Rostam Aziz: Mjadala wa Bandari unajadiliwa kishabiki. Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana

Mwekezaji ambaye Mkurugenzi wa Taifa Group, Rostam Azizi amesema kuwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi Nchi imekubaliana Serikali hisifanye biashara kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kuchochea maendeleo.

Amesema kwa upande wake hana tatizo na mjadala wa Bandari lakini katika kufuatilia mjadala huo anachukizwa mjadala huo kuwa wa kishabiki na kuibua udini na ubaguzi "Unamuona kiongozi mkubwa anaanza kuzungumza Uzanzibar na Utanganyika"

Amesisitiza kuwa mjadala huo umekuwa ukijadiliwa kishabiki sana huku akidai kuwa Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana.

Ameyasema hayo katika mjadala unaendelea Serena Hoteli leo Jumatatu, ambao umeandaliwa na taasisi ya Media Brains “Kulinda na Kuendeleza Umoja wa Kitaifa Wakati wa Mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi” (Protecting and Promoting National Cohesion in Times of Political and Economic Reforms).

Baadhi ya washiriki katika mjadala huo ambao wanatarajiwa kutoa maoni ni Katibu wa TEC, Padre Kitima, Jenerali Ulimwengu, Zitto Kabwe, Godbless Lema, Steven Wasira, Prof. Kitila Mkumbo

(Taarifa zaidi katika mjadala huu zitaenedelea kukujia).

View attachment 2662260
Kwenye mjadala huu nimewajua wakirito ni watu waina gani
 
Mnyamwezi wa Igunga Tabora

Ndiyo mbunifu alieifanya serikali kuanzisha mfumo wa Bima ya Afya

Mwaka 1995 akiwa mbunge wa Igunga alianzisha mfumo wa Bima ya Afya, mkapa aka copy kwake na kuuingiza serikalini.

Wewe mzalendo umefanya nini kwa Tanzania?
Naongezea ni mlipa kodi mkubwa
 
Ndiyo iendeshwe milele? Ndiyo bandari zote apewe mtu mmoja? Bandari ni swala la muungano au siyo muungano?
Tatizo lako umejaa kama kifutu kwa chuki,kasema hana shaka na mjadala wa bandari kinacho muudhi kuingiza Udini!!!
 
Huyu ni kabila gani?
Unauliza kabila kwani unataka kutambika hapa, achana upuuzi wa ukabila, kabila linamsaada gani katika maisha ya binadamu. Huyo ni mtanzania kabila lake halituhusu chcochote.
 
Kwanini watanganyika ni wazito hivi kuelewa? Ukisoma hoja yangu ililenga ukabika?
 
Rostam ana hoja nzuri, asipuuzwe.....

JokaKuu Mag3 Nguruvi3 Kalamu zitto junior
Mbona hana tofauti na hao wengine wote wanaopotosha kuhusu swala husika?

Kwani hoja ni kuwekeza kwenye Bandari, au ni uwekezaji wenye tija kwa Tanzania?

Huyo Roast umemsikia akichambua makubaliano yaliyosainiwa, na kupitishwa na Bunge?

Akichambua matakwa ya mikataba hiyo na kuonyesha kuwa hakuna madhara juu yake ni nani atapinga?

Mkuu 'Proved', hili swala la DP World hata kama ni zuri kwetu, mbona hawa wanaolipigia kelele sana ni kama wanawaona waTanzania wote hawana akili?
Azungumzie mikataba, uwekezaji hakuna anayeupinga.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Akifa wewe utakuwa tajiri? Ukute hata mlo wa mchana umekupita tu.
"Hukufikiri kabla ya kuandika". uliyoandika hapa (kama vineno vyako hapo chini ya jina lako vinavyokupasa ufanye).

Huyo uliyemjibu hapo juu, alikueleza kuwa anataka utajiri wa huyo Roastam?
 
..kupoteza muelekeo wa mjadala ni uamuzi wa wanaojadiliana.

..na mfano mmoja ni yeye Rostam anapojaribu kumlisha maneno Mbowe kuwa amezungumzia Utanganyika vs Uzanzibari tu.

..yeye Rostam mbona hakuzungumzia mazuri na mapungufu ya makubaliano ya Dubai / DP na Tanganyika?
Hawa akina Roast, ndio wenye serikali.
Serikali ya Samia inatengeneza' oligarch' wake, ambao ndio hawa hawa akina Roastam.

Roastam hana shida yoyote na ufanisi wa Tanzania, mradi yeye na shughuli zake zifane kwa njia yoyote iwezekanayo.
Samia anapigana usiku na mchana hawa watu waneemeke, hata kama Tanzania inaumia.
 
Mwekezaji ambaye Mkurugenzi wa Taifa Group, Rostam Azizi amesema kuwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi Nchi imekubaliana Serikali hisifanye biashara kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kuchochea maendeleo.

Amesema kwa upande wake hana tatizo na mjadala wa Bandari lakini katika kufuatilia mjadala huo anachukizwa mjadala huo kuwa wa kishabiki na kuibua udini na ubaguzi "Unamuona kiongozi mkubwa anaanza kuzungumza Uzanzibar na Utanganyika"

Amesisitiza kuwa mjadala huo umekuwa ukijadiliwa kishabiki sana huku akidai kuwa Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana.

Ameyasema hayo katika mjadala unaendelea Serena Hoteli leo Jumatatu, ambao umeandaliwa na taasisi ya Media Brains “Kulinda na Kuendeleza Umoja wa Kitaifa Wakati wa Mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi” (Protecting and Promoting National Cohesion in Times of Political and Economic Reforms).

Baadhi ya washiriki katika mjadala huo ambao wanatarajiwa kutoa maoni ni Katibu wa TEC, Padre Kitima, Jenerali Ulimwengu, Zitto Kabwe, Godbless Lema, Steven Wasira, Prof. Kitila Mkumbo

(Taarifa zaidi katika mjadala huu zitaenedelea kukujia).

View attachment 2662260
Na wanaopigia makelele ni maskini ambao hawachangii hata mia kwenye Kodi 😁😁
 
Rostam sio mtanganganyika, hivyo hana uchungu na raslimali za Tanganyika. Yeye aendelee kuchuma kwenye hili shamba la bibi. Hawezi kuumia Mzanzibari akiuza Tanganyika yetu.
 
Back
Top Bottom