspian Limited imefikia makubaliano na Kampuni ya South Africa Petra Diamonds ya kununua asilimia 31.5 ya hisa za Williamson Diamonds Limited(WDL) kwa thamani ya dola za Kimarekani million 15.

Caspian Limited ambaye ni technical services contractor wa WDL wamefikia makubaliano mwishoni mwa mwaka jana kama malipo ya malimbikizo ya madeni ya huduma (technical services) na huduma wanayotoa kwa Petra Diamonds Limited.

Petra Diamonds ilikuwa inamilikia asilimia 75 na serikali ya Tanzania asilimia 25.
Rostam Aziz ambaye ni Mwenyekiti na mmiliki wa Caspian Limited alisema:

“Caspian is a wholly Tanzanian owned company. It is also Tanzania’s largest mining contractor with over 30 years mining related experience. We have been the contractor of choice to most mines in Tanzania and have maintained long and successful relationships with companies such as Petra, De Beers, Barrick and AngloGold Ashanti. In addition, we also own the largest fleet of mining equipment in Tanzania. As a company, we are committed to adopting and adhering to the latest internationally recognised standards throughout all aspects of our business. “We have been contracting at the Williamson Mine, the largest kimberlite diamond mine in the world by surface area for close to 20 years and as such we are particularly pleased to enter into this next phase of our involvement at the mine as co-owners. We recognise its viability in providing sustainable employment and a significant contribution to the Tanzanian economy.”

Source: Reuters
Blacks tuko wapi ama tupo bizee na vumbi la kongo ,yaani akili inayotumika kuwaza ngono ni kubwa mno kuliko unaotumika kwa mambo ya maana na ya msingi
 
Una uhakika gani hao wazawa nao hawatoroshi kimyakimya kwenda huko South Africa? Pale mirerani ni wazawa watupu Ila kila leo wanatorosha Tanzanite kwenda kenya

Hii kauli ya kutorosha mawe mirerani ni ya kipuuzi kabisa huwezi chimba jiwe kwa shida afu upangiwe bei na soko la kuuza, Mimi binafsi utaniua tu.
 
Bora wafaidike wazawa kuliko makaburu wa south africa.

Ila watanzania tulivo na asili ya roho mbaya na upumbavu wa kiwango cha lami, lazima watu waanze kutoa kasoro ununuzi huu. Wataona bora hao makaburu waliokua wanatuma ndege private ndani ya mgodi na kusafirisha almasi kwenda South Africa kimya kimya.
Kwani Rostam na Makaburu wanatofauti gani?

Serikali imemuuzia hiza Rostam au Petra kauza hisa zake?
 
Sisi tunakwama wapi kuwa Kama wao au zaidi?

Chinese wengi waliopo hapa wanabackup kutoka china kwenye financial institutions na government support incase kuna opportunity imeonekana huku....

Indians na Arabs waliopo hapa wengi wana circles zao kwa ajili ya kupigana tafu, lakini pia ipo mikopo rahisi ndani ya familia isiyo na riba, Arabs wengi wanapata support kutoa Oman na UAE kwa kupewa mikopo bila riba au biashara mali kauli mfano mafuta na spare parts na wengine hata kwenda kupewa ajira uarabuni kiundugu kwa ajili ya kusupport wenzao huku..... Uwepo wao hapa unawapa chance ya kuziona opportunity na kuziingia huku wakipata unafuu kama wazawa...wengi unakuta wanarun biashara sio zao wenye nazo hawapo hapa na si watanzania...kazi yao ni kuleta mitaji na waliopo kutorosha hela kupitia njia mbalimbali... Lakini pia walioko nje huwapa connection za masoko uarabuni, umangani na uhindini huko....ndio maana akina Manji, Dewji,Fida hussein ndio wanunuzi na wauzaji wa nafaka na mazao mbalimbali, na madini, JPM alipojaribu kuweka miguu walimkomesha mazao yakadodea wakulima, na Tanzanite ikashuka bei..

Tanzania ina opportunities nyingi sana, Wazawa hawana maarifa, hawana mitaji, hawana acces ya masoko ya kimataifa, chanzo chake ni siasa za kijamaa toka uhuru na ubichwa ngumu wa wanasiasa kuendelea kuamini zama za mawe na ubaguzi wa kidini, kikabila, kindugu nk...

Unahitaji kuandika kitabu juu ya haya...na unaweza hata kutolewa roho, Marehemu Rev Mtikira alikuwa na mengi juu ya hawa watu..
 
Kumbe mgodi wa williamson ulishakuwa hauna thamani kabisa, yaani mgodi wote thamani yake ni kama dola milioni 48 tu kwani kama milioni 15 ni 31.5% basi 100% ni hiyo $47.5m ? Thamani hiyo ni chini kabisa ya gharama ambazo Waziri wa nishaiti anataka kutumia kukodi crane moja ya kufungulia maji bwawa la nyerere.
 
Nilifuatilia history yake, ni mtanzania wa kuzaliwa (by birth), mzawa wa wilaya ya igunga vijijini huko, mkoani tabora. Na ndio aliposomea shule na kukulia. Na alikua kichwa sana darasani mpaka kufikia alitoa A pekee ya hisabati tabora nzima NACTE darasa la 7 na form 4 kipindi hicho.

Aliproceed mpaka kusoma chuo Oxford University (UK) maswala ya uchumi na biashara. Na aliwaburuza kweli kweli. Then akaingia kwenye siasa na kugombea Ubunge hapo hapo Wilaya ya Igunga.

Mnyamwezi wa tabora huyo [emoji23][emoji23][emoji23]
Cooked
 
Kinachoendelea sasa ni looting of our national resources.

Through the so called investments.

Asipotokea mtu kusimama kidete we are all done.

Mzee iba na wewe utaendelea kulalamika hadi mwisho wa dahari. Everyman for himself dunia ya leo.
 
Nilifuatilia history yake, ni mtanzania wa kuzaliwa (by birth), mzawa wa wilaya ya igunga vijijini huko, mkoani tabora. Na ndio aliposomea shule na kukulia. Na alikua kichwa sana darasani mpaka kufikia alitoa A pekee ya hisabati tabora nzima NACTE darasa la 7 na form 4 kipindi hicho.

Aliproceed mpaka kusoma chuo Oxford University (UK) maswala ya uchumi na biashara. Na aliwaburuza kweli kweli. Then akaingia kwenye siasa na kugombea Ubunge hapo hapo Wilaya ya Igunga.

Mnyamwezi wa tabora huyo [emoji23][emoji23][emoji23]
Duh hakika ukitaka kujua story za tajiri tuulize sisi wanyonge.

Asante mkuu
 
Hii kauli ya kutorosha mawe mirerani ni ya kipuuzi kabisa huwezi chimba jiwe kwa shida afu upangiwe bei na soko la kuuza, Mimi binafsi utaniua tu.
Maswala ya kutorosha ww ndio umeyaleta alafu Sasa hivi unapingana nayo. Pumbavu mkubwa
 
Back
Top Bottom