Rostam Aziz: Dkt. Slaa alihongwa 2015 kuisaliti CHADEMA, akapewa Ubalozi

Rostam Aziz: Dkt. Slaa alihongwa 2015 kuisaliti CHADEMA, akapewa Ubalozi

Fisadi papa linajitokeza huyu SI ndio mmiliki WA dowans Leo anajifanya msafi,huyu ndio bingwa was kununua waandishi was habari
 
Rosti tamu kelele zote hizi anatetea wenzake (rangi yake) na kwa vyovyote yeye atafaidika na huu mkataba.
Anasema Slaa sio mwaminifu, ni sawa kabisa, sasa yeye Rosti Tamu ni mwaminifu? tangu lini? labda aanze kesho!
Nimkumbushe tu namna alivyopata umiliki wa Vodacom (T)
Dowans
Alivyokuwa ananunua waandishi wa habari amesahau pia?
 
Mchana wa leo Rostam amefanya mkutano na waandishi wa habari. Pamoja na mambo mengine ametoa tuhuma nzito kwa serikali na mahakama.

Amesema Dr. Slaa alinunuliwa wakati wa uchaguzi na kukisaliti chama chake cha Chadema na kisha kupewa ubalozi. Hizi ni tuhuma nzito za rushwa wakati wa uchaguzi.

Rostam anasema mashtaka ya mkataba wa kimataifa hayawezi kupelekwa kwenye mahakama zetu kwa sababu Mtu wa serikalini anaweza tu kupiga simu kwa hakimu au Jaji na kumpa maelekezo ya hukumu. Mahakama yetu ina majibu wa kujibu tuhuma hizo.

--
Watanzania wakumbuke kuwa, huyu mtu (Dkt. Slaa) alipokuwa CHADEMA mwaka 2015 alikisaliti chama chake wakati kukiwa kinaelekea kwenye uchaguzi, alikisaliti chama chake kwa kuhongwa, alihongwa ndipo akaasi na kukisaliti chama chake (CHADEMA). Alikaa zake pale Serena baada ya pale akapanda ndege kwenda Canada na kisha akapewa ubalozi

Kwa kifupi Dkt. Slaa hana uadilifu wala uaminifu wa kunisema, mtu ambaye hana msimamo, mbinafsi , anayeangalia maslahi yake na hajawahi kuchangia chochote katika uchumi wa nchi yetu kazi yake ni kupiga tu mdomo. Mtu wa namna hii kumjibu ni shida lakini ni lazima wakati mwingine umjibu
na aliyeitoa rushwa asemwe na kukamatwa apelekwe mahakamani,na huyu Rosti Tamu iko siku ataliwa
 
Back
Top Bottom